Kila Mwana CCM mwenye akili timamu anajua Kikwete ataighalimu CCM kufikia 2015

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
Ansbert Ngurumo

NILIWAHI kutoa ushauri huu. Na sasa narudi kusisitiza, kwamba Rais Jakaya Kikwete asigombee tena urais mwaka huu. Aandike historia.

Miaka mitano inamtosha. Nilisema, na nasisitiza sasa, kuwa hata Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, aliongoza kwa kipindi kimoja tu. Na anaendelea kuheshimika kuliko marais wengi wanaong’angania madaraka kwa kisingizio cha ‘kumalizia ngwe’ au ‘kukamilisha kazi’ waliyoianza.

Nina hakika Rais Kikwete mwenyewe, kama yu makini, anajua alishashindwa, na anatambua kuwa upepo wake kisiasa unavuma kuelekea asikotaka. Kiashiria cha kwanza ni umaarufu wake ambao umeshuka sana katika miaka minne iliyopita.

Lakini hata vituko vya kisiasa vinavyoambatana na urais wake, vyaweza kuwa onyo kubwa kwake, kama anaamini katika maonyo.

Baadhi yetu, tusingependa aanguke tena hadharani, au arushiwe jiwe, au apate ajali ya gari akiwa rais wa nchi. Kama matukio haya na mengine yanatokana na nguvu ya Mungu, au mapenzi ya watu kwa kiongozi wao, au uzembe wa wasaidizi wake, au hujuma za kisiasa; ni jambo jingine, lakini si viashiria vizuri kwa kiongozi wa nchi.

Na kwa matukio ya aina hii, rais ameandika historia ya pekee. Hatukutarajia rais aliyepachikwa jina la ‘chaguo la Mungu’ afikishwe katika mazingira dhalili na yenye kutia hofu kama haya, tena kutoka kwa watu wake mwenyewe.

Hata baada ya utafiti wa REDET kumpa matumaini, mwitiko wa wananchi haukuwa mzuri. Na bado hesabu za kisiasa zinaonyesha kuwa Kikwete aliyeingia madarakani kwa umaarufu wa asilimia 80 ya kura zilizopigwa, amepoteza nyingi hapa katikati. Hata akilazimisha, na akabahatika kushinda, zitakuwa pungufu.

Hivyo, kama anataka kutunza heshima na umaarufu wake, bora aachie hapa hapa, ili abaki na rekodi na kumbukumbu ya asilimia 80.

Kama atang’ang’ania kugombea, atazidi kuporomosha asilimia ya kura zake na umaarufu wake na wa chama chake; na hivyo kukipa wakati mgumu kitakapokuwa kinatafuta mrithi wake mwaka 2015.

Kwa hiyo, kama pia anakijali chama chake, ni vema akang’atuka kabla hakijapoteza hata kile kidogo kilichobaki. Na wanachama wenzake kama wanakijali chama chao, wawe na ujasiri wa kumweleza ukweli huu, waanze sasa kujijenga upya.

Wakiendekeza unafiki wa kisiasa wa kujikomba kwa viongozi wao, yatawakuta yale yaliyokikuta chama cha Labour Uingereza mwanzoni mwa mwezi huu. Kiongozi wao, Gordon Brown, alishaonywa huko nyuma, na tafiti zilishaonyesha kwamba yeye ndiye alikuwa tatizo, na kwamba kingepata nafuu kama kingepata kiongozi mwingine kabla ya uchaguzi.

Hata hivyo, wanasiasa mahiri ndani ya chama hicho, wakiwamo mawaziri na viongozi waandamizi waliokuwa wanafikiriwa kuwa wangeweza kuwa bora kuliko Brown, walisisitiza kwamba ‘Gordon Brown pekee’ angeweza kukivusha chama hicho kwenye uchaguzi.

