Kikwete's populist move backfiring?

BowBow,
Ni kosa la nani? Wahindi wakilipa below minimum wage wanalindwa na nani? Wanalindwa na viongozi waliochaguliwa na wananchi wa Tanzania. Hapo ndipo shida ilipo. Ili mradi kiongozi A kajengewa nyumba na Patel utasikia hizi kauli: "afadhali kuchimba madini kuliko kulima." Hilo lilishatamkwa na kiongozi mmoja wa awamu ya nne.

JSS
Kwa nini tena wanalalaika pale serikali hiyo hiyo ilipopandisha mishahara ya wafanyakazi? Labda ndio wamezinduka usingizini sijui
 
JK ni mchumi aliyeshindwa kuweka nadharia kwenye practice!

Kauli mbiu ya "maisha bora kwa kila mtanzania" ndiyo inamtesa. Mpambe wake EL anasema maisha bora kwa kila mtanzania hayaji kwa kupiga soga vijiweni, lakini hapo hapo anasahau kwamba kuna wakesha hoi wanavuja jasho kwenye viwanda na makampuni ya wahindi kwa ujira mdogo sana. Je, hao nao hawafanyi kazi? Au huko kwa wahindi ni vijiweni?

Walianza na mabilioni ya JK, naona yameisha na hakuna jipya tuliloliona na hatujui hata impact ya hayo mabilioni kwenye kuboresha maisha ya watanzania.

Sasa wamekuja na agenda ya mshahara ambayo madhara yake yako wazi sana. The moment serikali inasema kima cha chini kinatoka shilingi 48,000 mpaka 80,000 kwa mwezi, the next day ukienda sokoni kila kitu kimepanda bei, ukiuliza utaambiwa mishahara mipya. Kodi ya nyumba itapanda, kisa mishahara mipya. Bidhaa za viwandani zinazozalishwa na akina Patel, Subash na wengineo ndiyo zitapaa zaidi na finally hatutakuwa na mfumko wa bei, bali mlipuko wa bei, lakini figure za inflation zitabakia below 10 ili kulinda serikali ya JK.

Walalahoi kila kukicha wanajiuliza inflation ni mnyama gani, maana wanaambia inflation iko chini, lakini maisha bado ni magumu. Hivi mfumko wa bei kuwa chini una manufaa gani iwapo mshahara wa mtu unatumika kwa siku 5 unaisha?

Maisha bora kwa kila mtanzania bado ni ndoto ya masikini kuota ameokota burungutu la mamilioni. Hayaji kwa mabilioni ya JK wala kwa kuongeza mishahara ya wafanyakazi, bali kwa sera nzuri ambazo zitasaidia kuongeza uzalishaji na pato la taifa na hasa kwenye sekta ya kilimo na siyo kwenye madini na utalii ambako a good share of income inaishia majuu, Tanzania inabaki na figures tu kwamba iliuza dhababu yenye thamani $ milioni kadhaa na kilichobaki nyumbani ni aibu hata kutaja.

Ukizalisha mamilioni ya $ kwenye sekta ya kilimo, una uhakika kwamba a good share of hayo mamilioni yatabaki Tanzania kwa wakulima wako na hapo ndipo maisha bora kwa kila mtanzania yatakuja. Hizi biashara za mama lishe/ntilie/niwekee zinazotokana na mabilioni ya JK haziwezi kuboresha maisha yetu!

Hawa wahindi wanaotishia kufuta watu kazi hawawezi, ila watakachofanya ni kuongeza bei za bidhaa na kuongeza juhudi za kukwepa kodi ili waweze ku-maintain profit yao. Swala la kusema kuna over employment kwenye private sector kiasi cha kuhitaji kupunguza watu hilo halipo. Kuna makampuni ambayo yanatumikisha watu kwa masaa 12 kwa siku kwa same wage ya kufanya kazi masaa 8! Kampuni kama hiyo haiwezi kufuta watu kazi, itakachofanya ni kujisogeza serikalini ili ikwepe kodi na kuongeza bei za bidhaa. Vicious Circle nyingine.
 
Tanzania bwana watu wana mentality za ajabu sana, yaani unakuta mtu ana mamilioni ya fedha na kwa siku akitoka na wanae au marafiki anatumia karibu laki, lakini at the same time anamlipa mfanyakazi wake elfu kumi au elfu ishirini kwa mwezi wakati mfanyakazi ana familia na watoto vilevile.

Yaani wewe siku umeteremka nchini kama unatoka nje unakula vitu vikali baa halafu unamuachia tip muhudumu kitu kidogo tu kama elfu moja hivi unashangaa wenyeji wako wanakushangaa kishenzi. Wanaona huyu jamaa vipi? kumbe katika kukaa viwanja watu wamejifunza ku-appreciate service inakuwa ni uungwana tu kum-tip waiter.

