Kikwete ni rais bora zaidi ya wote

Nasubiri na kuomba sana niwe hai baada mwaka 2015 nione magazeti yakishindana kumuanika atakaekuwa rais mstaafu wa awamu ya nne,JK...yaani wataandika sana na tutayajua mengi sana kuanzia mchakato wa urais 1995 hadi suti 5...na zaidi
 
Dah watanzania kwa kulalamika, hebu elezeni mipango mizuri mliyonayo kichwani basi, maana mkilalamika bila ku-present your own good idea ili tuseme dah, unacholalamika ni kweli na una option au opinion nzuri, amasivyo huna tofauti na wale tulikuwa tunawaita "watoto wa mama, au kula kulala" maana pamoja na kuwa na umri na uwezo wa kuzalisha mali, chakula hawajakitafuta wao, ila kikiwa na kasoro duh, hilo varangati lake hapo mezani usipime? Hebu tutoeni aibu Wa-Tanzania, anzeni kufikiri positively, na muamue hapo mlipo mnataka kufanya nini kuibadili hii Tanzania, hata Raisi akiwa strong or weak, at the end of the day Tanzania stands high in terms of the developments adn in terms of inter-country politics and image.

Kufikiri kwako positive na kuamua kunawezaje kufanikiwa ikiwa mtoa dira kapinda? Mimi huwa nawashangaa sana nyinyi mliogoma kufikiri na kusema tusiilaumu serikali. Serikali dhaifu huwanyima fursa wananchi wake kupiga hatua, badala yake huwarudisha nyuma kila kukicha kwa mipango mibovu na kukosa uwajibikaji.

NAKUPA MFANO:
Umeshindwa kuendelea na masomo sababu mzazi ndio kakuacha bado shuleni tena nyuma mbali. Shule imeshindikana na sasa uko mtaani, lkn angalau mzazi alikuacha na kanyumba ka vyumba vitatu kakawa urithi wako. Unaishi humo sasa wewe na wadogo zako wawili. Vyumba viwili vimepangishwa na kimoja mmejibanza wenyewe.

Mtoto wa kiume ukaona sio busara kuishi kwa kodi, hata chakula haitoshi na hamna maendeleo. HODI FINCA, HODI PRIDE! Mkopo umefanikiwa 3milioni kibindoni. Safari ya Mwanza na hukukawia, SATO na SANGARA wamefika DSM biashara imeanza, safi kabisa. Wote wameisha, mtaji wa 1 mil umeleta faida ya laki 2, Mungu akupe nini ndani ya wiki 2 laki 2.

Biashara isiyokuwa haina tija, sasa safari ya 4 unaleta samaki wa milioni 2.5, kweli wamefika. BALAA LIMEANZA, Ngeleja na umeme wake wameanza mchakato wa kugawa giza na joto. La haula, samaki bila JOKOFU? Umefanikiwa kuuza wa laki 3 tu, waliobaki ni ugomvi na majirani kwani sasa wananuka. Apewe kijana elfu 20 akachimbe shimo tuwafukie. Hili limeisha, MAREJESHO YA MKOPO JE?

Kwa kuwa FINCA na PRIDE sio wakarimu kama Rais Kikwete, wao watakachofanya ni kuuza kale kakibanda kako ka urithi. Sasa maisha yamepata sura mpya. Mwanzo mlikuwa mnaishi ndani na akili zilitulia, sasa mnahifadhiwa kwa jirani akili zikiwa zimewaruka.

Kama una akili angalau kidogo, utakuwa umenielewa.

Tuachane na huyo wa mjini, kule kijijini umefika wewe? Ngoja nikupeleke......
KILIMO KWANZA, tumekiitika na tumeikubali sera. Yakaja MATREKTA, zabuni kapewa mhindi. Wakulima wote waliothubutu kukopa walipata, si ndio maendeleo bwana na tunaambiwa hata wafanyabiashara wakubwa hukopa, na mimi nakopa.

Trekta aliloleta Mhindi imefanya kazi nusu mwaka, kila kitu chali. Gharama za matengenezo milioni 3.3 na bado sijavuna. Hatimaye nimevuna, mhindi anataka malipo ya trekta na mahindi yapo ghalani. Sharti hapa niiuzie serikali ili Profesa ambaye anaishi mjini asife njaa endapo nitayauza Kenya.

Baada ya mlolongo mrefu, hatimaye nimelipwa. Nalipa trekta, nalipia matengenezo ya trekta na msimu ujao sina fedha ya mbolea. TREKTA la kichina limezua mambo. TUACHE TREKTA TURUDI HAPA......,MAZAO. Mazao haya ya nani hasa? NApolima mimi, kosa langu nini nisimuuzie mwenye hela nyingi kisa katoka Kenya badala yake nibebeshwe jukumu la kuilisha nchi? Kwani mshona viatu huko mjini anachaguliwa wateja? Mkenya 800 serikali 650, ungekuwa wewe ungemuuzia nani?

Hapa utaniambia FOOD SECURITY. Vijana waliojazana mjini, JKT na UTAALAM WAO wa Kilimo na Ufugaji PLUS mashamba ya serikali ambayo yana miundombinu na rundo la wataalam wa kilimo walioko mjini hawa wooote kwa ujumla wao hawatoshi kulima chakula cha kulisha nchi mpaka tukanyang'anyane mazao na mkulima aliyelima kwa utashi wake? Nakuongeza na work-force ya magereza., bado hawatoshi?

Sasa wewe mwenye akili sana, endelea kuniona mjinga kuikosoa serikali. Acha iendelee kuuza mashamba kwa wawekezaji huku yenyewe ikimnyang'anya mkulima mazao yake. Mwaka wa 8 Kenya kuna njaa na sisi tuna neema, lkn hilo halikuweza kutumika kunufaisha nchi. Kila siku ni upungufu wa fedha za kigeni: HAPA MNISAIDIE mie elimu yangu ndogo: HIVI TUKILIMA MAHINDI NA MCHELE MWINGI NA KUWAPA HAWA WAKENYA MASHARTI KUWA MAHINDI YETU TUNAYAUZA KWA US DOLA, INATUHUSU SISI KUJUA DOLA WATAPATA WAPI?

Profesa, ajira hewa zinakadiriwa kufikia 15,000. Sisemi kuwa zitamaliza shida ya ajira, lkn u wapi mfano wa namna ya kumshughulikia yule aliyekamatwa kwa kumlipa marehemu mshahara kwa miaka 8?

Kama upo na mimi bado, naomba uniulize kwa elimu yangu ndogo na kutokuwa kwangu graduate nafikiri nini kuhusu uchumi, nami nitatumia muda kidogo kukuwekea hapa mawazo yangu, uyakosoe na kuyakarabati halafu mimi na wewe tutakuwa tumeleta positive move kwa taifa.
 
Sina shaka kuwa kuna watu wasiopenda kukubali ukweli watakanipinga kwa kejeli na mbwembwe lakini hilo lakini ni bora kilicho gizani kikamulikwa ili kionekane!

Ni ukweli usiopingika kuwa serikali ya ya JK imechafuliwa na kashfa nyingi mbaya ambazo sina malengo ya kuzirudia na wala sitomjibia hizo. Lakini kama mwananchi mwema na msema kweli nakiri kuwa NIMEIONA NDANI YA JK DHAMIRA YA DHATI YA KUMSAIDIA MWANANCHI WA HALI YA CHINI NA HASA MKULIMA!

Pamoja na ushabiki wangu kwa CHADEMA,nimesikitishwa na vipaumbele vyao katika bajeti mbadala kwani ''KILIMO SIO KIPAUMBELE CHAO''.

