Kikwete Rais bora Tanzania kuzidi waliomtangulia

wanajamvi nawasalimu:

Nimewaza mda mrefu nikaona niweke slide hii maana nimeona ipo sawa kuifikiria sisi kama great thinkers:

Kikwete ni Raisi bora kuliko wote waliomtangulia hapa tanzania kwa sababu zifuatazo ( upo free kuongeza )

1. Amepanua democrasia kwa kiasi kikubwa hadi sasa hadi kijijini wanaujua ubaya na udhaifu wa serikari yetu.
2. kila chombo cha habari chaweza kuandika tuhuma hata kama ya jinai inayoihusu serikari pasipo kuchukuliwa hatua
3. amewafanya watu kuipenda sana CDM kuliko CCM hata waliomo CCM wanapenda kuwa katika chama Makini CDM lakin ndo hivo matumbo yao bado yana njaa.
4. asilimia 80 ya Raia wa Tanzania wanachukizwa na utawala wake ila wengine hawana jinsi wanaogopa kutema Vibarua

Kwa kuwa Kikwete alikuta System ikiwa vile lakin wananchi hawaelewi hivo akaona hawez nyamaza wakati wananchi wanaumia kwa mda wote, niyafanye haya yote, nioneshe kuwa mie ni dhaifu sana ili watu waanze kugundua na kujua nini kilichokuwa kinafanyika Ikulu ya Tanzania miaka ya nyuma.
Kwa Point hizo nahis Kikwete ni Raisi Bora Kuwazidi akina Mkapa, Mwinyi na Nyerere.

Ni kweli ndio maana hata yule tajiri wa sudan mo ibrahim anafikiria kumpatia zawadi/tuzo.
 
Heshima kwenu wanajamvi.

Mheshimiwa JK akitumia uzoefu na uelewa wake juu ya chama cha mapinduzi alijua kabisa ccm haiwezi na haitaweza kumtoa mzalaramo wa kimanzi chana,mkwere wa Chalinze mzee,Mluguru wa Mvua,Mgogo wa Kilangali,Mnyiramba wa San siro,Msukuma wa Ikigijo na Mzigua wa Mkanyageni kutoka kwenye ufukara,ulofa na upumbafu,akaamua kufanya mabadiliko.

Mheshimiwa sana Jk akaanza attempt namba moja kwa kuanzisha mchakato wa katiba mpya kinyume na ilani ya chama chake,mchakato ulienda vizuri hadi kutupatia rasmu ya pili ya katiba,waroho wa madaraka ndani ya ccm wakamjia juu Jk huku wananchi tukishindwa kabisa kumpa support na ushirikiano Mh.Jk. Mheshimiwa akajikuta yupo pekee yake,akazidiwa,akavunjwa moyo na kugeuka,ila namshukru Mungu hakukata tamaa.

Likaja suala la ESCROW,JK akaamua kulishughulikia kisanii ili kutuongezea hasira yetu dhidi ya ccm (Kumbuka hutuba yake pale airport) ni dalili nyingine inayoonesha dhamira nzuri ya Jk kwa nchi yetu.

Sasa Jk kaja na attempt nyingine kwa kutupatia Mh.Lowasa ili asaidie kukiondoa hiki kikundi kinachoitwa ccm ,kikundi cha waroho,walafi na wahujumu uchumi wa nchi yetu.

This time,please wananchi tunaombwa sana tusimuangushe,tumpigie lowasa kura zetu zote za ndiyo.
Kumbukeni ccm kulikuwa na potential candidates wengi including akina Salim A.Salim but aliwachinjia baharini na kutuletea mbeba vyuma mr.Magufuli ili kazi iwe rahasi kwetu.

NITAKUKUMBUKA SANA MH.JK.Mungu akulinde na kukutia nguvu

MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU MBARIKI JK,MUNGU UBARIKI UKAWA
 
Ni Kweli: Maana aliongeza deni letu la taifa kutoka trilioni 10 mpaka trilioni 40 katika kipindi chake cha miaka 10 ya utawala.
 
