Kikwete: Walioambukizwa UKIMWI ni kiherehere chao

Huyo ndiye JK ninayemfahamu, kukoboa ndio asili yake. Mwaka 2015 mkimuuliza mbona hukutimiza ahadi hii na ile na ile, atawajibu very simple, "si mlinipigia kura kwa viherehere vyenu". Wenye viherehere mpigieni kura JK.

Si alichatutukana waTanzania kwa kusema kuwa 75 % ni bendera fwata upepo!!!!
 
Let us make assumption kama yeye naye angekuwa nao, je na yeye angekuwa na kiherehere?
Kauli zingine kama kiongozi wa umma unatakiwa kuwa makini sana kabla hujatoa kinywani. Huu ugonjwa hauchagui, unaweza kupata kwa njia tofauti na seksi. Hizo kauli ni za kwenye show za taarabu/mipasho tena kwenye mabaa ya kienyeji.
 
Huyu astaili kwa gharama yoyote ile kurudi ikulu, hivyo ndio anaaga. Yeye alishapima? Mbona majibu yacd4 zake daktari wake alificha? Hatunaye, kwani neurological disorder ni moja ya madhara ya low cd4 concentration. Kuanguka anguka je? Wasiwasi mtupu. Hofu ya kutoka ikulu hiyoooooooooooooooooooooooo
 
Nina mashaka na mwandishi wa habari hii, either kumchafua mgombea au ndo wale zero runnures wasioelewa kile kinachoongelewa na kudakia dakia tu mambo. Iam sure JK hawezi tamka maneno haya. jamani waandishi mtaangamia kwa ufitini huko juu.
 
Nimesikia kuwa naye ni mgonjwa ila sijui..

Ila naamini sana siku moja atashitakiwa na ndiye atakuwa mfano wa maraisi kufungwa....... Juzi Obama kamfagilia ila nadhani ni kwa sababu hajui maovu yake, na jamaa alivyo na kiherehere cha kujipendekeza.. Ngoja siku maovu yakijitokeza...







Hivi wale watu waliompigia kura 2005 bado wanampenda na watampigia tena 2010????????? Kama ndiyo basi watakuwa vichaa wa kupelekwa Mirembe.....
 
Huyu Rais si mzima. Ana matatizo makubwa sana. Mbona anatoa kauli za ajabu-ajabu? Kwa kweli lazima awaombe radhi wenye VVU/Ukimwi.
kapitiwa jamani kwani hata yeye ameguswa kwa njia moja au nyingine na ndugu kuwa muathirika
 
Nilikuwa najaribu ku-list down idadi ya kauli za Mkubwa mwenzetu huyu, mmmh, ni nyingi sana ambazo hazieleweki na zile chache ambazo zinaeleweka basi ujue hazitekelezeki.

Nafikiri tulimdanganya tulipompamba kuwa yeye ni KIJANA na sasa anajitahidi kuwa kijana.....by the way sidhani hata kama vijana wako hivi labda wale wa CCM wa "Kariakoo" kama alivyodai Makamba.
 
Mh. Nashindwa kusema, Siamini hicho kilchosemwa na Mheshimiwa wetu, Anyway Mungu Mkubwa.Kama ni kweli asamehewe bure hajui anachokisema. Lakini kwa maneno anayozungumza siku hizi ni vigumu kuamini kama ni yuleyule wa mwaka 2005, Tusubiri tutasikia mengi.
 
Wakati wa utawala wake yalisikika maneno haya;
1. Nchi imekumbwa na ombwe la uongozi (Vacuum), yaani hakuna uongozi.
2. Tanzania ndio nchi pekee duniani inayoweza kufanya shughuli zake bila rais.
3. Kuna mama alikamatwa ikulu ati katumwa na Mungu awe rais, na kadhalika.
Maana yake ni kwamba tumeishi kwa miaka mitano bila rais!!!!!!!!!!!!!!
Bado tu tunahitaji miaka mingine mitano ya kutokuwa na rais???? Tafakari chukua hatua.
 
Nimesikia kuwa naye ni mgonjwa ila sijui..

Ila naamini sana siku moja atashitakiwa na ndiye atakuwa mfano wa maraisi kufungwa....... Juzi Obama kamfagilia ila nadhani ni kwa sababu hajui maovu yake, na jamaa alivyo na kiherehere cha kujipendekeza.. Ngoja siku maovu yakijitokeza...







Hivi wale watu waliompigia kura 2005 bado wanampenda na watampigia tena 2010????????? Kama ndiyo basi watakuwa vichaa wa kupelekwa Mirembe.....

Yangu macho
 
Nina mashaka na mwandishi wa habari hii, either kumchafua mgombea au ndo wale zero runnures wasioelewa kile kinachoongelewa na kudakia dakia tu mambo. Iam sure JK hawezi tamka maneno haya. jamani waandishi mtaangamia kwa ufitini huko juu.

Na ile ya Iringa ya kusema mpange ni nani ataleta kinga huiamini? Mie nilimsikia na nilishangaa sana.
Kwa kauli yake anataka kusema watu hukutana kwenye maguest house etc , ila wanatakiwa wajue nani ataleta kinga.
JK anatakiwa ajue kwamba watoto wa shule hubakwa njiani na makondakta, walimu na wauza chips na migo etc. Je hawa watapata wapi muda wa kupanga na kujua nani ataleta kinga?
Na wale wanaobakwa na wachungaji/ mashehe wanajiandaa saa ngapi?
Na wale wa kwenye ndoa , watatumia kondomu kivip ?
Jamani kupmenda mtu ni pamoja na kumwambia ukweli. Endapo kweli unampenda JK basi mshauri pale anapokosea ili jamii isimwone kituko.
Hayo ndo mapenzi lakini kama mtu unamcehekea wakati anachemka, hakika unafurahia anguko lake!
 
Yeye ndiye ana kiherehere kwani anao siku nyingi tu kwa vile anakula vizuri na kuchuja damu mara kwa mara ndiyo maana nywele hazija nyonyoka, ila kuanguka anguka huku inaashiria virusi vimesha changanya
 
JK na kunyanyapaaa! Jisomee gazeti la mwananchi, 29/09/2010

Akizungumza katika mkutano wake wa awali uliofanyika Kijiji cha Lalago, Kikwete aliunyamazisha umati huo baada ya kuanza kuelezea maambukizi ya Ukimwi yalivyoshamiri kijijini hapo na wilaya nzima ya Maswa.

"Ndugu zangu maambuziki ya ukimwi hapa yako juu sana. Maambukizi hapa Lalago ni asilimia saba, nikiwa na maana kuwa kati ya watu 100, saba wanaugua ukimwi. Maswa ina wagonjwa 3,000 wanaohudumiwa na serikali," alisema Kikwete.

"Sasa, naomba akina mama wanapokwenda kliniki, muombe kupima ukimwi. Ukipata Ukimwi unajitakia kwa hiari yako; unaweza kujikinga kwa kuwa kupata Ukimwi si bahati mbaya; ni bahati mbaya ni kwa mtu aliyebakwa au aliyeongezewa damu isiyo salama."
Kikwete aliongeza kusema: "Lakini wengine ni kwa viherehere; wanapanga kupata kwa kuwa mnapanga siku; saa; na mahala pa kukutania. Sasa basi, mkipanga mkubaliane, nani alete kinga, wewe
au yeye... ndugu zangu tufuate mafundisho ya viongozi wa dini kuwa msivunje amri ya sita.
"Wale ambao bado wasubiri wakati wao na wale ambao wako kwenye ndoa zao wadumishe uaminifu... hapa uaminifu ni mgogoro."
 
Nilileta hapa hoja kwamba hizi kampeni za sisiemu zinapingana na sera ya taifa ya kupunguza maambukizi kama siyo kumaliza kabisa. Mimi ninaamini kwamba serikali hii ambayo imenyanyapaa wananchi wake kwa miaka mingi na sasa inaendelea kunyanyapaa waathirika wa ukimwi ifikie kikomo october 31.

HAtuwezi kukaa na kushangilia mtu ambaye hana chembe ya huruma kwa wananchi wake wanaokufa kwa maambukizi eti ni kujitakia.
Kweli mdharau mwiba.....
 
Back
Top Bottom