Kilaini: Kikwete bado ni chaguo la Mungu

"Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu. Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme" (1Samweli 15:22-23)
 
MWALIMUU? ......Mimi naitikia AMINA! kwa sababu umemaliza yote. Mwenye sikio asikie.

Amina mkuu!

Mwenyezi Mungu alipowaweka watu wake kuwa wafalme haikuwa ni lifetime guarantee...walipoenda kinyume na maagizo yake aliwaondoa!!
 
Mungu anasema juu ya Wana wa Israel " Wamesimamisha wafalme, lakini si kwa shauri langu; wamejifanyia wakuu, lakini nalikuwa sina habari". ......Hivyo si kila aliyechaguliwa na wengi ni chaguo la Mungu.

Ungekuwa karibu ningukushika mkono, hivi mbona hawa viongozi wa dini wanaanza kupotoka na kuwa washabiki wa siasa??? Hawa ndio wale wachunga vipofu wanaowaongoza kondoo kuelekea shimoni. Je, Kilaini angefanya homework kidogo tu asingegundua mistari hii michache ambayo ingemfanya achelee kusema aliyoyasema?

Nimeanza kupata shaka naye, huenda nae ni kibaraka. Namuasa tu kwamba kama madhabauni panamshinda, na aache aje kwenye siasa tujue moja, sio anakuwa mdhabauni na kutoa kauli hafifu zinazochefua! Nilitegemea kauli zitokazo katika madhabahu zisiwe na walakini, lakini kwa kauli hii ya kilaini, nadhani anaidhalilisha madhabahu ya Mungu aliye hai! Akawaulize manabii wa baali na Dagoni lilichowapata pale walipofanya mzaha na Mungu aliye hai.

Hivi huyu kilaini anafanya mchezo sio? Kwa wale wananchi wanaokufa kwa kukosa huduma za afya, barabar, maji safi na salama, maisha magumu kutokana na mfumuko wa kutisha wa bei unaosababishwa na mfumo na serikali mbovu ya huyu anayemwita '...chaguo la Mungu...' anapeleka ujumbe gani? Hivi ni kwakuwa yeye yupo Dar es salaam, chakula cha kifahari, malazi ya kifahari, huduma za afya hadi nje ya nchi (india for example..) ndio maana anapata ulevi huu wa kuzungumza kivyepesi vyepesi tu kuwa anapendwa na watu????

Tukubaliane ukweli, hata kama serikali ni mbovu na kiongozi ni mbovu kupindukia, kuna watu ambao watang'ang'ania kiongozi huyo aendelee kuwepo kwa sababu tu yeye naye ananufaika, kiondozi akiondoka si na yeye mnufaiko unatoweka? Watu wa namna hii ni wabinafsi, HAWATUFAI! Labda atuambie anaposema chaguo la Mungu, ana maanisha Mungu yupi?

Haya mambo bwana yananishangaza, kuniudhi na kunifadhaisha kweli kweli..!
 
Wakuu zangu,
Maneno ya Askofu huyu yasichukuliwe kimzaha kabia. Kuna ukweli mwingi kuliko kufikiria vitu hivi kwa haraka pasipo kupima maneno ya Askofu.
Nilichomwelewa mimi Askofu kaelezea matatizo yaliyopo ktk Uongozi wa Kikwete na hakika ukisoma kwa makini utagundua kwamba Mambo yote haya yanatokana na UDHAIFU wa kiongozi huyu ktk utendaji kazi wake pamoja na kwamba alikuwa na malengo mazuri.

Tusijidanganye kabisa kwamba Kikwete hapendwi, bado wapo wengi wanampenda kwa ile nia yake nzuri kama wanavyosema wao na lawama hizi ziwafikie wale walioshindwa pamoja na kwamba JK kashindwa kuwachukulia hatua. Hisia hizi zipo kwa Watzanania wengi sanma kama vile wanavyoshindwa kukihukumu chama kizima cha CCM kwa Ufisadi na kushindwa kuongoza isipokuwa tuwashutumu baadhi ya viongozi wenye mapungufu hata kama chama kimeshindwa kuwachukulia hatua.

Bado CCM ni chaguo la wengi hivyo kuna ukweli mkubwa kwamba bado Kikwete ni chaguo la wengi..Hivyo maadam watu wamechagua hivyo basi bila shaka ni chaguo la Mungu. Huyu ni nchungaji mlitaka atumie kitabu gani au lugha gani zaidi?.. By the way hata mimi naamini - Nothing happens ,but by the power of the grace of God..

