Kila siku broken English

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,288
Lakini sijawahi kusikia tukibezana kwa broken Kiswahili.
Wazungu wanaharibu sana lugha yetu, kuonesha double standards tunawachekea tu.
 
Labda kwa sababu tofauti na sisi, wao hawakihitaji Kiswahili kwa ajili ya kutafuta degree au ajira!
 
Kwa sababu lugha yetu tunayoitumia ni Kiswahili, hakuna haja ya kujilazimisha kuongea Kiingereza wakati lugha hii ni tatizo kwako. Watu wengi hudhani kuongea kiingereza ni kielelezo cha ustaarabu (civilisation) na usomi - hii si kweli. Wazungu wakija hapa kwetu wanalazimika kuongea Kiswahili, japo wanachapia lakini hawana budi kukiongea sababu ndiyo lugha ya mawasiliano hapa kwetu. Sasa wewe mtanzania kwa nini ung'ang'anie kuongea Kiingereza broken hapa kwetu uswahilini?Ongea Kiingereza unapolazimika tu na katika mazingira yanayokihitaji, vinginevyo kama unalazimisha kuongea wakati hujui na hakuna ulazima lazima tukwambie tu kwamba unaongea broken English!
 
Labda kwa sababu tofauti na sisi, wao hawakihitaji Kiswahili kwa ajili ya kutafuta degree au ajira!

Lakini hata watu ambao wana matumizi ya Kiingereza sawa na sis mf. India, Pakistan na Nigeria huwa wanakosea sana, na wanajivunia namna wanavyozungumza.
Sisi ni mabingwa wa kufoji matamshi, huwezi kujua kama hiki ndio Kiingereza cha Tanganyika.
 
tufanyeje sasa Kingereza tukitupilie mbali au tuendelee nacho hivyohivyo hata kama ni Broken ilimradi anayeongea anaeleweka????????
 
baada ya miaka kama 50 hivi lugaha nyingi za makabila ya hapa tz zitakuwa zimepoteza mwelekeo kutokana na kiswahaili kuzimeza. baada ya miaka kama 100 hivi dunia itazidi kuwa kama kijiji na hivi ni lugha chache tu zitatumika kuwasliana. baadhi ya lugha zitapoteza umaarufu. sijui kiswahili kitakuwa na nafasi gani. kuna lugha amabazo zinajinyumbua na kushindana kuwa lugha ya dunia na kiingereza ni moja ya lugha hizo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom