Elections 2010 Kikwete ni msahaulifu au mzembe?

Kipimo cha kwanza cha ubora wa kiongozi makini ni uwezo wake wa kuteua/kuchagua wasaidizi makini wenye uwezo wa kutekeleza vision ya taasisi anayoiongoza. Kipimo cha pili ni umadhubuti na ujasiri wa kusimamia kile anachokiamini na cha tatu ni uwezo wa kukemea kwa nguvu na ikibidi kuwawajibisha wasaidizi wake wanapokengeuka au kutekeleza majukumu yao kizembe!!! Akipungua katika mizani hii huyo si kiongozi bora bali bora kiongozi.
 
TAFAKURI JADIDI



Kikwete wetu na Basil Pesambili Mramba!


Johnson Mbwambo
Septemba 22, 2010

WAPENDWA, leo, nimeshawishika kuandika rejeo (rejoinder) kuhusu makala iliyoandikwa na Msomaji Raia katika toleo la gazeti hili, wiki iliyopita, ukurasa wa 10, yenye kichwa cha habari: Rais Kikwete msahaulifu au mzembe?

Msomaji Raia alichagua kichwa cha habari chenye swali. Angeweza kuchagua kichwa cha habari hicho hicho bila ya kuweka alama ya kuuliza, lakini hakuchagua kufanya hivyo. Nadhani aliamua kumalizia kwa alama ya kuuliza ili kukwepa kuhukumu, na badala yake kumuachia msomaji aamue mwenyewe kama Rais Kikwete ni msahaulifu au ni mzembe.

Ingawa simfahamu Kikwete kwa karibu kama Msomaji Raia, lakini hata mimi nahangaishwa na kutafuta jibu la swali hilo hilo: Je, tatizo la Kikwete ni usahaulifu au ana tatizo jingine kubwa zaidi?

Yawezekanaje (kama alivyobainisha Msomaji Raia) Kikwete atoe tamko thabiti kwa Watanzania kwamba urais wake hauna ubia na mtu mwingine yeyote, na kisha miaka mitano baadaye rais huyo huyo awe na ujasiri wa kuuambia tena umma wa Watanzania kwamba urais ni suala la kifamilia? Yawezekana aliisahau kauli yake hiyo ya mwanzo?

Kwa hakika, ukitaka kuandika kauli ambazo Kikwete alipata kuzitoa na baadaye akatoa nyingine kinyume kabisa na zile za mwanzo, au hatua alizochukua na baadaye akafanya kinyume chake, unaweza kujaza kitabu kizima.

Chukulia, kwa mfano, tukio la wiki iliyopita la huko Rombo ambako alijipa ujasiri kupanda jukwaani na kuwasihi wana-Rombo wamchague tena Basil Pesambili Mramba kuwa mbunge wao kwa kipindi kingine cha miaka mitano kwa kuwa ni “mbunge safi”, na kummwagia sifa kemkem.

Akiwa ameunyanyua juu mkono wa Mramba, Rais Jakaya Kikwete alisema hivi kuhusu mgombea ubunge huyo wa CCM: “Huyu kwa maneno ya mjini ni mzee kijana kwani ni mwenye mawazo mapya yenye manufaa wakati wote…siyo wale wazee ambao wakichoka la mbele linawekwa nyuma na la nyuma linawekwa mbele. Huyu ubongo wake unajadidika, ni chimbuko la maarifa mapya (rejea blogu ya kampeni za CCM inayoitwa Chagua Kikwete 2010 ambayo anuani yake ni jakayakikwete2010.blogspot.com).

Tukio hilo la Rais Kikwete kumnadi Mramba kwa kummwagia sifa kemkem liliibua maswali mengi kichwani mwangu; hasa nikikumbuka kwamba ni Kikwete huyo huyo ambaye aliidhinisha Basil Pesambili Mramba apelekwe mahakamani kujibu tuhuma za ufisadi. Je, yawezekana Rais Kikwete amelisahau hilo au rais wetu ana tatizo jingine kubwa zaidi? Jibu unalo wewe msomaji.

Novemba 23, 2008, Basil Pesambili Mramba na Daniel Yona walifikishwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7.

