Kikwete - Tuhuma nzito dhidi ya CHADEMA


"Wakataeni, hata kama ni wakubwa kiasi gani katika uongozi wa siasa ama wa kijamii. Ni watu hawana maana na hatari wa ustawi wa Taifa letu," alisisitiza.

Hakuna atakayemsikiliza JK tena nchi hii kwa sababu yeye ni Raisi na inabidi atueleze mchango wake kwenye malalamiko yake kwanza kabla ya kutuhubiria........Sisi tunakwenda kwenye uchaguzi kumkataa yeye na timu yake yote ya kifisadi na tunasimika timu mpya yenye unyenyekevu kwetu wapigakura..................CHAGUA CHADEMA CHAGUA DR. SLAAAAAAAAAAAAAA
 
ccm bwana/bibi wana hubiri kupinga rushwa, amani, maendeleo nk, lakini matendo yao yapo tofauti na wanavyo sema.
Naona Kikwete kama kweli Mstaarabu nk ajitoe tu kwenye uchaguzi wa Mwaka Huu awaachie Lipumba na Slaa.
Angalau atabakisha heshima kidogo kwa wananchi na kwa Nchi yetu.

Kwenye red: Mkuu, chunga sana unayotamka. JK hadi sasa hajazungumzia rushwa na ufisadi kwani haoni kabisa kama hilo ni tatizo kubwa kwa nchi hii. Anaogopa kuwaudhi wale wahindi 4.
 
JK achana na mambo hiyo!!!!! Utajimaliza mwenyewe????? Radio na magazeti ya kiislamu(radio imani, magazeti ya annoor na alhuda) yanahubiri udini mkubwa mno huku yakimchafua waziwazi Dr. Slaa(ambaye wao humwita Padre Slaa)!!!! na wakati huohuo yakimpa JK sifa kemkem(hata ambazo hana)....Vyombo hivi vya habari vimediriki kuwaaminisha waislam kuwa makosa yaliyofanywa na marais wastaafu wa kiislam walisingiziwa tu ila hawakufanya wao bali yalifannywa na wasaidizi(au viongozi wenzao) wa kikristo....mfano ni mauaji ya Pemba, na yale ya Mwembe Chai!!!!!! Mbegu hii mbaya ya udini inayopandwa na wenzetu waislam haijawahi kukemewa na serikali hata mara moja!!!!!!! Badala yake, serikali na CCM wamekuwa ikikejeli matamshi yoyote yanayotolewa na viongozi wa dini ya kikristo (e.g., Kakobe and more recently Malasusa) hata kama yanatoa angalizo la kawaida juu ya uchaguzi lisilo na udini wowote!!!!!

Hii inatoa taswira kuwa serikali ya CCM haikerwi na udini unaoipa CCM competitive advantage ya forthcoming election....ila wanakerwa na udini ambao hauifagilii CCM..... Jicho hili la kengeza la JK lidhibitiwe mapema kabla halijaleta mazara kwa taifa.....

Unajua mkuu mimi siku zote nilikuwa nachukulia haya manenoi ni vijembe vya uchaguzi, mambo ya kina Tambwe, Guninita, Nape etc.

Ebo kumbe na raisi wa nchi naye yumo, kwa kweli imenisikitisha sana. Ni bora JK akaondoka na CCM yake lakini atuachie utaifa wetu, taifa letu na the so called amani na utulivu yetu. Anachofanya sasa ni hatari tena si kidogo!!!!!!!!

Athough siamini kama two wrongs can make a right. Hivyo basi kama magazeti ya kiislamu yanaeneza udini yakemewe na yadhibitiwe, the same to anybody, chombo chochote na chama chochote. Na kama ni Slaa ndiye anayeeneza udini, ukabila na umwagajik damu basi achukuliwe hatua mara moja!!!!
 
Raisi jakaya kikwete huwezi kuukimbia ukweli:

1. Unaweza kuleta ushahidi wapi chadema wamehubiri udini na ukabila?....akishindwa achukuliwe hatua!

2. Rais jk anahubiri jambo baya kuliko udini na ukabila! ufisadi...kwa kushindwa kuchukulia hatua mafisadi ...kumekuwa ndio chachu ya kujengeka udini na ukabila...haoni hilo.

3. Angewachukuli a hatua mafisadi papa wa5 tu wa nchi hii leo ageheshimika na heshima hiyo angeweza kukemea udini na ukabila.

4. Kikwete kwa ulegevu wake ata twikwa mzigo wa chochote kitakachotokea kwa taifa hili.historia haitamsamehe!
 
Kwenye red: Mkuu, chunga sana unayotamka. JK hadi sasa hajazungumzia rushwa na ufisadi kwani haoni kabisa kama hilo ni tatizo kubwa kwa nchi hii. Anaogopa kuwaudhi wale wahindi 4.

Chimuko la mgawanyiko na protest ya Watanzania kukumbatiwa kwa makusudi kwa MAFISADI NA WATOA RUSHWA wakubwa.

Umoja wa kitaifa umeanza kumomonyoka kupitia kujengeka kwa kikundi kidigo cha Mafisadi nwakikukbatiwa na Rais.

unategemea wananchi watakimbilia na kujiliwaza na nini kama sio udini na ukabila?

Please its healing at the cause and not at the effect... Tibu ufisadi na rushwa nchi itakuwa moja na hakuna atakaje jali dini wala kabila la mwingine.
 
hana jipya uyo kiumbe cha msingi ni kumfaya out nothing more
 
Mwalimu katika moja ya hotuba zake aliwahi sema yai bovu mimi naweza lijua, na ndivyo alivyo muona huyu jamaa hafai kuwa Raisi wa Nchi pamoja na yule wa Monduli juu, maana madhara yake ni makubwa kama haya tunayo yaona, uwaziri wa mambo ya nje sawa, nk lakini si uongozi wa nchi.
Huyu anafaa kufanya kazi under supervision, bila hivyo , ndiyo haya tunayaona, tunaomba Viongozi wa Juu Alhaji Ali Hassan Mwinyi na Bwana Pius Msekwa , Mkapa muokoe nchi mmumuombe kijana akae chini (ajitoe tu pensheni yake tutampa) lakini wale wengine tunao kama EL RA, Monja, Poteli, pembe za ndovu, wauza unga nk tunao .
uroho wa watu wachache usiharibu nchi.
 
Mi nashawishika kusema kuwa Tz ilikuwa haina kiongozi kwa kipindi cha miaka 5. Mshikaji hajui kuwa yeye ni Rais, hivo hahitaji kuahidi, anapaswa atende! kuhaidi ina maanisha jamaa amepoteza fahamu. Anahitaji kuzinduliwa kwa kufeli uongozi na kuua chama cha kifisadi.
 
[QUOTE

CCM wanavuna walichopanda.[/QUOTE]

Elinino, hii nimeipenda. sasa hivi ni kiwewe tu!!
 
watasoma namba wanaweweseka hawa hawana lolote raisi wa inchi unaongea upupu huuu? huyu jamaa hajawahi kuwa serious huyu kwenye hotuba zake, nani anahubiri dini sasa?chama gani kinahubuiri umwagaji damu kwenye kampeni?shame upon him
 
Kwa nini huyu anaropoka mambo ya uongo namna hii na wananchi hawamzomei? Kwa nini anashindwa kumtaja mtu anayehubiri umwagaji damu au ukabila? Anawadanganya wananchi huku akitumia magazeti ya kijinga kama HabariLeo kueneza hii propaganda yake. It really gets on my nerves... Grhhhh


Totally confused, meli yao inakwenda mrama!!!!!!!!!!!!!!!!
 
haya...yoootee mlochangia sasa tuyaweke kwenye vitendo ifikapo hapo tarehe 31 October!!!:smiling::smiling:
 
hahaaa JK kwa kweli kakamatika haswa...nani kasema anamwaga damu?wapi na lini?hahaa hata utishie watu mwaka huu hushindi ng'o....Umezoea kuchekacheka na kupigiwa kura sasa mwaka huu ni tofauti
 
Kwa mtu yeyote anayetangaza umwagaji damu na hata udini ni dhahiri hatufai katika nchi hii,na katika kufuatilia mchakato mzima wa kampeni za mwaka huu sijawahi msikia kiongozi yeyote akitangaza suala la udini wala ukabila.
Ninachoshangaa ni kuwa JK katoa wapi mambo haya?Au ndio msingi wake wa sasa wa kutaka kura kwa wananchi baada ya ahadi lukuki kutomfanya akubalikea kwa wapiga kura wengi mwaka huu?
Kwa mtaji huu kuhitimishe kwa kusema kuwa JK ndiye mwenye kuleta siasa za udini na ukabila maana yeye ndiye kaanza kuyasema hayo na anautangazia umma kuwa yeye ndiye.
 
Kajisemea Slaa wa watu juzi kuwa mwacheni mzee wa watu apumzike kwa amani ( JK) msimsumbue
 

Kikwete: Wakataeni wanaohubiri udini

Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Lindi;
Source: Habari leo



Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ameonya kuwa umwagaji damu na migawanyiko ya kidini inayohubiriwa na Chadema kutokea baada ya uchaguzi, vitakuwa yenye majuto makubwa zaidi nchini kwa sababu migawanyiko ya kidini itamhusu kila Mtanzania.

Aidha, Rais Kikwete amesema migawanyiko ya kidini itakuwa na athari kubwa zaidi kuliko hata ya kikabila.

“Ile ndiyo itakuwa siku ya giza, siku ya majuto wakati migawanyiko ya kidini itakapotawala katika nchi kwa sababu itamhusu kila mwananchi wa Tanzania,” alisema hayo jana katika mkutano wa kampeni eneo la Nyangao, Mtama, mkoani Lindi.

“Migawanyiko ya ukabila itakuwa kati ya kabila moja na lingine ama kati ya kabila moja na makabila mengine, lakini mgawanyiko wa dini utamhusu kila mwananchi wa Tanzania. Ni mgawanyiko hatari sana,” alisema Rais Kikwete ambaye alifanya kampeni Nyangao, Mchinga na Lindi Mjini.

Alisema mashindano ya sasa kwenye uchaguzi mkuu si ya nani yuko dini gani, au nani anatoka kabila gani. “Yetu ni mashindano ya hoja za kisiasa … ni mashindano kuhusu elimu, barabara, afya, maji … haya ndiyo maeneo ambako vyama vya siasa vinastahili kupambana si kwenye udini, ukabila, vitisho na umwagaji damu.”

Rais aliwataka wananchi kukataa viongozi wa kisiasa na kijamii wanaohubiri ulevi wa umwagaji damu na udini katika kampeni.

“Wakataeni, hata kama ni wakubwa kiasi gani katika uongozi wa siasa ama wa kijamii. Ni watu hawana maana na hatari wa ustawi wa Taifa letu,” alisisitiza.

Alisema ni dhahiri kuwa viongozi wanaohubiri umwagaji damu na udini ni watu ambao wameshindwa siasa na wanarukia dini na ukabila.

Alisisitiza kuwa CCM itaendelea kuhubiri amani, utulivu na upendo miongoni mwa wananchi wa Tanzania, kwa sababu sifa hizo ni muhimu sana ili wananchi waweze kujiletea maendeleo.
“Sisi si chama kinachohangaika kutuma vimeseji vya kupandikiza chuki za kidini kama wanavyofanya wenzetu.”

Kwa kufanya kampeni Lindi, mgombea huyo wa CCM sasa amemaliza rasmi kampeni zake katika mikoa yote ya Tanzania – kampeni ambayo ilifunguliwa rasmi Agosti 21 mwaka huu, kwenye viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam.

Baada ya Dar es Salaam, alikwenda Mwanza, Kagera, Kigoma, Rukwa na Mbeya, Morogoro, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Dodoma kabla ya kuingia mzunguko wa tatu ambao ulimfikisha Iringa, Mara, Mwanza tena, Shinyanga, Tabora, Singida na Dodoma tena.
Mgombea huyo wa CCM pia ametembelea visiwa vya Pemba na Unguja, Ruvuma, Mtwara, Pwani na Lindi.


My Take:

Walianza kukoment kwa mafumbo, chinichini na sasa wameibuka. Kumbe hata zile sms very likely ni mwongozo kutoka kwa JK.

JK sasa ameishiwa, yaani yeye bado ni raisi, Amiri jeshi mkuu halafu anaacha tu watu wanahubiri kumwaga damu na udini??????? Ina maana huyu jamaa haelewi kwamaba anapata upinzani kwa sababu ya poor perfomance na badala yake naamini ni kwa sababu ya dini yake??????? Poor JK, come on this is too low!!!!!!!!!!!!

Hao chadema anaowatuhumu ni akina nani? kwa nini hawachukuliwi hatua? JK pls njoo kwenye mdahalo uwaeleze watz unachoamini na wewe ujibiwe kwa hoja.




Ni jambo jema na la hekima kupinga udini athari zake wote tutazipata
 
Hivi ni mnyama gani yule kabla ya kufa hurusha hujaribu kurusha teke la mwisho????
hawakujipanga vizuri, walijua watu bado hawajaipata ile sumu ya ufisadi, mikataba mibovu, tena wakafanya makosa yanayowamaliza makosa hayo ni kuraaaaaaaaaaaaaaaa za maoooooooooooooooni. Wanataka kukifanya chama kuwa cha genge fulani la wateule wachache wakiwasahau wananchi wa kawaida.
Kama haitoshi, wakaanza siasa za majitaka. Its too bad you know.
 
ama kweli Nchi hii inaenda pabaya, angalia unafiki wa membe jana huko mtama, angalia comments za masheikh wa dar kuhusu gazeti la mwananchi hapo ndo utajua tumefika pabaya sababu ya JK
 
Suala la kukemea udini si la mtu mmoja ni la sisi wote wala si suala la kufanyia dhihaka. Tupinge kauli hiyo lakini tuelewe kwamba linatuhusu moja kwa moja. hapa JF, tunajenga nchi yetu kwa kukosoana bila kujali au kuuliza dini ya mtu ni utamaduni mzuri kwamba wote tupo kwa maslahi ya nchi. kama itatokea ubaguzi wa kidini ni dhahiri hata JF itaathirika.Ni busara tukaendelea kujenga nchi yetu bila kutanguliza udi
 
Back
Top Bottom