Kila mti umeteleza na kila shoka wamebaki na mpini: Ni wakati umefika

Mtaka Haki

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
492
149
NINAAMINI TENA KUWA HUU UCHAGUZI UTAKUWA WA KUSHANGAZA NAANZA KUAMINI MANENO YA WALE VIONGOZI WA DINI.
1. KILA MTI WALIOUSHIKA CCM KWA NIA MBAYA UMETELEZA NA WAMEKUTA INA MIIBA
A. Kumchafua Dr. Slaa kwa habari ya maisha binafsi kumempandisha chati mara dufu
B. Kuzuia wagombea wasishiriki mdahalo kumewatangaza wapinzani na kumewafanya iwe kama CCM hawagombei mwaka huu wanasindikiza tu.
C. Kule kujaribu kusambaza ujumbe wa simu kumegeuka kuwa hasara na majuto. Hasara ni nyingi.
Kama upelelezi utaenda vizuri kutawaweka wengi mahali pabaya kwani sasa mwenyewe amepatikana. Mgombea urais ameanza kuhusishwa na ukaribu na watu hawa. Hata kampuni ya Vodacom wengine wameshajitoa kwa kujua kumbe inaweza kutumika kwa jinsi hizo. Mimi ni mteja wao wa postpaid wamenikosa na wamelikosa shirika ninalolisimamia - wenzangu hawapendi niendelee nao hata wao wanajitoa kwani wamethibitisha sio makini.) Kuna siku watajachochea makubwa zaidi.

2. KILA SHOKA LILILOKAMATWA KUTAKA KUWAKATA WAPINZANI MIPINI IMENG'OOKA WAMEBAKI NA MIPINI NA WAPINZANI WAMEKAMATA SHOKA.

A. Kule kuwatishia wafanyakazi kwa ukali na kuwahakikishia kuwa haitawezekana kusikiliza kilio chao na kisha kukataa kura zao. Imekuwa kazi kuziomba tena kura hizo za wafanyakazi.
Nadhani hawakukumbuka kuwa wafanyakazi ni Waalimu, Polisi, Mahakimu, Wasimamizi wa uchaguzi, Mashushushu, madaktari, wauguzi, na taaluma nyingi. Na kwa bahati mbaya badala ya kuwaomba radhi bado ni kama kauli hiyo imetaka ionekana kuwa ni sawa.

B. Kule kuwapitisha na kuwakampenia watuhumiwa wa ufisadi kwa woga wa kupoteza majimbo yao kwa upinzani kumeongeza hasira za watu na kuongeza umuhimu wa kuleta mabadiliko ya haraka.

Kwa sababu za kushangaza na kwa kurudia rudia wagonjwa wa Ukimwi wameendelea kuitwa ni kiherehere chao.

3. MATAMKO YA KUSHANGAZA NA KUSHINDWA KUKANUSHA KAULI TATA.
A. Mgombea urais wa CCM kutokukanusha ulinzi wa majini juu ya mgombea wa uraisi kwa ccm , kumewaudhi sana wacha Mungu na kuwakatisha tamaa hata wana CCM wacha Mungu. Kwa sasa kituko chochote kinahusishwa na aidha ushirikina au ushauri wa kishirikina.

B. Kung'ang'ania kuwaita wenye ugonjwa wa ukimwi ni kiherehere chao kumewafanya wengi kuona wamenyanyapaliwa au kuna saikolojia inatumika.

C. Kusema wanaopata mimba mashuleni ni kiherehere chao kumeleta uchungu kwa watu wengi waliotarajia maneno ya faraja na ya matumaini.

HII SIO KUTAKA KWA VIONGOZI MUNGU HUWA WAKATI WA MWISHO WA KITU UKIFIKA HATA UKILAZIMISHA UTALETA HASARA MBAYA ZAIDI.
Wale waliomlaumu Katibu mkuu na kusema anasambaratisha chama sio kweli. Ni wakati wa kusambaratika tu umefika hata angekuwepo nani huwezi kuzuia. Nawahimiza walioko madarakani waruhusu Mungu apitishe upepo wake. HAUZUILIKI. WENYE HEKIMA WASIUPINGE UPEPO UTAWAVUNJA. JIUNGE NAO.
 
Back
Top Bottom