Kikwete's 'Maisha Bora kwa Kila Mtanzania'

bora maisha kwa kila mtz
hivi si ndio hawa hawa wanaochagua viongozi wale wale. NN alisema miafrika ndivyo tulivyo naunga mkono hili

na ndio hao hao watakao chagua tena waache wateseke kwa ujinga wao kwasababu wengine hata ukiwaelimisha hawataki wamekuwa wabishi mno
 
Nianze na kauli mbiu yangu: Miafrika Ndivyo Tulivyo! Kama kuna anayebisha basi na aje hapa anithibitishie visivyo na mimi nitaifutilia mbali.

Kingine, hivi kwani ni lini sisi (Tanzania/Afrika) tumekuwa na maisha bora? Kipya ni kipi hapo ktk hizo picha mpaka tumenyike kwa mshangao hivyo? Mbona hii hali ipo tokea enzi na enzi na wala hauhitaji kukata mbuga kwa sana kuiona? Sasa kipi cha ajabu hapo kinachouma sana?

Mwisho, hivi kweli mpo/wapo miongoni mwenu walioiamini hiyo kauli mbiu ya kampeni ya uraisi ya Kikwete? Kwamba eti ataleta maisha bora kwa kila Mtanzania...hayo maisha bora angeyaletaje? Angeyatoa wapi? Kisimani? Mimi katu sikumwamini. Nilijua ni yaleyale tu ya kuchonga domo kama ilivyo jadi yetu.

Namalizia kwa kusema: wenye uwezo hutenda na wasio na uwezo hujifanya wanao kwa kuongea. Wangekuwa wanaweza wangekuwa washatenda.

Alamsiki wana Jamiiforum! Ni mimi wenu mtiifu,

Nyani Ngabu/ Brasil.

Kuna msemo kuwa watanzania hupenda kudanganyika (gullible).... bila kuambiwa maneno mazuri na matamu kura itapatikana vipi? Hata kama ahadi zinazotolewa ni kama ndoto za alinacha, huwa ni bora kuliko bila!
 
Kuna msemo kuwa watanzania hupenda kudanganyika (gullible).... bila kuambiwa maneno mazuri na matamu kura itapatikana vipi? Hata kama ahadi zinazotolewa ni kama ndoto za alinacha, huwa ni bora kuliko bila!

Duh!! basi kama ni hivyo kweli tatizo ni kubwa zaidi ya nilifikiriavyo....
 
Does that have anything to do with Asian investors?
Even in India there are the rich and the poor.
Vote CCM
 
Does that have anything to do with Asian investors?
Even in India there are the rich and the poor.
Vote CCM


Moderators, why are you allowing this racist by the name of Raj Patel to insult us ? Raj Patel, please do us a favor, go to Calcuta and help your fellow Ponjoros. And by the way, don't forget to buy some deodorants for them.
 
mpaka awamu ya kwanza ya kampeni zake inamalizika hajawahi kutamka neno ..."MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA"...kwani anajua kuwa kawawezesha mafisadi kuwa na maisha bora zaidi...................ni laana kuwadanganya watu.........ahadi ya namna hii inaweza kutolewa na Mungu tu..........hata USA hakuna maisha bora kwa kila mmarekani............tunadanganywa kila siku kungali kweupe na tukiwa na akili zetu timamu pamoja na hayo yote hatuachi kupiga makofi mengi kwa ahadi hizi za kufikilika..................KIKWETE KAAMUA KUKATAA KUENDELEA NA AHADI/GIA ALIYOTUMIA KUWADANGANYA WATZ WAKIAMINI ANGEKUWA MKOMBOZI KUMBE NI MCHUMIA TUMBONI MWAKE................KUNA HAJA GANI KUMCHAGUA MTU AMBAYE ANAPINGANA NA FALSAFA YAKE MWENYEWE.? MNATALKA MDANGANYWE NAMNA GANI NDIPO MJUE KUWA KIKWETE HAFAI HATA KIDOGO.................SIKU HIZI KAULI MBIU NI ZAIDI....ZAIDI.........ZAIDI............ZAIDI........KILA KITU ZAIDI.....YAANI KUSAMEHE MAFISADI ZAIDI............
TUBADILIKE
 
Does that have anything to do with Asian investors?
Even in India there are the rich and the poor.
Vote CCM
Vipi ponjoro,chokrii,bana uliyezaliwa kwenye mitaro ya Bombay wewe kiswahili kwako hakipandi,you must be very ignorant to think that we are all stupid to predict what you want to earn , if you are an investor what has to do with our country politics, fake investor go to the street of Baroda where you can mess up things not in this lovely country of ours.
you are days are numbered
 
'Maisha Bora kwa Kila Mtanzania'
lazima wananchi wafanye kazi kwa bidii kubwa na viongozi wa kisiasa/serikali wawawekee mazingira mazuri yanayolenga mafanikio
wananchi wawe aggressive zaidi kwa kuona wanachozalisha kinatumika ipasavyo kwa kuwawajibisha viongozi wabovu.

hebu tujiulize kwa nchi zinazofanikiwa wenzetu wanafanyaje? tunaona CHINA watu wanavyotafuta pesa kwa kila njia na hapa dar wamejaa kila kona na sisi tunawapisha tu. kule kwao ukiiba mali ya serikali, unanyongwa na hakuna majadiliano.

kwa Tanzania yetu hii asilimia kubwa ya watu hatufanyi kazi, tunaota ndoto kuwa kuna siku chama cha siasa kilatuletea maendeleo. kivipi? lazima tujiulize hayo maendeleo yatakujaje? serikali itagawa fedha? itatoa wapi? ok kuna ufisadi lakini si huo tu unaosababisha kudumaa kwa uchumi wetu. bado kuna factors nyingine - uzalishaji hakuna!!!!!!! tunanunua kutoka nje kila kitu. angalia machinga hapa dar wanauza nini?

hivi kwa mazingira haya hata ukisema watu watasoma bure toka shule ya msingi mpaka chuo kikuu, upandishe mishahara ya watu nk utagundua kuwa itabidi serikali ikope zaidi ili ifanikishe haya au jamani serikali ita generate vipi hii pesa? ukinyanganya migodi Je watanzania tumejipanga kuchimba? any way najaribu kutafakali kwa sauti hapa sipati picha ya huko mbeleni
 
... Haaa na wewe naona sasa umekuwa msahalifu ujui kumbe wakati wa wadanyika kudanyika na T-Shirt na doti za khanga ndio umefika ,.. Cha msingi na ushauri wangu ni kwamba anza kumwelimisha bibi na nyanya yako kule kijijin nini faida ya kuzipata hizi khanga kwa sasa na madhara yatakayomkuta katika kipindi kijacho cha miaaka mitano...TAFAKURI!!!
 
pic1.jpg Pic 6.jpg View attachment 13598 Pic 5.jpg View attachment 13596 Pic 3.jpg Pic 2.jpg

Hivi hizi picha zinatufundisha nini kuhusu maisha bora kwa kila Mtanzania!! Hizi picha inasemekana zimepigwa TZ isipokuwa mmoja tu ambao ni ubalozi wa TZ in NY.
 
Picha zote hizo zinaonyesha jinsi ambavyo watanzania tulivyo na "Maisha bora" Mfano angalia jamaa aliyekaribu na kijiwe cha wana sisiemu anavyo enjoy usingizi na kivuli muruwa chini ya mti.
Au wanafunzi Darasani ambao wote wamepata Viti vya kukalia tofauti na zamani walikuwa wanakaa chini! na kwa kasi mpya ya sasa hivi watapata mawe mengine wayafanye Meza elewa Elimu ni muhimu karne hii ya Sayansi na Technologia
 
Back
Top Bottom