Kilewo: Wabunge wa Dar acheni kulalamikia kauli ya Magufuli, chukueni hatua

Mh.J.Magufuli hajakosea kupandisha bei za kivuko cha magogoni labda tu maneno aliyosema ya watu kuogelea ( kupiga mbizi ) kama hawana nauli na wananchi tunaomba wamkubali kwa hilo alilofanya. Kwa hawa wabunge wa Dar hawajui watendalo maana ktk kikao cha Bunge kilichopita Mh.Azan Zungu ktk mchango wake katika wizara ya ardhi alisikika akisema watu wa mabonde ya Jangwani hawatakiwi kuhama na kama serikali ikishinikiza wahame atawaambia waandamane lkn leo tumeshuhudia wakifa kwa wingi wakati wa mafuriko, kwa hiyo hata hili la bei baadae ndo ataona usahihi wake, pia kumbukeni Dr. Masaburi alisema wabunge wa Dar. wanafikiria kwa kutumia nini (makalio).
 
Magufuli waombe radhi wakazi wa Dar. Huyu jamaa sijui vipi unajua unaweza kuwa msomi wa wa juu kabisa lakini mdomo ukakuumbua!!!
 
bila shaka wabongo ndiyo walianza kumkebehi magufuli km kawaida yao ...
 
Acha ulalamishi ndugu yangu na usiwe selfish hivi hiyo 800 wenzio washaanza sikunyingi sana kuilipa.Uliza watu wanaokaa kibamba,bunju na kwingineko wanalipaje gharama za usafiri daily!!Hebu muwe reasonable bwana miaka 14 nauli haijawahi kupanda leo inaongezeka kidogo kelele kibao aaarghhh!!
 
Mkuu, ukitoa hiyo 200 unaoona ndogo vipi Guta unafahamu bei yake?kutoka 500 mpaka 1800. Vipi huko Mwanza, Kivuko cha Kamanga, na Busisi mnalipa bei gani mkuu?
Kumbuka hili ni Jiji hivyo basi upandishwaji wa nauli za Maguta ni mkakati wa kuyapiga vita Maguta katika Jiji la maraha DSM. Tumieni gari aina ya Pick Up na sio maguta Tumethubutu tumeweza na Tunasonga mbele.
 
Kwa wabunge posho ya shs 200,000.00 ni sahihi. Lakini shs 200.00 ili zimsaidie hata yule mfanyakazi anaeshinda hapo japo kupata kikombe cha chai imekuwa nongwa. Hiyo ndio bongo. Daladala nauli 300.00 kila kituo, kwenye maji hakuna kituo ni safari hadi mwisho, bado wabongo watalalama.
 
Nakumbuka miaka fulani tulifanya kazi na jamaa mlalamishi. Mimi na rafiki yangu tukajikuta tunambandika jina la utani la mzee wa manung`uniko! Wa-TZ tuache manung`uniko bwana. Mzee Walwa Maviro yuko sahihi!! Utani wa Kisukuma umemponza tu kwenye hiyo kauli yake! Otherwise well done!

What a lame excuse, utani wa kisukuma? Majukumu ya kitaifa unaleta masikhara then unasingizia utani wa kisukuma
 
Magufuli komaa; hakuna kuomba msamaha kwa sababu hujamtukana mtu!

Akomae eeh! Okay, wacha na sisi tukomae tusipande hilo likivuko lao tuone kama watavushana wao kwa wao! nchi ni ya kwetu lakini tumekuwa kama tuko UTUMWANI, Viongozi wa sasa mambo mengi wanajiamulia tu wenyewe! ngoja 2015 ifike!
 
hivi ni kweli makelele yote haya ni kutokana na ongezeko la sh 100??? maisha magumu kwa watanzania ni kuongezewa sh 100 au kwa wabunge kujiongezea laki 330??? haohao wabunge eti wanasimama na kuongea mishipa ikiwatoka mapovu mdomoni yakiruka eti huu si upuuzi huu jamani?
 
Nchi hii ni ya kinafiki sana, hawa wabunge wanataka kujiongezea posho kutoka tshs. 70,000/= mpaka tshs. 2,00,000/=, leo wanajifanya kuwaonea huruma wananchi kwa kuongezwa tshs. 100/=
Binafsi namuunga mkono Magufuri kwa sababu moja ifuatayo;

  • Wananchi wa dar es salaam hawataki mabadiliko, kama mnavyodai Magufuri kwamba kawatukana basi hayo ni matokeo ya kura zenu. Namuomba Mh Magufuri kama inawezekana ongeza bei maradufu iwe hata tshs. 500/= hivi, si walikubali wenyewe bila kushurutishwa kula ubwabwa wenu? walikubali kuvaa tshirt, kofia na vilemba vyenu?
 
Kutokana na kauli na maaumuzi magumu na ya kijasiri ya Mh Waziri Magufuli juu ya kupandisha nauli ya kivuko cha kwenda kigamboni Watanzania wengi wenye mtizamo wa kimaendeleo wanaona ni vyema sasa nchi ikapata kiongozi dikteta atakayesimamia maendeleo ya nchi kiubabe kama alivyo Magufuli.

Mh Magufuli amezidi kuonyesha ujasiri wake hadi kwa kupingana na wabunge wa chama chake katika kusimamia msimamo wake kwani wabunge wa Dar katika sakata hili waidhirisha dhahiri kauli ya meya wa Jiji kuwa wanafikiria kupitia Makalio kwani badala ya kuwaongoza wananchi waliowachagua kupinga mchakato wa katiba na kupanda kwa bei za vyakula kama mchele, dagaa, unga, mafuta ya kula, sukari etc wanaibuka kupinga ongezeko la nauli.

Hivi huyu mbunge wa Kigamboni alishawahi kupinga hata ongezeko la posho za wabunge jibu ni hapana sasa anawalaghai watumishi kwa kuungana nao kupinga ongezeko la nauli ya kivuko tu na sio kupinga ongezeko la gharama za Maisha kwa ujumla.

kutokana na kauli ya Magufuli naona sasa imefika wakati wa nchi hii kutawaliwa kidikteta ili kufanikisha maendeleo ya nchi kwani siasa zimekuwa nyingi kuliko utendaji hongera Magufuli simamia msimamo wako wasio taka wapige mbizi au wachonge mitumbi yao;

Kwani Magufuli alipinga posho nae? au unasahau naye ni Mbunge na posho ni swala la wizara ya Fedha kwa hiyo huwa anasikiliza kama Mbunge?
 
Ukitaka kujua kuna I'd zimeonganishwa basi pitia huu uzi.

Mtu alikuwa anajiqoute mwenyewe.
Dah kumbe na ww Umeona eeeh sijamuelewa kabisa kwanni alianzisha mada alafu akajipinga mwenyewe tena...... Sijui alikuwa anamaanisha nini au alitaka kupata maoni ya pande mbili kinzani

Duh siasa bhana
 
Unalolisema kamanda Kilewo ni la msingi sana lakini katika umoja huu wa wabunge hawa walioungana yaani wa upinzani na wa chama kilichounda serikali unafikiri ni rahisi hivyo kwa wabunge hawa wa ccm kukubali kuandamana na kuikosoa serikali kwa kumpinga waziri mwenye dhamana! Hakika ni vigumu na ndio maana wanaweza hata kuwapumbaza wabunge makini wa upinzani kwa kutatua matatizo ya wananchi kwa kupitia vyombo vya habari pasipo kuchukua action. Nakupongeza kamanda Kilewo kwa kuliona hili.
Naona Mamuya wa Kilimanjaro unaunga mkono hoja ya kilewo wa Kilimanjaro akina Manka,Mushi ,Munisi nk Toka Kilimanjaro karibuni muunge mkono hoja ya homeboy Kilewo
 
Back
Top Bottom