Kufikishwa kizimbani wakati ule kwa mawaziri hao wawili wa zamani kuliashiria mwanzo wa utekelezaji wa ahadi ambazo zimekuwa zikitolewa na Serikali ya Kikwete kuwa itawashughulikia vigogo wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi baada ya wananchi wengi kutoridhishwa na ukubwa wa majina ya watu walioshitakiwa katika kesi ya ufisadi ya EPA.

Ingawa katika mahojiano ambayo Kikwete aliyafanya na Tido Mhando na kurushwa na TBC (mwaka jana) aliahidi kwamba vigogo wengine watatu wangefikishwa mahakamani karibuni, sote tunajua kwamba mpaka leo hakuna kigogo mwingine aliyefikishwa mahakamani, na hivyo Basil Pesambili Mramba na Daniel Yona wanabakia kuwa vigogo pekee waliofikishwa mahakamani mpaka sasa.

Hivyo; inapotokea (kama ilivyotokea wiki iliyopita) Rais Kikwete anasimama jukwaani na kuwasihi wana-Rombo wamchague tena Basil Pesambili Mramba kuwa mbunge wao kwa kuwa ni ‘kiongozi safi’, inatuacha sote midomo wazi kwa mshangao.

Je, amesahau kuwa serikali yake imemfikisha Mramba mahakamani kwa tuhuma za ufisadi, na kesi bado inanguruma Mahakama Kuu? Ni kusahau tu au rais wetu ana tatizo jingine kubwa zaidi?

Lakini kuna upande wa pili wa shilingi wa kauli yake hiyo aliyoitoa Rombo kuhusu Basil Pesambili Mramba. Je, Mahakama Kuu inaweza bado kuendelea na kesi hiyo na kutoa hukumu ya haki; ilhali mkuu wa nchi (ambaye yu juu ya sheria) tayari ameshamsafisha hadharani Basil Pesambili Mramba kuwa ni “mtu safi”?

Je, Mahakama Kuu ambayo majaji wake huteuliwa na Rais, inaweza kuwa na ujasiri wa kumtia hatiani Basil Pesambili Mramba; ilhali mkuu wa nchi ameshamsafisha hadharani kuwa ni “mtu safi”?

Je, kauli ya Rais Kikwete aliyoitoa huko Rombo kumhusu Basil Pesambili Mramba, si kuingilia uhuru wa Mahakama? Je, Kikwete aliikumbuka kesi hiyo ya Mramba wakati alipokuwa akimnadi au aliisahau. Je, ni tatizo la kusahau au ni uzembe kama alivyouliza Msomaji Raia?

Binafsi, ningependa kuujua msimamo wa Jaji Mkuu, Augustine Ramadhani kuhusu kauli hiyo ya Kikwete juu ya Mramba; maana ni jaji mkuu huyo huyo ambaye, Februari 6, 2009, kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria Duniani, alimsifu Rais Kikwete kwa kutoingilia uhuru wa mahakama, hata mara moja, iwe ni kwa matendo ama kwa kauli tangu aingie madarakani.

Ningependa pia kusikia kutoka kwa Kikwete mwenyewe kuhusu suala hili hasa ikizingatiwa kuwa Februari 14, 2006 Ikulu ilisambaza taarifa kwa vyombo vya habari nchini iliyomnukuu Rais akisema kwamba hataingilia kamwe uhuru wa mahakama. Alitoa ahadi hiyo wakati akizungumza na uongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Sitashangaa Mahakama Kuu kuitupilia mbali kesi dhidi ya Mramba baada ya rais mwenyewe kumsafisha kuwa ni ‘mtu safi.’

Ndugu zangu, nimelijadili kwa kirefu suala hili la Rais Kikwete na Basil Pesambili Mramba, kwa sababu si mara ya kwanza kukerwa nalo.

Mara ya kwanza ilikuwa Agosti mwaka huu wakati Rais Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, aliposimamia kikao cha NEC cha kupitisha majina ya wagombea ubunge wa CCM na akawa na ujasiri wa kuruhusu majina ya Basil Pesambili Mramba na Andrew Chenge kugombea ubunge.