Ni kweli..... tutamkumbuka kwa kusamehe wahalifu waliochota pesa zetu Benki Kuu (EPA), kwa kuwa na mfumo mbovu wa usalama hadi twiga, simba, tembo na kadhalika wanapitishwa uwanja wa ndege KIA na kwenda Qatar, kwa kushindwa kusimamia raslimali ambazo zingewafanikisha wananchi.. nk. Kwa kweli tutampkumbuka kwa mengi aliyotufanyia watz
 
Asingefanya hayo leo tusinge taka mabadiliko,asante kwa kukubaliana na hoja yangu
 
Kundi la Wanamtandao lilianzishwa 1995 Kwa ushirikiano wa Jk, EL, Kingunge, Rostam, Sitta na usaidizi wa Kijana Mdogo Emmanuel Nchimbi. Mwaka huu October 25 Taifa linaenda kuzika Rasmi Mtandao. Na wote waanzilishi wa Hili Genge watastaafu na kustaafishwa kwa Maslahi mapana ya Nchi. Genge zima limestaafu kwa hiyari kasoro mmoja anaesubiri kustaafishwa kinguvu.Viongoz wote waanzilishi wa hili Kundi inapaswa watuombe Radhi kwa kugeuza Nchi kama Champions League
 
Heshima kwenu wanajamvi.

Mheshimiwa JK akitumia uzoefu na uelewa wake juu ya chama cha mapinduzi alijua kabisa ccm haiwezi na haitaweza kumtoa mzalaramo wa kimanzi chana,mkwere wa Chalinze mzee,Mluguru wa Mvua,Mgogo wa Kilangali,Mnyiramba wa San siro,Msukuma wa Ikigijo na Mzigua wa Mkanyageni kutoka kwenye ufukara,ulofa na upumbafu,akaamua kufanya mabadiliko.

Mheshimiwa sana Jk akaanza attempt namba moja kwa kuanzisha mchakato wa katiba mpya kinyume na ilani ya chama chake,mchakato ulienda vizuri hadi kutupatia rasmu ya pili ya katiba,waroho wa madaraka ndani ya ccm wakamjia juu Jk huku wananchi tukishindwa kabisa kumpa support na ushirikiano Mh.Jk. Mheshimiwa akajikuta yupo pekee yake,akazidiwa,akavunjwa moyo na kugeuka,ila namshukru Mungu hakukata tamaa.

Likaja suala la ESCROW,JK akaamua kulishughulikia kisanii ili kutuongezea hasira yetu dhidi ya ccm (Kumbuka hutuba yake pale airport) ni dalili nyingine inayoonesha dhamira nzuri ya Jk kwa nchi yetu.

Sasa Jk kaja na attempt nyingine kwa kutupatia Mh.Lowasa ili asaidie kukiondoa hiki kikundi kinachoitwa ccm ,kikundi cha waroho,walafi na wahujumu uchumi wa nchi yetu.

This time,please wananchi tunaombwa sana tusimuangushe,tumpigie lowasa kura zetu zote za ndiyo.
Kumbukeni ccm kulikuwa na potential candidates wengi including akina Salim A.Salim but aliwachinjia baharini na kutuletea mbeba vyuma mr.Magufuli ili kazi iwe rahasi kwetu.

NITAKUKUMBUKA SANA MH.JK.Mungu akulinde na kukutia nguvu

MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU MBARIKI JK,MUNGU UBARIKI UKAWA

Dakika 5 anazotumia Lowasa Jukwaani kuomba Kura hazitoshi kutushawishi, pamoja na makandokando aliyonayo hafai kua Rais wa Nchi hii.
 
Kundi la Wanamtandao lilianzishwa 1995 Kwa ushirikiano wa Jk, EL, Kingunge, Rostam, Sitta na usaidizi wa Kijana Mdogo Emmanuel Nchimbi. Mwaka huu October 25 Taifa linaenda kuzika Rasmi Mtandao. Na wote waanzilishi wa Hili Genge watastaafu na kustaafishwa kwa Maslahi mapana ya Nchi. Genge zima limestaafu kwa hiyari kasoro mmoja anaesubiri kustaafishwa kinguvu.Viongoz wote waanzilishi wa hili Kundi inapaswa watuombe Radhi kwa kugeuza Nchi kama Champions League
Mkuu 54 years ya uhuru nchi hii bado ina import mchele,ngano,mashudu ya soya beans.sukari nk.Miaka 54 ya uhuru 80% ya watanzania bado ni masikini,42% ya watoto wa Tanzania wana Udumavu,haya yanatokea huku 40% ya ardhi yetu ikiwa inafaa kwa kilimo na only 8% ndiyo inalimwa,huku serikali ccm ikiwekeza zaidi kwenye siasa badala ya ujuzi na maarifa ya watanzania, namba ya wasio jua kusoma na kuandika inaongezeka,wewe unakuja na habari la genge la mwaka 1995?Huko nyuma ccm ilishindwa nini?Pole sana
 
Dakika 5 anazotumia Lowasa Jukwaani kuomba Kura hazitoshi kutushawishi, pamoja na makandokando aliyonayo hafai kua Rais wa Nchi hii.
Mkuu actions speak more than words.ila nisikushangae sana ccm wameshakuaminisha katika porojo.
 
Kikwete na CCM yake kabakiza siku 28 pale Magogoni
JK aliahidi kuwa rais wa mwisho kuongoza Tanzania na watanzania masikini.Awamu ya tano ni awamu ya ELIMU,ELIMU,ELIMU.ELIMU kwa maana ya ujuzi na maarifa na hivyo kutufanya tuondokane na umasikini wa akili na ulofa wa kufikiria nchi hii itajengwa kwa misaada na kuomba omba toka kwa wazungu
 
mkuu hii ni gia ya reverse lakin itatupeleka tu. tukianza na sera ya uwazi na ukweli hii alianzisha mhe Ben na aliweza kuisimamia vizuri sana na ndio maana nzi zake kulikuwa na limitations za uwazi na kadhalika ingawa pia waandish wa habari hawakunyimwa habari.

Kikwete ni muhanga wa uovu aliourithi toka enzi za nyerere hadi leo ila pia mimi ningepewa nafasi ya kumshauri ningesema haya:
1) kikwete umekuwa mlegevu sana hasa katika usimamizi wa taifa hili kiasi kwamba kila mtu anakuja na lake na wewe unalisikiliza na kutaka kuliimpliment bila kulifikiria kiundani sana. Mfano mzuri hapa ningempa juu ya ya huu mradi wa magari yaendayo mwendokasi. binafsi sioni tija yake kama nia ni kupunguza que kwend amjini kwani pia magari hayo hayata punguza msongomano wa kutatua tatizo la msongamano wa magari. hainiingii akilini serikali inagharamia mabilion ya sh kujenga barabra tok jangwania hadi kimara tu kitu ambacho bado jangwani watu hawajafika mjini. mfano posta. ama kimara bado hujatoka nje ya dar. ingekuwa mimi ningesema hapana hebu tu improve bara bara za pembezoni ili tuwwe na matoleo mengi kwenda na kutokea mjini kuliko kung'ang'ania hii moja ambayo inapitisha magari mengi na katibu yote yaendao mikoa ya tz kasoro visiwani na lindi na mtwara.

2) CDM haijatumia udhaifu wa CCM ili kujipatia maarufu la wametumia sera, na mfumo uliokubalika toka chini hadi juu so hata kama ccm ingekuwa imara ila kwa kazi CDM iliyofanya ili kujitangaza imatosha kuipatia umaarufu mkubwa sana na si tu ndani bali hata nje ya nchi.