Sasa hao waarabu na wahindi au mtu yeyote anayelalamikia hicho kima cha chini unakuta faida anayotengeneza through hao wafanyakazi ni kubwa kishenzi still hawathamini na lazima wamnyenyekee kishenzi.

Serikali sasa cha maana kwa kuwatumia watendaji wake kama wakuu wa wilaya, wafanyakazi wa halmashauri wahakikishe kuwa bei hazifumuki ili mtu akipata mshahara wake aweze kumudu kununua bidhaa muhimu hapo taratibu watu wataanza kuona maisha yanakuwa yanawezekana na dhiki inapungua.
 
lakini bora waongeze tuu maana from the get go wamelaliwa sana wafanyakazi kwa miaka mingi na hao wahindi,najua ni mkwala tuu ila mambo ya kutafuta super profit tuu,kuna uonezi mkubwa sana unaendelea pale kwa wafanyakazi,hao employer wana wish kama wangeweza wafanyiwe kazi bure kama kuna huo uwezekano,hakuna excuse hapo na kuanza kuleta theory nyingi za uchumi eti massive layoff...walipe waache kulalia watu tunajua kinachoendelea

Wahindi wangapi wameajiri mabaameidi na wafanyakazi wanyumbani? Najua hapa tunazungumzia wa viwandani lakini athari kubwa zaidi itatokea kwa hawa wasio na njia mbadala ya ajira! Uamuzi ulifanywa haraka haraka bila kuangalia athari zake. Sasa bei ya umeme inapanda, je na mshahara nao ubalishwe ili wananchi waweze kumudu gharama mpya ya maisha? Wenye viwanda wanachotahadharisha ni kuwa mishahara mipya itaendana na upunguzwaji kwa wafanyakazi. Sitashangaa kama itatoka amri ya kuwazuia kupunguza wafanyakazi! Kama alivyosema mmoja, suala limekuwa mishandled.
 
Kwa kweli hili swala la mishahara wengi humu tuna approach tofauti, lakini ukweli ni kwamba wafanyakazi especially wahudumu bar,kwenye mighahawa, nyumbani, walinzi, vibarua wananyanyasika sana. na ukichukulia kndi kubwa la watanzania wako humu. Jee, wasiongezewe mishahara kwa sababu kutakuwa na mfumuko wa bei? kwa nini wao wabebe mzigo kwa niaba ya watanzania wengine? jiulize kweli mtu unamlipa 30,000 kwa mwezi akiwa na mke na watoto na extended family! Siku hizi hiyo hela hata kwa teksi haitoshi hapa mjini!

Kwa maoni yangu, kama ni kufunga mikanda watanzania wote tufunge mikanda, ila hili kundi la watu wengi liongezewe kipato! Kila idara ya serikali, TRA, Customs na wengineo wakifanya kazi vizuri madhara ya kupandisha mishahara hayatakuwa makubwa kama madhara ya kuwaacha wadanganyika wenzetu wakiambulia 30,000 kwa mwezi.
 
Kwa kweli hili swala la mishahara wengi humu tuna approach tofauti, lakini ukweli ni kwamba wafanyakazi especially wahudumu bar,kwenye mighahawa, nyumbani, walinzi, vibarua wananyanyasika sana. na ukichukulia kndi kubwa la watanzania wako humu. Jee, wasiongezewe mishahara kwa sababu kutakuwa na mfumuko wa bei? kwa nini wao wabebe mzigo kwa niaba ya watanzania wengine? jiulize kweli mtu unamlipa 30,000 kwa mwezi akiwa na mke na watoto na extended family! Siku hizi hiyo hela hata kwa teksi haitoshi hapa mjini!

Kwa maoni yangu, kama ni kufunga mikanda watanzania wote tufunge mikanda, ila hili kundi la watu wengi liongezewe kipato! Kila idara ya serikali, TRA, Customs na wengineo wakifanya kazi vizuri madhara ya kupandisha mishahara hayatakuwa makubwa kama madhara ya kuwaacha wadanganyika wenzetu wakiambulia 30,000 kwa mwezi.

