Kikwete: Pamoja na utoto wake, kijana alifanya kosa kubwa kukojolea msahafu!

Naomba kuelimishwa jamani, mtoto alikojolea msaafu au juzuu(kitabu cha watoto wa kiislamu wanachojifunzia madrasa)
 
Kama kweli JK hajakemea hiki kitenda atakuwa anaiharibu nchi yetu..inapofikia hatua ya watu kuvamia nyumba za ibada kama ishara ya kuonyesha hasira zao na Rais anakaa kmya ujue tunajitafutia laana kwa nchi.

Ni wamoja, yupo pamoja nao kama sio nyuma yao!
 
Kichwa cha thread kimeandikwa "Kikwete: Pamoja na utoto wake, kijana alifanya kosa kubwa kukojolea msahafu!

Mie nikaona huyu Kikwete hajui kwamba swala la utoto ni la kisheria hapa? Ngoja niangalie anavyochemka!

Kusoma habari hamna sehemu yoyote inayoshabihiana na kichwa hicho! Naona Kikwete anasihi waislamu kuwa wavumilivu etc etc.

Hivi hii ni lack of comprehension au uchochezi wa makusudi?

All of the above!
 
Waliobomolewa makanisa hata hawamjui yule mtoto. Hiyo kesi ilimuhusu huyo dogo na familia yake iliyokosea kumlea. Haikumhusu Askofu Marasusa. Wale waliovunja makanisa ni wenye akili timamu zaidi ya yule mtoto kwa makusudi walishuka mno na kuamua kufikiri kwa kiwango cha chinii sana kama yule mtoto. Jaziba zikitawala akili hushindwa kufanyakazi yake ipasavyo.
sasa watoto wa kikristo wanalelewa wapi?si kwenye Sunday schools?na makanisani,kipaimara,ubatizo...nk?
 
Mkuu sidhani kama ni najisi kuliko nguruwe, nina rafiki zangu wengi tu waislamu, wanakula nguruwe na kunywa bia, issue hii ni vizuri ikielezwa kwa ukweli.

bongo,usichanganye muislam na muumini wa kiislam,,,,,,,pia usichanganye mkristo na mmumini wa kikristo,,,,,,
muumin wa kiislam na wa kikristo anasali,na hanywi pombe,kwa ujumla hafanyi yote alokataza ALLAH,,,,,sasa ukisema wanakunywa bia sawa,waislam wanakunywa bia sikatai,lakin waumin wa kiisalm hawanywi bia,hawali nguruwe,hawazini,,,,,the same to waumin wa kikristo,
 
Huyu naye!!! Lingekuwa kosa KUBWA kama angefanya hivyo mwenyewe kwa ku initiate jamblo hilo. Lakini pale alikuwa anatoa ushaidi kuwa mwenzake anachosema ni uongo. Na kwa umri wake ni age za kujaribu mambo JK elewa hivyo au hujawahi kulea watoto uone jinsi wantavyo behave? Ndo maana hata yule aliruhusu quran ikojolewe akiamini mwenzie atadhurika. Mtu anayekasirika wakati mantiki iko wazi anafikiria chini ya kiwango cha watoto hao.
 
Kwa ushauri wangu mdogo tu,ninewaasa waislamu au walimu wa Madrsa wasiwaogopeshe watoto wanapotaka kuwaeleza kuhusu umuhimu wa vitabu vitakatifu,siyo Quaran tu vitabu vyote bibilia n.k.

Wawaeleze umuhimu wa vitabu hivyo na kwa nini ni vitakatifu na havitakiwi kuchezewa,na siyo kuwadanganya matokea yake watoto wanajaribu je ni kweli ni kifanya hivyo?

Leo amefanya mtoto mkristu kesho atafanya mtoto wa kiislamu na atakwambia alitaka kujua je ni kweli atabadilika kuwa kichaa,chizi ,mjusi au shetani?

Ni kama kwanye unyago na jando mwisho wa siku watoto wanajribu.Ona soma la biologia mwisho wa siku mwanafunzi wa kidoto cha kwanza anajaribu je nikifanya hivi kitatokea?
Tuwaelimishe na siyo kuwaogopesha watoto.
 
Bukyanagandi, kufanya kosa sio kosa bali kurudia. Huyo mtoto alifanya kosa kukojolea kuran, lakini kitendo cha watu wazima (wazazi) kuchoma majengo ya kanisa kinadhalilisha (a)utashi wa wazazi katika jamii yetu (b)inaharibu kabisa uislam. Naamini uislam ni mzuri kabisa ila kuna watu wameiteka hii dini kwa sababu zao.

Hadi sasa sijaelewa ni utashi gani huo kwa watu wazima kutaka kumkamata mtoto wa miaka 14 ili wamuue kwa sababu amekojelea kitabu cha dini? Hivi kuna kufilisika kwa hekima zaidi ya hapo?

Lakini kubwa ambalo nadhani ndugu zangu waislam wanatakiwa wajiulize ni hili, watoto wao wanafundishwa nini kwenye madrass zao? Chanzo cha ugomvi huu tunaambiwa ni mtoto mmoja alimwambia mwenziwe kuwa akikojolea kuran atageuka mjusi. HuyO (mwenye kuran) alipata wapi hayo maneno? Nani alimwambia kuwa mtu akikojolea kuran anageuka mjusi? Na huyo mtu atakuwa amefundisha uwongo kiasi gani?

Hapa unaweza kuona kizazi kinavyokuzwa na mafundisho yaliyopinda. Na hawa ndio watoto tunaotegemea wawe taifa la kesho!

FJM, nakubaliana na analysis yako 100% - mkuu nilizungumzia kuhusu Bush Jr ili kuwekea msisitizo kwamba Uislaam kama Uislaam sio tatizo, tatizo liko kwenye wahumini wachache ambao ni fanatic by default , wako overly bellicose bila sababu za msingi!

Mkuu hapa chini nimekuwekea maoni yangu niliyo andika hapo mwanzo kuhusu suala la Mbagara, ukiangalia kwa karibu utaona maoni yako yanarandana karibu sana na ya kwangu.

Mkuu, ukiangalia kisa kizima mtu unaona wazi wazi kwamba tukio hili ni la kupanga - si bahati mbaya wala nini sijuhi! Kilicho fanyika pale ni kumtegea bwana mdogo afanye kosa, hivi mtoto atakuwa na interest gani ya kubeba quran iliyo andikwa kwenye lugha ambayo ni ngeni kwake, walikuwa na uhakika gani kama mtoto si mpagani? Kwa nini hawakwenda kulalamika kwa wazazi wake? Makanisa yanahusika kivije na michezo ya watoto wadogo, repeate "watoto WADOGO?"

Wote tumepitia phase ya utoto, ni jambo la kawaida sana watoto kuwa Curious/inquisitive hasa wakielezwa jambo ambalo linaonekana ni kama mihujiza kwao, watafanya lolote wanalo ambiwa ili wa-quench kiu yao ya kuona mahajabu, katika mizingira kama hayo watoto wanakuwa wahanga wa kutumiwa vibaya na watu wazima wenye ajenda zao za SIRI.

Hizi vurugu za Mbagara zilikuwa zinafukuta kwa ndani kwa muda (juzi juzi walikuwa wanagombania sijuhi makaburi sijuhi ya kuzika mtoto mdogo kama sikosei!).

Walicho kuwa wanatafuta kwa muda mrefu ni kisingizio TU cha kuanzisha ZALI kwa kusingizia matendo ya watoto wadogo wasio tafakali MAMBO, walifikili Wakristo watahamaki na kutaka kulipiza kisasi hivyo kuwapa mwanya wakutimiza hidden agenda walizo kuwa nazo kwa muda mrefu! Ukweli wa mambo ni kwamba lengo lao limeshindwa miserably.

Labda nimalizie kwa kusema kwamba si waislaam wote wenye fikila za kutaka kuvuruga amani ndani ya TAIFA letu, bahati nzuri ni kwamba Marais Waislaam walio wahi kuongoza TAIFA letu ni wazalendo na weledi wanao tafakali mambo hawa-entertain fanatism zisizo kuwa na MSHIKO, oh yes "akili za kuambiwa wanachanganya na za KWAO" - matokeo yake TAIFA linabaki shwali bila labsha na ma-fanatics wanahishia in a SLAMMER.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Baba wasamehe hawajui walitendalo, wivu wa maendeleo yetu ndio unawasukuma kuharibu makanisa yetu na mali zetu, wivu wa kutokujituma na kuleta maendeleo katka maeneo yao ya kuabudu ndio unawafanya wafanye hivyo.
 
bongo,usichanganye muislam na muumini wa kiislam,,,,,,,pia usichanganye mkristo na mmumini wa kikristo,,,,,,
muumin wa kiislam na wa kikristo anasali,na hanywi pombe,kwa ujumla hafanyi yote alokataza ALLAH,,,,,sasa ukisema wanakunywa bia sawa,waislam wanakunywa bia sikatai, lakini waumini wa kiislamu hawanywi bia, hawali nguruwe, hawazini,,,,,the same to waumin wa kikristo,

Mkuu umeongea jambo la maana sana. Lakini niongeze tu kuwa muumini wa kiislamu hawezi kuunga mkono vitendo viovu vya mtu anayetumia jina la uislamu, muumini wa kiislamu asingeweza kufanya vurugu na kupiga watu. Lakini issue ni kuwa angalia kilichopo, waliofanya vurugu hizo wanasifiwa na kupongezwa, hakuna anayeoneshwa kuchukiza. Angalia hao waliofanya vurugu kama kweli hawazini, hawali ngurue, hawanywi bia, si vibaka and all evils that can be said of Mbagala, halafu uchambue.

Niambie itakuwaje kama siku mkristo anavamia msikiti kwa madai kuwa mtoto mwislamu amechoma biblia, kila ukipita kwenye mihadhara ya waislamu utasikia msururu wa matusi dhidi ya wakristo....nadhani utakuwa umesikia makafir ni kina nani, lakini ni nani wanaosema, ni waislamu au waumini wa dini ya kiislamu?
 
wana bodi.
Takribani wiki sasa lile sakata la quran ya wa islam kukojolewa tokana na mizaha iliyofanywa na watoto wa wili,moja toka iman ya kikristo na yule wa pili toka kwa waislamu.walisababisha mihemuko na kutoweka kwa amani na kuvumiliana kwa jamii mchanganyiko inayoishi pamoja tangu ukoloni.

Wana jf.kwa maoni yangu watoto hawa wote wanahusika moja kwa moja na tukio hilo.Naomba kufahamishwa yule mtoto wa kiislam aliyeshiriki mzaha na yule mwingine wa kikristo naye angali mahabusu?

Na kama hajakamatwa je haki iko wapi! Kwani wote wawili walisababisha taharuki ya kidini nchini. Huyu naye lazima atiwe mbaroni.ili haki itendeke. Kabla ya kumhukumu yule mtoto wa kikristo ambapo limefanyika kwamba hakupaswa kufanya hvyo. (KWANI HIYO NI SAHIHI HAKUPASWA KUKOJOLEA KITABU CHA DINI YA WAISLAMU).

Huyu naye atiwe mbaroni aungane na mtoto mwenzake ili wajutie matendo yao waliyofanya.kukamatwa yule wa kikristo pekee haki iko wapi!.
 
Kama kweli JK hajakemea hiki kitenda atakuwa anaiharibu nchi yetu..inapofikia hatua ya watu kuvamia nyumba za ibada kama ishara ya kuonyesha hasira zao na Rais anakaa kmya ujue tunajitafutia laana kwa nchi.
Raisi wetu ameelezewa kuwa na udini. Si ajabu anyaona yaliyotokea ni "jihad" ambayo kwa Imani yake ni halali. Mtoto Akikosea anakanywa na Hilo linaishia hapo. Katokana na tabia yake hasa ya mahusiano na wanawake mbalimbali inawezekan Mheshimiwa Raisi hakukanywa alipokua mdogo na Hilo linamfanya asielewe kwamba mtoto akishika kinyesi hakatwi mkono.
 
Tatizo ni kwamba uki-post kitu, au kuchangia kitu kwenye mijadala ya udini unajikuta kwa kukusudia au kwa kutokusudia (automatically) unachangia kuchochea vita hii nchini..! people should really think twice before going on with this discussion. hali sio nzuri, ila kuendelea kujadili haya mambo kunachochea zaidi na kujenga hasira miongoni mwetu. amini usiamini kila mtu anaiona dini yake kuwa ndo ya kweli! Elimu na historia inahitajika sana zama hizi. we were very peaceful before, with our lands, gold and all forms of resources, but other guys came with all their bibles and quran, now we have all the bibles and quran, and they took all our lands and gold! shame. now we are fighting for their quran and bibles!
 
Back
Top Bottom