Kili beer VS Kili marathon

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,173
481
Kili Marathon ya 9 tumeshuhudia jana tena Watanzania wanaondoka mikono tupu tufanyeje. Je ni sawa ama nini kifanyike.
 
mkuu huwezi kushindana na wenzako wakenya wanaofanya mazoezi....sisi kila jioni twala kitimoto na beer wapi na wapi?.....tujaribu draft au karata
 
Nakubaliana na wewe lakini hata wao huwa wanakunywa. Kuna tatizo zaidi ya hilo. Tukiondoa ukiritimba wanaweza kufanya vizuri zaidi.
Mfano: niliongea na wachezaji toka CCP moshi, wengi wao ni wanariadha wazuri sana lakini hawapati muda wa kufanya mazoezi. Utakuta mtu aling'ara kwenye mashindano fulani halafu viongozi wa jeshi wanawachukua kuwapa ajira. Wakishaajiriwa tu sheria za jeshi palepale. Unapelekwa lindoni wakati wa ratiba ya michezo. Unategema huyu mtu atakuwaje. Anaweza kweli kwenda lindoni na wakati huo huo kufanya zoezi? Hata ruksa za kushiriki mashindano ya kimataifa huwa ni shida kwao!
 
Hatujui tunachokifanya wala hatujui tunachokitaka kwa hiyo hapa tulipo hatujui tupo wapi tunaenda mbele au tuna rudi nyuma yaani tumechanganyikiwa kila sekta sio riadha tu!!!!!
 
Back
Top Bottom