BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,006
Date::1/21/2009
Kikwete asimamisha ununuzi magari ya serikali
Na Mwandishi Maalum, Pemba
Mwananchi
Kikwete asimamisha ununuzi magari ya serikali
Na Mwandishi Maalum, Pemba
Mwananchi
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa serikali yake inatafakari kusimamisha ununuzi wa magari ya serikali kwa muda, ili fedha zitakazookolewa katika zoezi hilo zitumike kununua matreka kwa ajili ya kuinua kilimo nchini.
Akizungumza wakati wa kukagua ujenzi wa barabara ya lami kutoka Jondeni hadi kufikia Makombeni, Kisiwani Pemba, katika siku ya pili ya ziara yake ya siku sita Tanzania Visiwani, Rais Kikwete alisema kuwa mawazo ya kusimamisha ununuzi wa magari ya serikali ni jitihada za serikali yake kuinua hali ya kilimo nchini.
Rais Kikwete alianza ziara ya Tanzania Visiwani juzi, katika Mkoa wa Kaskazini Pemba na jana, alimaliza ziara ya kisiwa cha Pemba kwa kutembelea mkoa wa Kusini Pemba. Aliondoka kwenda Kisiwa cha Unguja kuendelea na ziara yake.
Rais Kikwete tayari ametoa maelekezo kuhusu suala hilo la kusimamisha ununuzi wa magari ili kupata fedha za kuwekeza katika sekta ya kilimo. Inakisiwa kuwa serikali inaweza kuokoa kiasi cha kikubwa na kuridhisha cha fedha kwa uamuzi wa kusimamisha ununuzi wa magari katika serikali.
Wakati anakutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa wizara ya fedha na mipango ya uchumi kuhusu tathmini ya utendaji wa serikali yake katika miaka mitano iliyopita, Rais Kikwete aliuelekeza uongozi wa wizara hiyo Jumatatu wiki hii mjini Dar Es Salaam kuchukua hatua za kusimamisha ununuzi wa magari ya Serikali, ili kuokoa fedha za kuwekeza katika kilimo.
Rais Kikwete ametoa ufafanuzi huo kwa wananchi baada ya kuwa ameambiwa na wananchi katika eneo hilo kuwa walikuwa na mahitaji ya pembejeo ikiwa ni pamoja na tretka za kilimo. Wilaya ya Mkoani inahitaji kiasi cha trekta sita kwa ajili ya kilimo.
Kuhusu ziara za nje, Rais alisema kuwa hatua ya viongozi wa Tanzania kutembelea nchi za nje siyo kupoteza wakati wala fedha, bali ni jitihada za viongozi hao kujazia raslimali za maendeleo ya Tanzania.
Rais ametoa ufafanuzi huo wakati alipofungua mradi wa tanki la maji kwenye kijiji cha Kengeja, mradi ambao umegharimiwa na serikali ya Japan na utakaowanufaisha kiasi cha watu 19, 000 wa kijiji hicho na maeneo ya jirani.
Mradi huo uliogharimu jumla ya Sh milioni 138, ikiwa ni pamoja na Sh milioni 30 zilizotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na Sh milioni mbili za wananchi, ni mradi wa 10 wa maji kugharimiwa na Serikali ya Japan katika Tanzania Visiwani katika miaka saba iliyopita.
Alisema Rais: "Hivi bila kwenda kuzungumza na wenzetu wa Japan tungepata wapi miradi hii? Wajapan wangelijua vipi kijiji cha Kengeja? Kijiji cha Kengeja na watu wake wanawahusu nini Wajapan? Bila kuwatambulisha watu hawa wa Kengeja, Wajapan wangewajua wapi?"
Aliongeza: "Kunawatu wanatuambia tubakia hapa Kengeja na pale Moshi ama Arusha Tusipotoka kwenda kuwaona watu hawa, watashughulika na wale ambao wamekwenda na wamewaona."
Alisema kuwa maendeleo ya Tanzania yana sura mbili ya vyanzo vya raslimali. "Moja ni nguvu zetu wenyewe, na sura ya pili ni nguvu za marafiki watu...Vyote hivi muhimu sana na hivyo tutaendelea kusaka raslimali za maendeleo popote tunapoweza na kwa kutumia kila aina ya mbinu."
Last edited by a moderator: