Kilewo: Sintompongeza Rais juu ya swala la wapangaji kwani ni wajibu wake, mkuu wa mkoa ni bomu

Henry Kilewo

JF-Expert Member
Feb 9, 2010
899
1,084
Nukuu toka kwa Kilewo kwenye fb................

Ndugu zangu Watanzania: Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam bwana sadick, alinukuliwa na chombo kimoja cha habari, bwana sadick kupitia chombo hicho aliniponda kuwa najitafutia umaarufu kupitia wahanga wa mafuriko wale wapangaji, alipinga kauli yangu ya kuwa wapangaji wanastahili kupewa viwanja na huduma zote za msingi za kibinadamu kama ambavyo wanapewa wenyenyumba kwa kuwa waathirika wakubwa siyo wenye nyumba bali ni wapangaji. Bosi wake juzi amemuumbua kwa kuungana na Tamko la CHADEMA mkoa wa Dar es salaam nililolitoa kwa niaba ya chama.

Najiuliza ni kwanini mkuu wa mkoa alikuwa analazimisha wapangaji wasipatiwe viwanja na huduma mbalimbali za msingi..... jibu lake ni kuwa kila jiongozi tuliye naye anaangalia dili la kupiga badala ya kusimamia ukweli... ila sinto mpongeza Rais kwa hilo kwani ni wajibu wake wa kuwatumikia watanzania ila nampa pole kwakuwa na mkuu wa mkoa bomu........... Nitaendelea kuwapigania watu wangu...( Wananchi) mpaka haki itakapo tendeka kwa wote
 
Mecky Sadiki aliona akiwapa viwanja hadi wapangaji watakosa na wao vya dili,big up makamanda
 
Mecky Sadiki aliona akiwapa viwanja hadi wapangaji watakosa na wao vya dili,big up makamanda

Tunapenda watu wanaosimamia ukweli bila kujali cheo cha mtu, kwa hili naungana na mimi na kilewo pamoja na viongozii wengine wa CDM Dar es salaam, hongereni sana kazi zenu zinaonekana . binafsi niliona Tamko la Kilewo ITV kesho yake Asubuhi nikamuona bwana sadick akipingana na Tamko hilo.
 
kuongoza dsm si mchezo,huko kusini ndio maana wako nyuma,usitegemee cha maana toka kwa mkuu wa ccm wa mkoa bogus kama huyu,na jk didnt mean what he said,ni moja kati ya sanaa zake,katimiza ahadi gani?
 
Chadema waongezeeni vijana hawa wa Dar nguvu ya kisiasa ili jiji hili sasa lisimame imara kama mlima sinai.
 
mimi naishangaa serikali ya ccm,wenye nyumba ni matajiri waliovamia maeneo ya mabondeni wakajenga nyumba wakapangisha watu na hawakai.wanahatarisha maisha ya watu leo wananchi masikini wamechukuliwa vitu vyao wamezidi kuwa masikini zaidi leo wale waliofanya makosa ndio wanaooongezewa viwanja ili masikini wazidi kupanga .
ni akili gani hawa watu wanatumia?
kama ni mimi ningewapa wapangaji viwanja na kuwanyima wenye nyumba ili wajifunze,
mwenye nyumba ningempakiwanja kama alikuwa anaishi kwenye nyumba.

badala yake rais anachonganisha mkuu wa mkoa na watu wa mabwepande,kwani hana mamlaka ya kuamuru nini kifanyike?mbona analalamikia walioko chini yake?
tuacheni tuna msiba.
 
Mimi kwa upande wangu nampongeza Rais kwa moyo wake wa kibinadamu kuwajali wapangaji na hatimaye kuwapatia viwanja pamoja na huduma zingine za kibinadamu.
 
Nukuu toka kwa Kilewo kwenye fb................

Ndugu zangu Watanzania: Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam bwana sadick, alinukuliwa na chombo kimoja cha habari, bwana sadick kupitia chombo hicho aliniponda kuwa najitafutia umaarufu kupitia wahanga wa mafuriko wale wapangaji, alipinga kauli yangu ya kuwa wapangaji wanastahili kupewa viwanja na huduma zote za msingi za kibinadamu kama ambavyo wanapewa wenyenyumba kwa kuwa waathirika wakubwa siyo wenye nyumba bali ni wapangaji. Bosi wake juzi amemuumbua kwa kuungana na Tamko la CHADEMA mkoa wa Dar es salaam nililolitoa kwa niaba ya chama.

Najiuliza ni kwanini mkuu wa mkoa alikuwa analazimisha wapangaji wasipatiwe viwanja na huduma mbalimbali za msingi..... jibu lake ni kuwa kila jiongozi tuliye naye anaangalia dili la kupiga badala ya kusimamia ukweli... ila sinto mpongeza Rais kwa hilo kwani ni wajibu wake wa kuwatumikia watanzania ila nampa pole kwakuwa na mkuu wa mkoa bomu........... Nitaendelea kuwapigania watu wangu...( Wananchi) mpaka haki itakapo tendeka kwa wote

kwani sera yenu inakataza kumpongeza mtu alotekeleza wajibu wake?
 
Ndio aina ya watendaji wanomzunguka Rais na ndio maana nchi hii inayumba!!!! Uwezo wao wa kufikiri na kubuni umefika UKOMO, NAKUPONGEZA RAIS.
 
Back
Top Bottom