Elections 2010 Kikwete: Sijawahi kunyonga

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
RAIS Jakaya Kikwete amesema, tangu aingie madarakani Desemba 2005, hajawahi kuidhinisha kunyongwa kwa mtu yeyote.

Kikwete amesema, atatoa uamuzi wa kunyongwa au la kwa watu waliotiwa hatiani kwa kuua albino, suala hilo likifika mezani kwake.

Rais Kikwete alibainisha hayo juzi kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa, wakati akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni kuomba achaguliwe tena kuongoza Tanzania.

“Tuliendesha kura za maoni hapa juu ya suala la watu wanaoua albino.Baada ya kura hizo, wengine wanachunguzwa hadi sasa, wengine wamefungwa na mahakama,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:

“Baada ya hukumu ya mahakama, baadhi ya viongozi wa albino wamenitumia ujumbe na kutaka wale waliohukumiwa kunyongwa, niwanyonge.

“Sijawahi kunyonga hata mtu mmoja tangu niingie madarakani, lakini nitaamua suala hilo likifika mezani kwangu.”

Mahakama Kuu ya Tanzania katika mikoa ya Mwanza na Shinyanga, imetoa hukumu za kifo hadi kunyongwa mwaka jana kwa watu wapatao saba ambao iliwatia hatiani kwa mauaji ya albino.
 
RAIS Jakaya Kikwete amesema, tangu aingie madarakani Desemba 2005, hajawahi kuidhinisha kunyongwa kwa mtu yeyote.

Kikwete amesema, atatoa uamuzi wa kunyongwa au la kwa watu waliotiwa hatiani kwa kuua albino, suala hilo likifika mezani kwake.
Je huyu mbunge wako utamnyonga?

CCM yapitisha aliyetajwa kuuza viungo vya Albino

HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM) iliyokutana Dodoma kuchuja na kupitisha majina ya wagombea wake wa ubunge, imepitisha jina la mgombea ubunge aliyewahi kupigiwa kura na wanakijiji akitajwa ni muuaji na mnunuzi wa viungo vya maalbino, Raia Mwema imebaini.
 
Hii inathibitisha ni jinsi gani nchi hii isivyothamini utawala wa sheria. Na hili linafanywa kwa kusudi mahsusi, la kumweka mtu mmoja juu ya sheria za nchi. Kwani katiba ya nchi iliyo sheria mama ambayo rais anaapa kuilinda inasema je kwa mtu atakaethibitika kwa mashahidi kumuua mwenzie kwa makusudi? Hivi inatofautisha nafsi ya albino na ya mwingine aliyethulumiwa uhai?. Kwa mtizamo wangu huu ndio wakati muafaka wa kuibadili sheria ya kifo ama sivyo tumshtaki Rais kwa kutotekeleza majukumu yake ya kikatiba na hasa kutoupa thamani utawala wa sheria.
 
Mbona aliyetakiwa kumnyonga (MZURIMZURI),alishajifia mwenyewe. Sasa angemnyonga nani? Zombe et al,walikosea kwa makusudi kuiflame kesi,akapuruchuka.
 
kwa hiyo anajisifu kwa kuvunja katiba ya JMT. Na basi kuna haja gani ya sheria ya hukumu ya kunyonga???? Tukisema katiba iandikwe upya CCM wanasema iliyopo inatosha, kutekeleza hawataki. Anasema Jaji Mkuu Augustine Ramadhani?
 
ameshanyonga,kuua mara nyingi na tena anaendelea kufanya hivyo kila siku,kitendo cha kila baada ya dakika 5 mtoto 1 anakufa kwa malaria si kunynga huko?kila wakina mama laki moja wanaojifungua 520 wanakufa sio aina nyingine ya unyongaji ya kikwete?kima cha chini dhaifu cha mishahara kwa wafanyakazi kinachowapelekea kuwa na maisha kama ya popo si kuwanyonga wafanyakazi na familia zao?
 
