Kikwete: Tutawajibu wanaotusema!

With all due respect sir, inaonekana wewe ndiyo una chuki na sisi, kwa nini kutumia hela zetu kwenda kubembea Jamaica ?
 
Labda mimi sikuelewa kiswahili.

Rais JK kasema ktk jamii ndivyo ilivyo 15% watakupenda,15%watakuchukia hata ufanye nini, 70% wao wataangalia upepo unavuma vipi.
Hayo ndo kasema Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania .

Sijui ame cite study gani hii? Au kashakuwa "The Don killuminati Makaveli" na yeye?
 
Hamna mapigo yoyote.Ni mmbea tuuuu!
Aende akafundishwe Taarab na mke wake ndio aje kujibu mapigo!!!!
 
Mmesahau kwamba ni "chaguo la Mungu" mtamuuzi pengo nyie angalieni sana kauli zenu mnawaudhi viongozi wenu wa kanisa
 
I don't understand my president, ufisadi kwake nikitu cha kawaida na anawanyeshea kidole wanamwelekeza njia wapinga ufisadi. We are total lost!!
 
Kabembea huku akiomba afundishwe Ragae...aaah rais huyu machachari sana...:rolleyes:

Huyu jamaa hata hatufai anatufisadi kwa namna nyingine hawezi kuwa anatumia kodi zetu kupanga safari kila siku.
Na kama anasema wanaompinga wanachuki arudi nyuma na kukumbuka kuwa hao anaosema wanachuki ndo waliompigia kura.Kama kazi imemshinda si atundike daluga!
 
Rais wetu mpendwa Kikwete unatakiwa kuwa na hekima za kawaida tu kujua welekeo wa nchi yako. Achana na siasa za makundi na ubaguzi wa watu. Umechaguliwa na taifa hivyo watumikie Watanzania wote bila konesha jaziba!

Ninajua kuwa kutumia madaraka vibaya ni ufisadi hivyo safari zako za kwenda kubembea Jamaica na kufanya check up ya Ubongo Cuba ni ufisadi pia. Unatumia vibaya mali za Wananchi waliokuweka madarakani kwa kuzua safari zisizo na tija kwa taifa.

Wamekueleza vyema njia nzuri ya kujisafisha na ufisadi lakini kwa kuwa uoni basi ngoja tuone utakavyojibu mapigo na utakao wapeleka jela nao watakupeleka baada ya kusitaafu urais wako "so to every action there is equal and opposite reaction". Hivyo tenda haki na uache safari za nje zisizo na tija kwa taifa!
 
ana jeuri kwa sababu anajua 2010 atachaguliwa tu tena kwa landslide...haitaji hata kuiba kura, mitanzania itamchagua tuu for sure...kwani ni nani hapa nchini anayeweza kusimama kidedea na JK???
 
Raisi haipendi nchi yake, akae hapa akifanya nini...hizi kero kero kero hata yeye zinamkera!! anaona bora ajiendee zake viwanja ufaransa, denmark etc akaji resitishe...akirudi hapa ni bla bla za hapa na pale halafu huyooo...

yaani kama kungekuwa kuna kitu kinachoitwa longdistance presidency hapa duniani, huyu rais wetu angekuwa amesha hama nchi kitambo sana...
 
ana jeuri kwa sababu anajua 2010 atachaguliwa tu tena kwa landslide...haitaji hata kuiba kura, mitanzania itamchagua tuu for sure...kwani ni nani hapa nchini anayeweza kusimama kidedea na JK???

Haya maneno yana ukweli wowote? Yaani kati ya waTz 40 mil ni hakuna!?
 
hapa sasa ni kusubiri mambo ya mipasho tu dah! kazi ipo sasa mziki unaendelea
 
I don't understand my president, ufisadi kwake nikitu cha kawaida na anawanyeshea kidole wanamwelekeza njia wapinga ufisadi. We are total lost!!

Heheee Chaguo la Mungu siyo?

Wa-Anglican na Kizazi cha Nguruwe nasikia ndiyo tulimchagua Kikwete.

Asante yake kajawa Waislaam kwenye CCM na serikali yake.

Hahaaa, Pengo!!! Eti chaguo la Mungu. Sijui alikuwa akimaanisha Mungu yupi?

Maswala mengine heri ukae kimya kuliko uropoke.

Tumaini, usiwe na shaka. Mnataka Muislaam, huyo hapo mnaye. Au kwa kuwa alichaguliwa na Wa-Anglican?

NB: Kwa huku Tabora, hata awekwe NYANI wa CCM, Nguruwe wa CCM, Fisi wa CCM, nk so longer ni CCM basi atashinda. Minyamwezi bwana, huwa napata hamu ya KUI-hasi ili kizazi kipotee milele. Utafikiri siyo mijukuu ya Mirambo na Isike.
 
Haya maneno yana ukweli wowote? Yaani kati ya waTz 40 mil ni hakuna!?

ndio maana nimeuliza swali, nani anayeweza kusimama kidedea na JK mwakani akashinda urais??

nchi imenunuliwa kutoka kwa wananchi wenye maradhi ya umaskini na ujinga. Rushwa, ufisadi na ubabe umetawala kwenye chaguzi Upinzani bado haueleweki, ni maluwe luwe tu...

issue ni kwamba JK akisimama kugombea urais mwakani lazima tu atashinda...labda asigombee!!
 
"Nilipokuwa huko nilipima afya yangu na hasa akili na mishipa ya damu na wataalamu wakaniambia nipo salama. Ninatarajia kupumzika baada ya mwaka mpya,” alisema Kikwete. Hata hivyo, alisema pamoja na kuwa hali yake ni salama wataalamu wamemshauri kupunguza ratiba za kazi za kila siku"



Hahahaaaa

Jamaa ameanza kuwa makini kidogo. Angalao ameanza kuhisi kwamba anaweza akawa na matatizo ya akili.

Good stuff
 
SOURCE TBC1
Rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania amesema yote yanayosemwa kuhusu utendaji kazi wa serikali yake ni chuki binafsi kwa mtazamo wangu jamaa huyu ampendi mtu anayemkosoa embu naomba wanajamvi manguli wa siasa za bongo atupe aliyeisikia hii pale Dar int.airport leo
Inawezekana kwa mfumo uliomlea na kumkuuza unao mtazamo wa aina hiyo kwamba kuoneshwa mapungufu yako ni kuchukiwa. Nili-expect kwamba kabla ya kufikia sentenso hiyo, "chuki binafsi" alitakiwa kumwaga kwanza material evidence za utendaji wa serikali yake kuelekea maisha bora kwa kila mtz kisha awaachie wa-handisi wa habari na wananchi wengine wapime kwa utashi wao kama yasemwayo ni chuki binafsi au ukweli juu ya awamu yake.
 
Rais naye hajibu hoja,ishu ya msingi hapa kutuambia ni mambo gani wewe na serikali yako mnaweza kujivunia na kwamba umefikia wapi na maisha bora...si kuanza kutoka nje ya topic na kulalamika kuwa ni chuki.
Tatizo Rais wetu hakubali challenge na anataka aonekane yupo right kwa kutufanyia usanii...km anaongoza watoto vile. Halafu makamba anataka watu wakae kimya kwasababu hayo mamlaka yamewekwa na Mungu.
 
Back
Top Bottom