Kikwete: Wapinzani ndio wanaochochea vita dhidi ya Malawi

Status
Not open for further replies.
Kasi mpya ,Ari mpya , na nguvu mpya ya kutokumuenzi mwalimu Nyerere kwa vitendo.
 
Naomba mwongozo: Rais awaombe radhi watanzania kwa kuwadanganya kuhusu waliotamka kuhusu mambo ya vita kati ya Tanzania na Malawi.
 
Hata hao wamalawi watamshangaa sana maana nina imani wanafuatilia kauli mbalimbali za viongozi wetu. Kauli za kuashiria vita zimetolewa na serikali ya JK kama ifuatavyo
1. Samweli Sitta - Kaimu Waziri Mkuu
2. Bernard Membe - waziri wa Mambo ya Nchi za Nje
3. Edward Lowasa - Mwenyekiti, Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje
 
Mnisamehe ila ukweli JK hana sifa za kuwa kiongozi mkuu wa nchi. Huwezi ukaondoa option ya vita katika mgogoro wa mpaka. Mimi sijasikia mpinzani akizungumzia vita ni wana CCM sijui JK anaishi nchi gani na huo ni uoga pia
 
Tusubiri Ikuli itakanusha kuwa kuwa hajasema hivyo!

Au walimuelewa vibaya kwa kuwa alikuwa anaongea "Kizungu", uenda alimaanisha ni wapinzani katika mbio za urais na Si wapinzani akimaanisha upinzani wa kivyama!
 
Habari za inteligensia lowasa,membe,sitta watahamia upinzani ndo maana jk amesema ni wapinzani wanaochochea vita
 
Anadhiirisha ana ufahamu kwa kiwango gani, wapinzani gani wanachochea? Au wa ndani ya chama chake! Au anaweweseka kwani wakati wengi tunaona muda wake bado mrefu yeye anaona mfupi na chama chake hakionekani kama kitashinda hivyo anaogopa wasijetengua kinga ya raisi
 
Moderator,

Kuna thread zaidi ya 10 kwa ajili ya suala la Ziwa Malawi ambalo ni la Malawi kwa asilimia 100 kama alivyoweza kutamka kijasiri Joyce Banda mbele ya Kikwete na Kikwete akashindwa kukana hilo, na kama ambavyo watatamka leo mawaziri wa Malawi kwenye kikao na watanzania na ambapo watanzania wakiongozwa na Membe watashindwa kukana hilo.

Hivyo, kwa wingi huu wa thread ninashauri kwamba imeshakuwa topic very broad tunaomba uiweke kama lable hapo juu kama ulivyofanya suala la katiba mpya au chaguzi ndogo ili thread zote zinazohusu hili la Malawi ziwe grouped humo.

Thread zinaibu kila dakika.
 
kama kweli kauli hii imetoka kwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, basi anakila sababu ya kutuomba radhi watanzania wote kwa pamoja kwa kuongea uongo tena kupitia vyombo vya kimataifa. hii itatunyima nafasi kila kona kwani tutaonekana taifa zima la waongo,wazushi na wadhaifu,lakini kumbe ni tatizo la mtu mmoja na kakikundi kake kadogo ka uenezi.
 
Hata hao wamalawi watamshangaa sana maana nina imani wanafuatilia kauli mbalimbali za viongozi wetu. Kauli za kuashiria vita zimetolewa na serikali ya JK kama ifuatavyo
1. Samweli Sitta - Kaimu Waziri Mkuu
2. Bernard Membe - waziri wa Mambo ya Nchi za Nje
3. Edward Lowasa - Mwenyekiti, Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje

Nyasa times wamekuwa waki-copy and paste habari zote za mgogoro huu toka kwa The Citizen pia na Daily news. Nina uhakika wanajua wazi JK aliuma maneno. Na hiyo inajionesha jinsi gani JK ni kilaza. Inaonesha hakujiandaa na hilo swali ambalo ni swali tarajiwa kabisa

Nisingependa kuamini JK alidhani hatoripotiwa na vyombo vya habari

Na kama huyu Ritz hapa ndo Ridhiwan basi amwambie baba sisi tunaifualia Nyasa Times hadi comments za Wamalawi zinaletwa hapa JF
 
Hivi huku kusini mwa Afrika kuna nini?

Raisi wetu akipewa Microphone huku kusini inakuwaaga balaa.

Yule mwandishi wa BBC, Bw. Omar Mutassa anakumbukumbu nzuri ya majibu ya raisi wetu.

Kurugenzi ya Mawasiliano IKULU kazi yenu ni nini?

Je jukumun lenu ni moja tu, yaani kutoa statements za KUKANUSHA habari tu? tena zile za ukweli.

Nasikitika na hili si mara ya kwanza humu ndani kusema kuna PR crisis

kwenye lile jumba la magogoni. Shetani gani mbaya ameingia mule?

Lazima kujipanga kila kunapotokea suala zito na nyeti katika taifa na

kuhakikisha siku zote serikali na jumba lile linakuwa na kauli moja

sahihi na yenye maudhi yaliyojitosheleza. Katika wakati kama huu, utarajie

kuwa rais au kiongozi mkuu yoyote atakapokutana na wanahabari zaidi wale wa nje, swala la mgogoro

na Malawi litajitokeza na hivyo kuwa muhimu kujipanga na majibu sahihi.

Sasa inaonyesha raisi wetu amekwenda huko kwa ajili ya huu mgogoro lakini

hakuwa amejipanga kujibu maswali yanayohhusiana na mgogoro huu. Hii ni AIBU nyingine

na imenikumbusha maswali ya Bw. Mutassa kule Afrika ya kusini, Raisi aliishia kutoa majibu

ya ajabu kuwahi tokea.
 
Mnisamehe ila ukweli JK hana sifa za kuwa kiongozi mkuu wa nchi. Huwezi ukaondoa option ya vita katika mgogoro wa mpaka. Mimi sijasikia mpinzani akizungumzia vita ni wana CCM sijui JK anaishi nchi gani na huo ni uoga pia

Nadhani uko sahihi kabisa,JK huwa anajidai kuwa ni mjanja sana,but inactual fact akishatoka kwenye urahis ndo atajua kwamba alikuwa anachemsha,unajua ukiwa rais watu wanakupa sifa ambazo hata hauna ili usije wafukuza lakini ukiwa nje ya uwanja unaweza shangaa hata ICC ikakuhusu,anyway ndo mlichokichagua so msilalamike sana
 
Salva Rweyemamu, Primi Kubanga na wengineo.

kama jahazi limekwama ombeni msaada, wapisheni wengine

wafanye kazi vizuri.
 
kama kweli kauli hiyo imetolewa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, anakila sababu ya kutuomba radhi watanzania wote na kufuta kauli yake. kwani taifa zima litaonekana kama nitaifa la waongo,wazushi na wadhaifu wa kufikiri, kumbe ni mtu mmoja na kakikundi kake kadogo kauenezi.
 
kipande cha bbc kinachozungumzia kauli ya hiyo ya jk hiki hapa..ni kweli alitoa kauli hiyo
 

Attachments

  • bbc.mp3
    3.6 MB · Views: 68
HESHIMA ya taifa letu barani Afrika inaporomoka.

Nakumbuka kipindi cha Kambarage, kauli zake zilikuwa

kama moto nyikani, waandishi wa kitaifa na kimataifa walitambua.

Kumbuka majibu yake pale Jomo Kenyatta na ata pale Accra na Addis.

Waliokuwepo enzi hizo watakumbuka namna ukombozi wa Afrika ulivyokuwa

ni agenda kuu ya Kambarage na vita dhidi ya mikakati ya mabeberu.

Kauli zake ziliwapasua vichwa mabeberu na hata kuogopa encounter naye.

Ngoja niwape mkasa huu:

Nafahamu wengi wenu mwambkumbuka marehemu J>F Kennedy, aliwahi funga safari

mpaka USSR kukutana na Nikita Khrushchev, akiamini amejipanga na kwa vile yeye ni Mmarekani na

taifa lenye nguvvu angetawala mahojiano na kudictate vitu. Yaliyomsibu huko ni makubwa

hatosahau, kwa maneno yake huku akitamani kulia alitamka, "He walked all over me, made me look like a fool"

Kwa muda mrefu sana hakukuwai kutokea rais wa USA kukutana na raisi wa USSR, na hii ilidumu kwa muda

wa miaka mingi, Ndipo JFK alipoamini ana uwezo na nguvu ya kumface kiongozi wa USSR

Kisa hiki ni kukuonesha namna gani viongozi wengine huwa wamejiandaa na kujipanga kwa level za juu mno wanapokutana na maraisi wenzao na media za huko.
 
hata kama habari hii ingekuwa kwenye gazeti la udaku ningeiamini. Mkuu wetu hajawahi kutoa kauli thabiti yenye faida kwa taifa.

Akitoa kaauli nzito ni pale utamsikia
1. madai ya wafanyakazi hayatekelezeki na Mgaya ni mnafiki na mzandiki,
2. madai ya walimu hayatekelezeki
3. madai ya madaktari hayatekelezeki na kama wanaweza watafute mwajiri mwingine
4. wale ambao wamezama na meli ya Spice Islander watambuliwe kwa DNA (wakati meli haiwezi kuopolewa)

Ah nimechoka kuandika, ila mkuu wa kaya anaboa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom