Kikwete: Pamoja na utoto wake, kijana alifanya kosa kubwa kukojolea msahafu!

Mjenda Chilo

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
1,467
513
Too soft, hamna hata karipio au order.

Mh. Rais kaishia kuongelea ushauri aliowapa.

Amewataka waislam kutochukua maamuzi haraka wanapokuwa wamekasirika.

Amesema, pamoja na kuwa kijana ni mdogo lakini alifanya kosa kubwa kukojolea msaafu.

Chanzo: Leo hotuba ya Nyerere day
RAIS Jakaya Kikwete, amesema kuwa licha ya tukio la kijana wa Kikristo kukojolea kitabu kitakatifu cha Kuran kuudhi, lakini vurugu za kulipiza kisasi kwa kuchoma makanisa zinapaswa kuepukwa kwa vile si suluhu ya tatizo.

Akihutubia katika kilele cha kuzima Mwenge wa Uhuru, sherehe zilizokwenda sambamba na kumbukumbu za maadhimisho ya miaka 13 ya kifo cha Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, mjini Shinyanga, Rais Kikwete alisema amechukizwa na hatua za watu kujichukulia sheria mkononi.

Kauli ya rais inakuja ikiwa ni siku tatu tangu vurugu kubwa kutokea eneo la Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam na kusababisha makanisa saba na magari kadhaa kuharibiwa, baada ya mtoto Emmanuel Josephat (14) kudaiwa kukojolea kitabu hicho kitakatifu kinachotumiwa na Waislamu.

Rais Kikwete aliwaeleza wananchi kuwa ametembelea eneo hilo na kusisitiza kuwa kitendo hicho cha viongozi wa dini kuwahamasisha wafuasi wao kujichukulia sheria mkononi hakikuwa sahihi, kwa sababu kijana huyo alifanya tendo hilo bila kushurutishwa na kundi wala mtu yeyote.

Aliongeza kuwa iko haja ya wafuasi hao kujizuia na kutuliza hasira zao kwa kutafakari kwanza kwani hata kijana mwenyewe tayari alikuwa mikononi mwa Jeshi la Polisi.

"Kitendo cha kundi hilo la waumini wa Kiislamu kuingilia kazi za vyombo vya dola hakikuwa sahihi, kwa sababu kimesababisha mambo ya kusikitisha na yasiyokuwa na maelezo ya kujitosheleza ndani ya jamii.

"Niliwasihi kuwa pamoja na hasira walizokuwa nazo wawe na subira na kuvumiliana wakati viongozi wa dini zote mbili wanapojiandaa kukutana na kufikia muafaka," aliongeza.

Rais Kikwete aliwataka wananchi wajiepushe na vitendo vya kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani katika nchi, hivyo akawashauri wasichukue uamuzi wa hasira wakati wa tatizo kwa sababu kwa vyovyote vile ni lazima watadondokea kwenye makosa.

Alisema vijana 122 wanaodaiwa kutoka kundi la harakati za Kiislamu wakiwemo 36 vinara wakuu wa vurugu hizo, wanashikiliwa na polisi.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete aliwahamasisha Watanzania kuendelea kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao kwenye tume inayoratibu maoni bila kushawishiwa kwa ulaghai wa aina yoyote, kwamba hiyo ni haki na utashi wa kila mtu.

Akemea rushwa
Rais Kikwete katika hilo, aliwataka wananchi wote kuchukua jukumu la kupambana na vitendo vya rushwa pasipo kuwaachia kazi hiyo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Alisema vita hiyo ni ya kila mtu huku akiwapiga vijembe wale wanaolalamika uwepo wa vitendo hivyo pasipo kuchukuwa jukumu la kuwataja hadharani wahusika ili wachukuliwe hatua.

"Kama tunaendelea kulalamikia rushwa bila kuwataja wala rushwa haiwezi kutusaidia kuitokomeza. Rushwa ni hatari hasa inapoingia hata kwenye vyombo vya kusimamia sheria na kutoa haki," alisema.

CCM watoa kauli
Wakati huo huo, Chama Cha Mapinduzi, kupitia kwa Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kimelaani vurugu za kidini zilizotokea Mbagala Kizuiani.

Alisema kuwa CCM kinalaani tukio la kukojelewa kwa kitabu kitakatifu cha Kuran na vile vile vitendo vya kuvamiwa na kuchomwa moto makanisa na uporaji wa mali, akisisitiza kuwa havifanani na mila na desturi za Watanzania.

