Kila la heri kilimanjaro stars

IrDA

JF-Expert Member
Aug 26, 2010
743
350
Jamani leo tumiminika kwa wingi kuishangilia kilimanjaro stars uwanja wa taifa saa 10 jioni ikipambana na Djibout.Nawaombeni wadau msiangalie matokeo ya nyuma kwani mtoto kama ni wako hata akiwa na tabia mbaya humkani bali unamsaidia kubadilika.Sasa basi uwepo wetu uwanjani leo na support itawafanya wachezaji wapate hamasa ya kurekebisha makosa yao.Nawahaidi wadau mtegemee kushangilia idadi kubwa magoli tu leo.......tafadhali msikose mechi hii
 
Kikosi cha Kili Starz leo kimebadilika kwa takribani asilimia 60, Ngasa, Boban, Nditi, Nurdin n.k nje; Said Maulid,mwinyi Kazimoto, Mwaipopo ndani
 
Kikosi cha Kili Starz leo kimebadilika kwa takribani asilimia 60, Ngasa, Boban, Nditi, Nurdin n.k nje; Said Maulid,mwinyi Kazimoto, Mwaipopo ndani

ngoja tuone leo itakuwaje, tupeni update wadau, huyu mgonjwa wetu anaendeleaje.
 
mkuu mpira wa kili na hawa somalia unalingana. mashabiki wanawashangilia sana kili lakini wanakatisha tamaa. mi ndo naangalia hapa.somalia wamejaza wachezaji nyuma. tatizo ninalo liona ni mpira wa kili ni wa kibabe sana,mwinyi kazi moto anacheza madhambi sana hadi kapewa kadi. mia
 
timu ya kilimanjaro mbele wamewaweka msa hassan mgosi, said molali na ulimwengu ambao hawana mawasiliano kabisa. kama mgosi wakikwambia anacheza mchezo wa kulipwa huwezi kubali kutokana na kiwango chake duni. foward wetu wanapoteza mipira ovyo ovyo. mabeki wetu wanajitahidi iwapo saa nyingine wanajisahau halafu tatizo lingine wachezaji wetu wafupi ukilinganisha na hawa wenzetu. kwa mfano huyu said maulid mipira ya juu anaangalia tu sanasana atasukuma. mia
 
hatuna timu.. hao djibouti vibonde, kifupi ni kwamba kibonde kakutana na kibonde mwenzie
 
tumepata goli la pili kupitia kwa mwinyi kazimoto ambae amepiga mpira ukamgonga msa hassan mgosi mpira ukaingia nyavuni. mia
 
kili star wanabana sana uwanja inabidi wapanue. sasa hivi naona kazi moto ameamua kupiga mashuti kuelekea golini. mia
 
Mwinyi Kazimoto kafanyiwa faulu mbaya sana(teke la mbavu), sijui kama ataendelea na kasi yake
 
wakuu msione tumefunga goli mbili mkafikili kiwango kizuri. ukweli ni kwamba hata kili star ni vibonde tu sababu wanacheza bila marengo wala mpangilio.mpira sasa ni half time.
 
Back
Top Bottom