..kwa hiyo hii nayo ni ahadi ya uchaguzi?

..je, ipo kwenye ilani ya CCM au anajisemea tu?
 
ameshanyonga,kuua mara nyingi na tena anaendelea kufanya hivyo kila siku,kitendo cha kila baada ya dakika 5 mtoto 1 anakufa kwa malaria si kunynga huko?kila wakina mama laki moja wanaojifungua 520 wanakufa sio aina nyingine ya unyongaji ya kikwete?kima cha chini dhaifu cha mishahara kwa wafanyakazi kinachowapelekea kuwa na maisha kama ya popo si kuwanyonga wafanyakazi na familia zao?

Mkuu tuweke kumbu kumbu sahihi, Si kila baada ya dakika 5, bali kila baada ya sekunde 30 mtoto mmoja hufa kutokana na malaria

Nukuu za WHO WHO | 10 facts on malaria
 
fafanua kuhusu hili mkubwa Kamuulize Mange Kimambi kilichompata baba yake. Hata Erick Shingongo alitaka kuandika lakini AKADUMA (akala kona).Nafikiri wengi wamekufa INDIRECT.
 
Suala ili linaonyesha wazi kuwa nchi hii ipo chini ya utawala bora na utawala wa sheria..,kudhaniwa au kushukiwa kwamba umetenda kosa haina maana kwamba unastahiki kuukumiwa kwa kufanya kosa.,kuna tofauti kubwa kati ya kushukiwa na kutenda kosa..,haiwezekani mtu akanyimwa haki zake za kikatiba eti kwa kuwa anadhaniwa kutenda kosa fulani. Suala la kunyonga ni hukumu ya mwisho baada ya hukumu zote kuonekana hazikidhi kulingana na ukubwa wa kosa.,wapo wanaoona kuwa hukumu hiyo haina tija kwa jamii hasa ukizingatia mtu hapatiwi muda wa kutubia na kutumika kiuzalishaji,ingawa siungani nao sana katika hilo. kikwete anamamlaka ya mwisho kisheria kuidhinisha ikiwa mtu ameshahukumiwa kunywongwa mahakamani.,tujaribu kuwa waelevu wa mambo jaman....!
 
suley
  • profile.png
Join Date Tue Aug 2010
Posts 1

Karibu sana JF hatudanganyiki!
 
Nenda kamuulize Mange mwenyewe..... Kuna blog yake anaweza kukujibu. Kwa ufupi ni kuwa baba yake hayupo hai.
fafanua kuhusu hili mkubwa Kamuulize Mange Kimambi kilichompata baba yake. Hata Erick Shingongo alitaka kuandika lakini AKADUMA (akala kona).Nafikiri wengi wamekufa INDIRECT.
 
Suala ili linaonyesha wazi kuwa nchi hii ipo chini ya utawala bora na utawala wa sheria..,kudhaniwa au kushukiwa kwamba umetenda kosa haina maana kwamba unastahiki kuukumiwa kwa kufanya kosa.,kuna tofauti kubwa kati ya kushukiwa na kutenda kosa..,haiwezekani mtu akanyimwa haki zake za kikatiba eti kwa kuwa anadhaniwa kutenda kosa fulani. Suala la kunyonga ni hukumu ya mwisho baada ya hukumu zote kuonekana hazikidhi kulingana na ukubwa wa kosa.,wapo wanaoona kuwa hukumu hiyo haina tija kwa jamii hasa ukizingatia mtu hapatiwi muda wa kutubia na kutumika kiuzalishaji,ingawa siungani nao sana katika hilo. kikwete anamamlaka ya mwisho kisheria kuidhinisha ikiwa mtu ameshahukumiwa kunywongwa mahakamani.,tujaribu kuwa waelevu wa mambo jaman....!
Umepiga hodi kwanza kwenye jukwaa la utambulisho au wewe ni mzoefu hapa?
 
Back
Top Bottom