Kila ninayeongea nae anamlaumu kikwete. Hao asilimia 61 waliompigia kura wapo wapi?

Kingcobra

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,000
309
Jamani,
Huu siyo utani. Ninamaanisha nachosema. Yaani kila ninayeongea nae iwe ofisini, kwenye daladala na maeneo ya mapumziko, anamlaumu sana kikwete kwa jinsi anavyoongoza nchi. Wengi wanalalamika hali ya maisha kuendelea kuwa ngumu. Wengine wamefikia hata hatua ya kusema bora sikumpigia kura yangu. Sasa ninachojiuliza hivi hao wananchi asilimia 61 waliompigia kura mbona siwaoni kwa utafiti wangu mdogo tu??? Labda REDET waendeshe kura yao ya maoni wathibitishe hiki nachoongea.
 
Walimpigia lakini sasa wanajilaumu na kuigiza kuwa hawakumpigia.
 
Jamani,
Huu siyo utani. Ninamaanisha nachosema. Yaani kila ninayeongea nae iwe ofisini, kwenye daladala na maeneo ya mapumziko, anamlaumu sana kikwete kwa jinsi anavyoongoza nchi. Wengi wanalalamika hali ya maisha kuendelea kuwa ngumu. Wengine wamefikia hata hatua ya kusema bora sikumpigia kura yangu. Sasa ninachojiuliza hivi hao wananchi asilimia 61 waliompigia kura mbona siwaoni kwa utafiti wangu mdogo tu??? Labda REDET waendeshe kura yao ya maoni wathibitishe hiki nachoongea.
We msimamo wako vipi, unamwonaje mkulu? Nchi anaiwezea ee!!
 
Alipata kura za wanakijiji ambao wanaamini wamezaliwa kuwa maskini milele. Hao hawajui jinsi nchi ilivyo tajiri na kwamba utajiri wote unaporwa na mafisadi wanaolindwa na Chama Cha Majambazi.
 
Alipata kura za wanakijiji ambao wanaamini wamezaliwa kuwa maskini milele. Hao hawajui jinsi nchi ilivyo tajiri na kwamba utajiri wote unaporwa na mafisadi wanaolindwa na Chama Cha Majambazi.

Sikumpa kura yangu . mungu anisamehe mara 70.
 
ni wale akili mgando ambao bado wanavaa sare za watumwa mitaani...
 
Kati ya makosa ambayo daima tunayafanya ni generalization kama hii:

"... Alipata kura za wanakijiji ambao wanaamini wamezaliwa kuwa maskini milele. Hao hawajui jinsi nchi ilivyo tajiri na kwamba utajiri wote unaporwa na mafisadi wanaolindwa na Chama Cha Majambazi.".

Usidhani wanakijiji ni wajinga na "wa mjini" ndio mwenye akili au werevu. Kwa taarifa, ukombozi wa kweli wa nchi inaonekana utaanzia vijijini wala sio mijini sembuse Dar es Salaam. Si wajinga wale, ni suala la mobilization tu; mama na baba zetu kule vijijini wana akili za ajabu kuliko hata wasomi wetu mahiri wanaotetea ufisadi.

Mwenyekiti Mao TseTung alianzia harakati zake vijijini na China ndio kama inavyoonekana hivi leo. Hima, twende vijijini tukaibue vipaji vya ajabu vilivyolala huko.

Ni kwa mtazamo wakati mwingine tunakosea kwa kutoa majibu ya kijumla kwa mtazamo wa kikabila, kidini, kikanda, n.k. Haiwezekani watu wote kwenye kundi fulani wakawa wajinga. Tuchunge kauli zetu.
 
hao ni Usalama wa Taifa,mbwa wa serikali,wanauliza ili wapate data,even wewe waweza kuwa UT
 
Sijui mimi sijui,
Waliompigia wakina nani, hata sijui,
kama ni UWT sijui, au ni Kiravu na Makame, sijui
kijijini au mjini, sijui,
sijui mimi sijui!:coffee:
 
Kwa hiyo unataka kusema hao uliouliza ndiyo takwimu sahihi hali ya uchumi ndugu yangu ni duniani kote hushangai mvua hazinyeshi Kama unakumbuka Dar haikuwa kame kiasi hiki pengine nayo tuse na huo
 
ni wale akili mgando ambao bado wanavaa sare za watumwa mitaani...
Hayo ni matusi maana Kama sare watu wote wanava sare ila inatofaitiana ubora wa sare yenyewe sare zingine zinapendeza sare zingine zinatisha.
Kwa hiyo msione wivu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom