Kikwete unawakumbatia wa nini? Mwema, Othman, Chagonja, Zoka?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
Hivi ni kwanini Rais Kikwete hataki kuamini kuwa timu yake ya usalama nchini inaliangusha taifa na haina maono mapya ya kusimamia usalama? Matukio kadhaa yaliyotokea nchini ndani ya mwaka huu peke yake yanathibitisha kubomoka kwa mfumo wa usalama. Kikwete amekuwa na watu hawa kwa karibu miaka sita sasa na matukio yaliyotokea chini yao ingekuwa nchi nyingine hawa wangekuwa wa kwanza kuondolewa. Hivi hadi nini kitokeeawa ndio atajua watendaji hawa wa vyombo vya usalama ni janga kwa taifa?

Hivi hadi aje kusikia kuna waziri kauawa au kundi la wabunge wametekwa nyara? Inawezekana vipi watu hawa wakaendelea kuaminiwa kusimamia usalama nchini wakati matukio ya kutisha na yanaendelea kutokea na sasa imefika mahali kwa kweli ni point of no return? Mwisho wa siku itabidi waanze kutumia mbinu za kimafya kwani mbinu za kawaida za kiusalama zimeshindikana! Wameshindwa na hawawezi tena!!

FIRE THEM; KWANINI HAWAONDOLEWI?
Kwanini wao wenyewe hawaondoki!!?

Mara nyingi tunalaumiwa kwa kukosoa tu na kuwa hatupendekezi nini kifanyike; well wafukuze hawa kwanza kama hatua ya kwanza halafu waingize watu ambao wanaongozwa na weledi na siyo urafiki au ujamaa na wewe! Au mtatuambia tusubiri kutoa maoni kwenye tume ya katiba mpya!
 
Kiongozi shupavu hawezi kutumia mabavu kuongoza, nikiongozi dhaifu tu ndio atatumia mabavu kuficha udhaifu wake - JeneraliUlimwengu.
 
  • Thanks
Reactions: awp
Mkuu MM tatizo liko kwake rais wetu kwanza,amekuwa na udhaifu mkubwa sana kwenye maamuzi
hata kwa vitu vilivyo wazi sana,tatizo yeye mwenywe siyo mwajibikaji hivyo hawezi kumchukilia
hatua mtu mwingine ambaye hawajibiki kwenye nafasi yake itakuwa ni kichekesho.Tatizo lingine
ni safu yake aliipanga ya kujihami sana kiuanamtandao hivyo ni ngumu kuipangua.
 
Hakuna hoja ya msingi hapa ya kufanya viongozi hawa kujiuzulu

Kama mpaka hapa tulipofika kama nchi halafu wewe huoni hoja ya hawa viongozi kujiuzulu,basi either ni mmoja wao
au una maslahi binfsi katika udhaifu wao huu kiutendaji.
 
Kuna mashemeji zangu hapa ktk hili kundi na wengine ni marafiki zangu tumetoka nao mbali hivyo siwezi kuwafukuza kazi.

NINAAMINI HUU NI UPEPO TU UTAPITA.

Labda nione nimelengwa mimi mwenyewe na kitu chenye ncha kali ndo nitawachukulia hatua ila kwa sasa bado naridhishwa na utendaji wao wa kazi.
 
Kwanini hatutaki kutaja waziwazi kuwa Rais wetu ndio tatizo? tusizunguke kichaka tafadhali Mzee
 
Nafikiri wao wameagizwa kumlinda rais na wamefanikiwa sasa atawafukuzaje? Sisi wananchi ndiyo wakulaumiwa kwani huwa hatushinikizi mambo kwa nguvu tunahofu hata kudai haki zetu.
 
Mkuu nadhani mh.rais haoni tatizo kama timu yake ya usalam haina haiba ya kuendelea kuwa ktk nyadhifa walinazo,kuna uwezekano anashauri timu hii ya wanausalama i-deal na matukio kuliko source zinazosababisha ukosefu na uvunjifu wa amani nchini,lakini pia wakati mwingine twaweza kuwalaumu bure maofisa waandamizi ktk nafasi zao muhimu na kumbe twafaham tatizo ni yeye,muda wote yupo ziarani ughaibuni lini watafanya consultations na watendaji wake?na hata wakitaka kupata go-ahead kwake juu ya namna ya kudeal na mambo akionesha kutokujali wafanyaje?tatizo ni mh.rais mwenyewe na wala hakuna mchawi mwingine,mbegu hata za haya tunazozishuhudia sasa yeye ndiye mpanzi kwanini othman alaumiwe,au mwema ama zoka,huwezi kufanya usafi kwenye shamba pasi ridhaa ya mwenye shamba,yule ni boss wao akigoma kupokea ushauri wao wafanyaje?akitoa maelekezo yake wakatae na wanajua yeye ni boss,tatizo ni tuliempa dhamana na ambaye kama watz tuna mandate nae,hatuna mandate na othman,mwema wala zoka isipokuwa kikwete,kama hata muda wa kukaa nyumbani hana je kusikiliza matatizo ya wanawe na kutafuta majawabu sahihi atapata wapi.mkulu hajali kifupi hana uchungu wala uzalendo kwa nchi yake.
 
Labda ndiyo maelekezo waliyopewa. KWamba nguvu ya intelijensia yote ielekezwe kwenye mambo yanayohusu CHADEMA.
 
tuliambiwa tukiwagusa mafiasadi nchi itayumba

na inayumba

natfuta link ya iran, uamsho, kuchoma makanisa na fisadi mmoja papa
 
Tunashuhudia utendaji mbovu wa wanausalama kuliko wakati wowote tena changamoto zikiwa na nyepesi mno!!! System imefeli,inapambana na wanasiasa tu(tena kwa kuipigania CCM) kuliko kusoma vihatarishi (indicators) vya hatari vya usalama wa nchi!
 
Kwanini hatutaki kutaja waziwazi kuwa Rais wetu ndio tatizo? tusizunguke kichaka tafadhali Mzee

NIDHAMU YA WOGA NDO INAPELEKEA KUZUNGUKA POINT, nani asiyeogopa kuokotwa MABWEPANDE?

ILA KIUKWELI RAIS WETU NI MDHAIFU SANA.

Tena mkimpigia makelele sana anakwenda zake Marekani ku refresh mind.
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom