Kikwete, TCRA, Polisi, UWT mmedhamiria kuisambaratisha nchi yetu?

Kalunguine

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
2,543
134
Hakuna katika wakati mwingine wowote katika historia ya nchi yetu ambapo chombo cha habari kama vile redio Imaan kimeachiwa kufanya uchochezi wa Ki-jinga wa vita vya kidini. Ni katika utawala wa JK tu ndipo gazeti la serikali – Habari Leo likishishirikiana na magazeti ya Uhuru, Mtanzania, Rai na An-nnur vimetumika kuchochea chuki za kidini kwa manufaa ya utawala wa CCM unaomomonyoka kwa sababu ya kuendekeza unyonyaji wa kifisadi kwa wananchi kupitia mikataba feki ikiwemo Richmond, Dowans, n.k.

Bado tunakumbuka jinsi TCRA ilivyoruhusu meseji za kichochezi za Rashid Makame zilizotumwa kwa watumiaji wa Vodacom na Zain bila ridhaa zao wakati wa kipindi cha uchaguzi. Kilele cha uchochezi huo wa kidini unaopigiwa debe na JK kimefikiwa pale Diamond Jubilee. Watu wenye akili wanashangaa, huu ushirika wa JK, TCRA, Polisi, Usalama wa Taifa (UWT) kuacha uchochezi wa kidini kuendelea kupitia Radio Imaan na magazeti tajwa hapo juu kuna manufaa ya nani? Je nchi ikiteketea kwa udini ndiyo JK atafurahi? Hivi intelijensia ya vyombo vya serikali inayosemwa na Siad Mwema iko wapi katika uchochezi huu wa vyombo vya habari? Kwa nini nchi isambaratike katika mikono ya JK kwa minajili ya kufunika ufisadi wa Serikali ya CCM kwa kutumia mgongo wa uchochezi wa Radio Imaan na mlolongo huo wa magazeti?
 
Mkwere anadhani atashinda hiyo vita kirahisi asitegemee hivyo. Asubiri maumivu makali kutokana na mambo anayoyalea
 
Tatizo mkwere hayajui yote haya! kwani anasoma? saizi anacheck zake African Magic akimaliza anasikiliza bongo flavour! mtajiju! si mlimuita chaguo la mungu? kwani aliwaomba? tena wengine mlilala barabarani wakati wa kampeni! mkome na mkomae! mlisikia anatafutwa Tz mr Handsome? mjifunze uraisi sio sura!
 
Kitendo cha serikali kufumbia macho suala hili ni dhahiri kuwa moja kwa moja inahusika.Lakini tujiulize nini hasa dhumuni lao na kwa faida ya nani hasa? Eee mola tuwezeshe watz kutambua hila hizi na hatimae kuwapuuza kabisa....AAMEEEN!
 
Kitendo cha serikali kufumbia macho suala hili ni dhahiri kuwa moja kwa moja inahusika.Lakini tujiulize nini hasa dhumuni lao na kwa faida ya nani hasa? Eee mola tuwezeshe watz kutambua hila hizi na hatimae kuwapuuza kabisa....AAMEEEN!
JK, TCRA, polisi, UWT wamekaa kimya kwa sababu JK amechagua kutumia udini kama kichaka cha kuficha unyonyaji wa waziwazi anaowafanyia wananchi wake kupitia mikataba ya wizi. Ni ubinafsi uliovuka mipaka kwa kuwa hajali hata kama anajenga misingi ya vita vya kidini.
 
Mkwere anadhani atashinda hiyo vita kirahisi asitegemee hivyo. Asubiri maumivu makali kutokana na mambo anayoyalea
Hatashinda lakini anafanya maandalizi ya vita vya kidini nchi kwetu kama ilivyo Nigeria
 
Damu ya watanzania itamlilia daima, hataishi kwa raha tena, sijui kama tuna Rais....
 
Tatizo mkwere hayajui yote haya! kwani anasoma? saizi anacheck zake African Magic akimaliza anasikiliza bongo flavour! mtajiju! si mlimuita chaguo la mungu? kwani aliwaomba? tena wengine mlilala barabarani wakati wa kampeni! mkome na mkomae! mlisikia anatafutwa Tz mr Handsome? mjifunze uraisi sio sura!
Anajua vizuri sana kwani Polisi na intelijensia na usalama wa taifa wanafanya kazi gani? Yeye anajua hata maandalizi ya mkutano wa uchochezi wa Diamond Jubilee.
 
Gooood mpanzi, i concur with mawazo yako.
Mkuu Kikwete ana njia nyingi za kupata habari kuhusu nchi ikiwemo Polisi, usalama wa taifa n.k. Cha kushangaza vyombo vyote vya serikali vimekaa kimya kupalilia udhalili huo
 
It is important kwa hao wanao chochea fujo za kidini Tanzania chini ya kutetea Uislamu kujua kuwa nchi zote za jirani ya Tanzania sii za Kiislamu - Kenya; Uganda & Rwanda are over 85% christian; Congo; Mozambique; Burundi & Malawi are over 75% Christian; Zambia & Seychelles over 95% christian. It is only Comoro which is over 95% Muslim. The nearest countries to Tanzania which are majority Muslim are North Sudan [the South will secede into a new Republic] and Somalia which is a broken state. Agitating for religious chaos in TZ on the pretext of fighting for haki za Waislamu ni hatari sana na inaweza kuzifanya nchi zote jirani zetu kususia Tanzania kama ukoma. Katika miaka tisini kulianzishwa chama cha kiislamu Kenya na sasa kimekufa - I am glad Wakenya waliliona hilo mapema hata huko mkoa wa Pwani [Mombasa] ambako waislamu ni kama 50% of the population.

Very soon the Christians in Tanzania are also going to get tired of these hate radio messages ambazo zinatangazwa in the name ya kutetea haki za waislamu. Nao Wakristo wakianzisha radio zao [and God Forbid they should not do this] basi nchi inaweza kusambaratika. Ni rahisi sana kuwasha moto kuliko kuuzima - wenye hekima wanasema!
 
Dk. Slaa afanyiwa njama kufungwa
• Lengo ni kuwanyamazisha viongozi wengine wa upinzani

na Edward Kinabo


NJAMA nzito zinasukwa ndani ya Jeshi la Polisi, Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake ili kuhakikisha Dk. Willibrod Slaa anafunguliwa mashtaka mapya na kuhukumiwa adhabu ya kifungo jela kwa makosa yanayohusiana na vurugu zilizotokea jijini Arusha hivi karibuni, Tanzania Daima Jumatano limebaini.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka polisi, vigogo wa CCM na serikali wameamuru kuwatisha wapinzani na wananchi kwa jumla, kwa "kumtoa kafara kiongozi mkubwa wa upinzani, kwa mara ya kwanza" kama njia pekee iliyobaki kuinusuru serikali ya CCM madarakani.
Vyanzo hivyo, vinasema njama hizo ni kuhakikisha Dk. Slaa anatiwa gerezani ili kuwatisha na kuwanyong'onyeza viongozi wengine wa chama chake wanaodaiwa kuisumbua CCM na serikali yake kwa kufanya kile kilichoitwa "siasa mpya za kuhamasisha umma kuichukia na kuipinga CCM na serikali ili nchi isitawalike."
Hatua ya Jeshi la Polisi kushirikiana na Idara ya Habari (MAELEZO) kutengeneza na kutangaza video kupitia vyombo vya habari, yenye picha na ujumbe wa kikituhumu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kufanya uchochezi, imetajwa kama njia ya jeshi hilo kujikosha kwa mauaji, na vile vile kujenga mazingira ya kuwatia hatiani viongozi wakuu wa CHADEMA kwa kupalilia propaganda chafu dhidi yao, zisizoeleza chanzo cha kauli zao kali.
Hatua hiyo imekifanya chama hicho kutayarisha mkanda wa video utakaaoonyesha hali halisi ilivyokuwa ili kusahihisha kile ambacho chama hicho kimeita "uchakachuaji wa polisi."
Hata hivyo, baadhi ya wafuatiliaji na wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini wameliambia gazeti hili kuwa serikali "ikifanya kosa la namna hiyo la kufunga Dk Slaa, inaweza kujikuta nchi ikiwaka moto na kulazimisha wananchi kuing'oa serikali madarakani kwa nguvu kama ilivyotokea Tunisia katika siku chache zilizopita.."
"Yeyote aliyewashauri serikali na polisi kufanya hivyo haitakii mema serikali na CCM. Upepo wa sasa kisiasa ni mgumu na mbaya kwa serikali, hivyo inapaswa kufanya maamuzi makini, si kukurupuka; sasa hivi mabavu na dhuluma si mbinu nzuri ya kutumiwa na serikali; vinginevyo yatatokea yasiyotarajiwa," kilisema chanzo kimoja kutoka serikalini.
Katibu mkuu huyo wa CHADEMA pamoja na viongozi wenzake na wafuasi wao 31, walifunguliwa kesi Januari 6 mwaka huu, wakikabiliwa na shtaka la kukusanyika kinyume cha sheria Januari 5 jijini Arusha, siku ambayo chama hicho kilifanya maandamano ya amani kushinikiza kurudiwa kwa uchaguzi wa meya.
Maandamano hayo hata hivyo yalivurugwa kwa nguvu ya silaha na vipigo kutoka kwa Jeshi la Polisi, hatua iliyozusha vurugu na mashambulizi zaidi ya risasi zilizoua watu watatu.
Kesi hiyo imepangwa kutajwa tena keshokutwa katika Mahakama ya Mkoa wa Arusha.
Taarifa zaidi za uchunguzi zinasema vigogo wa CCM na serikali kwa kulitumia jeshi hilo la polisi na mawakili wa serikali, wataongeza mashtaka mapya dhidi ya Dk. Slaa na baadhi ya viongozi wengine wa chama hicho ili mwishowe wahukumiwe adhabu ya kifungo kwani shtaka moja lililopo sasa katika kesi hiyo iliyofunguliwa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, halina nguvu ya kuwapeleka gerezani kama watatiwa hatiani.
Wakati Dk. Slaa akiwa ndiye mlengwa mkuu, njama hizo zinalenga kutumia taratibu za kawaida za kisheria katika kuongeza mashtaka mapya ya kumtuhumu kufanya ‘uchochezi' yeye na wanasiasa wengine watatu ambao alihutubia nao mkutano wa hadhara katika Uwanja wa NMC jijini Arusha jioni ya siku hiyo ya maandamano.
Wanasiasa hao ni mbunge wa Moshi mjini, Philemon Ndesamburo, mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, na kada wao maarufu, John Heche, kutoka Tarime.
"Watadai kuwa Dk. Slaa na wenzake hao watatu walitoa kauli za uchochezi katika viwanja vya NMC na wataishawishi mahakama ione kwamba kauli zao zilikuwa chanzo kikuu cha vurugu zilizotokea Arusha na kusababisha watu wauawe ….na kwa hiyo watajaribu kuwahusisha moja kwa moja na vifo hivyo ili mwishowe waje wahukumiwe kwenda jela kwa kufanya uchochezi uliosababisha madhara makubwa kwa jamii," alisema mtoa taarifa wetu mwingine aliye karibu na baadhi ya wajumbe wa kamati maalum iliyodaiwa kuundwa siku mbili tu baada ya tukio la Arusha ili kufanikisha mkakati huo.
"Hivi sasa wanajaribu kuwaandaa vizuri wananchi kwa kuonyesha picha za video na kutoa machapisho mbalimbali kwenye magazeti ili waamini kuwa Dk. Slaa na viongozi wa CHADEMA ndiyo chanzo cha yote yaliyotokea Arusha," aliongeza.
Hatua ya Jeshi la Polisi kuitisha mkutano na waandishi wa habari kuwaeleza kile ilichokiita "taarifa ambazo wananchi hawajaambiwa kuhusu vurugu za Arusha zilizotokea Januari 5 mwaka huu" imeelezwa kuwa ni sehemu ya utekelezaji wa njama hizo ili kuuandaa vema umma uje unyamazie kile kitakachowafika viongozi hao wa CHADEMA.
Katika mkutano huo, Kamishna Paul Chagonja anayehusika na operesheni na mafunzo katika jeshi hilo, alitumia maelezo ya mdomo, maandishi na picha za video kutoa tuhuma dhidi ya viongozi wa CHADEMA kuwa ndio chanzo cha vurugu zilizotokea Arusha na kusababisha mauaji.
Tukio hilo lilifuatiwa na kurushwa zaidi kwa picha hizo za video katika vituo vya televisheni na redio na kuchapwa kwenye magazeti taarifa nzima ya polisi yenye maelezo hayo ya tuhuma dhidi ya viongozi wa CHADEMA.
Hata hivyo, picha za video zilizoonyeshwa kwa wanahabari wiki iliyopita na hata kurushwa kwenye vituo vya televisheni zilionekana dhahiri kupingana kwa kiasi kikubwa na maelezo na sababu zilizotolewa kama kigezo cha kuyasambaratisha maandamano hayo kwa silaha.
Picha hizo zilionyesha kundi moja tu la viongozi na wafuasi wa CHADEMA lililoanza maandamano kwa amani kutoka eneo ilipo Hoteli ya Mount Meru likitumia njia moja kuelekea Sanawari Mataa na hakukuonekana makundi mengine yaliyokuwa yakitumia njia nyingine kuandamana ambayo yangeleta bughudha na kuwapa polisi shida ya kulinda kama alivyodai kamishna huyo.
Aidha, picha hizo za video pia hazikuonyesha waandamanaji walioanza kufanya fujo au kuashiria kufanya fujo mpaka walipofika eneo la Sanawari Mataa ndipo Jeshi la Polisi lilipovuruga hali ya amani kwa kuanza kufyatua mabomu ya machozi.
Kwa upande mwingine, sinema hiyo iliyorekodiwa na Jeshi la Polisi kuhusu matukio yaliyotokea Arusha ilionekana kuchakachuliwa au kuhaririwa sana kwa kukatwa baadhi ya vitendo vya kikatili vilivyofanywa na askari polisi kama vile vya kumpiga sana na kumdhalilisha kijinsia Josephine Mushumbusi, ambaye ni mchumba wa Dk. Slaa.
Matukio mengine ambayo yalirushwa kwenye picha za vituo vya televisheni hapo kabla lakini hayakuonekana katika kanda hiyo ya polisi ni pamoja na tukio la polisi kuvunjavunja vioo na kuliharibu gari lililokuwa limewabeba Josephine na Mbunge wa Viti Maalum, Lucy Owenya.
Wakati picha hizo, ambazo polisi hawakuzitumia, zilionyesha kuwa vurugu zilianza baada ya polisi kuanza kuyatawanya maandamano hayo kwa mabomu na kuwakamata baadhi ya viongozi na wafuasi wa CHADEMA wapatao 31, Jeshi la Polisi limekuwa likitumia zaidi picha za video za mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya NMC jioni ili kuhalalisha hoja kwamba chanzo kikuu cha vurugu na mauaji yaliyotokea Arusha ni kauli za Dk. Slaa, Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, na wanasiasa wengine waliohutubia mkutano huo.
Picha hizo zilimwonyesha Dk. Slaa na Ndesamburo wakilalamikia kusambaratishwa kwa maandamano yao kwa mabomu, risasi na vipigo vya polisi pamoja na kukamatwa kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho, akiwemo mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, hivyo kuwasisitizia wananchi kuendelea kudai haki ikiwa ni pamoja na kuwatoa viongozi hao polisi walikokuwa wakishikiliwa.
"Kipande hicho cha mkanda wa Arusha ndicho watakachokitumia zaidi katika kuijengea nguvu kesi yao dhidi ya Dk. Slaa na wenzake kwamba walitoa kauli za uchochezi," alisisitiza mtoa habari wetu.
Mwanasiasa mwingine aliyewahi kushtakiwa na kuhukumiwa adhabu ya kifungo kwa kukutwa na hatia ya kutoa kauli za uchochezi ni mwenyekiti wa chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila.
Mtikila alifungwa jela katika gereza la Ukonga, Dar es Salaam Desemba 14, 1999 kwa hatia ya uchochezi na kutumikia kifungo cha mwaka
mmoja.
Mwaka huo alipatikana na hatia ya kutoa kauli chafu na za uchochezi dhidi ya viongozi wa CCM na serikali yake juu ya kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Horace Kolimba.
Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kinondoni, Gabriel Mirumbe, alimtia hatiani kwa maelezo kwamba mwanasiasa huyo alitoa maneno ya chuki dhidi ya viongozi wa CCM na serikali kwamba walimuua Kolimba na ni mashetani.


Dk. Slaa afanyiwa njama kufungwa
 
UWT huwa siwa wasikilizi hata siku moja kwanza kichwa cha mwenyekiti wao kinawaza ngono tuu..............
 
Jamani, mbona mimi sioni udini wowote Tanzania tofauti na madhehebu mengi tu tuliyonayo?
Lets be serious on issues partaining TZ's safari from 3rd world to 2nd world, otherwise we are reversing speedly to what i may call to 4th.
Yaan hadi rais anashadidia kabisaa kila mwezi kuwa kuna udini, hata ambae hakuwa na wazo hilo liaanza kujengeka, then what????????
 
Back
Top Bottom