Kikwete tangaza hali ya hatari - Kiula

Tatizo la hali ya hatari na hizo unazosema imergence laws, zinaweza kukosa macho na kuwakumba hata wasiohusika (inaweza kutumika kulipa visasi). Unaweza kushangaa hata wewe, JF ndani kwani inategemea utashi wa wanaoendesha operation. Ni rahisi kutamka ila shughuli yake ni hatari.

Tunahitaji au vyombo vya usalama vinahitaji meno ya ziada kuwashughulikia mafisadi. Sasa iwapo wao wataenda kuwakamata samaki wadogo hiyo tena itakuwa ufisadi mwingine.
 
"Kiula najiuliza.. nitoke vipi? Ishu ya ufisadi .... mengi wameshaongea kina Slaa...."
Kiula hii jinsi yako ya kurudi kwenye chati inazidi kukurudisha chini.. think better.

Rais hana haja ya kutangaza hali ya hatari kama dhamira yake kushughilikia ufisadi haiko dhahiri. Kama hajadhamiria kushughulika na ufisadi hata akitangaza hali ya hatari inasaidia kitu gani?

Hatuhitaji hali ya hatari kumuuliza Chenge amepataje vijesenti vyake akiwa mtumishi wa umma.
 
i think the guy was joking! HALI YA HATARI!
hali ya hatari tuwekewe kumbe tunawatafuta mafisadi mawaziri 30!!

kupelekwa kizimbani tunakubali, lakini sio hali ya hatari.

jk kila atakaeshutumiwa fisadi ama na vyombo vya habar vya nje au vyama vya upinzani vya tanzania, tafadhali msimamishe kazi na mfikishe mahakamani kwanza.
 
he means STATE OF EMERGENGY? emergency - an unexpected and sudden event that must be dealt with urgently. kwahiyo hili suala la ufisadi ni sudden event ambayo inatakiwa ishughulikiwe kwa uharaka hili kuliondosha? msaada wataalam.
 
asithubutu kutangaza hali ya hatari... ni wazo baya na wazo la hatari kufanya hivyo.
Mkuu Mwanakijiji heshma mbele
Mawazo yangu ni kuwa Mh rais hata asipotangaza hali ya hatari..hali tayari ni ya hatari!Umasikini uko kwenye red line..HATARI!Magonjwa,njaa..vyote viko kwenye hali ya hatari..Mh rais anachotakiwa kufanya ni kupiga signature tu kama kuhakiki!Wananchi ndio wako kwenye hali ya hatari na ni muhimu kwa mh rais kuacknowledge hilo na kufanya marekebisho makubwa ya kisheria na kiuongozi.Kuhakikisha kuwa kunawekwa alertness nationwide kama ya vita vya ukimwi,vita dhidi ya ugaidi..ama issue nyingine tu ambazo zinahitaji kampeni ya uhamasishaji na ushirikishwaji wa wananchi hususan vita hivi dhidi ya ufisadi kwenye wakati huu wa mpito.
 
he means STATE OF EMERGENGY? emergency - an unexpected and sudden event that must be dealt with urgently. kwahiyo hili suala la ufisadi ni sudden event ambayo inatakiwa ishughulikiwe kwa uharaka hili kuliondosha? msaada wataalam.

State of emergency is not just the collection of word but it is a jargon that should not be treated lightly (wanasheria wa JF wanaweza kunisaidia katika legal intrepretation yake). lakini state of emergency inatangazwa when there's coup d'etat yaani hatari ya nchi kupinduliwa etc. Katika kipindi hicho, wannachi wanaweza kupewa curfew yaani muda wa kutoonekana barabarani etc. Kama mtu umeshawahi kushuhudia state of emergency huwezi kulizungumzia kwa mzaha hivyo. Mi nadhani Mr Kiula alishindwa kujieleza vizuri, sidhani kama alitaka wanajeshi watoke kwenye baracks zao na kuingia mitaani kama walivyofanya Comoros!
Ufisadi unaweza kushughulikiwa na mahakama na sheria zetu. Na kama yeye Kiula alipelekwa mahakamni basi anajua kwamba ni kitu kinachowezekana, sasa wanajeshi wanaigiaje hapa?
Kama ni suala la kuwakamata mafisadi na kuwaburuza mahakamani hilo pia linawezekana bila hali ya hatari kutangazwa - where there's a will, there's a way, swali is there a will?
 
Hali ya hatari, mara nyingi, huendana na mambo yafuatayo:-

a. Utawala wa amri (ki-imla)usiozingatia au kuheshimu sheria;
b. Kufishwa kwa uhuru wa vyombo vya habari;
c. Kuundwa kwa tribunals kuchukua mahali pa mahakama;
d. Uongozi wa nchi kutegemea mawazo na utashi wa viongozi waliopo madarakani bila kuwa challenged na chombo chochote;
e. Kupunguzwa kwa Uhuru wa kutembea, kuzungumza na hata kuwaza na kupasha habari;
f. Polisi na majeshi kuwa na nguvu zisizo kifani katika kukamata raia na kuwadhibiti.

Kutokana na hayo, hili la hali ya hatari mmmh! Kiula aje na lingine. By the way, situation kama hii ingekuwepo wakati wa kesi yake angechukua mvua si chini ya 30.
 
Tafsiri yako nadhani ni makini.Na inapelekea kusema ushauri wake siyo!
 
Nitalifafanua hili makala yangu Jumatano na kuliweka sawa ili watu waelewe implication yake na kwanini ni kitu cha kukwepa kwa nguvu zote. Kiula amepotoka kwa hili.
 
Sidhani kama tunahitaji hiyo hali ya hatari kwanirais meshindwa kutumia sheria zililzopo kukabiriana nahicho kinachotaka kutangazwe hali ya hatari. Tukumbuke Kikwete alipongia alianza kulalamikiwa kuwa anawaonea watu naye alijibu kuwa hatungi sheria mpya bali anatumia au amsha zilizopo kihalali. Kwa sababu hiyo hiyo Kiula akumbuke tu kuwa rais haja_exploit wala ku_exhaust all legal means he has at hand. Sheria ya uhujumu uchumi bado haijafutwa. No Kiula we do not need any emergency declaration.
 
Back
Top Bottom