Kila la kheri Zanzibar, bye bye Muungano!

Mwandishi huyu ndio wale wanaitwa MAKANJANJA au rafiki yangu Dr Mwakyembe aliwahi kuwaita Bungeni kuwa ni UPE (uandishi pasipo Elimu).

Kwa wasijua maadili ya UANDISHI wengi wanaongozwa na USHABIKI ima wa kisiasa, kikabila au kiimani lakin pia anasukumwa na UBAGUZI na vitisho na dharau kwa jamii inayomsoma. jamii inawapasa kuwaogopa watu waandishi kama hawa kama wanavyo ogopa malaria.

Lula nasikitika sana kukwambia na kukukumbusha kuwa mTU MZIMA ATISHIWI NYAU. Nimekusoma vilivo na hoja zako dhaifu katika Gazeti la Raia Mwema.

Nakupa pole sana mwandishi lakin kumbuka DUA LA KUKU ...
lula kanena ukweli,nenden mmezid kulia2 kwenye korido.tuone nani alikuwa kupe.mmefaidi mno mali za tanganyika,mmedekezwa mno.watu 1mil mnasumbua watu mil 45?mmejaza wenyeviti wa mtaa(wabunge) kwenye bunge la j.muungano(et anachaguliwa na watu 3000),jipatien uhuru wenu murud kwenu ,mmejazana bara kwa uhuru,rudini mkaijenge nchi yenu
 
Lula kawa Kanjanja? Makubwa. Ni kiboko. Tena ilitoka kabla ya rasimu ya katiba mpay. Hongera sana kanjana Lula. Mwache Barubaru aliye bora akukashifu lakini ajue kuwa wakibaki wao watauana kama kuku.

Congo,

Kwanza unatakiwa UANDISHI ni TAALUMA ambayo mtu inampidi kujipinda mpaka kuipata na wala sio lele mama unalala nyumbani kisha kesho unajiita mwandishi kisa unajua kuchonga sana maneno.

Kumbuka kuwa UANDISHI una miiko yake na ethics zake. Hakuna kitu kibaya kwa mwandishi na ambacho ni SUMU kubwa kwa mwandishi kama USHABIKI iwe wa kisiasa, kiimani au kikabila jambo ambalo LULA amejidhihirisha nalo kwa jamii ya ZNZ na waZnz.

Mwandishi siku zote anaongozwa na maadili ya uandishi akiw kiwa na wajibu wa KUIPASHA JAMII, KUIELIMISHA JAMII na hata kuiburudisha Jamii na bila kuegemea upande wowote wa shilingi na kuacha maamuzi yarudi kwa wasomaji wa habari ile na sio mwandishi kuwaamulia wasomaji wake.

Nikirudi kwenye mada yako. Nafikiri dalili ziko Mlangoni. Mumeanza Mwanza kuchinja, Mtwara gas na sasa Arusha mabomu. Sijagusia hapo kuchuna ngozi, kuuwa vikongwe na kunyofoa viungo vya albino. lakin kubwa kuliko yote UDINI ambaolo ni donda kubwa linalotokota. Nje ya Muungano Tanganika mtaweza kukabiliana nayo hayo kwa pamoja ?

Tuombe kheir
 
Tuseme ni kweli zanzibar haitaki tena muungano na mimi ninaamini kuwa ndio hivo, hili si jambo jipya katika nchi yetu, Nyerere aliukataa muungano wa East African Community kwa sababu alizozijuwa yeye, zaidi ni kwamba kenya ilikuwa ikinufaika zaidi na East African Community kuliko tz. na wazanzibari wanahisi kwamba tanganyika inanufaika zaidi na muungano uitwao tanzania.................ni heri tu uvunjike na kil ammoja ashike njia yake

kumbuk amkuu muungano wa zanzibar na tanganyika si kitu adhimu
 
Back
Top Bottom