Kikwete: Tutatumia mkongo kufundishia wanafunzi

mlaizer

JF-Expert Member
Jan 31, 2011
233
41
17 March 2011
Fredy Azzah

RAIS Jakaya Kikwete, amesema serikali imebuni mpango maalumu wa kutumia mkongo wa mawasiliano, ili kukabiliana na upungufu wa walimu katika shule za sekondari nchini.

Katika kufanikisha jambo hilo, shule zote za sekondari zitaunganishwa katika mtandao huo ambao utawawezesha mwalimu mmoja kufundisha shule hizo wakati mmoja.

Alisema hayo jana jijini Dar es Salaam alipotembelea Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kukagua utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Januari mwaka 2006 na kutoa maagizo ya kuboresha elimu kwa miaka mitano ijayo.

"Pamoja na kuwa tuna tatizo la upungufu wa walimu kwa jumla, hali ni mbaya sana kwa walimu wa sayansi, mpaka sasa kuna upungufu wa walimu 34,000 na sisi kwa mwaka uwezo wetu ni kuzalisha walimu 10,000," alisema Rais Kikwete.


Alisema ili kukabiliana na tatizo hilo, serikali itaziunganisha shule za serikali katika mkonga wa taifa wakati ikiendelea pia kuzalisha walimu kadri itakavyoweza.

"Kutokana na idadi ya walimu wanaosoma, tatizo la walimu litaweza kwisha baada ya miaka mitatu, lakini sasa pamoja na walimu 10,000 kumaliza masomo yao kwa mwaka, unaweza kukuta bado tuna upungufu wa walimu 40,0000 kwa mwaka," alisema


"Tukiziunganisha shule zetu kwenye mkongo wa taifa ambao mpaka kufikia Juni mwaka huu utakuwa umekamilika, mwalimu mmoja akiwa hapa, anaweza kufundisha wanafunzi wa kemia nchi nzima kwa wakati mmoja." alisisitiza.


Alisema mpango huo ukifanikiwa mwalimu atakaye kuwa yupo kwenye darasa la shule husika, kazi yake itakuwa ni kusimamia wanafunzi kufanya mazoezi na yatakayotolewa na mwalimu aliyekuwa akifundisha kwa njia ya mtandano na kusahihisha kazi zao.


Alieleza kuwa, tayari serikali imeshafanya mazungumzo na kampuni moja ya Kimarekani ambayo itasaidia katika teknolojia hiyo.

"Wameshanionyesha jinsi tutakavyofanya kwenye maeneo ambayo yana umeme na hata yale yasiyokuwa na umeme," alisema Rais Rais pia aliitaka wizara kuweka bayana mipango yake kuhusu namna ya kuinua ubora wa elimu.


My take:

Inaweza ikawa ni kuboresha elimu au wamekurupuka? Hali ya shule za kata wanazifahamu kweli?
 
ili watoto wawe ICT conversant watahitaji ndio kuunganishwa na hiyo national IT infrastructure lakini ili hizi shule ziwe na PC, itabidi ziwe na UMEME

maybe tungeweka wazi policy zetu on SOLAR na other alternative energy
 
ili watoto wawe ICT conversant watahitaji ndio kuunganishwa na hiyo national IT infrastructure lakini ili hizi shule ziwe na PC, itabidi ziwe na UMEME

maybe tungeweka wazi policy zetu on SOLAR na other alternative energy

offcource hapa kunahitajika umeme wa uhakika .
 
Got to love JK dreams. It makes you wonder what kind of people he give him this kind of BS. His reasoning capacity is way-way low. He forgot that Tanzania needs to walk before we can run.

By the way, where's my TZS1700.00/1kg of sugar?

Give us a break.
 
serikali itatumia inveter au bettry za panasonic size AA, sipati picha kabisa.............yote hayo nikujaribu kuuzima moto wa mlipuko kwa kikombe cha maji ya nusu lita {km loliondo kwa babu vile} LOOOOOO!! I LOVE JK..........I MEAN JULIUS KAMBARAGE
 
oooh lord have mercy, hawa ndio viongozi mnaotegemea watengeneze viongozi wajau wa bara la Africa. Hata sijui aliiukia wapi angelala huko huko kwanza mbona kazi
 
huyu jamaa ana problem!
Sasa huo mkongo ataukonect vichwani au mgongoni mwa wanafunzi???

Yani anatembelea Wizara ya Elimu
- badala ya kuwabana wamueleze wamejipanga vipi kwa masifuri ya Form Four,
- Tatizo la capitation grant kuchelewa kufika na kufika kiduchu
- Tatizo la walimu - kwa nn sasa serikali imeanza kutoa walimu wengi lakini shule hazina walimu, wamefanya utafiti na kujua tatizo ni nini na wamejipangaje,

The list can go on and on.........yeye anasema wanafunzi wafundishwe kwa Mkongo.

Inasikitisha sana.
 
Nilidhani ni mimi peke yangu. Huo mkongo huo, uunganishe shule zote Tanzania nzima, wakati umeme wa jiji la Dar peke yake umekuwa tatizo sugu.

Mkuu hii nchi ibadili jina iitwe "The United Republic of Alf Lela U Lela" maana kila kukicha ni vituko.
 
Wazo kama hili angelitoa kama nchi nzima hakuna tatizo la umeme, maabara za uhakika na maktaba zenye vitabu vya kutosha, madawati na viti vya kutosha, nyumba za walimu na madarasa ya kutosha na vifaa vya kutendea kazi kwa walimu, hii ni pamoja na mshahara unao kidhi hali ya maisha. Sasa umeme wenyewe tatizo, maabara hakuna maktaba hakuna, madawati, viti, nyumba za walimu, mishahara na vitendea kazi ni tatizo. Halafu unakimbilia mkongo wakati haya madogo umeshindwa kuyatatua.

Hivi nani anayemshauri JK mbona wanamfanya adharaulike na kuonekana kituko mbele ya watu. Sipati picha hao watoto wamekaa chini kwenye sakafu halafu wanasoma kutumia projector kituko cha mwaka. Namshauri JK atafute washauri wenye akili hao jamaa wanampoteza.
 
ili watoto wawe ICT conversant watahitaji ndio kuunganishwa na hiyo national IT infrastructure lakini ili hizi shule ziwe na PC, itabidi ziwe na UMEME

maybe tungeweka wazi policy zetu on SOLAR na other alternative energy

ni ndoto tata kweliiii ni ndoto tata kweliiiiiiiiii nafanya tathmini ni ndoto tata kweli.. hatuwezi na haitakuja tokea may b after the collapse of si si em
 
:A S-omg:hivi huyo rais wenu ana akili timamu? u gotta luv this poor country...

ooooh god help us reach there!
 
Mkwere anapenda sana day dreaming nashindwa kumuelewa anaenda wizara ya elimu na kuanza kuhubiri habari za mkongo huo umeme uko wapi kwanza au watakakuwa wanatumia inverter, ups na battery.

Kwanza badala ya kuwabana wizara ya elimu kuhusiana na matokeo mabovu ya shule za sekondari kuna suala la walimu kushindwa kufika kwenye vituo vyao vya kazi sababu ya kutolipwa pesa zao kwa muda muafaka yeye amekazania mkongo tu sijui alipoenda kutembea huko Silicon Valley basi tokea siku hiyo amekuwa akiota mkongo tu hao SEACOM wenyewe kuna wakati huwa network yao huwa inakata.
 
"Tukiziunganisha shule zetu kwenye mkongo wa taifa ambao mpaka kufikia Juni mwaka huu utakuwa umekamilika"

Ndugu Spika Rais wa nchi anaposema uongo kwa wananchi kanuni inasemaje; leo ni mwezi wa tatu imebakia miezi 3 shule zote zitakuwa kwenye mkongo wa taifa- mkongo wenyewe huko wapi hadi sasa- kwenye mchoro sawa. Fibre iko wapi imeishia whitesand tu; connectivity ipi atatumia? porojo tu- njamani hivi hakuna laana kwa mtu mzima kudanganya!
 
Mmmh!
Tunapenda kukimbilia mambo makubwa wakati madogo yanatushinda.
Walimu hawatotosha kila siku, watu washaamua kuikimbia hiyo fani.
 
Sometimes it is good to have dreams no matter how long it will take to achieve them
 
Back
Top Bottom