Kila kitu Linux

Taso

JF-Expert Member
Jun 12, 2010
2,463
2,289
Wakubwa,

Mathalan Ubuntu.

Nime instal Gnome Phone Manager lakini sioni sehemu ninayoweza kwenda kui execute. Synaptic Package Manager inaonyesha ipo. Wapi, haisemi. Itakuwaje?

Nikitaka kutumia command line prompt kui execute kwenye terminal nitajuaje command ya hiyo package?

Ubuntu 10.04 LTS
 
Mobile Phone Manager kwenye System menu,

au gnome-phone-manager from shell.
 
unaweza uka excute kwa kutumia jina la application yako... mfano ukiinstall vlc then kwenye terminal ukiandika vlc then enter basi itarun... unless kama hairun itabidi u angalie vizuri extension ya application yako au update system yako.. kwasababu wakati mwingine unahitaji extra(latest) repositories kwa baadhi ya program ambazo hazitaki kurun hata kama ziko installed... au kama una broken dependencies....

tumia "apt-get update" command ku update au "aptitude update"
 
Kang, Fredwash, shukran wakubwa.
Fredwash, kwani "extension ya application yako" inatakiwa iwe nini?
Na hizo latest/extra repositories, kama ume instal package halafu hapo hapo ikakataa ku run kwenye terminal, itakuwaje inahitaji extra/lates repositories wakati umetoka dakika hiyo hiyo huko kwenye ma repositories ? Kwani synaptic ilienda kuipata hiyo package kwenye repositories nzee? Manake uki update dakika hiyo hiyo sielewi utapataje kitu kipya kama haikuziona huko kwenye repos dakika tano zilizopita. If i'm making any sense.
 
niliposema kuwa unahitaji kuinstall dependencies au repositories files ni pale ambapo umeinstall new application lakini inatokea kuwa pamoja na kuapdate ila kuna dependency files flani zinahitajika ili hiyo application iweze kuwa excuted... au sometimes unakuta zipo dependecies fila au repository ambazo ni broken... (zimeharibika) inabidi uzirepair kwa kuupdate na kureplace zilizopo... naamini nimejibu kulingana na nilivyokuelewa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom