Kikwete: Wapinzani ndio wanaochochea vita dhidi ya Malawi

Status
Not open for further replies.
Source: Amka na BBC (20/8/2012) monday

...anasema viongozi wa upinzani ndio wanaoongelea maswala ya vita dhidi ya wanyasa concern mgogoro.

AMESEMA KATU TANZANIA HAITAPIGANA NA MALAWI.

My take:
Lowassa, Membe, Sitta ni Wapinzani?

Ni kweli kabisa hata kushindwa kutekeleza ahadi ya uchumi unaopaa umesababishwa na wapinza especial CDM
 
RAISI JAKAYA KIKWETE KWA MARA NYINGINE TENA AMEWAANGUSIA LAWAMA VYAMA VYA UPINZANI NCHINI KWA KUCHOCHEA MGOGORO WA TANZANIA NA MALAWI NA RWANDA.

KWANINI RAISI WETU HATAKI KUWA MWELI NA BADALAYAKE KILA KITI ANAWASINGIZIA UPINZANI?.
IKUMBUKWE KUWA WALIOVALIA NJUGA MGOGORO WA TANZANIA NA MALAWI NI MAWAZIRI WAKE. BERNAD MEMBE NA WAZIRI MKUU ALIYE JIUZULI LOWASA,MPAKA KUFUKIA HATUA YA KUTANGAZA VITA.

MH.RAISI KATIKA HILI UPINZANI UNATOKA WAPI?

KWANINI UNAWAOGOPA MALAWI KIASIHICHO?

UNAPATA NINI KWA KUUDANGNYA ULIMWENGU?

MH.RAISI KWANINI UNASHINDWA KUSIMAMIA UKWELI? NA BADALAYAKE UNATAFUTA NGUZO YA KUEGEMEA?

ENDELEA KUJISOMEA.

RAIS Jakaya Kikwete amesema habari kuwa Tanzania iko mbioni kuingia vitani na nchi jirani za Malawi na Rwanda zinachochewa na baadhi ya vyama vya upinzani ambavyo vinataka kutumia matatizo yaliyopo kisiasa.

Akizungumza nchini Malawi mwishoni mwa wiki, Rais Kikwete alisema yeye kama Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania hajawahi kuagiza majeshi yake kuvamia nchi yoyote ile au kukaa mkao wa kivita.

“Mimi ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania. Sijawahi kuagiza majeshi yangu yakae mkao wa kivita na wala kwenda vitani. Hivyo kama mimi sijawahi kutoa maagizo hayo, taarifa zote mnazozisikia haziwezi kuwa za kweli,” alisema Kikwete mara baada ya kumaliza mkutano wake na Rais Joyce Banda wa Malawi.

Rais Kikwete alikwenda Malawi kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika jijini Lilongwe, Malawi.

Ziara hiyo ya Rais Kikwete ilikuwa katika kipindi ambacho nchi hizi mbili zimekuwa katika vuta nikuvute ya maneno kuhusu umiliki wa Ziwa Nyasa ambalo Malawi inadai lote ni lake huku Tanzania ikidai pia kumiliki sehemu ya ziwa hilo.

Kikwete, kupitia mkutano wake huo na Rais Banda, aliwahakikishia Wamalawi kwamba Tanzania haina mpango wa kuingia vitani na Malawi na kwamba kwa muda mrefu imekuwa ikifurahia uhusiano mwema baina ya nchi hizo mbili.

Vyanzo vya gazeti hili kutoka katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, vinaeleza kwamba katika mkutano huo baina ya marais hao wawili, makubaliano muhimu yalifikiwa.

“Kwanza ilikuwa ni kuundwa rasmi kwa kamati maalumu ya pamoja kati ya nchi hizo mbili ambayo lengo lake kubwa litakuwa ni kujadili nini kifanyike ili suala la Malawi limalizwe kwa amani.

“Nafahamu mkutano wa kwanza wa kamati hiyo umepangwa kufanyika Jumanne ya wiki hii, kule katika mji wa Mzuzu uliopo kaskazini mwa Malawi na baada ya hapo mambo mengine yatafuata,” kilisema chanzo hicho cha gazeti hili.

Raia Mwema lilielezwa kwamba wananchi wengi wa Malawi walimwamini Kikwete kwa sababu ya tabia yake ya kumwita Banda “Dada yangu” kila wakati alipomtaja, jambo lililoonyesha ukaribu baina ya viongozi hao.

“Kwa kweli ziara ya Kikwete Malawi ilikuwa na mafanikio makubwa, hususan katika suala zima la uhusiano baina ya nchi zetu mbili. Kama ungewaona viongozi hao wawili usingejua kabisa kwamba eti nchi zao zinakaribia au ziko kwenye mgogoro mkubwa, gazeti hili limeambiwa na mmoja wa wana diplomasia wa Tanzania waliokuwemo kwenye msafara wa Kikwete nchini humo.

Katika mkutano huo, Rais Banda alimshukuru Kikwete kwa kukubali kutumia muda wake mfupi nchini mwake kuzungumzia pia suala la Ziwa Nyasa kwa vile taarifa mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kupitia vyombo vya habari, zilikuwa zikiwatisha wananchi pasipo sababu.

Wakati huohuo, vyombo vya habari vya Malawi vimeandika namna viongozi wa SADC walivyokuwa wakiwatania marais Banda na Kikwete kutokana na mzozo wao kuhusu ziwa hilo.

Wakati akifungua mkutano huo, aliyekuwa Mwenyekiti wa SADC, Rais Armando Guebuza wa Msumbiji, alitania kwamba viongozi hao wana kazi ya kutanzua mgogoro huo wa Tanzania na Malawi, na Rais wa Zambia, Michael Satta, akadakia kutoka katika kiti chake na kusema; “Kama wataanza kupigana, tutakuwa tayari kupokea wakimbizi.”

Mbali na masuala hayo, mkutano huo wa SADC ulimpa uenyekiti Rais wa Malawi, Joyce Banda huku Rais Jakaya Kikwete akikamilisha ngwe yake ya kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi, Siasa na Usalama (TROIKA) ya SADC na Katibu Mkuu wa sasa wa Wizara ya Afrika Mashariki, Dk. Stregomena Tax Bamwenda akichaguliwa kuwa Katibu Mtendaji wa SADC, akimbwaga kwa kura Waziri wa Uwekezaji, Maliasili na Viwanda wa Seychelles, Peter Sinon.

Katika hatua nyingine, kijiti alichokiacha Kikwete cha uenyekiti wa Troika kimechukuliwa na Rais wa Namibia, Hifikepunye Pohamba. Pohamba aliwahi kuishi Tanzania kama mkimbizi wa kisiasa na taarifa zinaonyesha kwamba alikuja Tanzania (Tanganyika) kwa mara ya kwanza tarehe 9 Desemba 1961, siku ambayo nchi hiyo ilipata Uhuru wake.

RAISI JAKAYA KIKWETE KWA MARA NYINGINE TENA AMEWAANGUSIA LAWAMA VYAMA VYA UPINZANI NCHINI KWA KUCHOCHEA MGOGORO WA TANZANIA NA MALAWI NA RWANDA.

KWANINI RAISI WETU HATAKI KUWA MWELI NA BADALAYAKE KILA KITI ANAWASINGIZIA UPINZANI?.
IKUMBUKWE KUWA WALIOVALIA NJUGA MGOGORO WA TANZANIA NA MALAWI NI MAWAZIRI WAKE. BERNAD MEMBE NA WAZIRI MKUU ALIYE JIUZULI LOWASA,MPAKA KUFUKIA HATUA YA KUTANGAZA VITA.

MH.RAISI KATIKA HILI UPINZANI UNATOKA WAPI?

KWANINI UNAWAOGOPA MALAWI KIASIHICHO?

UNAPATA NINI KWA KUUDANGNYA ULIMWENGU?

MH.RAISI KWANINI UNASHINDWA KUSIMAMIA UKWELI? NA BADALAYAKE UNATAFUTA NGUZO YA KUEGEMEA?

ENDELEA KUJISOMEA.

RAIS Jakaya Kikwete amesema habari kuwa Tanzania iko mbioni kuingia vitani na nchi jirani za Malawi na Rwanda zinachochewa na baadhi ya vyama vya upinzani ambavyo vinataka kutumia matatizo yaliyopo kisiasa.

Akizungumza nchini Malawi mwishoni mwa wiki, Rais Kikwete alisema yeye kama Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania hajawahi kuagiza majeshi yake kuvamia nchi yoyote ile au kukaa mkao wa kivita.

"Mimi ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania. Sijawahi kuagiza majeshi yangu yakae mkao wa kivita na wala kwenda vitani. Hivyo kama mimi sijawahi kutoa maagizo hayo, taarifa zote mnazozisikia haziwezi kuwa za kweli," alisema Kikwete mara baada ya kumaliza mkutano wake na Rais Joyce Banda wa Malawi.

Rais Kikwete alikwenda Malawi kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika jijini Lilongwe, Malawi.

Ziara hiyo ya Rais Kikwete ilikuwa katika kipindi ambacho nchi hizi mbili zimekuwa katika vuta nikuvute ya maneno kuhusu umiliki wa Ziwa Nyasa ambalo Malawi inadai lote ni lake huku Tanzania ikidai pia kumiliki sehemu ya ziwa hilo.

Kikwete, kupitia mkutano wake huo na Rais Banda, aliwahakikishia Wamalawi kwamba Tanzania haina mpango wa kuingia vitani na Malawi na kwamba kwa muda mrefu imekuwa ikifurahia uhusiano mwema baina ya nchi hizo mbili.

Vyanzo vya gazeti hili kutoka katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, vinaeleza kwamba katika mkutano huo baina ya marais hao wawili, makubaliano muhimu yalifikiwa.

"Kwanza ilikuwa ni kuundwa rasmi kwa kamati maalumu ya pamoja kati ya nchi hizo mbili ambayo lengo lake kubwa litakuwa ni kujadili nini kifanyike ili suala la Malawi limalizwe kwa amani.

"Nafahamu mkutano wa kwanza wa kamati hiyo umepangwa kufanyika Jumanne ya wiki hii, kule katika mji wa Mzuzu uliopo kaskazini mwa Malawi na baada ya hapo mambo mengine yatafuata," kilisema chanzo hicho cha gazeti hili.

Raia Mwema lilielezwa kwamba wananchi wengi wa Malawi walimwamini Kikwete kwa sababu ya tabia yake ya kumwita Banda "Dada yangu" kila wakati alipomtaja, jambo lililoonyesha ukaribu baina ya viongozi hao.

"Kwa kweli ziara ya Kikwete Malawi ilikuwa na mafanikio makubwa, hususan katika suala zima la uhusiano baina ya nchi zetu mbili. Kama ungewaona viongozi hao wawili usingejua kabisa kwamba eti nchi zao zinakaribia au ziko kwenye mgogoro mkubwa, gazeti hili limeambiwa na mmoja wa wana diplomasia wa Tanzania waliokuwemo kwenye msafara wa Kikwete nchini humo.

Katika mkutano huo, Rais Banda alimshukuru Kikwete kwa kukubali kutumia muda wake mfupi nchini mwake kuzungumzia pia suala la Ziwa Nyasa kwa vile taarifa mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kupitia vyombo vya habari, zilikuwa zikiwatisha wananchi pasipo sababu.

Wakati huohuo, vyombo vya habari vya Malawi vimeandika namna viongozi wa SADC walivyokuwa wakiwatania marais Banda na Kikwete kutokana na mzozo wao kuhusu ziwa hilo.

Wakati akifungua mkutano huo, aliyekuwa Mwenyekiti wa SADC, Rais Armando Guebuza wa Msumbiji, alitania kwamba viongozi hao wana kazi ya kutanzua mgogoro huo wa Tanzania na Malawi, na Rais wa Zambia, Michael Satta, akadakia kutoka katika kiti chake na kusema; "Kama wataanza kupigana, tutakuwa tayari kupokea wakimbizi."

Mbali na masuala hayo, mkutano huo wa SADC ulimpa uenyekiti Rais wa Malawi, Joyce Banda huku Rais Jakaya Kikwete akikamilisha ngwe yake ya kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi, Siasa na Usalama (TROIKA) ya SADC na Katibu Mkuu wa sasa wa Wizara ya Afrika Mashariki, Dk. Stregomena Tax Bamwenda akichaguliwa kuwa Katibu Mtendaji wa SADC, akimbwaga kwa kura Waziri wa Uwekezaji, Maliasili na Viwanda wa Seychelles, Peter Sinon.

Katika hatua nyingine, kijiti alichokiacha Kikwete cha uenyekiti wa Troika kimechukuliwa na Rais wa Namibia, Hifikepunye Pohamba. Pohamba aliwahi kuishi Tanzania kama mkimbizi wa kisiasa na taarifa zinaonyesha kwamba alikuja Tanzania (Tanganyika) kwa mara ya kwanza tarehe 9 Desemba 1961, siku ambayo nchi hiyo ilipata Uhuru wake.

Kwani hujui kwamba vyama vya upinzani hususan CUF na CHADEMA wao kazi yao ni kuconganisha tu ili wajinufaishe kisiasa? Rais ni Mtu mzima na ana vyanzo vingi vya habari. wewe kama hujui, bora ukae kimya au waulize werevu
 
Labda wapinzani anamaanisha akina Lowasa na Membe waliotangaza mkao wa kivita. Inawezekana alikuwa anazungumzia wapinzani wa position yake ya Urais!!
 
kwani hujui kwamba vyama vya upinzani hususan cuf na chadema wao kazi yao ni kuconganisha tu ili wajinufaishe kisiasa? Rais ni mtu mzima na ana vyanzo vingi vya habari. Wewe kama hujui, bora ukae kimya au waulize werevu
leta ushahidiwa upinzani kukusika,au membe na lowasa nao ni wapinzani?
 
slaa aliongea mgogoro ukiwa umeshaanza sikunyingi so msitafute pa kujishika

aliongea hadharan baada ya mgogoro lakini kaongea kichinichini muda mrefu. dr slaa na chama chake wanatumia fursa za mivutano inayojitokeza kujiimarisha kisiasa.
 
Sasa hata mvua zisiponyesha tutakuja kusikia Rais wetu akisema vyama vya upinzani vina ikosanisha serikali hii na MUNGU kwa manufaa yao ya kisiasa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom