Kikwete to USA (May 2009)

- Mkuu Jasusi dataz ziko sawa, anakuja na delegation ya watu 40, kwa hesabu niliyopata jana toka pale kwenye kuchukua viza ya US, na wote hao wanalipiwa hii safari na kodi yetu.

- Halafu mind you kwamba, akifika LA lazima balozi wetu US asafiri kutoka DC na maofisa kama watano toka ubalozini kwenda kumpokea na kusaifi naye ndani ya US, ti is incredible yaani ajabu na kweli!

- Halafu September, atarudi tena huko US, yaani UN kwenye General Assembly! na watu zaidi ya 40.

Mungu Aibariki Tanzania.

FMES

Ndiyo maana hatuendelei. Nchi masikini tunataka matumizi kama vile sisi ni matajiri. Viongozi wenyewe wa magharibi siwasikii waki safiri namna hii. Kama Obama mwenyewe most of the time he is at home na at least afew times per week ataongea na taifa lake kwa njia moja au lingine. The fact is we are poor, huku kutaka maisha tusiyo yaweza yata tuponza.
 
Assuming avarage bei ya round trip ticket kwa delegate mmoja ni $3000, bado subsistence allowance/perdiem, off pocket allowance, outfit allowance. Hesabu yake inaweza fika $ 200,000 more or less.
 
Wajameni, kusafiri pia ni hobby, its my hobby too sema tuu mfuko hauruhusu. Hata ningekuwa mimi, ni kanyaga twende kwa kwenda mbele.
Tatizo ninaloliona ni hili la matumizi ya fedha za umma kufanyia window shopping, then safari nyingine ndio really shopping.
Msiumie na gharama za safari hizo, ni vijisenti tuu, fungu la ukweli ni linalotiwa ndani na sio linalotumika.
Safiri mkulu safiri, endelea kutubembelezea budget support, 2010 Election support na bila kusahau ukarabati wa yale magofu pale mlingotini na mushroom sattelite city ya Subash anayokujengea na airport ndani, bado reli tuu ndio hakuna!.
Safari tamu jamani, Akiwa NY ni Intercontinental labda sasa abadilishe akiwa DC ni Marriot, ni raha tuu za kukuwezesha kusahau shida za nyumbani na kuachana na kelele za mlango.
Safiri baba safiri, wewe ni msafiri kafiri wa safari salama.
 
Rais Kikwete pamoja na Ujumbe wake wanategemea kukutana na Watanzania huko Los Angeles (CA),Kutakuwa na utambulisho na baadaye Rais ataongea na kujibu baadhi ya maswali ya Watanzania waishio huko,Ili kujua utaratibu na venue wasiliana na mratibu wa shughuli hiyo Ms.Assenga au Uongozi wa Watanzania Los Angeles.

Rais atakutana na Jumuiya ya Wafanyabiashara weusi (African American) waishio huko Los Angeles na miji ya karibu na siku ya Jumatano Jioni atahudhuria hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na USDFA,Kutokana na Mchango wake Binafsi wa kupambana na maradhi na kuboresha Ustawi wa Afya ya Jamii Tanzania na Afrika kwa ujumla...Sifa na maneno hayo yapo kwenye kadi ya mualiko wa shughuli hiyo iliyoandaliwa na CEO wa USDFA, Bw.Ted Alemayehu.

Katika ratiba ya awali ilielezwa kuwa Rais alikuwa na safari ya kwenda Houston (TX) kuzindua DICOTA "Diaspora Council Of Tanzanians in US" uzinduzi uliopangwa kufanyika tarehe 20/may...Uzinduzi wa organization hiyo umeaahirishwa mpaka Septemba,Rais atakapokuja tena kwenye General Assembly.Kamati ya Uandaaji wa shughuli hiyo inayoongozwa na Dr.Lennard Tenende imethibitisha kutokuwepo kwa shughuli hiyo.

Siku ya Alhamis Rais atakwenda Washington DC,ambako pamoja na mambo mengine atakutana na Uongozi wa World Bank na Uongozi wa State Department.Pia imeleezwa kuwa Rais atakutana na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa ambaye yupo Washington DC kwenye mkutano wa GLCA "Global Leadership For Climate" Rais Mstaafu Mkapa anatarajia kurudi nyumbani Ijumaa.

Rais Kikwete atamaliza Ziara yake Ijumaa baada ya Mkutano na Naibu katibu Mkuu wa UN ,Dr Asha Rose Migiro.Hii ni mra ya pili kwenye mwezi huu Rais kukutana na Naibu Katibu Mkuu,mara ya kwanza ilikuwa mwanzoni mwa mwezi walipokutana Copenhagen,Denmark.Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa Dr.Migiro amekuwa karibu na siasa za Tanzania katika siku za karibuni.Rais na Ujumbe wake wanamaliza Ziara yao Ijumaa jioni!
 
Hakuna kiongozi ambaye amesafiri kuliko Mwl. Nyerere, unabisha?
Hizi sasa zimekuwa fitina(soma subject matter)

Asafiri nani?

Wale walio safiri na kutuingiza katika mikataba mibovu wana tofauti gani?

We shall hold him responsible if he is entertaining the status quo; That is kama anatuingiza katika mikataba ambayo hayatukuwa yanakubalika, kwa wakati, na kutokuwa na manufaa kwa Wananchii

Kuna wakati nilikuwa na wasiwasi kuwa ehh ohh.. Raisi wetu hayuko, basi leo hatupati umeme-mapolisi watakuwa wanakamtakamata ovyo-kumbe!

Sasa nafikiri Chama kinabidi kijiulize tuna Mwenyekiti kweli? Wa Chama?
Au tunamtu tumemuendoz kwa Urahisi kuwa Raisi? Manake huwa anasafiri hana mda na mambo-'Manung'uniko' ya wanachama=wananchi=Watanganyika=Wazanzibari=Watanzania

Kwa kweli baada ya mda wake kuisha, 'Manung'uniko' ya...Yatakuwa kero, kero hizi ndio tunataka zifanyiwe kazi, Maofisiahadi???? Kama zitakuwa(safari) nje ya manufaa "Ya" Atakuwa the best candidate to sacrifice,wa kwanza,kwa ufisadi-ajiangalie, mark my word!

so what akisafiri?
 
Rais Kikwete pamoja na Ujumbe wake wanategemea kukutana na Watanzania huko Los Angeles (CA),Kutakuwa na utambulisho na baadaye Rais ataongea na kujibu baadhi ya maswali ya Watanzania waishio huko,Ili kujua utaratibu na venue wasiliana na mratibu wa shughuli hiyo Ms.Assenga au Uongozi wa Watanzania Los Angeles.

La hasha bwana/bibi Mwawado. Hapana.

Tunaomba umwambie huyo Ms. Assenga yeye ndio awasiliane na sisi kupitia njia kama matangazo rasmi tovuti ya Ubalozi.

Mrudishie ujumbe, tafadhali, kwamba hatuwezi tukajipanga foleni ofisini kwake au kwenye simu yake ya nyumbani maelfu ya watu tunataka kujua taratibu za ziara.

Hii ni karne mpya, hivi ni vitu vidogo sana kutandawaza habari. Mshindwe hata hayo?
 
Rais Kikwete pamoja na Ujumbe wake wanategemea kukutana na Watanzania huko Los Angeles (CA),Kutakuwa na utambulisho na baadaye Rais ataongea na kujibu baadhi ya maswali ya Watanzania waishio huko,Ili kujua utaratibu na venue wasiliana na mratibu wa shughuli hiyo Ms.Assenga au Uongozi wa Watanzania Los Angeles.

Rais atakutana na Jumuiya ya Wafanyabiashara weusi (African American) waishio huko Los Angeles na miji ya karibu na siku ya Jumatano Jioni atahudhuria hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na USDFA,Kutokana na Mchango wake Binafsi wa kupambana na maradhi na kuboresha Ustawi wa Afya ya Jamii Tanzania na Afrika kwa ujumla...Sifa na maneno hayo yapo kwenye kadi ya mualiko wa shughuli hiyo iliyoandaliwa na CEO wa USDFA, Bw.Ted Alemayehu.

Katika ratiba ya awali ilielezwa kuwa Rais alikuwa na safari ya kwenda Houston (TX) kuzindua DICOTA "Diaspora Council Of Tanzanians in US" uzinduzi uliopangwa kufanyika tarehe 20/may...Uzinduzi wa organization hiyo umeaahirishwa mpaka Septemba,Rais atakapokuja tena kwenye General Assembly.Kamati ya Uandaaji wa shughuli hiyo inayoongozwa na Dr.Lennard Tenende imethibitisha kutokuwepo kwa shughuli hiyo.

Siku ya Alhamis Rais atakwenda Washington DC,ambako pamoja na mambo mengine atakutana na Uongozi wa World Bank na Uongozi wa State Department.Pia imeleezwa kuwa Rais atakutana na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa ambaye yupo Washington DC kwenye mkutano wa GLCA "Global Leadership For Climate" Rais Mstaafu Mkapa anatarajia kurudi nyumbani Ijumaa.

Rais Kikwete atamaliza Ziara yake Ijumaa baada ya Mkutano na Naibu katibu Mkuu wa UN ,Dr Asha Rose Migiro.Hii ni mra ya pili kwenye mwezi huu Rais kukutana na Naibu Katibu Mkuu,mara ya kwanza ilikuwa mwanzoni mwa mwezi walipokutana Copenhagen,Denmark.Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa Dr.Migiro amekuwa karibu na siasa za Tanzania katika siku za karibuni.Rais na Ujumbe wake wanamaliza Ziara yao Ijumaa jioni!

Hiyo ya awali! Na hiyo mpya-Kukutana na 'Weusi'...Kuboresha afya na jamii?

Jamii aliyoiacha hapa Tanzania au huko 'Diaspora'?
 
Kusema ukweli safari hizi zinatutoa jasho la damu walipa kodi wa bongo hasa wale tulioko bongo kwenyewe. Wale mlioko nje kulipa kodi ni option, lakini wale tunaomenyeka hapa bongo, tuko kikaangoni.

Safari kama hizi haziwezi kuwa na umuhimu wowote mbali na kuridhisha ego ya kiongozi wetu. Hamna zaidi.

Katika safari hizi, utajua jinsi nchi inavyoliwa. Hawa watu hulipwa full board wote katika mahoteli ya gharama. In addition kila ofisa hulipwa per diem allowances $300 kwa kila siku.

Jumlisha gharama za ndege n.k. akiamua kuahirisha angalau nusu ya safari zake tu kwa mwaka, na fedha ambayo ingetumika ikaelekezwa pale Muhimbili National Hospital;

1/Tungeongeza idadi ya madaktari na manesi kuweza kuwahudumia wagonjwa. Sasa hivi unakuta ward in wagonjwa kati ya 80 hadi mia ishirini wakihudumiwa na nesi mmoja au wawili.

2/Tungeongeza Majengo ya wards na vifaa pale Muhimbili National Hospital ambapo unakuta wagonjwa wamelala chini wamepangwa kama dagaa kwa wingi wakihudumiwa na manesi waliochoshwa na wingi wa kazi, wenye mishahara midogo, wasiondelezwa na waliojichokea.

Hata mawaziri na viongozi wengine (kila safari ya rais yuko na mawaziri kadhaa). Wengi wao safari zao haiwi published au hazizungumziwi kama hizi za rais. Lakini ukweli ni kuwa viongozi wakubwa wengi hutumia less than 25% of thier time in office. Maana yake ni kwamba more than 75% ya working time viongozi wetu hawako maofisini mwao, wamesafiri!!! Bahati mbaya sana nyingi ya hizi safari ni za nje.

Inabidi tufikie mahala hizi safari ziwe zinakuwa controlled. Kiongozi awe na limit ya kusafiri nje ya nchi. Lakini eee shetani tusaidie, ni nani atakaye fanya hilo ikiwa rais yuko nje siku zote??? We have a sattellite president na inabidi tuwe tunamwangalia hewani siku zote.

Ndio maana serikali hata kile kidogo inachoweza haifanyi!! Bandari ya Dar inaongoza kwa wizi, uzembe na urasimu; Tanesco inaongoza kwa rushwa, uzembe, urasimu na inakaribia kufirisika; Reli imekufa hakuna wa kuizika; Madini waCanada wanabeba bila kodi (mizigo ya kodi inawasakama wafanyakazi na wafanya biashara ndogo ndogo).

Ukitaka kujua kuwa hali si nzuri tembelea ward yoyote pale muhimbili. You will know jinsi tulivyo hoi bin taaban.
 
Na ukiangalia government departments nyingi haziperform si kwa sababu ya mishahara midogo au marupu rupu madogo wanayolipwa wafanyakazi (nakubali hilo ni sehemu ya tatizo), lakini tatizo kubwa zaidi ni kukosa usimamizi. Hakuna supervision at all levels. Viongozi wote wako busy kusafiri nje 'kututafutia misaada'!!!!

Inabidi kwenye election manifesto, hili la kutafuta misaada nje tuwe tunaambiwa. Ili tujue kuwa siku hawa viongozi wasiposafiri woote tunaangamia kwa njaaa.!!!
 
Okay...LA kuna nini hasa anachoenda kufanya? LA ni entertainment capital...mambo ya hollywood, etc. Ingekuwa DC sawa. Huu ni mchanga wa macho.
 
mbinu nyingine.. are you kidding me? Have you ever heard CCM ikisema curbing government spending? kufunga mianya ya extravagances kama iliyoko kwenye ripoti ya CAG au mfumo mzuri wa kodi?

Kwa kadiri misaada inaendelea kutawala hawaoni haja ya kutafuta mbinu mbadala!

On the other hand.. unajua wizi mkubwa wa fedha za umma unafanywa katika trip hizi.? Wakati akiwa anapitia UAE miezi michache iliyopita baadhi ya wapambe walinunua injini za magari yao kuziweka kwenye ndege kwa hela ya walipa kodi wa Bongo.. na JK hajui hilo!

Mwanakijiji na wengineo mimi bado napata tabu sana kwa kweli na sielewi kwa kweli hivi hawa jamaa walipogombea urais walikujuwa ni nini wataenda kufanya huko ikulu kuiendeleza hii nchi na wananchi au waliutaka tu urais then basi? Katika karne hii kuwa na rais ambaye anaamini katika maendeleo ya nchi kwa kutegemea misaada peke yake huko ni kuliwa ndugu zangu.

Mwanakijiji umetaja mfumo wa kodi. Naomba niongeze kidogo, last week kulikuwa na thread hapa ya kodi. Kuna watu kariakoo wanapata 100ml mpaka 1b lakini wanalipa kodi laki 7 mpaka 1m si kwa kuevade no na kwa mfumo mbovu wa kodi tulionao, tax net yetu iko na shida kubwa kupita maelezo. Na kuna dollars kibao tunazipoteza kwenye income tax ya rent income. Wanaomiliki apartments na nyumba nyingine za kupangisha hawalipi income zaidi ya land rent simply kwa sababu kitilya na wenzie wa TRA wamelala usingizi wa pono. Naambiwa kuna survey ilifanywa kuhusu hilo na report ilikuwa submitted miaka imepita sasa hakuna kilichofanyika kama ile kamati ya madini ya kikwete. Na uzembe wa bandarini ndio usiseme. Hivi ccm na kikwete hawayaoni yote haya? So kazi yao nini basi kusafiri tu nje na bakuli la misaada? POLE SANA TANZANIA.
 
napenda kuwatakia heri nyingi na baraka ziwamiminikie kwa wingi kama safari za kikwete nje na ndani ya nchi.
wana jf hoyeeeee
 
Kwa wale mlioko Los Angeles mheshimiwa rais Kikwete anawasili huko Tuesday. Atakutana na Watanzania pia. Atawasili Washington D.C jumatano lakini hana mpango wa kukutana na Watanzania kwa kisingizio kuwa Jumuiya ya Watanzania Washington bado ina mzozano wa uongozi. Atakutana na Hillary Clinton jumatano hiyo na Ijumaa anaingia NY.

Thats what he all knows! let him enjoy but soon he will be accountable! This is not the same Tanzania he think he is ruling.. we need leaders not rulers!
 
Mwanakijiji na wengineo mimi bado napata tabu sana kwa kweli na sielewi kwa kweli hivi hawa jamaa walipogombea urais walikujuwa ni nini wataenda kufanya huko ikulu kuiendeleza hii nchi na wananchi au waliutaka tu urais then basi? Katika karne hii kuwa na rais ambaye anaamini katika maendeleo ya nchi kwa kutegemea misaada peke yake huko ni kuliwa ndugu zangu.

Mwanakijiji umetaja mfumo wa kodi. Naomba niongeze kidogo, last week kulikuwa na thread hapa ya kodi. Kuna watu kariakoo wanapata 100ml mpaka 1b lakini wanalipa kodi laki 7 mpaka 1m si kwa kuevade no na kwa mfumo mbovu wa kodi tulionao, tax net yetu iko na shida kubwa kupita maelezo. Na kuna dollars kibao tunazipoteza kwenye income tax ya rent income. Wanaomiliki apartments na nyumba nyingine za kupangisha hawalipi income zaidi ya land rent simply kwa sababu kitilya na wenzie wa TRA wamelala usingizi wa pono. Naambiwa kuna survey ilifanywa kuhusu hilo na report ilikuwa submitted miaka imepita sasa hakuna kilichofanyika kama ile kamati ya madini ya kikwete. Na uzembe wa bandarini ndio usiseme. Hivi ccm na kikwete hawayaoni yote haya? So kazi yao nini basi kusafiri tu nje na bakuli la misaada? POLE SANA TANZANIA.

A sattelite president hawezi kukaa na watu wake wakakuna vichwa kuona ni jinsi gani wakusanye mapato. Money can be easily obtained by flying where ever provided you have the guts to beg.

Kodi Tanzania ni percentage ndogo ya kodi ambayo ingekusanywa. Wanaolipa kodi Tanzania ni wafanyakazi through PAYE na Wafanyabiashara wadogo wadogo. Wafanya biashara wakubwa hulipa kodi wanazopenda wenyewe. Hii si issue. Issue ni kuwa who cares??

Nyumba zote zilizosajiliwa hulipiwa property tax ambayo ni flat rate (kama sikosei elfu kumi kwa mwaka) na hii haitegemei thamani ya nyumba. Maana yake ni kuwa mwenye two storey residential house Mbezi, hulipia kodi sawa na mwenye kibanda cha vyumba viwili pale manzese.
 
Kusafiri na watu 40, mbona wengi mno? Anyway ni njia mojawapo ya kupeana ulaji.
 
Huyu JMK sasa ni kituko.

Kikwete bila shaka anashauriwa vibaya
ama anadanganywa... na watu ambao hawamtakii mema ama wanafaidika na safari hizo za Kikwete......................

Utasemaje ni kituko wakati umeshamkingia kifua kwamba "anashauriwa vibaya"? Kwamba sio kosa lake, lakini umeandika dissertation nzima kumlaumu. Unajichanganya changanya. Wabaya ni hao "wasiomtakia mema," au?

Hii idea kwamba kila anachofanya Rais ni cha kuambiwa na wengine, washauri, inatoka wapi hii loopy idea hii?
 
Rais
Rais Kikwete atamaliza Ziara yake Ijumaa baada ya Mkutano na Naibu katibu Mkuu wa UN ,Dr Asha Rose Migiro.Hii ni mra ya pili kwenye mwezi huu Rais kukutana na Naibu Katibu Mkuu,mara ya kwanza ilikuwa mwanzoni mwa mwezi walipokutana Copenhagen,Denmark.Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa Dr.Migiro amekuwa karibu na siasa za Tanzania katika siku za karibuni.Rais na Ujumbe wake wanamaliza Ziara yao Ijumaa jioni!

Dr Migiro amekuwa karibu na siasa za Tanzania au Rais wa Tanzania? Nini kimejificha hapa?
 
Huyu JK sasa ni Vasco da Gama. Mbona anapenda sana kusafiri? Hivi budget ya safari za Ikulu kwa mwaka huu haijaisha kweli?
 
Inaelekea Obama hana time ya kukutana na Kikwete
~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*

Rais aenda Marekani kikazi
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 17th May 2009

Rais Jakaya Kikwete aliondoka nchini jana mchana kwenda Marekani kwa ziara ya kikazi ambako atakuwa na shughuli katika miji mitatu ya nchi hiyo, ukiwamo mji mkuu wa nchi hiyo, Washington, D.C.

Wakati wa ziara yake, Rais Kikwete atakutana na kuzungumza na viongozi wa Kampuni ya Teknolojia ya Kompyuta ya IBM mjini San Francisco kuhusu jinsi kampuni hiyo inavyoweza kusaidia zaidi maendeleo ya teknolojia hiyo nchini. Tayari kampuni hiyo ya IBM imetoa wataalamu wa kuanzisha shule ya kisasa ya teknolojia ya kompyuta katika Chuo Kikuu kipya cha Dodoma kutokana na maombi ya Rais Kikwete kwa kampuni hiyo.

Rais Kikwete pia atakuwa mgeni rasmi katika hafla rasmi iliyoandaliwa na Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Madaktari wa Marekani kwa ajili ya Afrika - Doctors for Africa (USDFA) - kwa kushirikiana na taasisi ya Los Angeles World Affairs Council. Hafla hiyo itafanyika mjini Los Angeles.

Katika hafla hiyo, Rais Kikwete atatunukiwa nishani kwa kutambua mchango wake katika maendeleo ya afya katika Tanzania na Afrika kwa jumla. Mjini Washington, D.C. Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa taasisi za kimataifa za fedha kuhusu hali ya sasa ya uchumi duniani na jinsi taasisi hizo zinavyoweza kuisaidia Tanzania kukabiliana na machafuko ya uchumi duniani.

Rais pia atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa idara za Serikali ya Marekani.
Rais Kikwete vile vile atashiriki katika tukio maalumu la kuadhimisha umuhimu wa maji salama duniani la Global Safe Water. Kwenye tukio hilo, lililoandaliwa na taasisi ya Mohan Corporation, Rais Kikwete anatarajiwa kukabidhiwa gari maalumu la kusafisha maji ambalo linaweza kutumika popote iwe mijini ama vijijini.
 
Na nyinyi watanzania ambao mtabahatika kukutana na huyu mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, mwelezeni haya tunayolalamikia.

Sio kwamba hapa tunaonyesha ujasiri, halafu mbele yake tunaufyata.
 
Back
Top Bottom