Kwa hili nimeona na nimetambua kwanini CCM itaendelea kutawala kwa muda mrefu,chakusikitisha hata AFYA za wananchi nazo sio muhimu kwa kwa waandaji wa bajeti mbadala. Hili limenifanya niamini kuwa kambi ya upinzani ilyopita ilyokuwa na mchanganyiko wa vyama vyote vya upinzani ilitufaa sana kuliko hii ya chama kimoja.

Kitendo cha JK kuongeza bajeti ya umwagiliaji mpaka kufikia bilioni 40 kimeonyesha dhamira yake ya kumhakikishia mkulima anavuna na kuondokana na njaa halafu umaskini. Kwa nchi ambayo asilimia 80 ya wananchi wake ni wakulima huwezi kuondoa kilimo kama kipaumbele, huu kwangu ni ujuha!

Ninawataka waliondaa bajeti hii mbadala warudi wakazingatie maslahi ya wachache na kuweka maslahi ya ya walio wengi mbele. Kwa ujumla nimekereka nayo na kama wakulima hatutoanza kujaaliwa kwenye bajeti mbadala ni vipi tukiwapa nchi?

Nampongeza JK na serikali yake kwa hili ila hizo pesa zilizotengwa zitolewe mapema ili wananchi wanufaike nazo!

Mnapenda sana kutumia hiyo red, huh!!! HATUDANGANYIKI. HE IS THE WORST PRESIDENT OF ALL TIME.
 
kwa vipaumbele vilivyoanishwa ndani ya bajeti kuhusu kilimo ni dhahiri kuwa kilimo kitachukua muda kukua hata kama kikiongezewa mamilioni hayo na mengine! kuhusu miundo mbinu kama chachu ya maendeleo natoa tick,lakini kwa kilimo? sidhani!

Sababu ni kubwa ni kuwa, msingi mkubwa wa ukuaji wa biashara yoyote ni soko, kama kuna uhakika wa masoko yenye bei za kuvutia uzalishaji, basi binadamu atahangaika tu ,atapata hizo pembeje, huduma za ugani hata kama asipo saidiwa na serikali! sasa soko la mazao ya kilimo nini?

Ni viwanda vya usindikikaji, ambavyo vinaweza kuanzishwa kwa juhudi za kuunganisha Veta, SIDO, USHIRIKA, na huduma za kibenki! kila pazalishwapo zao pawe na kiwanda cha kusindika na kuongeza thamani! serikali ikisimamia vyema juhudi hizi za wadau hawa, amabao watamobilise, vijana, watapatiwa ujuzi,na vtendea kazi pamoja na mikopo katioka kuanzisha viwanda hivyo, ambavyo vitakuza ajira na kuimarisha soko la mazao hivyo kuleta msukumo (stimulant) katika ukuaji wa kilimo,ufugaji, uvuvi,na hata madini!

Nasikitika inawezekana unachokisema hukijui au unapotosha makusudi! Kwa nchi ambayo wananchi wake asilimia zaidi ya sabini (70%) wanaishi maisha yao kwa kutegemea kilimo sidhani **** unawatendea haki kwa kupuuza kilimo chao na kuweka nguvu na vipaumbele kama ulivyoainisha! Ni wendawazimu kuchukua ndoo kwenda kumkamua maziwa kuku, lazima ifikie mahali tuwe wakweli kuliko kuwa wabinafsi, kwa kilimo hiki unachokitaka cha mkulima kupuyanga kujitaftuia pemebejeo tena zikiwa na bei ya juu tutaangamiza taifa hili, Kwa kilimo cha kusubiri kudra za mwenyezi Mungu kushusha mvua ya kutosha na yenye mtawanyiko safi kukidhi unyweshaji wa wa mazao kipindi chote cha msimu ni dhahiri kuwa ni dalili za kukata tamaa na kusubiri kufa!Tutende haki, Fikisha Maji ya kutosha (irrigation) kwa mkulima tuone kama viwanda havitajengwa, Fikisha maji ya kutosha (irrigation) kwa mkulima tuone kama masoko hayatapatikana, fikisha maji kwa mkulima (irrigation) tuone kam uchumi wa nchi utaendelea kukua kwa kusuasua!Tuache siasa tufanye hili moja tu "FIKISHA MAJI YA UMWAGILIAJI KWA MKULIMA" tuone kama umaskini haujakoma nchi hii, tuone kama vijana watakimbilia mijini nk,yangu nihayo tu
 
Sina shaka kuwa kuna watu wasiopenda kukubali ukweli watakanipinga kwa kejeli na mbwembwe lakini hilo lakini ni bora kilicho gizani kikamulikwa ili kionekane!

Ni ukweli usiopingika kuwa serikali ya ya JK imechafuliwa na kashfa nyingi mbaya ambazo sina malengo ya kuzirudia na wala sitomjibia hizo. Lakini kama mwananchi mwema na msema kweli nakiri kuwa NIMEIONA NDANI YA JK DHAMIRA YA DHATI YA KUMSAIDIA MWANANCHI WA HALI YA CHINI NA HASA MKULIMA!

Pamoja na ushabiki wangu kwa CHADEMA,nimesikitishwa na vipaumbele vyao katika bajeti mbadala kwani ''KILIMO SIO KIPAUMBELE CHAO''.

Kwa hili nimeona na nimetambua kwanini CCM itaendelea kutawala kwa muda mrefu,chakusikitisha hata AFYA za wananchi nazo sio muhimu kwa kwa waandaji wa bajeti mbadala. Hili limenifanya niamini kuwa kambi ya upinzani ilyopita ilyokuwa na mchanganyiko wa vyama vyote vya upinzani ilitufaa sana kuliko hii ya chama kimoja.

Kitendo cha JK kuongeza bajeti ya umwagiliaji mpaka kufikia bilioni 40 kimeonyesha dhamira yake ya kumhakikishia mkulima anavuna na kuondokana na njaa halafu umaskini. Kwa nchi ambayo asilimia 80 ya wananchi wake ni wakulima huwezi kuondoa kilimo kama kipaumbele, huu kwangu ni ujuha!

Ninawataka waliondaa bajeti hii mbadala warudi wakazingatie maslahi ya wachache na kuweka maslahi ya ya walio wengi mbele. Kwa ujumla nimekereka nayo na kama wakulima hatutoanza kujaaliwa kwenye bajeti mbadala ni vipi tukiwapa nchi?

Nampongeza JK na serikali yake kwa hili ila hizo pesa zilizotengwa zitolewe mapema ili wananchi wanufaike nazo!

Umesikia mafuriko na madudu kuhusu zao la KAHAWA jana Bungeni? Au unamzungumzia Mkulima gani kama sio huyu anaelazimishwa kuuza buni yake kabla ya kuiongezea ubora (THAMANI) na mawaziri kutumia ukuu wao kunufaika juu ya hilo?. Mbeya kuna vinu 13 vya kuongeza ubora wa Buni kabla ya kuuzwa lakini vikao visivyo halali kwa jina la wadau likapisha maagizo ya kununuliwa bila kuongeza thamani ili wazunguke na kunufaika wao walioko madarakani na biashara zao. Wezi wakubwa nyie na mwenyekiti Dhaifu wenu.

Huu ni uhaini sio uongozi,
Ni genge la dhuluma kwa waTz........
Watz tumelamba Joker na mchezo unaisha!
 
watu msio na mbadala wa maisha zaidi ya kujipendekeza cwapendi!!!tena bac tu ningekuwa na uwezo wa kusema neno na likawa ningesema maana nyinyi ni wanafiki na wafikiria pa fupi kwani...amefanya nini mpaka awe bora kuliko wote au wewe ni Efram Kibonde wa TBC nini..maana mnaishi kwa kujikomba anyway labda mazingira unayoishi yamekuharibu au ndo ulivyolelewa hapo uswahilini
 
Sina shaka kuwa kuna watu wasiopenda kukubali ukweli watakanipinga kwa kejeli na mbwembwe lakini hilo lakini ni bora kilicho gizani kikamulikwa ili kionekane!

Ni ukweli usiopingika kuwa serikali ya ya JK imechafuliwa na kashfa nyingi mbaya ambazo sina malengo ya kuzirudia na wala sitomjibia hizo. Lakini kama mwananchi mwema na msema kweli nakiri kuwa NIMEIONA NDANI YA JK DHAMIRA YA DHATI YA KUMSAIDIA MWANANCHI WA HALI YA CHINI NA HASA MKULIMA!

Pamoja na ushabiki wangu kwa CHADEMA,nimesikitishwa na vipaumbele vyao katika bajeti mbadala kwani ''KILIMO SIO KIPAUMBELE CHAO''.

Kwa hili nimeona na nimetambua kwanini CCM itaendelea kutawala kwa muda mrefu,chakusikitisha hata AFYA za wananchi nazo sio muhimu kwa kwa waandaji wa bajeti mbadala. Hili limenifanya niamini kuwa kambi ya upinzani ilyopita ilyokuwa na mchanganyiko wa vyama vyote vya upinzani ilitufaa sana kuliko hii ya chama kimoja.

Kitendo cha JK kuongeza bajeti ya umwagiliaji mpaka kufikia bilioni 40 kimeonyesha dhamira yake ya kumhakikishia mkulima anavuna na kuondokana na njaa halafu umaskini. Kwa nchi ambayo asilimia 80 ya wananchi wake ni wakulima huwezi kuondoa kilimo kama kipaumbele, huu kwangu ni ujuha!

Ninawataka waliondaa bajeti hii mbadala warudi wakazingatie maslahi ya wachache na kuweka maslahi ya ya walio wengi mbele. Kwa ujumla nimekereka nayo na kama wakulima hatutoanza kujaaliwa kwenye bajeti mbadala ni vipi tukiwapa nchi?

Nampongeza JK na serikali yake kwa hili ila hizo pesa zilizotengwa zitolewe mapema ili wananchi wanufaike nazo!

Mtende wa Haki;
Rais tunaye, waongozwa hawapo, serikali tunayo, watawaliwa hatupo. Kama basi iko hivyo, unategemea nini? Sisi huku chini tunafanya nini? Je kweli tunatenda haki kama ipasavyo, ili nasi tupate hiyo haki ya kuwalalamikia viongozi wetu? Katika level yangu ya chini hapa nilipo ukinidhulumu elfu 10,000/= unaniumiza zaidi kuliko aliyeiba hata billion moja kwenye hela ambayo ni public. Lazima tuongee ukweli halisi, japo yule mwizi public ni mkubwa na ni mbaya zaidi kuliko huyu wa elf 10, 000/= yangu.
Kwa maana hiyo kwa level ya maisha yangu, anayenidhulumu elfu 10,000/= yangu ni mbaya zaidi kwangu kuliko yule aliyeiba 1,000,000,000/= ambayo ni public. Katika micro level anayekudhulumu elfu kumi na kwa maisha yetu jinsi watanzania tulivyo, anaweza akasababisha hata kukugharimu maisha ya watu nyumbani kwako (yaweza kuwa kwa mfano, 5,000/= ilitakiwa ipeleke mgonjwa kwa daktari, ambaye baada ya kutokwenda amefariki, kwa sababu hapakuwepo na hela nyingine). Mimi ninapoilalamikia serikali huwa kila siku narudi katk level ya chini kwetu sisi walala hoi, je tunatendeana haki? Je japo serikali haitutendei haki kama tunavyodai, je sisi walala hoi nasi tunafanya mambo kama tunavyotakiwa kufanya? JAMANI SISI HUKU CHINI KWELI TUNATENDEANA HAKI? TUNATENDA HAKI? Sitetei serikali kulalamikiwa, ila .....
 
Sina shaka kuwa kuna watu wasiopenda kukubali ukweli watakanipinga kwa kejeli na mbwembwe lakini hilo lakini ni bora kilicho gizani kikamulikwa ili kionekane!

Ni ukweli usiopingika kuwa serikali ya ya JK imechafuliwa na kashfa nyingi mbaya ambazo sina malengo ya kuzirudia na wala sitomjibia hizo. Lakini kama mwananchi mwema na msema kweli nakiri kuwa NIMEIONA NDANI YA JK DHAMIRA YA DHATI YA KUMSAIDIA MWANANCHI WA HALI YA CHINI NA HASA MKULIMA!

Pamoja na ushabiki wangu kwa CHADEMA,nimesikitishwa na vipaumbele vyao katika bajeti mbadala kwani ''KILIMO SIO KIPAUMBELE CHAO''.

Kwa hili nimeona na nimetambua kwanini CCM itaendelea kutawala kwa muda mrefu,chakusikitisha hata AFYA za wananchi nazo sio muhimu kwa kwa waandaji wa bajeti mbadala. Hili limenifanya niamini kuwa kambi ya upinzani ilyopita ilyokuwa na mchanganyiko wa vyama vyote vya upinzani ilitufaa sana kuliko hii ya chama kimoja.

Kitendo cha JK kuongeza bajeti ya umwagiliaji mpaka kufikia bilioni 40 kimeonyesha dhamira yake ya kumhakikishia mkulima anavuna na kuondokana na njaa halafu umaskini. Kwa nchi ambayo asilimia 80 ya wananchi wake ni wakulima huwezi kuondoa kilimo kama kipaumbele, huu kwangu ni ujuha!

Ninawataka waliondaa bajeti hii mbadala warudi wakazingatie maslahi ya wachache na kuweka maslahi ya ya walio wengi mbele. Kwa ujumla nimekereka nayo na kama wakulima hatutoanza kujaaliwa kwenye bajeti mbadala ni vipi tukiwapa nchi?

Nampongeza JK na serikali yake kwa hili ila hizo pesa zilizotengwa zitolewe mapema ili wananchi wanufaike nazo!
Kutumwa kubaya haswaa!! wewe nawe nini sasa umeleta hapa? taja % kwenye bajeti siyo unaleta namba hapa! Una ROHO NGUMU NINAKUSIFU KWA KULETA THREAD HII umepewa bei gani?
 
Mjomba, usidhani utapata chochote katika kumtetea JK. Wewe umefaidika na nini katika kilimo kwanza? Taja angalau faida mbili tu. Nduguzo wanateseka na serikali ya JK kwa ahadi hewa. Maisha bora kwa kila Mtanzania yako wapi? usiwe kama pimbi tafakari kwanza kabla ya kutoa mada.:sad:
 
Naweka ukweli wazi kuwa:
sijawahi kutana na J Kikwete.
Sija wahi wasiliana naye kwa namna yoyote ile.
Sihitaji chochote toka kwake kama Jk.
Sina masilahi yoyote yale katika msimamo wangu huo usiotegemea hisia, bali ukweli.

Narudia tena kwa msisitizo wa kina: JKikwete ni bora kuliko maraisi wote waliomtangulia, ambao sehemu kubwa waliongoza serikali ya Tanzania kijanja-kijanja.
 
Jk ni rais dhaifu kuliko wote waliopita. Hata ukimwekea kidole kwenye jicho yeye aka! Hana shida. Kama Nyerere alikuwa dikteta basi tunataka madikteta kama Nyerere kuongoza tanzania
ahaaa ahaaaa teeehee teeheee Rais dikteta sasa tumeshampata tuwache kupiga mayowe tulicho kitaka sasa tumekipata
 
Naomba niliweke wazi hili kuwa Rais Kikwete ni rais bora kuliko marais wote waliomtangulia hapa Tanzania. Nathibitisha hoja yangu kwa ushahidi ufuatao(conclusive evidence):

1. J.Kikwete siyo dikteta, wakati JK Nyerere alikuwa dikteta mkubwa sana, akifuatiwa na Mkapa.Nyerere alitaka mambo yote ktk nchi yaende kama anavyotaka yeye. Hakuwa tayari kukosolewa.Mkapa naye hivyohivyo.

2.J.Kikwete ni mtu mwenye utu, ubinadamu. Nyerere, mwinyi, Mkapa hawa jamaa walikuwa hawana utu, ni unyama tuu.

3.J.Kikwete ni mtu muungwana ambaye yuko tayari muda wote kusikiliza na kufanyia kazi maoni hata ya vyama vya upinzani.Anaheshimu mawazo ya watu bila kujali itikadi za vyama husika. Nyerere alifuta vyama vyote vya upinzani miaka ya sitini, akaleta dhana ya chama kushika hatamu ili imulinde yeye na madaraka yake. Mkapa daima aliporomosha matusi kwa vyama vya upinzani.

4.J.Kikwete anaheshimu sana utawala wa sheria(Rule of Law). Hapendi kuingilia UHURU WA MAHAKAMA. Wakati waliomtangulia wote walikuwa tayari hata kuingilia uhuru wa mahakama kwa masilahi yao.

5.J.Kikwete ni mtu ambaye hana mawaa na mtu yeyote.

6.J.Kikwete amekuwa tayari kuanzisha mchakato wa kuandika katiba mpya. Kitu ambacho watangulizi wake wote hawakuwa tayarisha licha ya misukumo ya kimahakama na wanaharakati.Nyerere ndiye alikuwa kinara wa kuvuruga katiba ya nchi kwa masilahi yake. Mwaka 1977 kwa makusudi kabisa akiwa anajua, alitengeneza mkakati wa kuhakikisha katiba ya nchi inatengenezwa na kamati ya chama, siyo wananchi.Ukisoma historia ya constitutional development ktk nchi hii kuanzia katiba ya 1961 hadi 1977 utajua who is Nyerere. Vinginevyo hutamjua Nyerere.

7.J.Kikwete ni mtu wa Mungu na Changuo la Mungu, ni zawadi ya Mungu kwa watanzania kwani kweli anaheshimu uhuru wa kuabudu, haki za binadamu, hana ubaguzi wa aina yoyote ile.

Take note: Kama mtazamo wangu huu si wa kweli basi mtakuja kunikumbuka mwaka 2015 atakapopatikana raisi mwingine. Kumpata Raisi mwenye fadhiri za kiutu, kibinadamu, kizalendo, kidemokrasia, kihaki, kama Kikwete ni ngumu sana!

God Bless you!
unaikumbuka hii post yako? leo ni 2016.
 
Jk ni rais dhaifu kuliko wote waliopita. Hata ukimwekea kidole kwenye jicho yeye aka! Hana shida. Kama Nyerere alikuwa dikteta basi tunataka madikteta kama Nyerere kuongoza tanzania
bila shaka sasa hivi unafuraha ya kutosha. maana Magu ni zaidi ya nyerere.
 
Naweka ukweli wazi kuwa:
sijawahi kutana na J Kikwete.
Sija wahi wasiliana naye kwa namna yoyote ile.
Sihitaji chochote toka kwake kama Jk.
Sina masilahi yoyote yale katika msimamo wangu huo usiotegemea hisia, bali ukweli.

Narudia tena kwa msisitizo wa kina: JKikwete ni bora kuliko maraisi wote waliomtangulia, ambao sehemu kubwa waliongoza serikali ya Tanzania kijanja-kijanja.
Ukilalamika mtu kama wewe utaeleweka!Tulikuwa na mawazo yanayoshabihiana
 
Back
Top Bottom