Kikwete: Nisingepewa Elimu na Kanisa ningekuwa nafanya biashara ndogondogo Chalinze!

Mada ni majina teh teh teh!

Hata mimi nimesikia japo mtangazaji alimkatisha haraka yule Dr asiendelee kuongea.so tujadili hili je lina ukweli?? Usipotezee embu kuwa na weledi kwenye kuchangia mada tafadhali!hizi ni zama za ukweli na uwazi embu zindukaaa
 
Hata Padre Slaa alivyosoma seminari alikuwa anatumia jina la baba yake wa kambo kwa mujibu wa jamaa zake wa Karatu.

Wewe na yule Dokta Kasoga aliyekurupuka kudai ati Kikwete alitumia jina la Samuel Luhanga ni wakurupukaji tu, mada inayozungumzwa ni nyingine, ninyi mnazusha mengine.

Dk. Kasoga naweza kumsamehe, lkn wewe ujinga umekujaa maana ungeweza kujifunza kwa makosa ya Dk Kasoga [kuchanganya mambo yasiyohusiana] na kujirekebisha, lkn kwa ajili ya chuki zako kwa Dk. Slaa, umeshindwa kabisa kuficha donge lako. Chuki iliyopitiliza inakushushia heshima yako Ritz.
 
Wakuu.

Hayo ni majina tu yasitutuzue, kama aliamua kuchukua majina kwa ajili ya kupata elimu na imani yake haiku tetereka akabaki kuwa imara haliwezi kuwa tatizo, jina hubaki kuwa jina kama utambulisho na kwa watu makini jina haliwezi kuwa imani!

Lakini imani ikibadilika ndio utata na tatizo huanzia hapo. Kama JK alibadili jina na imani yake ya kidini ikabadilika kutokana na jina basi hapo ndio penye tatizo. kumbukeni kwenye nchi za kiarabu ambako kuna watu wa dini za imani nyingine unaweza kukuta mtu ana jina la kiarabu ambapo kwa huku Tanzania tungesema kuwa ni jina la kiislamu lakini mtu huyo huwa ni mkristo. Tarik Azizi kwa mfano amekuwa akisemwa kuwa hakuwa muislamu japo jina lake kwa haraka huonekana kuwa la kiislamu.

Nchi ya misri kwa mfano, kuna ushahidi wa watu wengi wenye majina ya kiarabu ambao si waislamu bali wakristo. Kwa JK mjadala kama ilikuwa ni kubadili jina na kumnyima mtu mwenye jina lake fursa ya kusoma hapo ndio penye tatizo ukiachilia mbali lile swala la Kiimani.
 
Mie sioni tatizo kabisa, tatizo lingekuwa kama hakusoma yeye ila alinunua hicho cheti kutoka kwa Samweli. Lakini kama alisoma yeye shule kwa jina la samweli tatizo liko wapi?
 
Kwa mujibu wa Dr. Ngowi wa University of Bagamoyo aliyealikwa katika kipindi cha malumbano ya hoja. Anasema alisomea shule za seminari na kutumia jina la Samwel Luhanga na baadaye ndipo akatumia jina la Jakaya Mrisho Kikwete. Tuna mengi ya kujifunza.

Hongera Samwel Jakaya Kikwete


Chanzo: ITV malumbano ya hoja

Nimetazama kipindi hicho, kimemalizika muda dakika kadhaa zilizopita. Siyo Dr Ngowi aliyesema hilo. Ni Dr Kasoga mhadhiri wa chuo kikuu cha Bagamoyo. Mimi pia nimeshangazwa na taarifa hiyo. Lakini kama ni ya kweli, inamuongezea credit Mwalimu Nyerere kwa uamuzi wake wa kutaifisha shule za misheni, kwamba baada ya utaifisho huo waislamu walikuwa na uhuru kamili wa kusoma katika shule hizo bila kulazimika kutumia majina ya kikiristo au kuigiza ukiristo.

Majuzi nimemaliza kusoma kitabu cha historia ya shule ya Ilboru kilichoandikwa mwaka 1969. Ilboru ilikuwa shule ya kiluteri na ilianza miaka ya mwanzoni ya 1940's. Katika sehemu fulani kitabuni mle, kuna ripoti ya mkutano mmojawapo wa bodi ambako walilalamikia suala la kulazimishwa na serikali (baada ya uhuru) kuanza kudahili wanafunzi wa imani nyingine. Bila msukumo na shinikizo la serikali ya Nyerere, baadhi ya shule za madhehebu ya dini kamwe zisingekubali kusomesha watoto wa dini tofauti na ya wenye shule. Ndio maana naungana na wote wanaomsifu Mwalimu Nyerere kwa jitihada zake za kuondoa matabaka Tanzania, na mfano wa leo wa Mh Samuel Luhanga ni kumbukumbu nyingine nzuri sana to Nyerere's credit.
 
Kwa mujibu wa Dr. Ngowi wa University of Bagamoyo aliyealikwa katika kipindi cha malumbano ya hoja. Anasema alisomea shule za seminari na kutumia jina la Samwel Luhanga na baadaye ndipo akatumia jina la Jakaya Mrisho Kikwete. Tuna mengi ya kujifunza.

Hongera Samwel Jakaya Kikwete


Chanzo: ITV malumbano ya hoja
Sishangai "Sam, Sammy have been sweet names with sweet guys"
 
Back
Top Bottom