Mkandara, kwa heshima na unyenyekevu mkubwa sana naomba nitofautiane na wewe pamoja na Mhashamu Askofu Kilaini. JK alikataliwa na Baba wa Taifa 1995 pamoja na kwamba alikuwa anapendwa na watu. Mimi ni mmoja wa wale tuliodhani Mwalimu Nyerere alimuonea. Lakini leo hii nakubaliana kabisa na maoni ya Baba wa Taifa kwamba JK alikuwa hafai kuwa Rais wa Tanzania. Mwaka 2005 chini ya wanamtandao na kwa kupenyeza rupia (hongo) zilizotokana na kampuni feki ya Kagoda etc wakaiba BOT na kuzitumia fedha hizo kwenye kampeni akapata ushindi wa Tsunami. Wananchi masikini wakaimbishwa wimbo mpya wa "Ari mpya, Kasi mpya na Nguvu mpya". Haikuchukua mwaka mambo yakagonga mwamba. Leo hii wimbo huo umekufa kifo cha mende na hata yeye mwenyewe hautaki kabisa. Anachoweza ni kufanya ni kusafiri nje kila mwezi au kuwa mtu wa mipasho kama alivyoonyesha pale Diamond Jubilee alipokuwa akimnanga Mgaya wa TUCTA mbele ya wazee wa DSM.

Je Baba Askofu akiwa na Mapadre ambao hawatimizi wajibu wao kwa kanisa ataendelea nao au atawatimua katika jimbo/diocese yake? Kama mawaziri na watendaji wengine ni wabovu JK anapaswa kuwafukuza na sio kuwachekea. Vinginevyo na yeye pia ni mbovu.
 
Mnaweza kusema yooote mabaya kuhusu huyu mchungaji lakini dini zetu sote zinasema matokeo ya kila kilichopo kimewezeshwa na Mungu. Hata hao waliosema kuhusu Saadam Hussein, Hitler, Pharaoh na viongozi wote wabaya wametokea kwa kuwezeshwa na Mungu ambaye pasipo kuwepo kwa watu kama hawa tusingekuwa na Historia zao au ya dunia iliyokuwa na mitihani..

Hivi kweli tungemzungumzia vipi Moses na maajabu yake pasipo Pharaoh Ramsi 11 (the second), Yesu na majaribio yoote yale ya kina Yuda, Peter,Saul, Pilato, Maria Magdalena, maswahaba wake (wanafunzi) na wengineo pasipo Mungu kuwachagua watu wao kuwa mtihani kwake..

Hivi ndivyo nilivyomwelewa Mchungaji, JK ni mtihani kwetu, mtihani ambao sisi tunatakiwa kupambana nao na kuiweka historia sawa kwani ujio wake umetufundisha mengi sana kuhusiana na Uongozi mbovu. Hatujawa na mtihani kama huu na Mchungaji katueleza wazi kwa nini Kikwete anapendwa na wananchi...

Tatizo letu hatupendi kuamini wala kusikia sababu za kupendwa kwa Kikwete lakini ukweli utabakia kuwa zipo sababu.

Hata huyo Hitler alikuwa na wafuasi na wapenzi wake ambao walikuwa na sababu za kumfuata na kumpenda. Hivyo mtu akikubaliana na sababu hizo, kisha ukaziandika au akahutubia haimfanyi mtu huyo kuwa kichaa au mwendawazimu. Kama mchungaji, imani yake inampekelekea kusema yote haya -YAMEANDIKWA..Hivyo basi ni jukumu letu kujifunza kutokana na hayo.

Hapo nyuma niliwahi kumsoma Rev.Kishoka kjtk mada yenye maneno kama haya, kwanza sikumuelewa kabisa kisha nilikuja kuipata picha kamili alikuwa analenga kitu gani...Leo hii namsoma tena Mzee Mwanakijiji akizungumzia sababu za kumpenda Kikwete..Unatakiwa kuwa makini unaposoma...

Laa sivyo Inaudhi sana kuzisoma lakini ukweli ni kwamba wapo watu wanamkubali sana Kikwete pamoja na mapungufu yote hayo - Being Great for not doing anything!
 
Jamani hebu tuache kumsingizia Mwenyezi Mungu kwa kila tunachofanya...
 
Wanadamu wanapoamua kujitenga na Mungu nae hukaa mbali nao. Si kweli hata kiogo kuwa kila maamuzi yanayofanywa na wanadamu basi yana baraka za Mungu! Mnapofanya jambo lolote bila kumuhusisha yeye kwanza basi atakaa pembeni wala hatatia mkono wake hapo.

Kauli kama hizi za "Chague la Mungu" zinatumiwa vibaya sana na watawala wetu kuhalalisha utawala wao.
 
Naaminii Askofu kilaini ametoa mawazo yake kulingana na utashi wake wa kibinadamu. dhamana yake ya uchungaji inampa nafasii ya kukubalika na kueleweka zaidii kwa jamii.

yeye kusema kikwete ni chaguo la mungu ila amekosaa usaidizii bora kutokana na wale aliowachaguaa..Yesu kwenye maandiko hakulaumu wasaidizi wake wale wanadamu kwa makosa yao bali alijitoa yeye mwenyewe kwa ajili ya dhambi zetu ili kuufanyaa ukiristoo mioyoni wa watu. Kitendo cha ASKOFU kilaini kulaumu mawazirii anakiuka maandiko yasemayoo toa kibanzi katika jichoo lako na sio boriti kwenye jicho la wengine.

Naamini askofu anatambua nguvu kubwa aliyo nayo mh raisi kikatiba na ndio maana anatarajiwaa kufanya teuzi bora kwa kujiridhisha kupitia taasisi za umaa (usalama nk).

Leo hii tuna mawaziri wenye kashfa za kufoji vyeti ila bado mh raisi amewakumbatia na kuwa kimyaa?? je hawa wanamwangusha au yeye anajiangushaa?

Kuna mawazirii walionyeshaa uwezoo mdogoo kwenye utendaji ila bado wapo na utafitii hauhitajiki kuwatambua!! kuna walionyeshaa uwezo mkubwa katika kusimamia utekelezaji wa majukumu yao ila hawapewi nafasii stahilii ya kutenda maeneo muhimuu kwa wakatii uliopooo...
 
Kwa taratibu za kanisa katoliki kama aliamishwa DSM kwa sababu ya kuongelea sana siasa kuliko kuwarudisha wakatoliki kwenye mstari wa kwenda mbinguni basi kinachotakiwa kufuata ni kumpeleka Roma akamsaidie Papa kazi za pale Vatican. Ni ngumu kusema kuwa Askofu Kilaini ameongea nje ya uaskofu wake. Nafikiri amesahau utii na amekosa adabu kufuatana na kiapo alichotoa.

Hawa maaskofu wengine wana shida, kwani kule Same askofu kaiba sadaka na kujenga majumba yake binafsi na kufanya starehe na wengine wanakufa njaa mpaka tuliombwa kanisani tutoe michango kwa ajili ya jimbo lile!

Ndio maana huko Anglikana na kwa waluteri wanawashana makonde tu!
 
Nadhani hapa ameongea kama Kilaini na si kiongozi wa dini

Huenda uko shahihi Masa lakini inabidi tuelezwe ili tusiassume. Inakera kweli yaani huyu askofu anataka kutuambia kuwa Mungu anawachukia watanzania na kuichukia Tanzania kiasi hiki kweli jamani? Unajuwa vitu vingine vinatia uchungu sana. Hivi ile sifa s'where in the bible kwamba askofu asiwe mtu wa kutumia mvinyo mwingi bado inafuatwa siku hizi? I doubt.
 
Wanadamu wanapoamua kujitenga na Mungu nae hukaa mbali nao. Si kweli hata kiogo kuwa kila maamuzi yanayofanywa na wanadamu basi yana baraka za Mungu! Mnapofanya jambo lolote bila kumuhusisha yeye kwanza basi atakaa pembeni wala hatatia mkono wake hapo.
Kauli kama hizi za "Chague la Mungu" zinatumiwa vibaya sana na watawala wetu kuhalalisha utawala wao.
Maneno haya mawili -Chaguo la Mungu na Baraka za Mungu yana maana mbili tofauti kabisa. Kikwete kama rais aliyechaguliwa na wananchi, anaweza kuwa chaguo la Mungu (kuteuliwa) ili kutupa mtihani huu lakini haina maana Kikwete ana Baraka za Mungu..Chaguo means - chosen among us to be who he is!

Hata katika Matendo mabaya yapo chaguo la Mungu kwa mfano mabalaa. majuzi kulitokea ajali ya ndege walikufa abiria wote akapona mtoto mmoja tu. Naweza kusema waliokufa ni chaguo la Mungu (wafe) na yule alopona ni chaguo la Mungu (apone). Hizi ni lugha za waumini kama huna imani ya dini unaweza kusema - Hakuna Mungu, kama yupo kwa nini asiwaokoe wote.. Hii pia inaweza kuwa na ukweli kwa wasioamini Mungu.
 
You might be right on this lakini kumbuka kuwa kauli hizi zilianza kutolewa hata kabla hajachaguliwa kuwa Rais....
 
You might be right on this lakini kumbuka kuwa kauli hizi zilianza kutolewa hata kabla hajachaguliwa kuwa Rais....
Ni kweli kabisa ila kilichotakiwa sisi ilikuwa kuelewa kwamba
1. Wapo watu waliochaguliwa na Mungu kuwa Mtihani kwetu..
2. Wapo watu waliochaguliwa na Mungu kutuongoa.
Ni muhimu sana kuelewa kwamba Kuchaguliwa kwa mtu haina maana ya Kubarikiwa..Wengi tunafanya makosa haya kwa sababu tumesoma vitabu vya dini au mafundisho ya mitume waliobarikiwa kuwa ni chaguo la Mungu. Haiwezekani kuwa kinyume, kumbe hata wale waliotujaribu imani zetu nao pia walichaguliwa lakini hawakubarikiwa na Mungu ila shetani.
 
Wakuu zangu,
Maneno ya Askofu huyu yasichukuliwe kimzaha kabia. Kuna ukweli mwingi kuliko kufikiria vitu hivi kwa haraka pasipo kupima maneno ya Askofu.
Nilichomwelewa mimi Askofu kaelezea matatizo yaliyopo ktk Uongozi wa Kikwete na hakika ukisoma kwa makini utagundua kwamba Mambo yote haya yanatokana na UDHAIFU wa kiongozi huyu ktk utendaji kazi wake pamoja na kwamba alikuwa na malengo mazuri.

Tusijidanganye kabisa kwamba Kikwete hapendwi, bado wapo wengi wanampenda kwa ile nia yake nzuri kama wanavyosema wao na lawama hizi ziwafikie wale walioshindwa pamoja na kwamba JK kashindwa kuwachukulia hatua. Hisia hizi zipo kwa Watzanania wengi sanma kama vile wanavyoshindwa kukihukumu chama kizima cha CCM kwa Ufisadi na kushindwa kuongoza isipokuwa tuwashutumu baadhi ya viongozi wenye mapungufu hata kama chama kimeshindwa kuwachukulia hatua.

Bado CCM ni chaguo la wengi hivyo kuna ukweli mkubwa kwamba bado Kikwete ni chaguo la wengi..Hivyo maadam watu wamechagua hivyo basi bila shaka ni chaguo la Mungu. Huyu ni nchungaji mlitaka atumie kitabu gani au lugha gani zaidi?.. By the way hata mimi naamini - Nothing happens ,but by the power of the grace of God..
Nadhani kusema chaguo la Mungu kwa maana ya 'sauti ya wengi, sauti ya Mungu' hakuna tatizo kama kweli watu wengi kweli walifanya hivyo. Lakini ni upuuzi kama leo baada ya kuona kwamba watu walichagua vibaya na kujutia walichofanya tunarudia tena kusema ni chaguo la Mungu. Kama tumekoso la kusema bora 'tunanyamaze wengine wasitujue kuwa tu wapumbavu, kuliko kusema hivyo na tukadhihirisha upumbavu wetu'.

Kama leo bado tunaweza kusema 'ni chaguo la Mungu' pamoja na maanguko yote hayo je, tutasemaje kama angukuwa kafanya walau machache?
 
Ni kweli kabisa ila kilichotakiwa sisi ilikuwa kuelewa kwamba
1. Wapo watu waliochaguliwa na Mungu kuwa Mtihani kwetu..
2. Wapo watu waliochaguliwa na Mungu kutuongoa.
Ni muhimu sana kuelewa kwamba Kuchaguliwa kwa mtu haina maana ya Kubarikiwa..Wengi tunafanya makosa haya kwa sababu tumesoma vitabu vya dini au mafundisho ya mitume waliobarikiwa kuwa ni chaguo la Mungu. Haiwezekani kuwa kinyume, kumbe hata wale waliotujaribu imani zetu nao pia walichaguliwa lakini hawakubarikiwa na Mungu ila shetani.
Mkuu huku kwetu kauli za namna hii zinatumika vibaya, watu wanatumia kauli kama hizi kujipigia debe! Unapotoa kauli kama hizi wakati tunaelekea kwenye uchaguzi unategemea bibi yangu wa kule Tukuyu ataielewa vipi?
 
Kuna msemo unaosema sauti ya wengi ni sauti ya Mungu. Kama huo msemo ni kweli basi kila kiongozi aliye chaguliwa kidemokrasia na wengi ni chaguo la Mungu. Vote 2010.

Huyu Mungu tutambebesha na mizigo isiyo haki..Kwani mungu ndio alitoa amri wakatoe rushwa ya kanga ,Sukari ba baiskeli ???
Kikwete yuko hapo kwa vile tu watanzania wengi hatujawa na Mwamko Kisiasa
 
Gurtu,

Mkuu bado unachanganya Chaguo la Mungu na Baraka za Mungu. Matendo ya Kikwete yanaweza kutokuwa yamebarikiwa na Mungu lakini haiondoi ukweli kwamba ndiye rais wetu.Haikuwa bahati nasibu au chaguo la shetani kuwa rais wetu. Kiimani Mungu alimwezesha kupata nafasi hiyo kupitia kwako wewe na wengine waliomchagua..

Sasa Matendo ya Kikwete ndiyo yatamhukumu yeye aidha yenye baraka za Mungu alipofanya mazuri na ya kheri au baraka za Shetani pale alipofanya mabaya na ya shari.

Hata wewe ni Chaguo la Mungu kuwepo duniani na mtihani kwa wengine au mwokozi wao ktk nafasi ulizopo, pamoja na kwamba sijui mafanikio yako kama ni plus au zero. Ni matendo yako tu ndio yatakuhukumu wewe, sii kukataa uwezo wa Mungu kutuchagua sisi ktk nafasi za majaribio..
 
Nafikiri alikuwa anaongea kwa binafsi yake, hakuliongelea kanisa la katoliki.

Kikwete angekuwa mtu safi angeng'angania kwenye usafi. asinge waachia wale walioiba hela za maskini wa tz za EPA, mwizi wa epa anakuja kulipa hela aliyoiba halafu anaruhusiwa kwenda home kukaa na familia yake raha mstarehe, wakati yule aliyeiba simu ya mkononi amechomwa moto na wananchi polisi wakimuona bila kumwokoa. Kuna watu rundo zima wamekaa lokapu miaka kama minne hata kesi zao hazijasikilizwa kwa makosa ya kubambikizwa tu, ila inapokuja mtu amekamatika kaiba kabisa na vizibiti tunavyo akaambiwa arudishe halafu atasamehewa labda kwasababu yeye wizi wake ulikuwa wa kitajiri, hiyo hakuna usawa.

Pia hauwezi kusema kuwa anaangushwa na mawaziri, yeye ndo ameshika rungu anaweza kumbonda waziri yeyote akitaka, angalia lowasa pamoja na kwamba ana kashfa, lakini angeweza kujifunza uchapa kazi wake kama mfano tu akayaacha yale ya kashfa zake,....ukiwa na rungu unayo responsibility kulitumia, kama haulitumii unatakiwa kuachia ngazi watu wenye uwezo wa kuwaadibisha hao mawaziri etc waingie kazini.

Sisi kama watz tumempa dhamana ya uongozi, anatakiwa kuutumia ipasavyo kama dhamana ya watz na si dhamana ya chama kimoja au familia yake....
 
Mkuu huku kwetu kauli za namna hii zinatumika vibaya, watu wanatumia kauli kama hizi kujipigia debe! Unapotoa kauli kama hizi wakati tunaelekea kwenye uchaguzi unategemea bibi yangu wa kule Tukuyu ataielewa vipi?

Bibi wa Tukuyu atahimiza na wajukuu wote kumpigia kura kwa vile ni chagua saafi kutoka kwa mwenyezi mungu.imefika wakati tufunge na kuomba ufunuo kutoka kwa mwenyezi mungu.
haya mambo ya kubebana hayafai tena ndio maana tunaipeleka nchi kusikoeleweka
 
Back
Top Bottom