Kikwete siyo Makini: Prof. Anna Tibaijuka hakupaswa kuwa Waziri

Hayo maghala yalikuwepo toka enzi ya Nyerere miaka ya sabini.Je mwaka 1978 Prof.Tibaijuka alikuwa mkuu wa UN Habitat.?

Pili je ni makambi ya jeshi yalijengwa karibu na makazi ya watu au watu walijenga karibu na makambi ya jeshi?
Naomba majibu halafu utajua validity ya thread yako
Je umoja wa mataifa unaruhusiwa kuingilia shughuli za kila siku za serikali za nchi?

Kwenye hoja ya kwamba watu ndo walijenga karibu na kambi za jeshi, napata kigugumizi kuikubali. Maana kwa kusema hivyo, ni sawa na kusema Dar haikupaswa kuwa na wakazi. Maana pande zote za Dar es salaam zimezungukwa na kambi za jeshi zenye silaha. Tuanzie Mbagala, Kigamboni, Mgulani, Tabata (makuburi), uwanja wa ndege, gongo la mboto, upanga, changanyikeni, kunduchi, Lugalo etc. Hadi hapo unaweza kuona kwamba mahali salama kwa maisha ya binadamu kwa Dar es salaam Nzima ni magomeni na manzese tu. Sasa watu milioni nne wote waliopo Dar es salaam wangetosha kuishi Magomeni na Manzese?
 
Ok. Prof. Anna Tibaijuka hakufaa kuwa Waziri.

How about Sophia Simba? Hawa Ghasia? Celina Kombani? Mtoto wa Mwinyi (ambaye ndio muhusika nambari one wa hayo maghala ya silaha za maangamizi) and the list goes on....

Kikwete sio Makini. PERIOD.

Anna is far better when you compare to other JK team members
 
Akiwa katibu mkuu wa UN-Habitat alishindwa kuishauri serikali madhara ya maghala ya silaha kuwekwa kwenye makazi ya raia (kama aliishauri chochote au ninamsingizia aweke ushahidi jamvini). Hata licha ya tukio la Mbagala kutupa fundisho, lakini Professor hakuwa tayari kuona kuwa kuna haja ya kusema japo neno tu.

Tunapozungumzia waziri wa ulinzi kujiuzulu, mimi nasema hata Prof na yeye anapashwa kujiuzulu.

Kwa hiyo ndo kusema JK alikurupuka tu kumteua huyu mama kuwa waziri. JK alipashwa kumuacha tu huyu mama apumzike nyumbani.

mchunga ng'ombe nawasilisha hoja.

Anna Tibaijuka kachaguliwa Director of Executive UN-HABITAT mwaka 2000 hayo maghala unayosema Marais wetu watatu, Mkapa, Mwinyi, Kikwete, wote wameyakuta yameishajengwa, sasa nakushangaa wewe kumshutumu Huyu Mama kwa akili yako unaweza kusema (Japan Quake Tsunami) kashindwa kushauri Japan kujenga vinu vya Nuclear karibu na makazi ya watu, mwisho wa hii Thread yako tumeona chuki zako binafsi dhidi ya Anna Tibaijuka unamuita mchunga ng'ombe, sasa hapa kuna uhusiano wowote kati ng'ombe na maghala ya mabomu nadhani umefyatuka tu na hii Thread yako
 
Tibaijuka ni Fisadi kama Mafisadi wengine.Tibaijuka kwanza kawadhulumu wananchi wa Muleba aridhi yenye hecta zaidi ya 2000 ha,eneo hili liko karibu na hifahi ya pori Biharamulo.Hata kama ana hati miliki je,kigezo cha miliki ya aridhi ni pesa??? kama una pesa basi ndio ununue Tanzania yote???? masikini watafanyaje??? jibu ni kwamba watakuwa watumwa au manamba ,tunaelekea kwenye mfumo wa Ukabaila hii ni hatari sana.Huyu mama ndo tulimtegemea hatusaidie lakini ndo ''Fisadi wa Aridhi''.

Katiba mpya itusaidie katika hili,itamke wazi kuwa mtu amiliki kiasi gani cha aridhi!!!sio kigezo cha pesa alizonazo mtu kidetermine,maana mwisho wa siku vizazi vijavyo vitateseka sana.

''Waziri Kivuli wa Aridhi'' tusaidie kuhusu shutuma hizi za Tibaijuka kunyanganya Wana Muleba Aridhi,Tafadhali njoo Muleba uchunguze .Wananchi wanalalamika chini chini hawana pa kusemea

Waziri aridhi kivuli fuatilia hili!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
CHADEMA futilia hizi shutuma hapo Muleba
 
Ok. Prof. Anna Tibaijuka hakufaa kuwa Waziri.

How about Sophia Simba? Hawa Ghasia? Celina Kombani? Mtoto wa Mwinyi (ambaye ndio muhusika nambari one wa hayo maghala ya silaha za maangamizi) and the list goes on....

Kikwete sio Makini. PERIOD.

asante.
 
Mama Ana Kajenga shule kwenye ardhi ya unyanganyi hapa muleba. Walishiriki ktk kuuza Meli yetu ya Mv Muleba,hatujui hata hela iliyopatikana waliifanyia nini! Yan ni kama meli ilizama kusikojulikana,ni hajabu na inabidi waombe sana,tukija kushika madaraka wakati wako hai watajuta. Mwanzo kabisa mama Anna alivochaguliwa waziri alianza kwa mkwara anavunja nyumba za watu eti viwanja vya wazi,nikawaambia kuna prof.Tibaijuka is not a "waziri material" wachache wakabishi,aya sasa tuambie tangu amekuwa waziri kashaomba likizo?mbona hatumsikii akitenda kazi? Elewa mama alikimbia UN aliposhushwa cheo na kupangiwa kazi chini ya mfanyakazi wake,na kwa kutambua kuwa ajira yake ilishafika kikoma na kufanya kazi chini ya mkataba kawakimbia UN. Kaja kwenye siasa! Tiba isn't dependable.
 
Crap period! Mwenye kufungua hii thread alizaliwa juzi. Hiyo kambi ya jeshi ililuwepo hata kabla makazi ya watu kushamiri karibu na kambi.
Hakuna corelation yoyote kati ya Tibaijuka na makambi.
Uliza historia kabla ya kukurupuka na thread.
 
Akiwa katibu mkuu wa UN-Habitat alishindwa kuishauri serikali madhara ya maghala ya silaha kuwekwa kwenye makazi ya raia (kama aliishauri chochote au ninamsingizia aweke ushahidi jamvini). Hata licha ya tukio la Mbagala kutupa fundisho, lakini Professor hakuwa tayari kuona kuwa kuna haja ya kusema japo neno tu.

Tunapozungumzia waziri wa ulinzi kujiuzulu, mimi nasema hata Prof na yeye anapashwa kujiuzulu.

Kwa hiyo ndo kusema JK alikurupuka tu kumteua huyu mama kuwa waziri. JK alipashwa kumuacha tu huyu mama apumzike nyumbani.

mchunga ng'ombe nawasilisha hoja.

We mpuuzi, inaonekana una fundo na Prof. kafie mbali mpuuzi
 
Wakati tunaendelea na majibizano mwenye taarifa zifuatazo atujulishe wengine;

1. Mafanikio aliyoyapata Prof. Tibaijuka akiwa UN Habitat. Atoe details ya yale yote ya kukumbukwa kama kiongozi.

2. Sababu za kuondoka kwake UN Habitat.

Si suala la chuki kumchambua kiongozi. Hakuna sababu ya kushikana mashati. Tujadili kwa upole na tuwatetee wapendwa wetu na tuwashutumu wabaya wetu kwa hoja zenye ushahidi. Tusiwe wepesi kutetea au kushutumu.
 
Mkuu MsandoAlbero, sababu zilizomtoa Prof. Tibaijuka kule UN Habitat ni issue nyingine kabisa!
 
Consultant,

Nilifikiria hivyo ila sina data za kutosha kwani nakumbuka iliwahi kuripotiwa kwenye the East African kuhusu kuondoka kwake.

Kama unakumbuka hebu irushe hewani tujadili. Nitajitahidi kuchimbua kwenye archives tuone.

Naamini yeye mwenyewe angependa kuainisha mafanikio yake kwa muda aliofanya kazi huko lakini ameipigia kimya sasa sijui kwa nini. Au aliwaeleza wananchi wa Muleba?

GSANA, hebu tusaidie katika hili kamanda.
 
Anna Tibaijuka kachaguliwa Director of Executive UN-HABITAT mwaka 2000 hayo maghala unayosema Marais wetu watatu, Mkapa, Mwinyi, Kikwete, wote wameyakuta yameishajengwa, sasa nakushangaa wewe kumshutumu Huyu Mama kwa akili yako unaweza kusema (Japan Quake Tsunami) kashindwa kushauri Japan kujenga vinu vya Nuclear karibu na makazi ya watu, mwisho wa hii Thread yako tumeona chuki zako binafsi dhidi ya Anna Tibaijuka unamuita mchunga ng'ombe, sasa hapa kuna uhusiano wowote kati ng'ombe na maghala ya mabomu nadhani umefyatuka tu na hii Thread yako

umekurupuka wewe.

mchungang'ombe ni mimi; siyo Prof.

simshutumu. hata kama ningemshutumu si kama Prof. Anna; ningemshutumu kama Executive Secretary wa UN-Habitat. upo?

kwa nini hakutumia nafasi yake nyeti kwenye shirika la makazi kupaza sauti kuzionya serikali kutunza maghala ya silaha kwenye makazi ya watu hasa baada ya tukio la Mbagala?
 
We mpuuzi, inaonekana una fundo na Prof. kafie mbali mpuuzi

nina haki kuzungumza dukuduku zangu kwa kiongozi wa nchi yangu. huwezi kuninyamazisha. mabomu yalikuwa kwenye makazi ya watu na yeye alikuwa kwenye shirika linalohusiana na makazi ya watu. ndo maana alikwenda kibera enzi ya vurugu za uchaguzi kenya na tulikuwa tukimsikia bbc akizungumzia kuhusu makazi na usalama wa watu. hii ya mabomu vipi?

kama alipitiwa aseme.

hakuna chuki binafsi hapa wala fundo.
 
Mbona hujakanusha nilichosema, umetukana na data huna.

Kwamba Tibaijuka alikula hela za mradi zilizotolewa na Sweden. Mmewe akiwa balozi Stockholm akafungua tawi la umoja wa wanawake ubalozini ku channel fedha za mradi. Wa Sweden wakasikia umoja wenyewe umekuwa tata huku Tanzania, na umefutwa, wakati wao wanatoa hela. Kuuliza wakaambiwa Tibaijuka hakufata taratibu na alishindwa kazi, na wakati anapokea hela zao mradi ushafutwa.

Tibaijuka alipewa kazi na hela ya kuandika Katiba ya umoja wa wanawake usofungamana na CCM, akashindwa. Siku ya presentation alichofanya akagawa copy and paste ya Katiba ile ile ya Umoja wa Wanawake wa zamani imebadilishwa jina, na mengine machache ambayo hayakufata hadidu za rejea alizopewa. Serikali ikamwambia umeshindwa kazi hapo hapo Nkurumah Hall, chuo kikuu.

Tibaijuka akaeneza kwamba serikali inapiga vita umoja wa wanawake.

Serikali ndio ilim contract Mwalimu Tibaijuka kutoka chuo kikuu kuandika katiba ya umoja wa wanawake mpya. Serikali hiyo hiyo ingewezaje kumpinga? Na Serikali hapa tunaongelea Wizara ya Wanawake, ambayo siku zote inaongozwa na wanawake. Wanawake wapingeje umoja wao? Wao ndio walimpa kazi akashindwa, na hela kala na Katibu wake.

Sweden wakamuandama balozi Stockholm, mme wa Anna. Mambo ya Nje wakamrudisha wizarani. Akaugua shinikizo la damu, akafa.

Ni vyema kabla hujaleta hoja yako ifanyie utafiti yakinifu Kwa kadri ninavyofahamu BAWATA ilishasajiliwa nakuanza kazi ikilenga uwakilishi wa mwanamke wa kitanzania bila kujali itikadi ya chama kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa. Na kweli walishajizolea wanachama kibao. Kina Anna Abdala kutoka UWT wakaisi kufunikwa na BAWATA wakahaha baada yakuona kasi ya BAWATA wakaanza propaganda za kuwa BAWATA ina muundo wa chama cha kisiasa wakaishawishi serikali kukifuta na kweli serikali ikakifuta BAWATA wakaenda mahakamani baada ya miaka mingi wakashinda kesi. Kuhusu kula hela za Waswidishi naomba udhibitisho.Hivi kama kweli agelikuwa amefuja hela zao UN ingemteua kwenye kazi kama ile na Waswidish wasilalamike? Je wakati yuko UN-HABITAT kama alitoa ushauri kwa serikali ambayo tunajua fika si sikivu ikaukataa ushauri wake yeye angefanyaje na wewe na mimi tungejuaje kama ameshauri au hakutoa ushauri? Na ushauri wake ulitegemea kuukuta hapa jamvini? Vilevile si kweli kwamba mmewe alirudishwa wizara ya mambo ya nje akitokea Sweden alipotoka huko alipelekwa USSR baadae Kenya.
 
Tibaijuka aliwahi kufanya ufisadi Umoja wa Wanawake.

Wengi hawakuelewa undani wa sakata lile walimwona Tibaijuka kama heroin kwa sababu alipojaribu kupotosha mada alisema serikali inapinga kuanzishwa kwa umoja mpya wa wanawake ulio huru kutoka CCM.

Tibaijuka alifuja hela zilizotolewa na wa Sweden kuanzisha umoja wa wanawake. Wakati huo mmewe ni balozi wa Sweden. Tibaijuka unalijua hili ndani ya dhamira yako na una bahati hukufunguliwa mashtaka.
sasa wewe unaojua undani mbona hauweki wazi?Au na wewe umetumwa na Asha Rose Migiro kumharibia huyu mama'etu mchapakazi kiasi hata Wakenya walimkubali na kufikia kupinga kutolewa kwake UN Habitat.Anna Tibaijuka ana heshimika sana duniani kama mchapakazi na mtu mwenye msimamo ndio maana hata aliyeanzisha post ameshindwa kabisa kupata weak link ya kujaribu kumchafua mwishowe ameishia kutoa hoja za aina ya Makamba and the likes.
 
Mama Ana Kajenga shule kwenye ardhi ya unyanganyi hapa muleba. Walishiriki ktk kuuza Meli yetu ya Mv Muleba,hatujui hata hela iliyopatikana waliifanyia nini! Yan ni kama meli ilizama kusikojulikana,ni hajabu na inabidi waombe sana,tukija kushika madaraka wakati wako hai watajuta. Mwanzo kabisa mama Anna alivochaguliwa waziri alianza kwa mkwara anavunja nyumba za watu eti viwanja vya wazi,nikawaambia kuna prof.Tibaijuka is not a "waziri material" wachache wakabishi,aya sasa tuambie tangu amekuwa waziri kashaomba likizo?mbona hatumsikii akitenda kazi? Elewa mama alikimbia UN aliposhushwa cheo na kupangiwa kazi chini ya mfanyakazi wake,na kwa kutambua kuwa ajira yake ilishafika kikoma na kufanya kazi chini ya mkataba kawakimbia UN. Kaja kwenye siasa! Tiba isn't dependable.
hebu tuambiae aliuza meli in what capacity?Unajua kisa cha huyu mama kutoka UN?Kiongozi yeyote makini lazima ajue wakati wa kung'atuka...ulitaka aendelee kuwa chini ya junior appointee pale UN after years spent as a senior most director hapo Nairobi!
 
Ni vyema kabla hujaleta hoja yako ifanyie utafiti yakinifu Kwa kadri ninavyofahamu BAWATA ilishasajiliwa nakuanza kazi ikilenga uwakilishi wa mwanamke wa kitanzania bila kujali itikadi ya chama kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa. Na kweli walishajizolea wanachama kibao. Kina Anna Abdala kutoka UWT wakaisi kufunikwa na BAWATA wakahaha baada yakuona kasi ya BAWATA wakaanza propaganda za kuwa BAWATA ina muundo wa chama cha kisiasa wakaishawishi serikali kukifuta na kweli serikali ikakifuta BAWATA wakaenda mahakamani baada ya miaka mingi wakashinda kesi. Kuhusu kula hela za Waswidishi naomba udhibitisho.Hivi kama kweli agelikuwa amefuja hela zao UN ingemteua kwenye kazi kama ile na Waswidish wasilalamike? Je wakati yuko UN-HABITAT kama alitoa ushauri kwa serikali ambayo tunajua fika si sikivu ikaukataa ushauri wake yeye angefanyaje na wewe na mimi tungejuaje kama ameshauri au hakutoa ushauri? Na ushauri wake ulitegemea kuukuta hapa jamvini? Vilevile si kweli kwamba mmewe alirudishwa wizara ya mambo ya nje akitokea Sweden alipotoka huko alipelekwa USSR baadae Kenya.

Unasema mimi nifanye utafiti yakinifu halafu wewe unaanza na "kwa kadri ninavyofahamu." Tunataka ukweli, sio "kwa kadri ninavyofahamu..." Hatuongelei usajili wa Bawata. Nimeongelea alivyokula hela za wa Sweden. Hicho kitu hukijui ndio maana umeniomba uthibitisho. Kwa hiyo usiniambia sijafanya "utafiti yakinifu."

Tibaijuka alikula hela za kuandika Katiba, Katiba hakuandika, siku ya ku present Nkurumah Hall wakamsimamisha katikati kwa sababu ilikuwa ni copy and paste ya Katiba ya zamani.

Wa Swedish hawakupinga uteuzi wake UN kwa sababu hela walimkabidhi mumewe ambae alifungua tawi la umoja wa wanawake ubalozini Stockholm ku channel pesa, bila kujua mkewe anazifisadi Dar-es-Salaam. Hivyo wakampinga Balozi Tibaijuka mwenyewe mpaka akaondolewa, akapewa dawati wizarani, akaugua shinikizo, akakaa siku chache akalala na babu zake. Na mikono ya Anna itahesabiwa hukumu juu ya damu ya mumewe na hela za watozwa ushuru wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom