Kila mtu atakula kwa jasho lake-mkulo

Mkulo acha hizo,, acha kuwa kama wale akina nanihii,,, umesahau juzi jaman hapo ndo unanifurahisha sana, wewe wa kusema watu wale kwa jasho,,? wewe unafanya nini ofisini kama sio kusoma magazeti na kupokelewa mkoba wako pale wizarani na yule mzee nanhii? mi nakuona sana pale wizarani, ambavyo yule mzee yuko bize kukupokea,
Tatizo sio kula kwa jasho, tatizo hata hilo jasho letu mnakula sisi tule nini? au sikukuelewa ulivyosema tule kwa jasho. naamini mtu akishiba analewa, wewe sio yule mkulo wa moro...
 
hahaha jamani sicheki kwa uzuri ni huzuni tupu. Ila watanzania ebu tukumbuke tunapopiga kura tunakuwa tunaangalia wapi? Unajua mambo mengine tunsababisha sisi wenyewe. Tulipewa mheshimiw mwenye uwezo tukasema eti ni mwarabu atatuburuza, tukaona ni vizuri tumpe handsome boy sasa tena tunalalama kwa nini tuwe na msimamo ndugu zangu.

Kitendo cha huyo mkulo kusema hayo, for Godsake, atajuta asifikirie Mungu anahongwa au ana ubia na mtu katika lolote. Machozi ya wenye haki hayaendi bure. Safari tunayo kama wana Israel miaka 40, tutafika hata kwa magoti au mikono. Mungu atutie nguvu.
 
Waziri wa fedha mustafa mkulo amesema kuwa kila mtu atakula kwa jasho lake,na kuwataka wananch wasitegemee hali ngumu ya uchum waliyonayo kama itaisha,pia amesema serikali haitafuta kodi za mafuta ng'o

Kwani yeye huyu waziri anafikri anakula jasho lake?? Hajui kuwa anakula josho la walipa kodi wa inchi ya Danganyika.
 
Akili ni nywele kila mtu ana zake.
Huo ndio uwezo wote alionao Mkulo, amefika e.t.c yake.
 
Back
Top Bottom