Mimi nadhani wengi hata hiyo 30000 hawapati! Mabaameidi wengine wanaambiwa watajilipa wenyewe kutokana na tips na shughuli nyingine zinazoambatana na sehemu hizo. Mimi naona serikali wangetazama kima cha chini anachotakiwa kulipwa mfanyakazi yeyote bila kuchanganua professions. Huu mshahara washinikize kwa kutoa adhabu ambaye hatalipa na kuwawekea wafanyakazi kama hao nyanja za kupeleka malalamiko yao pale watakapoonewa. Hapo waajiri wataamua kama wanaweza au hawawezi kuulipa na kama hawawezi basi kibarua kitaota mbawa. Hili ni lazima tulikubali. Wasiwasi wangu ni kuwa serikali itawafuatilia hao wanaowaita wahindi wakati wenyewe wakiendelea kuwaajiri ma hausgeli kwa mishahara na mazingira duni ya kufanyia kazi! Kwa upande wangu mkazo ungewekwa kwenye kuhakikisha kuwa wafanyakazi wote wanafanya kazi katika mazingira bora na salama, wahakikishiwe wanapata haki za kuwa na likizo, malipo pindi wanapoumia, wanakuwa wamefikia umri wa kuajiriwa n.k. Tuhakikishe yote haya ndiyo tukazanie hiyo mishahara.
 
Mpaka sasa hakuna kampuni lililosema litafunga biashara, ila yatapunguza wafanyakazi! hao watakaobaki wakilipwa vizuri na malengo ya kampuni yakafikiwa kuna ubaya gani? kwanza makampuni mengi yenye ufanisi yanalipa zaidi ya kiwango kilichowekwa isipokuwa ya wahuni wachache. Kama CTI wanaona srilanka, bangladesh na afganistani panalipa hawajazuiliwa kuwekeza huko.
 
principles of human sustainable development doesnt say kwamba kumpa mtu pesa ni kumwezesha kimaisha, still wakiongeza mishahara bila kuangalia other salient issues tutaihishia kwenye kuwawezesha wachache inhali majority of the citizens watakuwa kwenye absolute poverty,we must put human being centered to development,kuongeza kipato chake inaweza kuwa ni soln, lakini pia inaweza kuwa sio BEST solution...!!,wataaalamu wa uchumi embu tusaidieni hapa......
 
Mpaka sasa hakuna kampuni lililosema litafunga biashara, ila yatapunguza wafanyakazi! hao watakaobaki wakilipwa vizuri na malengo ya kampuni yakafikiwa kuna ubaya gani? kwanza makampuni mengi yenye ufanisi yanalipa zaidi ya kiwango kilichowekwa isipokuwa ya wahuni wachache. Kama CTI wanaona srilanka, bangladesh na afganistani panalipa hawajazuiliwa kuwekeza huko.

Wafanyakazi wengi wako kwenye informal sekta- mabaameidi, hausgeli, mafundi mchundo kwenye gereji bubu, wauza gahwa, mama ntilie n.k. Hawa hii mishahara haitawagusa ila wataguswa na mlipuko wa bei utakaoambatana nao. Ndiyo maana nadhani tukazanie kwanza mazingira bora na salama ya kufanyia kazi POPOTE ndiyo tukazanie hii mishahara ambayo hatuwezi ku"enforce".
 
Mtu wa Pwani , Masatu na mtoto wa Mkulima mko wapi mbona sijawaona kutia neno hapa ama hamjapaona ?

Mimi nilisema hakuna kitu mkasema Lunyungu sina zuri haya sitaki kusema zaidi mengine mmesha yasema .
 
serikali lazima ilinde wananchi wote na wao sio wajinga ,wamefikia uamuzi huo bada ya kuangalia vitu vingi kiutaalam na hawakurupuka,lakini haiingii akilini kumlipa mtu 30000 huku akikufanyia kazi masaa nane au zaidi kila siku na wakati mwingine na weekend yupo kazini tuu,nafikiri mnajua jinsi housegirls/boys wanavyofanyishwa kazi masaa hata 18 kwa siku na hawana haki yeyote,tujifunze kuwa binadamu sio uhuni uhuni tuu wa kutafuta faida kubwa huku ukiumiza wengine,nasema hivi kwa sababu hali halisi naijua jinsi watu wanavyoonea watu kwenye ajira
 
Mara nyingi tatizo linalokuwepo kwenye kutangaza kima cha chini siku zote ni ongezeko la bei maana watu wa viwandani wanasema gharama zimeongezeka n.k. Lakini bado tuna EWURA ambayo kazi yake ni kumlinda mlaji(consumers)kama gharama zimeongezeka mfano5% per product basi bei ya hiyo product isipande kwa zaidi ya 5% viningevyo kutakuwa na kitu wanakiita Money illussion (Unaongeza 10 then unatoa 10).

Mimi bado naamini hakuna kiwanda hata kimoja kitakachopunguza wafanya kazi kama inavyosemekana. Tanzania ni sehemu pekee nadhani Duniani unaweza kupata net profit margin 20% to 60% from the first year of operation.
 
