Kikwete's speech live on TVT

nasikia italy ataonana na wafanyabiashara wa huko.
sijui kwenye ujumbe wake atakuwa na wafanyabiashara pia?

Kwa kweli Umdhaniaye ndiye.. yaani JK alivogeuka na kupwaya kwa nguvu zote hata sikutegemea yaani!

Kweli nimeanza amini tetesi za kwamba JK ni rubber stamp lipo kundi linalo endesha nchi!

Sikutegemea atoke kwa vitisho badala ya kujibu hoja! am confused!!
 
Kwa kweli Umdhaniaye ndiye.. yaani JK alivogeuka na kupwaya kwa nguvu zote hata sikutegemea yaani!

Kweli nimeanza amini tetesi za kwamba JK ni rubber stamp lipo kundi linalo endesha nchi!

Sikutegemea atoke kwa vitisho badala ya kujibu hoja! am confused!!

Rwabugiri hakuna kundi linaloendesha nchi, bali kuna kundi ambalo linaipeleka nchi pabaya. Wameamua kuyafumbia macho na kuyadharau malalamiko yote yanayotolewa na nwananchi katika kila kona ya Tanzania.
 
JK hasiwatishe watanzania. Watanzania sasa wamesoma na wanaelewa.

Hakuna mtu wa kuleta fujo.

Fujo atazileta yeye anayekaa na makundi ya majambazi kibindoni. Anasema PCCB wanachunguza wanachunguza nini? Wakati anatetea akina Mzindakaya na wengine?

Yeye mwenyewe ameisha tetea karamagi, na makampuni ya kigeni yanayohitwa ya serikali wananchi wakikasirika, nani analeta fujo?

Wananchi au yeye anayetaka kuficha ukweli? Tunaomba afanye kazi aliyowamba wananchi na siyo blabla zisizokuwa na maana.

Nafikiri kuna haja ya kutafuta mkakati wa kupambana na hawa mafisadi maana hawataki kwenda mahakamani, wanataka tusahau. Mimi nashauri hili tuweze kuwaonyesha kuwa hatutaki kukumbatia mafisadi tuwabadilishe majina yeyote yule anayetetea mafisadi naye ni fisadi.

Organisation yoyote inayotetea mafisadi nayo ni fisadi.

Kwa kuanzia ukisema karamagi ongeza neno FISADI, Chenge(FISADI), CCM(Chama cha Mafisadi)-kinatetea(samahani kwa wana CCM ambao nao hawataki/wanachukia mafisadi), hii siyo kwamba tunahukumu hila hatuna muda/jinsi ya kupata ukweli ni kazi yao kujisafisha.
 
Kwa mtaji huu hii nchi ni budi sasa wananchi wakaamua kuichukua nchi yao mikononi mwa hawa tuliowapangisha sasa wanaingiza uchafu hadi sebuleni kwa mwenye nyumba.

Natafuta mpangaji mwingine kwenye nyumba yangu Tanzania kwani wa sasa anaingiza mno uchafu hata wakati mwingine anaenda haja kubwa na ndogo humhumu ndani mwangu siwezi kuvumilia uoza huu.

Mapamabano ya kifikra yanaendelea.
 
...ni vigumu kumtimua mtu kama karamagi na rostam ..ambao binafsi walitumia MABILIONI ya pesa zao a mfukoni..wanajilipa!!

au mtu kama membe na lowassa ambao ni archtect wa mbinu zote chafu na safi!!
 
Uzuri wa JF watu wako consistent, na huu ni ushahidi kuwa hawamuonei Jiwe, bali hata JK alipozingua watu walimpa makavu live!.

Ila cha kumshukuru JK ni kwamba pamoja na JF kumkalia kooni, lakini hakuifunga au kuiletea mizengwe kama Jiwe alivyojaribu mwaka jana mpaka tukaenda kuomba hifadhi kwenye mtandao wa Wakenya!

JF haicheki na mtu, ni mwendo wa kumkoma nyani giladi!
 
Back
Top Bottom