3) ubadhirifu tunaouona kwa serikali si kwamba kikwete ameufanya utokee bali ni kwamba sekta nzima ya record keeping na secrecy katika taifa hili ilivyozorota. huwez ukawa ni mtu wa records usijue confidential recods zinakaa wapi na mafail ya kawaida yanakaa wapi. hii inatokana na kuajiriwa kwa watu ambao hawana maadili ya kazi hainiinii akilini kwamba kapuku kama mimi naweza kwenda wizarani na nikapewa nyaraka muhimu za serikali hii pasi hata mtu kuona vibaya..pia usiri kati ya wale wanaokaa naye nao unahusika sana tu. unamkuta mtu hana usiri ni mnafiki, mpenda rushwa na vyakula kiasi kwamba hana kifua cha kuhifadhi vitu. ulaya ili upate siri ni kazi sana unless umamuekea vifaa vya kumnasa akiongea.
naona kwamba hapa nitasema sana. naomba niwasilishe.

Anachoongea MAGUFULI majuakuani tuseme nini kwa mfano?
 
wanajamvi nawasalimu:

Nimewaza mda mrefu nikaona niweke slide hii maana nimeona ipo sawa kuifikiria sisi kama great thinkers:

Kikwete ni Raisi bora kuliko wote waliomtangulia hapa tanzania kwa sababu zifuatazo ( upo free kuongeza )

1. Amepanua democrasia kwa kiasi kikubwa hadi sasa hadi kijijini wanaujua ubaya na udhaifu wa serikari yetu.
2. kila chombo cha habari chaweza kuandika tuhuma hata kama ya jinai inayoihusu serikari pasipo kuchukuliwa hatua
3. amewafanya watu kuipenda sana CDM kuliko CCM hata waliomo CCM wanapenda kuwa katika chama Makini CDM lakin ndo hivo matumbo yao bado yana njaa.
4. asilimia 80 ya Raia wa Tanzania wanachukizwa na utawala wake ila wengine hawana jinsi wanaogopa kutema Vibarua

Kwa kuwa Kikwete alikuta System ikiwa vile lakin wananchi hawaelewi hivo akaona hawez nyamaza wakati wananchi wanaumia kwa mda wote, niyafanye haya yote, nioneshe kuwa mie ni dhaifu sana ili watu waanze kugundua na kujua nini kilichokuwa kinafanyika Ikulu ya Tanzania miaka ya nyuma.
Kwa Point hizo nahis Kikwete ni Raisi Bora Kuwazidi akina Mkapa, Mwinyi na Nyerere.

Ahsante kwa uzi mwanana. Unajua tatizo sio Kikwete kama binadamu,tatizo ni mfumo wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali.Nakumbuka JMK alipoingia madarakani alijitahidi sana kubadili mfumo,lakini aliishia kupigwa vita na kutishiwa "Mamlaka" yake!!Ninafahamu hawezi kutamka wazi kuwa CCM haifai,lakini utaona kwa Vitendo vyake na amesema wazi amechoka na anataka kupumzika.
ONDOA CCM KWA MANUFAA YA TAIFA
 
Hata mie naamini Rais Kikwete ndiye Kiongozi bora nchi hii imewahi kupata. Mbali na Mwalimu Kupigania uhuru, Ukombozi wa Afrika na vita ya Uganda. Mhs Rais Kikwete kakumbana na changamoto nyingi sana na kwa kiasi kikubwa amekabiliana nazo kwa ufanisi. Historia itamkumbuka na Watanzania ambao hawafuguka macho sasa hivi akili zitawarudia atakapokuwa amestaafu. Kafanya mengi katika uongozi wake na Mungu Ambariki
 
Ukawa ni wataalam wa kubadirisha CD kweli,, siasa za propaganda ndizo zitakazoiua CDM,, poleni sana team EL, ila kwenye mioyo yenu mnajua kwanini mnampenda el,, mimi binafsi namkubali magufuri kiutendaji?? kwa maslahi mapana ya taifa CHAGUA MAGUFURI,,, mioyo yenu inajua ni sababu zipi mnazo kumpenda El,, ila van wengi najua maslahi binafsi na wenzangu na mimi wafuata mkumbo/kelele au tunawaita oyaoya...
 
Porofesa kabisa,dokita kabisa JAKAYA MRISHO KIKWETE Oyeeeeee
TEZI TUME Oyeeeeeee
 
Back
Top Bottom