Elections 2010 Kikwete Ukiiba Kura au Kutumia Dola Jiandae Kuchapisha noti ya trilioni 1

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
JK ameshindwa. Hilo analijua.

Kitendo cha kutumia wanajeshi wanafiki kuwatishia wananchi, kimechefua si tu Watanzania bali wahisani ambako huwa anapenda kwenda kufanya umatonya.

Tanzania siyo paradiso kiasi cha kuona utawala wa sheria unakiukwa hata wahisani wakafumba macho. Wanaweza kuipuuza nchi yoyote isiyoheshimu haki za binadamu na utawala wa sheria. Na wako tayari kwa hilo. Ndiyo sababu Kikwete anahaha: vitisho vya jeshi, meseji za uchochezi n.k. Tunajua unajua fika kwamba kuiba kura is not an option this time around. Na Watanzania tunataka mabadiliko.

Kwa hiyo Kikwete na wenzako msithubutu kuiba kura, au kuua raia kwa kisingizio cha kuingia madarakani. Utajuta kama Mugabe wa Zimbabwe.

Nasubiri Jumamosi utakapoanguka tena jukwaani, kesho yake Jumapili unaanguka wewe na utawala wako wa mafisadi.

Imekula kwako JK.
 
Nadhani kikwete atatuma watoto wake dubai wakaishi huko.... Makamba yeye juzi katuma mkwe wake (mke wa January) kwenda marekani kupata mtoto huko (na uraia wa USA)
 
Kwenye database yetu tuna KIBAKI, MUGABE sasa tunasubiri wa tatu anayefuata ni nani kungangania madaraka.
 
Nadhani kikwete atatuma watoto wake dubai wakaishi huko.... Makamba yeye juzi katuma mkwe wake (mke wa January) kwenda marekani kupata mtoto huko (na uraia wa USA)

Kama wataweza kuvumilia maisha ya usawa. Maana huko watakakokimbilia hakuna cha mtoto wa rais wala nini. Ukikanyaga sheria inakula kwako. Wamuulize mtoto wa Charles Taylor kimempata nini... wamesahau the great sons of Saddam Hussein?
 
Mungu yuko upande wetu wana-mabadiliko hataweza kuiba wala kuua tumemuomba mungu naye ameitika.Kikwete ni sauti iliyo nyikani.Mungu ametenda tunakaribia kuingia mjini mpya aliotuandalia
 
Back
Top Bottom