Kila wanapotaja maneno kupima viwanja moyo wangu unaenda mbio.

hengo

JF-Expert Member
Jun 6, 2011
402
50
Jamani leo ni bajeti ya Wizara ya aridhi, nyumba na maendeleo ya makazi,nimekaa kusikiliza michango ya waheshimiwa mbalimbali juu ya bajeti hii,wengi wao wanaisisitizia serikali kupima viwanja.
Kwa keli mimi mwezenu kila wakitaja Kupima viwanja moyo uanenda mbio maana wazee wangu ,ukianzia babu na bibi kisha baba na mama wanaishi kwenye viwanja ambavyo havijapimwa, tangu walipokusanywa enzi za miaka ya 1970`s enzi za vijiji vya ujamaa hadi leo hawana hati viwanja ya hivyo.Kama serikali itakuwa sikivu na kuamua kupima viwanja itakuwaje?nahofia bomoabomoa na ukizingatia wamezeeka wote nitawapeleka wapi?.

Lakini pia nami nina kakiwanja kangu sehemu nako haka hati,maana viwanja vilivyo pimwa hasa mijini vinauzwa bei juu.Sasa napo nikipokonywa nitakuwa mgeni wa nani?
 
Ok haupaswi kuwa na wasi wasi hata kidogo, kwa ababu zoezi la upimaji kwa ujumla wake ni zuri sana, kwa sababu mara nyingi wanavyopima wanabariki eneo lako ili hata kupata hati iwe rahisi kwa sababu kama ni DAR ni asilimia 30 tu ndio viwanja vimepimwa, sasa unafikiri 70% wa nyumba dar zibomolewe itakuwaje, na ndio maana kama umefuatilia sehemu iliyobomolewa maeneo ya Mbezi beach ni maeneo ya ufukwe ambapo watu wa mazingira ndio wamesimamia zoezi la uvunjaji na sio ardhi. Viwanja ambavyo havijapimwa si rahisi kuvunjwa kwa sababu hakuna anayejua matumizi yake ila vilivyopimwa ndio rahisi kwa sababu wanaangalia mchero wanakwambia hii ni eneo la wazi.
 
Usiwe na wasiwasi kwani wakija kupima viwanja vilivyopatikana unaulizwa kama unaweza kulipia au lah,ila ukisikia wanakuja fanya hv jenga vibanda kwenye kila robo heka ya viwanja vyenu basi hapo watakulipa then utapata viwanja vyote hvyo cha msingi uwe na hela ya kuvilipia gharama ya upimaji ambayo haizidi laki2 kila kiwanja
 
Zoezi la upimaji wa viwanja ni nzuri hata kama kuna kajieneo lako litachukuliwa kwa sababu ya huduma. lakini mara nyingi walio na maeneo madogo wanaachiwa maeneo yao na wao kuchangia gharama kidogo ya upimaji. Usiogope mkuu.
 
mkuu si uwapimie sasa hivi,nadhani ukienda serikali ya mitaaa uwaambie umepoteza hati watakuambia upeleke majirani unaoishi nao kama mashahidi,utapewa hati then utaenda kupima upewe hati sina uhakika lakini....
 
Asantini wote kwa kunishuri vizuri na kunitoa wasiwasa
 
Back
Top Bottom