Elections 2010 Kikwete vs Wenje - Mwanza mjini

Kwa habari nilizo zipata sasa hivi jana wpambe wa Masha waliwakutanisha Masha na wanafunzi wa CBE tawi la mwanza.....waliwanunulia chakula na kuwapatia fedha 10k each person attended the meeting.....rushwa hiyo
 
Ama kweli mwaka huu si mchezo..Kama sikosei JK anakwenda Mwanza hii ikiwa ni mara tatu. Kama nimekosea naomba mnisahihishe!
 
Leo habari zilizopo ni kuwa vijana kwa wazee wengi wamejitolea kuwa mawakala wa Wenje hata kama kutakuwa hakuna malipo yeyote kwao,wako tayari kwa ulinzi wa kura. Wapambe wa Masha wanaendelea na vikao visivyo rasmi Mwanza Hotel na Mwanza Institute Club kutafuta njia za kunusuru anguko hili.
Nadhani kinachotafutwa sio ushindi tena ila kunusuru asishindwe kwa aibu kubwa. Wamekata tamaa.
Angalia isije ikawa wanapanga wizi mkubwa wa kura kwani kwao piga ua lazima washinde. Huyo jamaa aliwahi kuniambia lazima ajenge jengo kama lile la Mafuta pale Posta. Hivyo uwaziri ndiyo njia yake ya kuchuma zaidi.
 
mkutano wenyewe umejaa wapiga debe wa hapa pale stendi ya sahara na hiyo ni baada ya kupewa tshirt,kofia na pesa za kahawa.ccm haina jipya mza na wasukuma wa mwaka huu hawadanganyiki
 
Naomba kufahamishwa - huyu Ridhiwani Kikwete ana nafasi/cheo gani ndani ya CCM/Serikali ya Baba yake??

Ni mtoto wa mkulu!!! Babake kazidiwa sana imebidi aongeze nguvu!!!! JK kaweka record mpya kwa kuwa rais wa kwanza TZ kupigiwa kampeni na familia badala ya makada wa chama!!!!! Very shameful!!!!!
 
Kwa habari nilizo zipata sasa hivi jana wpambe wa Masha waliwakutanisha Masha na wanafunzi wa CBE tawi la mwanza.....waliwanunulia chakula na kuwapatia fedha 10k each person attended the meeting.....rushwa hiyo
Huo ni uzushi mtupu, Wenje anachangiwa hata mafuta ya gari atatoa wapi pesa za kuwahonga wanafunzi wa CBE? hizo tabia halisi za CCM haziwezi kuigwa na CHADEMA. HIvi sasa Wenje yuko uwanja wa Milongo wakati JK yuko viwanja nvya Sahara ,lakini huwezi amini idadi ya mahudhurio ya Wenje yalivyo.
 
msome vizuri amesema MASHA and not WENJE
 
Kwa hiyo kikwete atawambia viongozi wadini kwamba bado ni chaguo la Mungu au amekuwa wa shehe Yahya..dunia ina mambo kwelikweli
 
Wakuu wa kidini kumbukeni na kuuiga mfano waliotoa wenzenu huko Mbeya walipo kataa futari. Lengo lao lilikuwa kwamba hiki ni kipindi cha campaign na isingekuwa busara kualikwa kula na mgombea wa chama chochote. Maana wao ni viongozi wa waumini walio wanachama wa vyama mbalimbali. Basi ninyi wa huko mwanza mna waumini wenye itikadi za vyama mbalimbali, sasa mantiki ya mgombea wa upande mmoja kuwakusanya ni nini? Uepukeni huo mtego mnaotegwa tafadhali. Jamaa yupo radhi kuwaahidi chochote mtakachotaka maana ameshajishuku mwenyewe. Teteeni haki na hiyo jifungeni viunoni mwenu kama mkanda uliowafunga watanzania pamoja kama ndugu moja. Raia wanawaangalieni ninyii na hata uwasikiapo wakisema Mungu kasema hivi ama vile ni kile walichokisikia kutoka kwenu. Itunzeni hiyo heshima mliyoheshimiwa na Mungu katika utakatifu wake. Muoneni shetani katika kona zote na mkemeeni kwa nguvu za uweza wa Roho mtakatifu.
 
JK kaweka record mpya kwa kuwa rais wa kwanza TZ kupigiwa kampeni na familia badala ya makada wa chama!!!!! Very shameful!!!!!

Wapi Mzee Mwinyi? wapi Salmin? wapi Sumaye? wapi Warioba? wapi Mkapa? Wapi Tingatinga?

Ni ishara tosha kwamba Mkwere HATAKIWI na hata wenye TANU/CCM yao; sema tu hawewezi kukiri udhaifu hadharani!
 
Pamoja na mambo yote lakini naomba wapenzi wa Chadema tumwombee Dr. Slaa. Kuna nguvu za giza toka kwa Watawala za kumumaliza hivyo anahitaji ulinzi wa Roho Mtakatifu. Tumuombee Sana!!!

Mtu yeyote mwenye mapenzi mema na Dr. Slaa basi atumie muda wake kuomba kwa ajiri yake kila siku kabla ya uchaguzi huu. Mungu wa Israel Anaweza.
 
Huo ni uzushi mtupu, Wenje anachangiwa hata mafuta ya gari atatoa wapi pesa za kuwahonga wanafunzi wa CBE? hizo tabia halisi za CCM haziwezi kuigwa na CHADEMA. HIvi sasa Wenje yuko uwanja wa Milongo wakati JK yuko viwanja nvya Sahara ,lakini huwezi amini idadi ya mahudhurio ya Wenje yalivyo.

Mkuu soma vizuri sio wenje ni masha ndio alikutana na wanafunzi wa CBE...
 
Kwa habari nilizo zipata sasa hivi jana wpambe wa Masha waliwakutanisha Masha na wanafunzi wa CBE tawi la mwanza.....waliwanunulia chakula na kuwapatia fedha 10k each person attended the meeting.....rushwa hiyo

Mkuu hizi taarifa ilibidi mzifikishe TAKUKURU hata kama hawatafanya chochote lakini for future reference tu
 
Dr Slaa kokote kule uliko hakikisha unarudi tena Mwanza kufanya vitu vyako ili kuhakikisha chadema inauteka mkoa huo.

Mwanza hakuna uhaja wa kurudi hata kidogo.........................Anatakiwa Mikoa ya kusini tu kufunga dili.........................
 
Back
Top Bottom