Nilimtarajia Kikwete angeweka ngumu majina angalau ya watu hawa wawili yasipitishwe kwa kuwa Chenge bado anaandamwa na kashfa ya rada na Mramba yeye amefikishwa kabisa mahakamani kujibu tuhuma za ufisadi baada ya serikali yake mwenyewe kusaka na kuridhishwa na ushahidi dhidi yake.

Ndugu zangu, Mwalimu Nyerere alikuwa na msemo wake: Caesar’s wife must be above suspicion; yaani ile suspicion tu ingetosha kwa Kikwete kuwaengua Chenge na Mramba. Na kusema kweli, kwa Mramba si suspicion tu; kwani serikali yenyewe ilishafanya uchunguzi na kuridhika na tuhuma dhidi yake, na ndiyo maana iliamua kumpeleka mahakamani.

Sasa, Mwenyekiti huyo wa CCM kuruhusu kupitishwa jina la Basil Pesambili Mramba kugombea ubunge katika kikao kile cha NEC, lilikuwa kosa kubwa kwake kufanya lakini kurudia tena kosa hilo hilo kwa kusimama tena hadharani na kuwataka wana-Rombo kumchagua tena Mramba kuwa mbunge wao kwa kuwa ni ‘kiongozi safi’, hakika kunaibua maswali kuhusu uwezo wa uongozi wa rais wetu huyu!

Najua wapo wasomaji watakaouliza: Angefanyaje? Mimi nadhani, baada ya kufanya kosa lile la kwanza, angekataa kufanya kosa la pili la kumkampenia Mramba; hasa kwa sababu kuna kesi ya ufisadi mahakamani dhidi yake.

Alipofika Rombo angekataa kabisa kumsimamisha Mramba na kumpigia kampeni. Angepanda jukwaani na kujipigia mwenyewe kampeni, na kisha kuendelea na safari yake.

Nyerere alifanya hivyo mwaka 1995 alipokataa jukwaani kumpigia kampeni mgombea wa CCM wa jimbo la Musoma Mjini, Dk. Emmanuel Magoti, kwa kuwa alikuwa na tuhuma za rushwa. Nyerere aliwaambia wapiga kura kwamba angekuwa yeye angempigia kura mgombea wa NCCR, Balozi Ndobo (na ndivyo wapiga kura wale walivyofanya).

Kwa mtazamo wangu, kama kweli Kikwete angekuwa ni mfuasi wa Nyerere, angefuata nyayo zake kwa kufanya hivyo hivyo huko Rombo kwa Mramba.

Niishie hapa, lakini huyo ndiye Kikwete wetu. Kama alivyohoji Msomaji Raia katika makala yake ya wiki iliyopita; nami sijui kama tatizo la rais wetu ni kusahau tu au ana tatizo jingine kubwa zaidi! Tafakari.
 
NUKUU HII IMENIKUNA VILIVYO:- "Wameniambia kuwa Kikwete ni mzigo kwao na kwa taifa. Pili, Kikwete hana risasi za kuwaua Watanzania wote wanaolalamika na kuteketea kwa umaskini mbele ya utajiri wa taifa letu. Hukumu yao kuna siku itatolewa, kama si mwaka huu, basi wakati mfupi ujao.
Na wakati huo hata kama atakuwa hayupo duniani (sote twaenda huko), hata kutemea mate picha yake, kutampa mtu usingizi wa siku moja.
Tatu, uongozi usio na maadili huzaa mamluki wengi. Hivi sasa siri nyingi za Ikulu zimezagaa mitaani kwa sababu tu Kikwete ameruhusu Ikulu pawe pango la mafisadi, wanajimu, wafanyabiashara na matapeli. Watu wasio na maadili hawawezi kutunza siri za nchi, ndo maana hata mikataba ya siri inavuja.
Hawa siku moja watasimama kizimbani, si kama washtakiwa, bali kama mashahidi dhidi ya uongozi wa Kikwete uliokosa mwelekeo na kushindwa "

HII MAKALA EPITOMIZES APPLIED CHRISTIANITY KABISAAAAAAAAAAAAAAAAA...............................................

Ukisoma BIBLICAL DEUTORONOMY 32: 35 yanena busara zifuatazo:- "VENGEANCE IS MINE, AND RECOMPENSE; FOR THEIR FOOT WILL SLIP IN DUE TIME, AND THE DAY OF THEIR CALAMITY IS AT HAND, AND THINGS TO COME HASTEN UPON THEM"

Ukisoma BIBLICAL DEUTORONOMY 32: 36 yanena hivi....."HE WILL JUDGE HIS PEOPLE AND HAVE MERCY UPON HIS SERVANTS; WHEN HE SEES THEIR POWER IS GONE, NOR IS THERE ANY REMAINING; BOND OR FREE"

BIBLICAL DEUTORONOMY 32: 37 imekoleza kama ifuatavyo:- "HE WILL SAY: "WHERE ARE THEIR GODS, THE ROCK IN WHICH THEY SOUGHT REFUGE?"

BIBILICAL DEUTORONOMY 32: 38 imebainisha yafuatayo:- "WHO ATE THE FAT OF THEIR SACRIFICES, AND DRANK THE WINE OF THEIR DRINK OFFERING? LET THEM RISE AND HELP YOU, AND BE YOUR REFUGE."

BIBLICAL DEUTORONOMY 32: 39 imeaasa yafuatayo:- "NOW SEE THAT I, EVEN I, AM HE, THERE IS NO GOD BESIDES ME, I KILL AND I MAKE ALIVE, I WOUND AND I HEAL, NOR IS THERE ANY WHO CAN DELIVER FROM MY HAND."

Ukienda kwenye PSALMS 50:50:15 MWENYEZI MUNGU kwenye UTUKUFU wake alinena yafuatayo:-- "CALL UPON ME ON THE DAY OF TROUBLE I WILL DELIVER YOU, AND YOU SHALL GLORIFY ME."

Katika PSALMS 50:21 MWENYEZI MUNGU alitahadharisha yafuatayo:- "THESE THINGS YOU HAVE DONE AND I KEPT SILENT AND YOU THOUGHT I WAS ALTOGETHER LIKE YOU BUT I WILL REBUKE YOU AND SET THEM IN ORDER BEFORE YOUR EYES." Mwisho wa nukuu.

MWENYE MACHO NA ASIKIE KWANI MWENYEZI MUNGU AMESIKIA KILIO CHA WATANZANIA.....VOTE CHADEMA VOTE DR. SLAA.........
 
Nashukuru Mungu hii makala imeleta changamoto. Jamani tukapige kura basi walau huyu mtu apate kuitikisa sisiemu, hata kama ushindi haupo ila ushindani.
 
Makala nzuri na imejaa kila aina ya ukweli lakini bado ina ile tabia maarufu ya kitanzania: Woga na Unafiki. Kwanini? Katika uma wa viongozi wenzake wa CCM (pamoja na mwandishi wa hii makala) hajapatikani hata mmoja mwenye ujasiri wa kumwambia ukweli? Mbona wananung'unikia uvunguni tu?

Ndg yangu mbona wamemwambia mara nyingi na akaishia kuita wanaongea maneno ya vijiweni! Sikio la kufa halisikii dawa
 
Hii inaonyesha hulka yetu waTZ, kunung'unika lakini tunashindwa kuweka jitihada za kutosha kubadili mfumo huu mbovu.
Nawalaumu sana wale wanaoshiriki vikao vya CC na NEC wakashiriki kutoa maamuzi mabovu kisha utawasikia wakilaumu kama vile hawamo; huu ni unafiki mkubwa![/QUOTE]

Wanafiki katika maisha ya ukombozi wa mwanadamu hawadum kabisa, utoweka kama upepo; yaani hawaishi kati ya watu mara wanaporejea kwa muumba wao. Wanachoacha nyuma yao ni jamii yenye majonzi, na isiyoelewa ni kwa nini walifanya waliyofanya
 
You are innocent until proven guilty inthe court of law and not the other way round, whereby you are guilty until proven innocent. Think about it........:sleepy:
 
Back
Top Bottom