Hata waliokuwa wanaonekana bora kuliko yeye, wakajiingiza kwenye maigizo ya kisiasa ya kusisitiza, tena kwa mbwembwe kuwa ‘Gordon Brown ndiye bora.’ Sasa baada ya kubwagwa na kuondolewa Ikulu, ndipo wanahangaika kutafuta mrithi wake – tena wale wale waliosema yeye alikuwa bora, sasa wanataka kumrithi. Walichelewa kwa ajili ya nidhamu ya woga na maigizo ya kisiasa.

Hata hapa kwetu, wapo watu waliojivika nidhamu ya woga, wanaosisitiza kwamba CCM hakiwezi kushinda bila Kikwete; na wanadanganywa na tafiti na hisia kuwa Kikwete ni maarufu kuliko CCM; na hivyo yeye ndiye mwanachama bora anayefaa kukiongoza chama hicho.

Kwamba hata akishindwa kazi, yeye bado ndiye bora. Sasa ubora kwao ni kitu gani? Na kama huyu aliyenigwa kiasi hiki ndiye bora, basi chama kimekufa!
Hawa hawa watamzuia kumaliza urais ‘akiwa juu,’ na watakinyima chama chao fursa ya kupata mwamko na nguvu itakayokiwezesha kujijenga upya. Na yeye akiwasikiliza hawa, akasubiri hadi ashuke sana umaarufu, atakuwa anakichimbia kaburi CCM.

Hivyo, CCM kinapaswa kumsaidia kutambua kuwa kinahitaji kujengwa upya kwa kuwa na mgombea tofauti na yeye. Au basi, kama wanaogopa kumwambia wahamasishe wana CCM makini, wenye uwezo, waweke majina mwaka huu.

Hadharani wanaweza kusema watakalo, lakini kila mwana CCM mwenye akili timamu anayefuatilia mambo ya kisiasa hapa nchini, anajua kuwa CCM ya Kikwete inazidi kumong’onyoka.

Kwanza, kimerithi ubabe na udikteta uliotumia dola kuvimaliza vyama vya upinzani na kuvidhalilisha mbele ya umma kwa muda mrefu.
Bahati mbaya, wakati wanavishughulikia vyama hivyo, hawakujua kwamba ipo siku chama chao kingemaliza kazi hiyo na kuanza kujibomoa chenyewe kwa makundi hasidi, hadi kuwafanya baadhi yao kutamani kujiondoa kwenye chama hicho.

Hata sasa wapo wanachama wengi makini wa CCM ambao wanatamani kukikimbia chama chao lakini, kwa mtazamo wao, hawajaona chama kingine mbadala cha kujiunga nacho.
Baadhi yao wameshaanza kukiri kimya kimya jinsi walivyoshiriki kuviua vyama vya upinzani, na kwamba sasa dhambi hiyo inawarudi wao katika zama hizi za ‘CCM ya mipasho ya Waswahili.’

Na kinachoifanya CCM ya Kikwete isikalike ni ile dhambi ya fitina na ubaguzi – zana ambazo wanamtandao wa Kikwete walizitumia kumpitisha mtu wao kupata madaraka.
Ni fitina hizo zilizozaa makundi ya sasa ndani ya CCM, ambazo zinapochanganywa na uwezo mdogo wa watawala waliopo, zimezidi kudhoofisha heshima ya CCM mbele ya wanachama wake na wananchi kwa jumla.

Sasa wanaongoza kwa kulazimisha. Na udhaifu huu ndiyo sababu kuu inayomfanya rais aliye madarakani, anayetaka kugombea tena, aone kwamba hawezi kuchaguliwa bila kununua kura.

Nasisitiza tena. Sitachoka kuandika kwamba hii ndiyo sababu inayowafanya CCM wachangishane bilioni 50 chafu na safi kujaribu kumpitisha Kikwete.
Sisi ambao hatukumkubali Kikwete tangu awali hatusikitiki. Leo kila mtu anagundua kuwa hatukumchukia, bali tulimgundua, na tulikuwa sahihi.

Baadhi ya waliomtengeneza na kumwingiza madarakani sasa wanasikitikia uamuzi wao. Wengine sasa wamegeuka watetezi wa mabadiliko tuliyokuwa tunayazungumzia siku zote.
Watu pekee wanaomtetea hadharani ni wale ambao kuwapo kwake Ikulu kunawapa chakula. Wana hofu kwamba akiondoka, anaweza kuondoka nao.

Ndio hao wanaowekeza nguvu zao zote kuhakikisha anagombea – bila mshindani bila kujali kwamba yeye aliwahi kupinga dhana hii ya rais aliye madarakani kugombea bila kupingwa. Baadhi yao wanasema ‘wameshamwongezea’ kura atakazopata, kutoka asilimia 80 hadi 89.

Tunasubiri kuona kama atagombea peke yake, na kama atazipata hizo wanazomtabiria (wanazomtafutia). Na hawajui kwamba kwa kauli zao hizo, kama itakuwa hivyo, watakuwa wametujengea taswira chafu ya mfumo wa uchaguzi, na kutukosesha imani katika uadilifu na umakini wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Lakini lililo wazi hadi sasa ni kwamba umaarufu wa Kikwete umeshuka, na hiyo ni ishara kwamba wakati wake wa kukaa madarakani umeisha pia. Wamsaidie kulitambua na kulitumikia hilo.

Na sasa wananchi wanasema kuwa kutokana na madudu ya Serikali ya Kikwete, enzi za Watanzania kutukuza na kuogopa Ikulu zimepita. Zama za watu kuogopa urais zimetokomea kadiri siku zinavyozidi kwenda.

Nguvu pekee ya ukuu na utukufu wa Ikulu ilikuwa kile ambacho Baba wa Taifa, Julius Kambarage Nyerere, alikiita ‘utakatifu’ Ikulu. Na Ikulu takatifu ilitengenezwa na mawazo matakatifu, mikakati mitakatifu, mipango mitakatifu, miadi takatifu na matendo mengine matakatifu yanayofanyika katika jumba hilo kuu la utawala.

Utakatifu huo wa Ikulu ndio ulilenga kumpa rais jeuri na enzi za ‘Kimungu.’ Na ‘Umungu-mtu’ wa rais ndiyo ulimpa ujasiri wa kuchapa viboko baadhi ya wasaidizi wake, wakiwamo mawaziri waliotuhumiwa kula rushwa.

Ikulu iliheshimiwa na aliogopwa. Rais alikuwa rais kwelikweli, na ni wachache sana waliothubutu kutamani kugombea urais. Umoja na uimara wa serikali vilitokana na uadilifu wa rais mwenyewe, na baadaye wasaidizi wake, katika kusimamia misingi ya utaifa na raslimali za taifa.

Kilichotafuna tunu hizi katika awamu ya nne, ndicho kilichoudhoofisha urais wa Kikwete. Na kilichoutafuna urais huo ndicho kimewafanya Watanzania wakaibuka na kusema wazi kwamba taifa linakabiliwa na ombwe la uongozi.

Ombwe hili ndiyo msalaba mwingine ambao watu wakweli na waadilifu, kwa nyakati mbalimbali tangu Februari 2008, wamethubutu kumweleza Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, kuwa ndilo kosa lake kuu.

Kwamba miaka zaidi ya 10 aliyoitumia kuhangaika kumtafutia kura Kikwete, ndiyo imelisababishia taifa ombwe hili, ambalo hata wafadhili wameanza kulisema (nasikia walimuita JK na kumweleza) na kuonyesha kwa vitendo kwa kukataa kutoa sehemu yao katika bajeti yetu ijayo.

Ombwe hili ndilo limeanza kuwafanya baadhi ya wananchi kuanza kurejesha fikra zao katika utawala wa Serikali ya Awamu ya Tatu ya Rais Benjamin Mkapa.Nina hakika hata Rais Mkapa mwenyewe, akirejea hotuba zake za kumpitisha mgombea wa CCM katika vikao vya uteuzi miaka minne iliyopita, hajivuni.

Na ingawa Rais Mkapa ‘alimshughulikia’ vilivyo Sumaye ili kumzuia asimpiku Kikwete mwaka 2005, anapokaa na kutafakari tukio hilo katika macho ya kinachoendelea leo, hawezi kufurahi.

Sana sana, anachoweza kujisuta kimya kimya, na kujivunia kimoja; kwamba walioingia madarakani wanambeza yeye na hata kuandaa mikakati ya ‘kumchafua’ na kujisafishia njia, sasa wamekwama, na wanamtafuta kupiga naye picha na kummwagia sifa walizokuwa wanamnyima.

Ombwe hili ndilo linawasukuma baadhi ya wana CCM sasa kuwaza kumuunga mkono mtu mwingine jasiri na mwenye nguvu atakayethubutu, akajitoa mhanga kuokoa taifa lake, akajitokeza kuwania urais kupitia chama chao, kushindana na rais aliye madarakani, kumsaidia astaafu kwa amani; hata kama itabidi awe mzee sana, walau aongoze serikali ya mpito itakayosaidia kurekebisha mfumo wa utawala wa nchi hii.

Watu hawa waliojizungushia ombwe, ndio waliokuwa wanahaha kutumia vyombo vya habari kuisambaratisha serikali ya Mkapa, hadi wakamfananisha Sumaye na ‘ziro.’
Lakini leo hii kama wangepewa fursa ya kuchagua ziro ya Sumaye na ombwe la Kikwete, wangechagua nini?
Tukianzia pale alipoishia Mkapa mwaka 2005 na aliko Kikwete leo, wapi bora? Labda tulijadili hili kwa kina.
 
Wakiendekeza unafiki wa kisiasa wa kujikomba kwa viongozi wao, yatawakuta yale yaliyokikuta chama cha Labour Uingereza mwanzoni mwa mwezi huu. Kiongozi wao, Gordon Brown, alishaonywa huko nyuma, na tafiti zilishaonyesha kwamba yeye ndiye alikuwa tatizo, na kwamba kingepata nafuu kama kingepata kiongozi mwingine kabla ya uchaguzi. Hata hivyo, wanasiasa mahiri ndani ya chama hicho, wakiwamo mawaziri na viongozi waandamizi waliokuwa wanafikiriwa kuwa wangeweza kuwa bora kuliko Brown, walisisitiza kwamba ‘Gordon Brown pekee' angeweza kukivusha chama hicho kwenye uchaguzi. Hata waliokuwa wanaonekana bora kuliko yeye, wakajiingiza kwenye maigizo ya kisiasa ya kusisitiza, tena kwa mbwembwe kuwa ‘Gordon Brown ndiye bora.' Sasa baada ya kubwagwa na kuondolewa Ikulu, ndipo wanahangaika kutafuta mrithi wake – tena wale wale waliosema yeye alikuwa bora, sasa wanataka kumrithi. Walichelewa kwa ajili ya nidhamu ya woga na maigizo ya kisiasa. Hata hapa kwetu, wapo watu waliojivika nidhamu ya woga, wanaosisitiza kwamba CCM hakiwezi kushinda bila Kikwete; na wanadanganywa na tafiti na hisia kuwa Kikwete ni maarufu kuliko CCM; na hivyo yeye ndiye mwanachama bora anayefaa kukiongoza chama hicho.
Nimeupenda mfano wa chama cha Labour, ni kweli wengi wa wale waliokuwa wanamsifia Gordon wakati bado akiwa Waziri Mkuu hata baada ya tafiti kuonyesha yeye ndiye alikuwa tatizo ndio hao hao wanaogombea kurithi kiti chake na kuponda uongozi wake akiwemo David Miliband.

Inaonyesha ni kiasi gani viongozi wengi walivyo wanafiki wanakupenda wakati bado uko madarakani, ni sawa na hapa kwetu kuna wanasiasa wamewahi kusema watampigania Kikwete hadi waende kaburini na bila Kikwete hakuna CCM maneno ambayo nafikiri watakuja kuyakana huko mbele ya safari.
 
Huu ujumbe mzee ulifaa uwe ni kwa CCJ, haya majitu ya CCM hawajui watendalo. Ila hawa CCJ wanaotaka itikadi katika kundi la nyani naona wamekuja kuharibu mikakati yetu. Wamefanya nchi zima CCM watambe peke yao na hawajui hilo, wakija kujua too late
 
Wakuu inasikitisha sana watu bado tunaangalia gharama ya uongozi wa JK kwa CCM lakini hamzungumzii gharama ya uongozi wake kwa Tanzania. So far mmeona inflation inakwenda juu, Donors wamekata misaada (kwa kisingizio cha msuksuko wa uchumi wakati kwenye nchi nyingine wanaendelea kutoa), sheria haziheshimiwi na kuna watu clearly wako juu ya sheria, hakuna hata utekelezaji wa sera za uchumi......why do we talk of CCM first and not Tanzania. Pamoja na kuwa mimi ni mwana CCM i do not care much kama CCM ikifa au ikisambaratika, lakini Tanzania ikifa i will cry loud.
 
Wakuu inasikitisha sana watu bado tunaangalia gharama ya uongozi wa JK kwa CCM lakini hamzungumzii gharama ya uongozi wake kwa Tanzania. So far mmeona inflation inakwenda juu, Donors wamekata misaada (kwa kisingizio cha msuksuko wa uchumi wakati kwenye nchi nyingine wanaendelea kutoa), sheria haziheshimiwi na kuna watu clearly wako juu ya sheria, hakuna hata utekelezaji wa sera za uchumi......why do we talk of CCM first and not Tanzania. Pamoja na kuwa mimi ni mwana CCM i do not care much kama CCM ikifa au ikisambaratika, lakini Tanzania ikifa i will cry loud.
Ni kweli tunatakiwa tuzungumzie gharama yake kwa taifa lakini hatutakwepa kuizungumzia CCM kwa vile ni chama tawala, kuvurugika kwake kutasababisha taifa zima kukosa mwelekeo. Kwa kipindi cha miaka minne tu JK kaifanya CCM mapande mapande sasa watu wanahofu baada ya miaka mitano ijayo CCM itakuwaje chini ya uongozi wake.
 
Kwanza Luten Big up! Wewe ndo Mzalendo haswa huungi mkono chama bali unaunga mkono sera nzuri
 
Mimi mchango wangu hapa ni kuwashauri watanzania Makini wafanye yafuattayo; Kwanza tuchague Wabunge wengi sana wa Upinzani ili wakina Dr slaa wawe wengi. Ili kama Kikwete atagombea na kushinda kimizengwe basi iwe rahisi kwa bunge kupiga kura ya no comfidence! hii ndo njia pekee ya kumuondoa ka mizengwe itatumika hapo october.
Tumechoka jamani. Hivi wa Tz wenzangu hamuoni maisha yalivyo panda? Ukienda na Tsh 10000 dukani kununua kilo Mbili Za mchele na Sukari Kilo Mbili na Vocha ya Simu 2000 Pesa inakuwa imekuisha imebaki nauli ya Daladala. Je haya ni maisha wadau??? Tuwe wakweli hapa.
 
Mwacheni agombee aone maajabu. Watu huwa wanaamini kwamba CCM itashinda daimaaaaa! Hivi ujasiri huo wanaupata wapi? Watu kama hao watashangaa matokeo ya kura 2010.
 
Mwacheni agombee aone maajabu. Watu huwa wanaamini kwamba CCM itashinda daimaaaaa! Hivi ujasiri huo wanaupata wapi? Watu kama hao watashangaa matokeo ya kura 2010.

Naona umesahau vitisho vya yule Sheikh wa pale Magomeni Mikumi. Wagombea wa upinzani bado wanajiuliza wagombee au waache. Nakwambia sembe tamu mwana-wane, hakuna aliyetayari kuliacha hivi hivi akiona. Kweli watu wanaogopa kifo!!!!!!!!!!!

 
Back
Top Bottom