Kile kinachoendelea Uganda ni sawa na zimwi la maonesho Afrika

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
KILE KINACHO ENDELEA UGANDA NI SAWA NA ZIMWI LA MAONESHO AFRIKA.

Makala yangu no 05. Juu ya ziara yangu East, Central & Great lake zone of Africa.
Na: Comred Mbwana Allyamtu.

Uganda ni nchi inayopatikana Afrika ya Mashariki ya bara la Afrika. Imepakana na Kenya upande wa mashariki, Sudan Kusini upande wa kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa magharibi, Rwanda na Tanzania upande wa kusini. Uganda inamiliki sehemu ya ziwa la Viktoria (Nyanza) kwa karibu 39.4% ikiwa inamiliki sehemu kubwa ikiwa nyuma ya Tanzania inayomiliki 49% na Kenya 11.6%. Uganda ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki toka katika jumuiya ya mwanzo na ya awamu ya pili ya mwaka 2002 na uchumi wake ni GDP 24 billion US$ kwa mujibu wa takwimu ya WB ya mwaka 2016. Sarafu yake ni Uganda shilingi. Na ndio nchi ya tatu (3) kwa ukubwa wa uchumi Afrika mashaliki ikiwa nyuma ya Kenya ambayo GDP yake ni 46 billion US$ na Tanzania GDP ni 35 billion US$.

Pamoja na hiyo Uganda ndio taifa linaloongoza Africa mashaliki ambayo Cut Tax Ratio (CTR) ni ndogo kuliko nchi zote. Mji mkuu wake ni Kampala na ndio jiji kuu kabisa kibiashara, kiuchumi,kisiasa na katika shuguri zote za kiserekali. Tarehe 26/8/2016 niliwasili kampala Uganda kuanza ziara yangu nchini Uganda nikitokea Jamuhuri ya Afrika ya kati nikipitia nchi ya kongo-DRC katika jimbo la Oriontale na kuvuka mpaka wa Bunagana na kuingia nchini Uganda. Hii sio mara yangu ya kwanza kuizuru kampala kwani nimewahi kuizuru nchii hii mwaka 2010, 2013, na 2014 lakini kwa awamu hii ziara yangu imekuwa nikielekea Uganda kama nyumbani kwani nje ya kuijua Uganda kidpromasia lakini pia huwa najihisi vizuri haswa na pia kujiona niko nyumbani kutokana na kuwa na ndugu, jamaa na marafiki wa kutosha.

Nikiwa kampala awamu hii nimejifunza mambo mengi yaliyo pelekea kuandika makala hii ya leo. Kama nilivyo ahidi na kuendelea kutekeleza kile nilicho ahidi kufanya katika ziara yangu toka mwanzo mpaka nchii hii ya Uganda toka kwenye makala yangu ya Burundi No-01, nikiwa nchini Burundi. Makala ya Rwanda No-02, nilipokuwa nchini Rwanda. Makala yangu ya DRC-Kongo No-03, nilipokuwa kongo-DRC na makala ya Jamuhuri ya Africa ya kati No-04, nilipokuwa nchini Afrika ya kati pamoja na hii ya sasa ya Uganda ya No-05. Hivyo pamoja na shukurani nyingi toka kwa wadau wangu wote ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa wakinipa ushirikiano wa karibu sina budi kutoa shukurani zangu kwao lakini kwa nafasi ya pekee kabisa namshukuru mwenyezi Mungu kwa kuendelea kunijalia afya bora na yenye nguvu kuendelea kuzunguka nchii hizi kwa afya njema na kunijalia uhai. Mwisho shukrani zangu kwa serikali ya nchi yangu ya Tanzania kunipa ushilikiano wa karibu katika masuala yote ya dipromasia niwepo nje ya nchi yangu.

HISTORIA YA UGANDA.

Eneo la Uganda limeona uhamiaji wa vikundi vingi waliowazidi wenyeji asili (walioishi huko tangu miaka 50,000 BC kama si 100,000 BC). Kusini liliingiliwa hasa na wakulima Wabantu. Kaskazini iliona kufika kwa Waniloti kwa mfano Waluo na baadaye Karimojong miaka ya 379 AD. Tangu karne ya 15 himaya mbalimbali zilianza kujengwa na kati ya hizo ni hasa falme za Buganda chini ya utawala wa watawa walioitwa "KABAKA", himaya ya ANKOLE, BUNYORO na TORO zilizoendelea kuwa muhimu hadi kuja kwa ukoloni katika mwanzoni mwa miaka ya 1880's na kwa kiasi fulani kama urithi wa kiutamaduni hata katika Uganda ya kisasa. Na Karne ya 19 iliona kufika kwanza kwa Waarabu na baadaye kwa Wazungu. Kila mmoja alileta dini yake yaani Uislamu na Ukristo wa Kikatoliki na wa Kianglikana.

Katika mashindano juu ya Afrika ya Kati Waingereza walifaulu katika kushindana na Waarabu, Wafaransa na Wajerumani. Walienea kwa mapatano na Buganda wakisaidiana kukomesha upinzani kutoka falme za jirani. Na Baadaye Waingereza walikuwa na nguvu ya kutosha kuamua hata mambo ya ndani ya Buganda wakatangaza Uganda wote kuwa nchi lindwa tangu mwaka 1894. Mala baada ya makubaliano yalijulikana kama "mkataba wa Mutesa na Uingereza'' uliyo ipa mamlaka Uingereza juu ya Uganda yote na kumpa mamlaka madogo ya mlango wa nyuma (Indirect rule). Utawala wa ukoloni Uganda uliendelea mpaka miaka ya 1962 pale Uganda ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa Uingereza.

VUGUVUGU LA UHURU NCHINI UGANDA.

Militon Obote ndiye alie anzisha vuguvugu la ukombozi nchini Uganda, Milton Obote alikuwa mtu wa Kabila la Walang'o kutoka kaskazini mwa Uganda, na alikuwa akipinga madai ya Baganda kuwa na haki za kuchukuwa madaraka na pia urithi wa zama za ukoloni. Kupitia muungano wa chama chake cha Uganda People's Congress UPC - uliokuwa na wanachama kutoka nchini kote, alifanikiwa kushinda wingi wa kura bungeni na kufanikiwa kuunda serikali mwaka 1962 na kuchaguliwa kuwa Waziri mkuu wa kwanza wa Uganda na Kabaka Mutesa kuwa Rais wa kwanza wa Uganda asie na mamlaka makubwa.

Tofauti na Kabaka Mutesa aliekuwa na maono ya kuendeleza utamaduni wa ukoloni, wanasiasa wa wakati huo waliona fursa kwa Dr Militon Obote kuweka mwanzo mpya katika taifa la Uganda. Mara Baada ya uhuru Milton Obote tarehe 15 Aprili 1966, aliisimamisha katiba ya Uganda na kujitangaza kuwa rais ikiwa ni pamoja na kumfuta kazi Rais Kabaka Edward Mutesa II, Mfalme wa Buganda na rais wa kwanza wa Uganda. Pia alimlazimisha kwenda uhamishoni Edward Mutesa II, Mfalme wa Buganda na rais wa Uganda wakati huo. Baganda walikuwa kabila lililopendelewa zaidi na Wakoloni wa Kiingereza Kwa Winston Churchill wakati huo akiwa naibu waziri anaehusika na makoloni ya Uingereza, Baganda walikuwa watu wastaarabu, alisema mtaalamu wa Historia Frank Schubert "ni ufahamu huu kwamba Baganda walikuwa watu maalumu, uliochochea harakati za Wasomi wa Kiganda kutaka madaraka".

SIASA UGANDA BAADA YA UHURU.

matatizo ya ndani ya kisiasa nchini Uganda na kwamba viongozi wa kisiasa kama Obote wasingeona haya kulitumia jeshi, hata kwa kulibebesha jukumu kubwa la kujiimarisha. Historia imeenea mapinduzi ambayo hayakupelekea kuwepo na serikali za kiraia toka utawala wa awamu ya kwanza mwaka 1966 na Mwaka 1971 pale Obote alipopinduliwa na Idi Amin na akaenda kujichimbia uhamishoni nchini Tanzania, ambako alipambania na hatimaye kurudi madarakani mwaka 1980 kabla ya kuondolewa tena miaka sita baadae na rais wa sasa Yoweri Museveni. Kwa mantiki hii kabla atuajaanza kutazama kwa upana na upembuzi wa kina juu ya ujio wa Museveni na utawala wake miaka ya 1986 ni vyema tuutazame utawala wa Idd Amin Nduli Dada ulioanza mwaka 1971-1979.