Baa maids na wenye baa. Wastani wa crate za bia kwa siku ni 5.
faida ni shi 26,500 .Average price ni sh 19,700 na faida ni 5,300kwa crate

Wakiuza hivyo hivyo kwa mwezi faida ni sh 795,000. Wahudumu hapa ni 4 kaunter 1 mlinzi 1 supervisor/meneja 1. Jumla ni 7
wote wakilipwa 65,000. itakuwa 455,000.00 .

Balance 340,000.00 . umeme na maji =65,000.00 kodi ya nyumba say 150,000.00 . Matumizi mengine kama glasi , usafi nk say 50,000 kwa mwezi.balance sh. 75,000. ???????

Wenye mabaa watajiju. Mkitaka ongezeni bei za bia hadi sh 2,000.00 kwa chupa halafu tuone kama sisi wanywaji tutasogelea .Labda mafisadi tu. then breweries watasinzia mchana maana no enough sales .Baadae watapunguza wafanyakazi, kodi kwa serikali itapungua kuanzia PAYE hadi income and corporation tax etc.
Then we remain with the same formula =MAISHA BORA KWA KILA MBONGO?. Ngoja tuone.
 
wanaoathirika zaidi ni hawa wa formal sector, na ndio serikali inawapigania. kule informal bei ya sukari ikipanda na posho ya kibarua inaongezeka, mfano siku za nyuma kibarua alilipwa shs 1200 kutwa, sasa ni shs 7000 na hakuna mkopo jua likichwa mpe chake.

kimsingi uchumi wetu hautajengwa kwa kuwawezesha mama lishe, bamedi na ujenzi wa viwanda vya soda na whitedent. pia uchumi wetu hautakuwa kwa CRDB kukopesha mitaji ya kwenda hongkong kuleta tv feki. fikra hizi za kichagga sijui zitaisha lini?
 
Mawazo mazuri sana, Mkuu Eddy. Hivi unadhani nchi yetu itaendelea vipi tukishaondoa informal sekta? Wapi kwa mtazamo wako tuwekeze?
 
Mkuu Heshima mbele, tuwekeze kwenye slogan yetu "Dare to talk openly" thamani yake muulize Binti Fatma Karume, Dr.Idrissa na mh.Zitto. Ukiipuza utafanywa ndondocha kama David Mattaka. Mipango mizuri bila kuwakemea wahuni wa siasa na uchumi maendeleo tutayasikia tu.
 
Jamani hawa waajiri mara nyingi sio wakweli. Angalia hata haya makampuni makubwa ya madini. Wanachota lakini hawataki kukubali kwamba wanapata faida. Wewe uliona wapi kampuni ya madini hailipi kodi, dhahabu bei juu soko la dunia lakini bado wafanyakazi wanagoma na kufukuzwa kazi. Huu ni uhuni, lazima tukubali mara nyingine theories za uchumi ziwekwe pembeni kidogo ili hawa jamaa walazimishwe kukaa kwenye mstari kwanza, halafu baadae tujipange na kuona kama ni kweli uchumi umeporomoka kutokana na mishahara kuongezeka au ni usanii tu wa waajiri.

Kumbukeni hata dala dala dar walitaka nauli iongezwe na kutishia kugoma, mbona walipolazimishwa waliweza ku-operate kwa nauli ile ile mpaka leo! Our economy is largely informal, and the markets in which it operates is very imperfect. Thus you cant predict anything prior to full fledge operational status.
 
Kumbukeni hata dala dala dar walitaka nauli iongezwe na kutishia kugoma, mbona walipolazimishwa waliweza ku-operate kwa nauli ile ile mpaka leo! Our economy is largely informal, and the markets in which it operates is very imperfect. Thus you cant predict anything prior to full fledge operational status.

Kwa hiyo ndiyo kusema tukubali mambo "trial and error" tu.

Kuna watu wanasema hata ile bajeti huwa ni geresha kama mchezo wa kuigiza tu, matumizi na mapato ya kweli ni tofauti tu.
 
Mkuu Heshima mbele, tuwekeze kwenye slogan yetu "Dare to talk openly" thamani yake muulize Binti Fatma Karume, Dr.Idrissa na mh.Zitto. Ukiipuza utafanywa ndondocha kama David Mattaka. Mipango mizuri bila kuwakemea wahuni wa siasa na uchumi maendeleo tutayasikia tu.

Mh. Zitto naelewa lakini hao wengine wawili? Wamefanya nini cha kuwaingiza kwenye huu mjadala?
 
Back
Top Bottom