"Kitendo cha kukojolea kitabu kitakatifu cha Waislamu hakikubaliki, na kitendo cha kuvamia na kuchoma moto nyumba za ibada za Wakristo na kufanya vurugu pia hakikubaliki," alisema Nape


Source: Tanzania daima
 
Kama kweli JK hajakemea hiki kitenda atakuwa anaiharibu nchi yetu..inapofikia hatua ya watu kuvamia nyumba za ibada kama ishara ya kuonyesha hasira zao na Rais anakaa kmya ujue tunajitafutia laana kwa nchi.
 
Too soft, hamna hata karipio au order Mh. kaishia kuongelea ushauri aliowapa. Leo hotuba ya Nyerere day

Kosa kubwa ni la yule anayefahamu thamani ya Kuran aliyempa mtu akijua analokusudia kufanya ni kuikojolea. Je huyu kweli alikuwa anaithamini hiyo Kuran? Na je alikojolea wapi? Ilikuwa darasani, kichakani au chooni? Je inaruhusiwa kuipeleka Kuran chooni???
 
ungekuwa ni wewe ungeliongeleaje? amekosea kuwashauri waliofanya hivyo?

Waliobomolewa makanisa hata hawamjui yule mtoto. Hiyo kesi ilimuhusu huyo dogo na familia yake iliyokosea kumlea. Haikumhusu Askofu Marasusa. Wale waliovunja makanisa ni wenye akili timamu zaidi ya yule mtoto kwa makusudi walishuka mno na kuamua kufikiri kwa kiwango cha chinii sana kama yule mtoto. Jaziba zikitawala akili hushindwa kufanyakazi yake ipasavyo.
 
Too soft, hamna hata karipio au order Mh. kaishia kuongelea ushauri aliowapa. Leo hotuba ya Nyerere day
huko madrassa, hawa vijana washauriwe kuvitunza hivyo vitabu na sio kufanyia biashara ya kuwaringishia wenzao au kuwatia majaribuni. kama ni kuwa adhibu hao vijana basi wote wawili kwa adhabu ile ile, ili iwe fundisho kwao.
 
Hotuba ya JK leo wakuu kwenye Nyerere day, ameongelea hii saga ya wazee wa vi dont touch. Ila sijamsikia akipiga mkwara amesema amewashauri waislam wasifanye maamuzi wakiwa na hasira ila kwa yule mtoto amesema alifanya kosa kubwa sana pamoja na utoto wake kukojolea kitabu kitakatifu.
 
Sijaelewa hasira za waislam zimetokana na nini, ikiwa mazungumzo yanatolewa kwamba wale vijana/watoto walibishana bila shaka wote ni wakosaji.

Ikiwa yule mtoto muislam ndiye aliyeanzisha uongo kwamba ukikojolea msahafu unageuka na akaruhusu kuiweka iliikojolewe basi naye anastahili adhabu, je ni adhabu gani amepewa?

Sasa suala la hasira ni la nini, iwapo msahafu wenyewe una uwezo wa kumgeuza mkosaji awe mjusi kwanini wasingeacha huyo mtoto ageuke?

Kama si kweli kwamba msahafu una uwezo wa kugeuza mtoto atakayeikojolea, basi uongo umedhihirika.
Je hasira ya kiwango kikubwa hivyo imesababishwa na nini?
 
Sijaelewa hasira za waislam zimetokana na nini, ikiwa mazungumzo yanatolewa kwamba wale vijana/watoto walibishana bila shaka wote ni wakosaji.

Ikiwa yule mtoto muislam ndiye aliyeanzisha uongo kwamba ukikojolea msahafu unageuka na akaruhusu kuiweka iliikojolewe basi naye anastahili adhabu, je ni adhabu gani amepewa?

Sasa suala la hasira ni la nini, iwapo msahafu wenyewe una uwezo wa kumgeuza mkosaji awe mjusi kwanini wasingeacha huyo mtoto ageuke?

Kama si kweli kwamba msahafu una uwezo wa kugeuza mtoto atakayeikojolea, basi uongo umedhihirika.
Je hasira ya kiwango kikubwa hivyo imesababishwa na nini?

kuna mlinzi nje ya geti
 
Kesho dhaifu anaenda zake sijui oman hapo anawaza safari tu.mi nipo mlimani na akina mtatiro na easter wassira ,nitarudi baadae
 
Back
Top Bottom