Idd Amin Nduli Dada Alikuwa mwanajeshi aliepanda ngazi kuwa jenerali na mkuu wa jeshi la Uganda mwaka 1970, na ilipo fika Mwaka 1971 alimpindua rais Milton Obote na akajitangaza kuwa rais mpya, lakini wengine hawakumtaka. Mara moja baada ya kutwaa madalaka alianza kuwatesa wafuasi wa Obote na watu wote waliompinga. Kuna makadirio ya kwamba jumla ya watu 100,000 hadi 500,000 waliuawa katika miaka minane ya utawala wake. Kwa mujibu wa report iliyotolewa na Uingereza japokuwa madai haya hupingwa na badhi ya wataalamu wa mambo ya utawala na historia ya Uganda kwa kile wanachosema kuwa ni "Propaganda za Kimagharibi". Kwa upande huu hudai kuwa Idd Amin alikuwa kiongozi safi na alikuwa mtu aliye pinga utawala wa Ubepari na kuchukia mfumo wa mataifa ya magharibi kitu kilicho mchochea kaa la moto na kumfanya atengenezewe Propaganda zilizo mfanya aonekane mbaya na mtu wa Hovyo na muovu mpaka leo.

Lakini wanao dai kuwa utawala wake ulikuwa wa kidikiteta na kinyama wanamini kuwa utawala wake ulishiliki kwa ukaribu kuharibu uchumi wa Uganda kwa ufisadi na majaribio ya kuongoza biashara. Hatua kubwa ya uharibifu ilikuwa kufukuza watu wote wenye asili ya Kihindi na kugawa maduka na biashara yao kwa ndugu au wafuasi wa rais. Takriban watu 80,000 walipaswa kuondoka kwao wakihamia Uingereza, Marekani au Canada, na hasa Mnamo Oktoba 1978 Amin alianzisha vita dhidi ya Tanzania kwa kuvamia sehemu za mkoa wa Kagera. Rais Julius Nyerere wa Tanzania aliamua kumwondoa Amin kabisa na jeshi la Tanzania likatwaa Kampala tarehe 11 Aprili 1979 Amin alitorokea Libya, halafu nchini Irak na mwishowe Saudia alikopewa kimbilio na hifadhi ya kisiasa kwa masharti ya kutoshughulikia siasa tena. Aliishi huko mpaka Alipokufa mjini Jeddah tarehe 16 Agosti 2003.

VITA YA KAGERA NA USHAWISHI WA TANZANIA NCHINI UGANDA.

Kama nilivyo eleza hapo mwanzo kuwa Mnamo Oktoba 1978 Amin alianzisha vita dhidi ya Tanzania kwa kuvamia sehemu za mkoa wa Kagera kwa kudai kuwa ni sehemu ya Uganda Rais wa Tanzania wa wakati huo Julius Nyerere aliamua kuchukia maamuzi ya kumpiga kama alivyo bainisha mwalimu Nyerere mwenyewe kwa kusema *"Nguvu ya kumpiga tunayo Uwezo wa kumpiga tunao nia ya kumpiga pia tunayo na sababu ya kumpiga tunayo"* kwa maamuzi hayo Tanzania ilifanya uamuzi wa kuivamia Uganda na kumpiga kijeshi Mara baada ya Mapambano ya Vita vya Kagera, Mwanzoni mwa mwaka 1979 Vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania vilifanikiwa kumng'oa Madarakani Dikteta Amin wa Uganda na kumpachika Ndugu Yusufu Lule kama Rais wa Muda wa Taifa hilo Jirani. Lule hakudumu sana madarakani kwa kuwa mwezi Juni, 1979 naye aling'olewa madarakani kwa kutofautiana na Baraza la Ushauri la Taifa la Nchi hiyo juu ya uteuzi wa nafasi za Mawaziri, na nafasi yake kuchukuliwa na Ngudu Godfrey Binaisa.

Miezi kadhaa baada ya kuchukua madaraka kwa Binaisa katika Serikali ya Uganda bado mambo ya kuendesha nchi hiyo hayakuonekana kwenda vizuri, Changamoto za kujenga upya nchi hiyo iliyoharibiwa na vita zilikuwa kubwa, huku Jeshi jipya la nchi hiyo likiwa na kashfa ya kufanya ukatili kwa wananchi na pia kushiriki kwenye uhalifu na uporaji. Ili kuimarisha mambo ya Kiutawala ya Nchi hiyo ilimbidi Rais Nyerere ambaye bado vikosi vya Jeshi lake vilikuwa havijaondoka Uganda, ampeleke Waziri Hussein Ramadhani Shekilango kwenda kuisaidia mambo ya Kiutawala ya Nchi hiyo.

Mwezi Mei, 1980 ilizuka sintofahamu kubwa katika Utawala wa Uganda, Rais Godfrey Binaisa alimuondoa Jeshini Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Nchi hiyo (zamani akiitwa Chief of Staff) Ndugu David Oyite Ojok na kumteua kuwa Balozi wa Uganda Nchini Algeria, sababu kubwa ikitajwa kuwa ni nidhamu mbaya ya Jeshi la nchi hiyo hasa kwenye masuala ya Ukatili kwa wananchi na Uporaji. Uamuzi huo wa Rais Binaisa haukumfurahisha Kiongozi huyo Namba 2 wa Jeshi la Nchi hiyo, hivyo alikataa Uteuzi mpya, na wanajeshi waliokuwa Watiifu kwake wakatangaza kumuondoa Madarakani Rais Binaisa aliyekuwa akilindwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika Hekalu la Rais la Entebbe.

Misururu mirefu ya Magari ikaonekana katika Jiji la Kamapala, ambapo Wanajeshi watiifu kwa David Ojok walikuwa wakiyapekuwa magari yote yaliyokuwa yakitoka na kuingia ndani ya jiji hilo ili kuhakikisha hakuna silaha, huku pia wakikiteka Kituo cha Redio cha Taifa cha Nchi hiyo. Wanajeshi wafuasi wa Ojok waliweka vizuizi katika barabara zote za Jiji la Kampala na kuamua kuyalinda majengo yote nyeti ya Serikali likiwemo Jengo la Nile Mansion Hotel ambalo ndilo lililokuwa na Ofisi nyingi za Wizara nyeti za Serikali ya Nchi hiyo. Kung'olewa kwa Binaisa kulifanywa na Tume maalum ya Watu sita, ambayo ilikuwa ni sehemu ya Baraza la Ushauri la Taifa lililomng'oa Rais Lule, huku matendo ya Tume hiyo pamoja na Ojok kwenye wiki hiyo yakihusishwa zaidi na Rais Milton Obote aliyekuwa ughaibuni, ambaye aling'olewa Madarakani na Amin mwaka 1971. Obote alikanusha kuhusika na matendo hayo ya Ojok yaliyokuwa yakiteteresha hali ya ustawi wa nchi hiyo japo haikubadili ukweli kuwa marafiki hao lao lilikuwa moja.

KUIBUKA KWA MUSEVENI NA UTAWALA WAKE.

Uchaguzi wa mwaka 1980 ulimrudisha madarakani Milton Obote aliyeanzisha upya udikteta na kuua watu ovyo. Wapinzani wake wakiongozwa na Museveni walirudi porini wakashika silaha chini ya wanamghambo wa Nationa Resistance Amry (NRA) ambayo baadae ilibadilishwa jina na kuitwa NATIONAL RESISTANCE MOVERMENT (NRM) waliokiwa wakiongozwa na Yoweri Kaguta Museveni Katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kundi la Museveni likashinda na kutwaa serikali tangu mwaka 1986. Museveni mwenyewe ambaye alitokea kwenye tawi la vijana la chama cha Obote cha UPC, ametumia njia mbalimbali kuzigawa jamii ambazo Obote alizihodhi kabla yake. Kupitia jeshi lake la waasi ambao kwa sehemu kubwa walikuwa wanatokea Magharibi mwa Uganda, alifanikiwa kulishinda jeshi la serikali lililokuwa linadhibitiwa kwa sehemu kubwa na maafisa kutoka kaskazini hasa Walango na Wacholi.Yoweri Kaguta Museveni, alikuwako kati ya wanamigambo waliosaidiana na Watanzania katika vita vya kumpiga Amin Dada. Hata hivyo Yoweri Kaguta Museveni amezaliwa mwaka 1944 huko Ntungamo, Wilaya ya Ntungamo, nchini Uganda ni Rais wa sasa wa Uganda tangu 29 Januari 1986. Alichukua madaraka baada ya kushinda vita vya msituni chini ya kundi la National Resistance Movement na kushinda katika chaguzi za urais za mwaka 1996, 2001 na 2006.

Kwa muda mrefu, kabla ya kuwa rais wa Uganda, Museveni aliongoza vita vya msituni dhidi ya serikali za Idd Amin aliyetawala toka mwaka 1971-79, na serikali ya Milton Obote aliyekuwa madarakani mwaka 1980-85. Kutokana na mafanikio ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi na kukubali kwake kufuata sera za Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani, Museveni alipata sifa kubwa toka kwa viongozi wa mataifa ya Magharibi. Mwishoni mwa miaka ya 1990, Museveni alikuwa akielezewa kuwa ni mfano bora wa kizazi kipya cha viongozi wa Afrika. Hata hivyo uongozi wake umetiwa dosari na mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na ushiriki wake katika vita vya wenyewe kwa wenyewe katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda katika miaka ya 1993 mpaka 1994 Mambo mengine ni pamoja na ukiukwaji wa haki za kisiasa unaofanywa na serikali yake dhidi ya wapinzani kama vile Kizza Besigye na kitendo cha kubadili katiba ya nchi hiyo ili aweze kugombea urais mwaka 2006.

Tangu mwaka 1986 Museveni alifanikiwa kujenga mfumo ambao unamhakikishia kukaa madarakani kwa miongo kadhaa. Lakini mbinu zake zinafanana sana na za Obote kwa njia kadhaa. Katika mapambano dhidi ya kundi la waasi wa LRA kaskazini mwa Uganda, Museveni anarudia ulinganifu kati ya makundi ya wakaazi mbalimbali, na anaongeza bajeti ya jeshi kila mara. Na kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake Obote, anawaacha huru wanajeshi wake, hata wakati baadhi yao wametuhumiwa kwa kufanya unyama kaskazini mwa nchi hiyo. Toka mwanzo historia ya uganda imekuwa ni chafu katika siasa ikiwa ni pamoja ukiukaji mkubwa wa katiba, machafuko ya kisiasa, kuzuka kwa waasi na mapinduzi kitu inayoifanya historia yake iwe kama "Zimwi la Maonesho Balani Africa" kimsingi ukitazama utaona kuwa Uganda ilipata uhuru wake tarehe 9 Oktoba 1962 kwa katiba ya jamhuri yenye serikali ya kibunge tena Rais akiwa Kabaka Sir Edward Mutesa II na waziri mkuu Milton Obote. Lakini Mwaka 1967 Obote alibadilisha katiba akamfukuza Kabaka nchini. Serikali ya Obote ilipinduliwa na mkuu wa jeshi Jeneral Idi Amini mwaka 1971 hapa Utawala wake ulikuwa kipindi cha udikteta ulioharibu uchumi wa nchi na misingi ya dola. Takriban watu 300,000 waliuawa chini ya Amin ama wapinzani wa siasa yake ama watu wa makabila yaliyotazamwa kuwa maadui wa serikali. Raia wenye asili ya Asia walifukuzwa katika nchi na mali yao yote kutwaliwa na serikali. Na hapa ndipo museveni kwa msaada wa Tanzania alianzisha kikundi cha waasi kulichompinga Idd Amin ikumbukwe kuwa museveni alikuwa akiishi Tanzania na ndiko alikokuwa akifanya kazi yake ya ualimu kule mkoani Kilimanjalo wilayani Moshi.

Lakin katika mapigano ya waasi katika Vita vya wenyewe kwa wenyewe kundi la Museveni likashinda na kutwaa serikali tangu mwaka 1986. Museveni alichaguliwa rais katika kura bila vyama vya upinzani za 1996 na 2001. Pia Mwaka 2005 ulikuwa na uchaguzi wa vyama vingi wa kwanza ambapo Museveni alipata kibali cha bunge kwa badiliko la katiba lililomruhusu kugombea urais tena mwaka 2006 akachaguliwa mara ya tatu. Wakati upinzani ukiendelea kulalamikia ushindi wa Yoweri Museveni kwenye uchaguzi wa Februari 18, mwaka huu hofu ilitanda juu ya uwezekano wa kubadilishwa katiba ili kumuwezesha rais huyo kubaki madarakani maisha yake yote. Museveni, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 71, aliingia madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 1986, na tangu hapo ametajwa kama mmoja wa viongozi barani Afrika, waliojipendekeza kwa nchi za Magharibi kwa kupambana na ugaidi. Lakini kwa mujibu wa katiba ya sasa inamzuwia kushikilia tena wadhifa huo kwenye uchaguzi ujao, kwa kuwa atakuwa tayari amezidisha miaka 75 inayokubalika kugombea urais.

Upande wa upinzani, wachambuzi na wapiga kura, wanasema walitarajia Museveni angebadilisha kipengele cha umri, kwenye uchaguzi uliofanyika Februari 18, uliompa ushindi wa asilimia 60 ya kura zote. Kwenye uchaguzi huo, chama cha Museveni cha National Resistance Movement (NRM) kilifanikiwa kupata viti 275 vya ubunge kati ya 381. Upinzani unapinga matokeo hayo, ukisema yalikuwa ya kughushi, huku NRM ikizitupilia mbali tuhuma hizo. Wakosoaji wa Museveni wanasema kiongozi huyo mkongwe anafuata njia potofu ya viongozi wa Afrika wanaojaribu kukaa madarakani maisha yao yote, huku wakipuuza wito wa kuzingatia ukomo wa kuwapo madarakani. Viongozi wengi hukumbwa na woga wa kuachia ngazi, na sababu zake hazielezeki, alisema Nicholas Sengoba, mwandishi wa makala za uchambuzi katika gazeti la Daily Monitor la Uganda nilipomtembele katika ofisi zake zilizopo mtaa wa Sir Opolo Avenu jijini kampala hivi karibuni.

Kwenye mahojiano ya televisheni yaliyorushwa na shirika la utangazaji la Uingereza, BBC Museveni alionekana kuonyesha wazi uwezekano wa kubadilishwa kwa kipengele cha ukomo wa urais, pale aliposema, "hatuamini katika ukomo wa muhula, kama hamuwataki viongozi kukaa madarakani maisha yao yote, basi msiwapigie kura". Museveni aliyeongoza vita vya msituni na kumuingiza madarakani katika miaka ya 1980, amekuwa akihusishwa na juhudi za kuleta amani na kuinua uchumi wa Uganda, ingawa bado nchi hiyo inayotazamiwa kuwa mzalishaji mkuba wa mafuta ina changamoto kubwa ya miundombinu duni. Binafsi nilishuhudia matatizo makubwa ya huduma ya maji katika mikoa ya magharibi mwa nchi hiyo pamoja na ubovu wa barabara hasa hasa maeneo ya kaskazini mwa Uganda.

Wakosoaji wanampinga kwa kusema kuwa hakufanya jitihada za kutosha za kuondoa tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana na pia kwenye vita dhidi ya ufisadi. Pia anakosolewa kwa kushindwa kusogeza madaraka kwenye ngazi za chini katika juhudi zake za kuiendeleza Uganda Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye aliyetangazwa kupata asilimia 35 ya kura kwenye uchaguzi wa Februari 18, mwaka huu anamtuhumu Museveni kuuvuruga uchaguzi huo, na ameapa kuwa alikuwa akitarajia kuwa rais huyo angelifanya njama za kubaki madarakani, "Iwapo atabadilisha katiba ama la, udikteta kamwe haukubaliki nchini Uganda Licha ya kampeni yake ya ufidhuli, hatutasimama hadi udikteta utakapoondolewa madarakani," alisema Besigye.

Kwenye baadhi ya mitaa mjini Kampala, wananchi wengi waliopiga kura wakati wa uchaguzi wa feb 18 mwaka huu walisema wangeshtushwa kama Museveni angeachia madaraka, ama kwa kutaja jina la atakayempokea ama kustaafu. Zaidi ya robo tatu ya Waganda wapo chini ya miaka 30, na hawajawahi kumjua rais mwingine zaidi ya Museveni. Kwenye taifa hilo lililowahi kukabiliwa na historia ya muda mrefu ya vurugu chini ya viongozi kama Idi Amini, aliyeendesha serikali iliyojaa ukatili na mauaji ama mateso kwa kiasi cha watu 300,000 katika miaka ya 1970, Museveni anaonekana tafauti na anatajwa kama mdumishaji usalama. Hata hivyo, aliyewahi kuwa rais wa Marekani, Bill Clinton, alimtaja Museveni kama kiongozi wa kizazi cha sasa cha viongozi wengine wa Afrika wanaoififisha demokrasia. Na sasa, raia wengi wa Uganda wanamfananisha na rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, ambaye mwezi huu ametimiza miaka 92, bila ya kuonyesha dalili za kuachia madaraka.
1472827123462.png

MY TAKE.
Uganda ni miongoni mwa nchi balani Africa ambazo zimeendelea kuchafua utukufu wa historia ya democrasia katika Afrika. Kung'angania madalakani na kuifinyanga democrasia nchini mwake imetajwa kama uendelezaji wa mfumo ukoloni mweusi na kutokuheshimu matakwa ya umma ambayo ni katiba. Katika ziara yangu ya mwisho katika hii nchi ya Uganda ndio itakuwa misho wa muendelezo wa makala zangu katika ziara hii ambayo sasa niko katika maandalizi ya kulejea nyumbani Tanzania hivi karibuni kwa kuendelea na majukumu mengine ikiwa ni pamoja na uchmbuzi wa makala zingine mbalimbali. Pamoja na hivyo nini Tanzania tunajifunza kutoka katika Uganda? Hili ni swali ninalowaachia wasomaji wangu.

"Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Uganda, Mungu wabaliki Waganda, Mungu baliki fikra za waafrika".

Na: Comred Mbwana Allyamtu.

copy rights reseved
written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu
Kwa Tanzania
+255679555526.
+255765026057.

Kwa Rwanda
+250733153930
+250788214234

Kwa DRC
+243 977 860 824
Email- mbwanaallyamtu990@gmail. Com
1472827104421.jpg
 
Email- mbwanaallyamtu990@gmail. ComView attachment 392414
 
1472827854783.png
 
Baliki-Bariki
Balani-Barani
Lejea-Rejea

Kuna sehemu unasema Idd Amin aliua takribani Waganda 100,000 mara 500k lakini aya zinazofuata una andika aliua Waganda 300K
 
Biggest up Bro makala nzuri sana nafikiri hii ni formal series basi jitahidi kuzingatia usahihi wa kisarufi kuna mahali pengi unashindwa kutofautisha 'L' na 'R' pia statistics zipo twisted kidogo.

Kudos.
 
Mmmh aisee tunashukuru kwa kutupa historia ya Uganda, natumaini kwa kuwa alipigana bega kwa bega na JWTZ kuikomboa Uganda basi watampandisha cheo na kuwa general na akija huku JWTZ liwe linampa heshima kama general Mstaafu wa JWTZ
 
Ulichoeleza no historia ya kisiasa na kiutawala. Uloyaeleza yote MTU anaweza kuyapata kwenye machapisho na vyanzo vingine vilivyopo tayari. Isitoshe imerudiarudia mambo. Kama ulifika Uganda kama ulivyodai simulizi yako ingejikita kwa uliyoyaona na si historia. Kwa sisi tunaoijua Uganda hakuna kipya kilichoelezwa na mengine hauko sahihi. Mfano, Museveni hakumpindua Obote. Wakati Museveni anaingia Kampala Obote alishafukuzwa na wenzake. Nchi ililkuwa chino Jenerali Tito Okello. Majeshi ya Tanzania hayakuivamia Uganda. Yalipigana vita kumuondoa katika eneo alilovamia Kagera. Aliposhindwa akakimbia na majeshi ya TZ yakamkimbiza mpska ndani ya Uganda mpaka akakimbia nchi.
 
Mkuu, maudhui ya makala yako ni nzuri plus uhalisia wa siasa za Africa especially nchi ya Uganda. Ila kuna mambo mengi ambayo unatakiwa uyafanyie kazi ili kuboresha makala zako ikiwa ni pamoja na kuto-bore wasomaji. kumbuka pia, Nchi ya Uganda imekuwa kwenye misukosuko ya kisiasa tangia enzi za Milton Obote, Iddi Amini-Dada na hata huu uliopo wa sasa (Yoweli Kaguta Museven), hivyo Machungu ya utawala wa kiimla haujasahaulika kwa waganda wengi. Mimi ushauri wangu ni hivi:-
  1. Jaribu kuzungumzia vitu muhimu ambavyo vitamfungua macho msomaji wa makala. Hivyo utatumia paragraphy chache lakini zenye ujumbe mzito. Epuka kurudia rudia maneno.
  2. Hukufanya utafiti kuhusu maoni ya waganda kuhusu utawala uliopo. Wangapi wanampinga museveni? na kwa nini wanampinga? na in case wanampenda ni kwa nini?
  3. Sheria za nchi ya uganda zinasemaje kuhusu ukomo wa Rais? hapa namaanisha Katiba ya Nchi ya Uganda inasemaje kuhusu ukomo wa Rais? JE Museveni kubakia madarakani kwa karibia miaka 30 kumeisaidia vipi Uganda in term on internal political stability?
  4. KWenye Makala yako sijaona tatizo ni nini, je tatizo ni Museveni or mufumo wa Utawala wa Nchi ya Uganda? vipi kuhusu waganda wenyewe? je wananchi hawastahili kulaumiwa in whatever happening in Uganda? je wametimiza wajibu wao inavyotakiwa?
  5. Siasa nzuri hujenga uchumi mzuri and viceversa. uchambuzi wako haujasema chochote kuhusu uchumi wa Uganda unavyoathiri siasa ya Nchi husika. vipi kuhusu uasi wa LRA na issue ya Joseph Kony?
  6. Kumbuka ku-acknowledge source ya taarifa yako. kwani baadhi ya taarifa nyingi naona umezikopi mahala, (wikipedia) etc)
  7. vipi kuhusu Jumuia ya Africa Mashariki na siasa za Uganda? vipi kuhusu influence ya Rwanda na Tanzania?
After all, Keep up the good work.
(Urakoze, Thanks)
prof
 
Maswali mazuri kutoka kwa Prof. Huyu mchambuzi wetu akishindwa kuyajibu aseme tumsaidie. (Urakoze nawe)
 
Ulichoeleza no historia ya kisiasa na kiutawala. Uloyaeleza yote MTU anaweza kuyapata kwenye machapisho na vyanzo vingine vilivyopo tayari. Isitoshe imerudiarudia mambo. Kama ulifika Uganda kama ulivyodai simulizi yako ingejikita kwa uliyoyaona na si historia. Kwa sisi tunaoijua Uganda hakuna kipya kilichoelezwa na mengine hauko sahihi. Mfano, Museveni hakumpindua Obote. Wakati Museveni anaingia Kampala Obote alishafukuzwa na wenzake. Nchi ililkuwa chino Jenerali Tito Okello. Majeshi ya Tanzania hayakuivamia Uganda. Yalipigana vita kumuondoa katika eneo alilovamia Kagera. Aliposhindwa akakimbia na majeshi ya TZ yakamkimbiza mpska ndani ya Uganda mpaka akakimbia nchi.
Ok Asante kwa mawazo yako na maoni yako mkuu
 
Ok Asante kwa maoni yako na mawazo yako
Ulichoeleza no historia ya kisiasa na kiutawala. Uloyaeleza yote MTU anaweza kuyapata kwenye machapisho na vyanzo vingine vilivyopo tayari. Isitoshe imerudiarudia mambo. Kama ulifika Uganda kama ulivyodai simulizi yako ingejikita kwa uliyoyaona na si historia. Kwa sisi tunaoijua Uganda hakuna kipya kilichoelezwa na mengine hauko sahihi. Mfano, Museveni hakumpindua Obote. Wakati Museveni anaingia Kampala Obote alishafukuzwa na wenzake. Nchi ililkuwa chino Jenerali Tito Okello. Majeshi ya Tanzania hayakuivamia Uganda. Yalipigana vita kumuondoa katika eneo alilovamia Kagera. Aliposhindwa akakimbia na majeshi ya TZ yakamkimbiza mpska ndani ya Uganda mpaka akakimbia nchi.
 
Maswali mazuri kutoka kwa Prof. Huyu mchambuzi wetu akishindwa kuyajibu aseme tumsaidie. (Urakoze nawe)
Hii ni makala haina maana kuwa uchambuzi wangu ndio kila kitu pale ambapo kuna pengo ni bora mwenye uwezo na kuifahamu zaid kuongezea kwa faida yangu na wengine humu.

Hivyo ningependa yale ambayo mimi sikuyaelezea ni vyema kuyajazia mwingine.

Asante.
 
Back
Top Bottom