Kikwete: Tutatumia mkongo kufundishia wanafunzi

Kuna vitu vingine vinahitaji uwe kichwa ngumu kuvitamka mbele ya watu hasa ukiwa kiongozi wa kitaifa.

Hakuna suluhu ya umeme hadi sasa,

IT mjini kwenyewe bado watu wamesinzia, itakuwa vijijini tena kwa watoto wa shule na walimu waliovunjika mioyo?

Haya mengine ni maigizo, kufikia huko tunahitaji kufanya kazi na si maneno ambayo unayesema leo unakuja kuyarudia baada ya miaka mitano kupita.

JK hana jipya
 
kabla ya kusema maneno aiyoyasema. kwanza afanyie kazi suala la umeme na hapo litakapofanikiwa ndo aongelee hayo aliyoyasema. zaidi ya hapo ninamwona kama muuza kahawa.
 
It is pathetic! Kwani ni lazima aendelee kutoa ahadi? Huku Mkulo anahangaika na Budget isiyotosha yeye anaendelea na ahadi zake! Anyway...nina hakika kuna mchongo mahali wa mkopo "wahisani" fulani wanataka kuuza kazi yao na alivyolewa madaraka ameshachekacheka nao tunabandikwa deni jingine hapa. Hata wagagagigikoko walikuwa wamejipanga. Hivi wataalamu/washauri wako wapi? Si ajabu alipotamka hivi kuna watu walitaka kujificha chini ya meza wasihusishwe nae. JK...Give us a break!
 
Kweli Mungu ametujalia Rais.

Hivi hii ahadi si alishaitoa 2 years ago na wa kina MMKJJ wakaichambua sana humu. Sasa amesahau anatuahaidi tena?? Nafikiri dawa ya babu haijafanya kazi eneo fulani.

Sasa kama maji tu ambayo yako bwelele kina kona ya Tanzania yanatushinda, Umeme ambao kutokana na resources tulizonazo za maji, natural gas nk. zinatushinda, I can imajine this??

Ananikumbusha hadithi za abunwasi za kujenga nyumba hewani!!!
 
ili watoto wawe ICT conversant watahitaji ndio kuunganishwa na hiyo national IT infrastructure lakini ili hizi shule ziwe na PC, itabidi ziwe na UMEME

maybe tungeweka wazi policy zetu on SOLAR na other alternative energy

This is just to support you..
hapo ndipo ninapoona maagizo na abunuwasi,unazungumzia kuunganisha shule za serikali kwenye hiyo National ICT infrastructure bila kusema hayo mengine ambayo yatafanya hiyo idea iwe implemented yanakuwa solved vipi??kama ulivyoainisha tunahitaji umeme wa uhakika,tunahitaji PC's za uhakika na technicians...Hapo ndipo na-conclude hizo ni sound tuu hakuna jipya
 
Namshauri JK atafute washauri wenye akili hao jamaa wanampoteza.

Smart B, kutafuta washauri wenye akili unahitaji kuwa na akili, with him I do not think this is possible. Ninajuwa jamaa anashida kubwa sana lakini bado nadhani kwenye hili waandishi wamemnukuu vibaya. Ina maana jk hajuwi matatizo yanayokabili sector ya elimu nchini? Hivi kweli jk anadhani uhaba wa waalimu pekee ndio source ya zile zero zake na Lowasa za form 4?

Ni kama juzi karopoka akiwa TRA eti deputy CAG aajiriwe ili aweze kuaudit vitabu vya hamshauri, hivi ni nani amemwambia ufisadi umekithiri kwa kuwa halmashauri haziauditiwi? Mbona kila mwaka CAG anakuja na report inayoonyesha wizi unaoongezeka kila mwaka na hakuna hatua zinazochukuliwa? CAG wa watu (I feel sorry for him) anasoma report kila mwaka bungeni kinachofuata makofi basi mchezo umekwisha. Imefika mahali sioni tofauti ya CAG na mzee yusuf wa taarabu, tena angalau taarabu inaburudisha nafsi, audit report isiyofanyiwa kadhi haina ladha kabisa. Jk hivi ni lini utaielewa nchi unayoiongoza au mpaka umalize muda 2015?
 
Sometimes it is good to have dreams no matter how long it will take to achieve them

Mnenge, this is over and above normal human dreaming, may be it is hallucination and nausea!! If wishes were horses even beggars would ride
 
It is pathetic! Kwani ni lazima aendelee kutoa ahadi? Huku Mkulo anahangaika na Budget isiyotosha yeye anaendelea na ahadi zake! Anyway...nina hakika kuna mchongo mahali wa mkopo "wahisani" fulani wanataka kuuza kazi yao na alivyolewa madaraka ameshachekacheka nao tunabandikwa deni jingine hapa. Hata wagagagigikoko walikuwa wamejipanga. Hivi wataalamu/washauri wako wapi? Si ajabu alipotamka hivi kuna watu walitaka kujificha chini ya meza wasihusishwe nae. JK...Give us a break!
ni kweli mkuu atuache tupumzike sasa, Tufikilie na mengine!
 
17 March 2011
Fredy Azzah

RAIS Jakaya Kikwete, amesema serikali imebuni mpango maalumu wa kutumia mkongo wa mawasiliano, ili kukabiliana na upungufu wa walimu katika shule za sekondari nchini.

Katika kufanikisha jambo hilo, shule zote za sekondari zitaunganishwa katika mtandao huo ambao utawawezesha mwalimu mmoja kufundisha shule hizo wakati mmoja.

