Kilango asema hana Ugomvi na Lowassa

Status
Not open for further replies.
mna kazi! sasa hivi watu wanaangalia kwa umakini kwani your next president ni EL..
Hata kama EL angekuwa hajajiuzulu uwaziri muu kwa skendo ya Richmond, ilikuwa, bado na itaendelea kuwa rahisi sana kwa ngamia kuingia kwenye tundu la sindano kuliko EL kuwa president wa nchi hii
 
Mh Kilango Malecela Anne, naona ameanza kukukosa washauri! wakati mwingine ukikaa kimya unaonekana na busara zaidi kuliko kuanza onyesha rangi yake kuelekea uchaguzi mkuu, mara anataka kumtoa mzee Ndesa Pesa leo tena yeye na Lowassa damu damu.....kwa sisi hatujui ndege wa rangi moja huwa pamoja! Kama anampenda Lowassa basi anapenda na Ufisadi wa Lowassa...mama pata ushauri wa Mzee Malecela kabla hujaenda low ki hivi
 
Mama Kilango naye awe anapima maneno anayoongea, anaropoka sana huyu mama yetu matamshi yake yanaweza kutafsiriwa vibaya na ikamharibia. Mambo ya kutokuwa na chuki ama kinyongo ayaweke moyoni mwake kuna haja gani ya kuyatamka hadharani unless anataka kujipendekeza kwa Lowassa! Na kwa nini awe na mawazo ya 'kuvamia' majimbo ya wengine wakati lake analo? Si awaache wanaowania kugombea kwenye majimbo hayo wao wenyewe ndio waseme ama wavalie njuga mapambano kwenye majimbo husika? Je ni background yake inafanya awe hivyo?

Unamwonea. Haropoki. Anasema anachoamini. Kwani jamani kila siku mtu aseme tunachopenda? Mama ana uhuru wa mawazo kulingana na imani ya chama chake cha siasa. Ana mipaka - CCM
 
kama ni kweli basi huyu mama anatakiwa akapimwe akili and i started getting the feeling that what Sofia Simba said holds water
Kigogo inakuwaje tena! mie sidhani kama AK ana sababu ya kuwa na chuki binafsi kwa Lowasa. Mie nadhani AK anaupigia kelele mfumo wa kifisadi uliopo uliopo Tz ambao lowasa yumo. Anataka mafisadi wafikishwe katika vyombo husika si kwa sababu anawachukia binafsi bali ni kwa sababu wamefanya matendo ya kifisadi na kuliingiza taifa katika umaskini. Kwa iyo kama ningekutana na AK akaniambia eti ana mchukia Lowasa sana nadhani nisingemuelewa kabisa angekuwa na matatizo binafsi.
Kwanza hii post imeandikwa kishabiki, amfagilia Lowasa! hajamfagilia kwa tendo lolote alilofanya Lowasa zaidi ya kusema hana ugomvi nae kitu ambacho ni obvious!


We do not see things as they are: we are see things as we are

NANYI MTAIFAHAMU HIYO KWELI NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU
 
Hata kama AK angetangaza anamchukia Lowasa na anatamani akose jimbo labda isingesaidia kwenye vita hii ya ufisadi. Ninakumbuka kauli moja ya TGNP inayosema "adui zetu sio wanaume bali mfumo dume". Utakapoanza kuwachukia wanaume kwa ajili ya mfumo dume ni hatari sana


We do not see things as they are: we we see things as we are

A woman can be strong, confident and sexy

NANYI MTAIFAHAMU HIYO KWELI NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU
 
Na Hamis Mkotya-Huyu Mwandishi hamjamshitukia tu siku zote hizi???? Mpaka mnaanzisha uzi ( thread) kwa ajili ya kile alichokiandika ! Chukua magazeti 30 ya mtanzania na utaelewa kwa nini kaandika hivyo na ataendelea tena na tena .Lakini hamna neno ndio uhuru wa vyombo vya habari huo !Ni haki yake.
 

Attachments

  • CAD1HJEI.jpg
    CAD1HJEI.jpg
    3.6 KB · Views: 40
  • lowasa.jpg
    lowasa.jpg
    2.8 KB · Views: 40
  • CAZ2XKL9.jpg
    CAZ2XKL9.jpg
    3.1 KB · Views: 37
  • Kilango.jpg
    Kilango.jpg
    3.2 KB · Views: 39
..kwa kweli matendo na kauli zake ktk wiki hii vimeidhalilisha ile Tuzo ya Mwanamama Jasiri aliyotunukiwa na Wamarekani.

..kama siyo MWOGA basi atakuwa ni MBABAISHAJI tu.
 
mna kazi! sasa hivi watu wanaangalia kwa umakini kwani your next president ni EL..

- Sawa sawa mkuu, hawa marafiki wawili somehow huwa tunau-underestimate urafiki wao, kuna something EL anakujua sisi wote hatukijui maana haiwezekani akafanya yote anayoyafanya bila woga tena wazi wazi, tufike mahali wa-Tanzania tukubali kwamba kuna something hatukijui EL anakijua je nini hicho?

- Maana habari on the ground ziko very loud and clear, kwamba he is coming yaani EL!

Respect.


FMEs!
 


1. Kilango amfagilia Lowassa


2. , alisema kwazi kuwa hana ugomvi wala kinyongo chochote na kiongozi huyo aliyewahi kuwa waziri mkuu.


- Hakuna mwenye kinyongo na Lowassa, isipokuwa wananchi wengi tuna kinyongo na matendo yake alipokuwa Waziri Mkuu kwa kuliletea taifa letu hasara kubwa.

- Eti kutokua na kinyongo na mtu as a person ni kumfagilia? This is lowest nimewahi kuona humu JF, tufike mahali tuwe kama tunavyoaminika na taifa I mean what a news au ndio ile ile tabia ya kuongelea tunaowapenda tu!

Respect.


FMEs!
 
Kuna msemo unaosema "Silence can never be misquoted". Mama Kilango kutokana na habari hiyo hapo juu hajamfagilia Lowasa per se ika maneno yake it leaves space for a lot of interpretation. Kama hana kinyongo nae alikua hana haja ya kusema hivyo.
 
FMES,

..Mama Kilango alipaswa kufafanua kwamba hana kinyongo na Lowassa, lakini ana kinyongo na matendo yake yaliyolitia taifa hasara kubwa.

..ingefaa sana Mama Kilango afafanue msimamo wake kuhusu suala hili, vinginevyo wananchi watakuwa na haki ya kuamini kwamba ameamua kujiunga na mafisadi.
 
FMES,

..Mama Kilango alipaswa kufafanua kwamba hana kinyongo na Lowassa, lakini ana kinyongo na matendo yake yaliyolitia taifa hasara kubwa.

..ingefaa sana Mama Kilango afafanue msimamo wake kuhusu suala hili, vinginevyo wananchi watakuwa na haki ya kuamini kwamba ameamua kujiunga na mafisadi.

- Swali lilipaswa kuwa baada ya yote ya ufisadi yaliyofanywa na Mbunge aliyewahi kuwa Waziri Mkuu Lowassa, akiwa kwenye madaraka je una kinyongo naye kama kiongozi mwenzio ndani ya CCM au huna? (Sasa katika kujibu swali Mama Kilango anatakwia kukumbuka kwamba Lowassa hajahukumiwa popote pale zaidi tu ya mahakama yetu ya wananchi.)

- Angejibu sina kinyongo naye then hii intepretation yako ingekua sawa sawa tena kwa 100%, otherwise naona ni yale yale tu ya JF na Mama Kilango, Malecela, Zitto, Freeman, na Kikwete hawa ndio the love of JF, au?


es!
 
FMES said:
- Swali lilipaswa kuwa baada ya yote ya ufisadi yaliyofanywa na Mbunge aliyewahi kuwa Waziri Mkuu Lowassa, akiwa kwenye madaraka je una kinyongo naye kama kiongozi mwenzio ndani ya CCM au huna? (Sasa katika kujibu swali Mama Kilango anatakwia kukumbuka kwamba Lowassa hajahukumiwa popote pale zaidi tu ya mahakama yetu ya wananchi.)

FMES,

..thank you very much.

..wote wawili, yaani muuliza swali[mwandishi], na muulizwa swali[kilango] kwa maoni yangu wana makosa.

..lakini kwa hali ilipofikia, ningetemea Mama Kilango afafanue kwamba hapendezwi na mwenendo wa Lowassa alioisababishia taifa hasara kubwa. kinyume chake labda yeye na Lowassa ni damu-damu.

NB:

..kwa upande mwingine ukiangalia hayo majibu ya Mama Kilango kwamba hajatoa hela kwa ajili ya jimbo la Lowassa, mara adai hata hajui Monduli iko wapi, mara kuna kampeni chafu etc etc. hivi huoni kwamba ina-sound kama vile Mama Kilango amekuwa "compromised"?
 


FMES,

..thank you very much.

..wote wawili, yaani muuliza swali[mwandishi], na muulizwa swali[kilango] kwa maoni yangu wana makosa.

- Hapana unless ni lazima tu umuhukumu Mama kilango maana sio siri ndilo hasa lengo lako, lakini kama ni fairness sielewi muulizwa swali anakuwaje na makosa sawa na muuliza, Mama kilango amesema hana kinyongo na Lowassa kama binadam akijbu swali aliloulizwa ambalo limesema Lowassa halikusema anything else,

- Katika siasa siku zote hujibu swali usiloulizwa unajibu uliloulizwa tu, kwa hiyo anyways uamuzi ni wako maana naona ni lazima Mama Kilango awe na makosa tu ndiyo itakupa raha, lakini mwenye akili akisoma hapa ataweza kuchambua pumba na mchelle ulipo!


..lakini kwa hali ilipofikia, ningetemea Mama Kilango afafanue kwamba hapendezwi na mwenendo wa Lowassa alioisababishia taifa hasara kubwa. kinyume chake labda yeye na Lowassa ni damu-damu.

- Nafikiri nimesema tayari katika siasa hujibu swali ambalo hujaulizwa, na muandishi anazo akili za kujua kwamba Lowassa hajahukumiwa kwenye sheria yoyote Tanzania, ndio maana asingeweza kuuuliza swali linalotakiwa. Hayo mengine ni speculations tu zisizo na facts ambazo JF siku hizi tunaanza kuwa very good at!

NB:

..kwa upande mwingine ukiangalia hayo majibu ya Mama Kilango kwamba hajatoa hela kwa ajili ya jimbo la Lowassa, mara adai hata hajui Monduli iko wapi, mara kuna kampeni chafu etc etc. hivi huoni kwamba ina-sound kama vile Mama Kilango amekuwa "compromised"?

- Ninaamini kwamba mawazo yako ndio yako very compromised maana unalazimisha kwa nguvu hpoja zisizokuwepo, Mama kasema hajawahi kufika Monduli wala hajui iko wapi na wala hakushiriki kwenye shughuli yoyote huko, sasa unasema ksuema hivi ni kuwa compromised wa Lowassa? Sasa huoni kwamba JF tunaanza kuwa very good at speculations bila hata facts wala evidence!

- Otherwise, Mama Kilango my best friend she is doing just fine, sasa hivi anatafuta kumalizia kiwanda cha kusindika Tangawizi anachokijenga huko jimboni kwake na ni majuzi tu Rais amekifanyia fundraising kubwa sana, kwa hiyo wananchi wanapatiwa exactly walichoahidiwa, unajua kipimo cha kujua mafanikio ya anything unachokifanya kwenye maisha, angalia elimu ya maadui zako wakiwa wengi na bila hoja wala facts, basi ina maana uko juu sana!

es!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom