Yaani unaweza kuona uongozi wa pamoja wa wabunge wetu wa Dar es Salaa! kama siyo wabunge wote, viongozi wengi wa kuchaguliwa hapa Tanzania.
Wameungana pamoja kutetea nauli za kigamboni, kwa maslahi ya kisiasa kama alivyosema mh. Dewji na si jingine.
Nilisikia kwenye redio, wapo redio kwamba kuna zahanati / hospitali inayoitwa Tungi Kigamboni, dawa za mseto wanazo dozi kumi kwa ration ya miezi mitatu, daktari kwa sasa yupo likizo hakuna wa kumshikia nafasi yake, maabara haina mpimaji vipimo, ukiugua wanabashiri huu utakuwa ni ugonjwa fulani, halafu unaandikiwa dawa ya kununua duka la dawa.
Zahanati hiyo ipo Kigamboni, lakini mbunge wa eneo hana habari kushughulika na matatizo hayo na mengineyo.
Ukiwauliza hawa wabunge, kazi za msingi walizo ahidi kufanya, hawajafanya chochote kwa tathimini ya mwaka mmoja waliopo madarakani.
Mbunge wangu, madaraja yameharibiwa na mvua, barabara zimeharibika, lakini mbunge wetu hajafanya mkutano wowote na wapiga kura wake, lakini amepata muda wa kwenda press conference.
Tunaweza kujiuliza swali la msingi Tanzania, hivi viongozi wa kuchaguliwa, wabunge, serikali za mitaa, madiwani wanaonyesha uongozi wowote? Au uongozi hauwezi Tanzania ? Basi kwanini tunapoteza muda kuchagua viongozi ??
Kwani kulipa nauli halali ni suala la haki nalo? Mbona hao wabunge wengine wana bishara ya daladala wasishushe nauli za daladala zao au wasafirishe wananchi bure kama kweli wanawapenda wananchi wao?kama wewe ni kiongozi wa chama ndani ya dar, ulishindwa nini na wewe kuwaongoza wananchi kuzidai haki zao kama hawo wabunge wameshindwa?
Mimi niseme tu kwamba wa kulaumu si tu wabunge bali hata viongozi wa kisiasa.Dar ni makao makuu ya vyama vyote vya upinzani,kwanini hawachukui hatua? Tukija hata kwenye chama pekee tegemeo cha chadema mbona harakati zao wanafanyia tu mikoani? Mbona vyama vikubwa duniani harakati zake ziko miji mikuu? Chadema hawajawahi hata kuitisha mkutano wa hadhara hapa Dar tokea uchaguzi mkuu.Sasa badala ya kufanya haya mtegemee wabunge wa CCM waongoze harakati Dar? Think twice!
Hivi zile Boat za Azm Dewji ziliishia wapi?...maana nakumbuka Mh POMBE alizikomalia kweli kweli
Hivi zile Boat za Azm Dewji ziliishia wapi?...maana nakumbuka Mh POMBE alizikomalia kweli kweli