Alisema hayo jana jijini Dar es Salaam alipotembelea Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kukagua utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Januari mwaka 2006 na kutoa maagizo ya kuboresha elimu kwa miaka mitano ijayo.

"Pamoja na kuwa tuna tatizo la upungufu wa walimu kwa jumla, hali ni mbaya sana kwa walimu wa sayansi, mpaka sasa kuna upungufu wa walimu 34,000 na sisi kwa mwaka uwezo wetu ni kuzalisha walimu 10,000," alisema Rais Kikwete.


Alisema ili kukabiliana na tatizo hilo, serikali itaziunganisha shule za serikali katika mkonga wa taifa wakati ikiendelea pia kuzalisha walimu kadri itakavyoweza.

"Kutokana na idadi ya walimu wanaosoma, tatizo la walimu litaweza kwisha baada ya miaka mitatu, lakini sasa pamoja na walimu 10,000 kumaliza masomo yao kwa mwaka, unaweza kukuta bado tuna upungufu wa walimu 40,0000 kwa mwaka," alisema


"Tukiziunganisha shule zetu kwenye mkongo wa taifa ambao mpaka kufikia Juni mwaka huu utakuwa umekamilika, mwalimu mmoja akiwa hapa, anaweza kufundisha wanafunzi wa kemia nchi nzima kwa wakati mmoja." alisisitiza.


Alisema mpango huo ukifanikiwa mwalimu atakaye kuwa yupo kwenye darasa la shule husika, kazi yake itakuwa ni kusimamia wanafunzi kufanya mazoezi na yatakayotolewa na mwalimu aliyekuwa akifundisha kwa njia ya mtandano na kusahihisha kazi zao.


Alieleza kuwa, tayari serikali imeshafanya mazungumzo na kampuni moja ya Kimarekani ambayo itasaidia katika teknolojia hiyo.

"Wameshanionyesha jinsi tutakavyofanya kwenye maeneo ambayo yana umeme na hata yale yasiyokuwa na umeme," alisema Rais Rais pia aliitaka wizara kuweka bayana mipango yake kuhusu namna ya kuinua ubora wa elimu.


My take:

Inaweza ikawa ni kuboresha elimu au wamekurupuka? Hali ya shule za kata wanazifahamu kweli?


JK ni mtu asiye na soni!!! Wameshindwa ku-curb power problem, pamoja na kutuhahakikishia 2006 kuwa tatizo la umeme litakuwa historia, sasa na huu mgawo haya yanawezekana kweli!! waTZ waliounganishwa kwenye umeme hawafika hata 20% Shule za kata nyingi ziko kwenye tatizo la umeme!! Yaani kwa shule za kata kutokuwa na umeme ni jambo la kawaida!!!

JK, JK, JK tusamehe na haya angalau ufanye yanayowezekana...
 
"Wameshanionyesha jinsi tutakavyofanya kwenye maeneo ambayo yana umeme na hata yale yasiyokuwa na umeme,"

STORY ZA ABUNUASI MIXA NA ZA BULICHEKA.
 
Mkuu hii nchi ibadili jina iitwe "The United Republic of Alf Lela U Lela" maana kila kukicha ni vituko.

perfect! Hvi anajua gharama ya bandwidth na vifaa vingne ni kiasi gani? Dawa ndogo sana upande wa ualimu, pandisha mishahara na weka mazingira ya kazi. Kuna wanafunzi wengi wanamaliza vyuo vikuu wanakosa kazi kwa muda mrefu, wape mikataba wafanye kazi. Pia kila mwalimu wa shule ya kata somo analofundisha mwanafunzi akipata A, B na C , mpe nyongeza nono ya mshahara. Me mwenyewe nitakimbia uhandisi nikafundishe kama kaka yangu mtiga alivofanya
 
Ugua maradhi yote lakini ya akili usiombe ndugu yangu.jk ni mwongo asiye na kumbukumbu ndo maana anarudiarudia ahadi alizokwishazitoa which means hana jipya namfananisha na tapeli wa kisiasa na wala siyo msanii kama wengi wanavyomjua.
 
sawa lakni sasa kama bado kutakuepo uhitaji wa mwalim katika shule ili kusimamia na kusahisha mazoezi si jambo linabaki palepale kua tuahitaji waalim??
wakati mwingine nadhani raisi anatamani kui deliver nchi lakini mbinukama hizi ni too advaced kwetu. hap tuweke tu mikakati ya kuzalisha maticha wa kutosha.
 
This is a dream!! mipango ya kukurupuka! ndo hayo ya kuamka na kusema sekondari iwe kila kona ya nchi na wanafunzi 100% wadahiliwe sasa; wakati ukiwa huna walimu. matokeo yake ndo hayo!! sasa ndoto nyingine mkongo in 3 months time; mwalimu mmoja anaweza kuhadharisha (lecture) nchi nzima kwa wakati mmoja (nchi zilizoendelea hawajafikia hatua hiyo). A joke or a day dream!!!!!!!!!!!!
 
Mimi nilijua tu hawezi kupona kwa kikombe cha babu kwa sababu si mtu safi, na msanii hawezi acha fani yake. By the way hivi kanuni zinasemaje kwa rais kuwaongopea raia wake? naomba muongozo.JK lakini tumekukosea nini mpaka unatuongopea mchana kweupe? Au ndiyo kagonjwa kamefika utosini?
 
Back
Top Bottom