Elections 2010 Kikwete ni msahaulifu au mzembe?

Kha! Watanzania kuna nini tena? Sitaki kuamini kuwa huyu jamaa atarudishwa na watz madarakani
 
Hii inaonyesha hulka yetu waTZ, kunung'unika lakini tunashindwa kuweka jitihada za kutosha kubadili mfumo huu mbovu.
Nawalaumu sana wale wanaoshiriki vikao vya CC na NEC wakashiriki kutoa maamuzi mabovu kisha utawasikia wakilaumu kama vile hawamo; huu ni unafiki mkubwa!
 
siamini kama Lowasa na Malecela ni waoga kiasi hiki yaani mnashindwa kumwambia swahiba wenu mpaka muandike kwa kujificha,kuna mahali mmekosea na wachambuzi tumebaini "ukiwa kwenye vikao vya chama wanasema hujafika????????Lowasa ndio mtu pekee alieandikwa na gazeti langu kuwa hajafika kwenye kikao cha chama kilichofanyika recently,wandugu ujasusi unataka umakini sio kukurupuka tuu,read your steps ,brothers.Sijafurahia unafki huu kwani hata kama jk ana matatizo makubwa nyie mlioyaona na bado mnapiga makofi kuonyesha mnamuunga mkono kwenye vikao vyenu mna matatizo makubwa kuliko yeye,jiangalieni,jitambueni,jeukeni,kuweni wazi na chagueni leo hii bwana wa kumtumikia.
 
Je ni viongozi gani wa Juu kichama na kiserikali waliotofautiana na raisi wamejiuzulu kupinga serikali ya Kikwete? Lakini sitaki kuamini kwamba makosa ya raisi hawayaoni.Wanaitikia ndio mweshimiwa lakini huku wakijua wanaipeleka nchi pabaya,huko ni kusaliti nchi,afadhali ya chief Mangungu alikuwa hajui atendalo.
 
Makala nzuri na imejaa kila aina ya ukweli lakini bado ina ile tabia maarufu ya kitanzania: Woga na Unafiki. Kwanini? Katika uma wa viongozi wenzake wa CCM (pamoja na mwandishi wa hii makala) hajapatikani hata mmoja mwenye ujasiri wa kumwambia ukweli? Mbona wananung'unikia uvunguni tu?
Kumwambia ukweli wapi? huku si ndo kumwambia ukweli? au mpakamtu amfuate jukwaani amchape kiibao kama alivyofanyiwa Mwinyi pale diamond?
 
Tatizo ni wasaidizi wake, wanaomshauri kauri za kusema. perhaps (i am not ruling this out) wanamshauri anakataa kuwasikiliza, i was suprised alipo sema hakukataa kura za wafanyakazi. Rais anatakiwa na intergrity ya kweli hata kama umesema uongo the you may do two things kubali kuwa umekosea and then omba msamahaa au simamia uongo wako badara ya kuukana.

Kukana kauri yako mwenyewe unasababisha intergrity inashuka na watu wanaweza wasikuamini tena,

Kwenye lililoongelewa kwenye makala halina ubishi kwani sasa hivi amefanya kama vile familia nzima ni Raisi, wanafanya kazi za Rais kuanzia baba mpaka watoto
 
Unapokuwa na Rais ambaye afya yake ya UBONGO ina tatizo kila aliye karibu naye ataitumia nafasi hiyo kadri anavyoona inafaa. Hivyo ndivyo mama Salma na familia wanavyofanya; ndivyo Msekwa, Makamba wanavyofanya; ndivyo mawaziri wengi wa cabinet yake wanavyofanya na EL enzi zake kabla ya kujiuzulu ndiye alikuwa mtawala halisi wa nchi hii.
 
bul2.gif
anakumbuka marafiki na kusahau ahadi


naweza kudai kumfahamu kikwete kuliko wengi wa mashabiki wake wanaohudhuria mikutano yake ya kampeni. Nimefanya naye kazi jeshini na serikalini kidogo, lakini nimefanya naye kazi sana kwenye chama. Nimekuwa naye kwa karibu kama rafiki (siyo swahiba) kwa mambo ya kawaida. Anaweza kuandika hotuba nzuri ya kunisifia siku ya mazishi yangu. Haya yanatoka moyoni.
Mwaka 2005 yaliandikwa mengi ya kumsifia. Yakasemwa mengi ya kushadidia sifa zake – muungwana, mtu wa watu, mstaarabu, chaguo la mungu, tumaini lililorejea, mkombozi wa watanzania, musa wa pili na chaguo la watanzania.
Akazoa kura nyingi zikiwamo za wapinzani, maaskofu, vijana, wasomi, wafanyakazi, wakulima, wachimbaji wadogo, wahamiaji haramu, wanajeshi, na wanafunzi. Naam, hata mama ntilie au kwa jina la utani mama lishe! Matumaini yalikuwa makubwa.
Tuseme ukweli, walioonya wazi juu ya hatari ya huko mbele walikuwa wachache sana, na waliodiriki kufanya hivyo kwa uwazi, ilibidi usiku wawe wanahama vyumba vya kulala!
Wapo wachache, hata nikidai mimi ni mmojawapo sitaaminiwa kwa maana hakuna ushahidi wa waliokataa ghiliba hii ndani ya chama chetu. Miaka mitano imekuwa ya mateso makubwa kwetu.
Tumesutwa, tumetukanwa na wanaojifunza kutukana. Tumeitwa majina na tumefikia kuhudhuria vikao vya chama na kuandikwa kuwa hatukuhudhuria kwa sababu ya ukimya wetu.
Kwenye vikao vya kahawa, tumetumiwa wajumbe wa kutuambia hatuwezi kumfufua aliyekwishakufa (nyerere), hatuwezi kurudisha nyuma saa iliyokwishakwenda mbele, wakati umepita, tukae kimya. Nani atabishia simulizi yangu hii? Waliokuwa wachambuzi na wasemaji wa kuwatia moyo watanzania wako wapi? Wote hao wamekwenda, zimebaki sifa zao!
Nirudi kwenye hoja yangu ya leo. Hivi rais kikwete ni msahaulifu au mzembe? Mbona anakumbuka marafiki wake wa zamani na wa karibuni lakini anasahau ahadi zake na kauli zake?
Walio karibu naye katika kampeni watakubaliana nami kuwa kikwete ana kumbukumbu kali juu ya watu aliowahi kuwa nao zamani. Kila sehemu anayofika kwa mkutano atakuambia nani anazaliwa pale, atauliza yuko wapi siku hizi, ataagiza mwambie amtafute wazungumze au ataagiza apatiwe hiki au kile kama ameambiwa kuna shida.
Akiambiwa alikwishakufa, atabadili ratiba akahani msiba au aitiwe mzazi au mjane ampe ubani. Atakumbuka hata dondoo ndogo sana za urafiki wake na mtu huyo.
Hii inavutia wengi na waandishi wetu wameagizwa na kuamriwa kuhakikisha matukio kama hayo yanakuwa katika picha na kurasa za mbele za magazeti.
Wakati huo huo, kikwete ni msahaulifu wa ahadi zake kwa watu binafsi na hata kwa umma. Wapo wanaodai hili si tatizo lake, ni tatizo la watendaji wake ambao wanapaswa ama kuchukua kumbukumbu na kutekeleza au kumkumbusha. Mimi nadhani ni tatizo lake – nitaeleza sasa.
Uaminifu wa kutekeleza ahadi huanza na kauli. Kikwete ni msahaulifu wa aliyoyasema. Ama hatunzi kumbukumbu za aliyosema, au hafikirii madhara ya kauli zake, au yote mawili kwa wakati mmoja.
Alipoingia madarakani alisema “urais wake hauna ubia”. Alilenga kuwajibu waliokuwa wanamsakama kuwa ametekwa na marafiki. Juzi juzi wakati anachukua fomu ndani ya chama, pale dodoma, akakausha macho na kusema; “urais ni suala la kifamilia”. [/color back stubber selfish, ignorant, mwenye visasi, upendeleo.....
Alilenga kuwajibu waliokuwa wanahoji kitendo cha mtoto wake ridhiwani kuzungusha fomu ya kutafuta wadhamini. Mpaka hapa inaonyesha kikwete amesahau alisema nini 2006 au sehemu zote mbili hakufikiri kabla ya kusema. Urais ni taasisi. Urais ni utumishi wa umma. Rais ni mbia wa urais na wananchi wa tanzania. Ndiyo maana mtu haamki asubuhi na kujitangaza kuwa yeye ni rais. Anakwenda kuwaomba wananchi wamchague awe rais. Akishakuwa rais, haina maana urais ni mali yake na familia yake.
Ni kituko kikubwa kwa rais kusema alivyosema kikwete katika hafla hiyo ya dodoma. Katika nchi zenye mifumo makini, serikali ingechukua hatua, au chama husika kingechukua hatua na kama vyote viwili vingeshindwa, basi, wananchi wangechukua hatua kupitia sanduku la kura.
Siyo siri kuwa hivi sasa familia ya rais kikwete imeingia kwa nguvu za ajabu katika uendeshaji wa nchi na hakuna mtu ndani ya chama wala serikali anayeweza kuthubutu kulikemea jambo hili. Uliokuwa ubia wa urais kati ya kikwete na marafiki zake, sasa umegeuka ubia wa kikwete na familia.
Siku hizi si jambo la ajabu kumwona mama salma anaingia ndani ya vikao vya kamati kuu. Kamati ya maadili wananung’unikia kwenye korido, kamati kuu wanaongelea chini chini, wajumbe wa nec hao ndiyo basi! we are not ready for democracy, uhuru wa kuongea bado ni kitendawili. Tutaongea kinachotakiwa sio unachotaka....
Mama salma sasa anafanya majukumu ya kichama bila kibali cha kikao chochote, na mbaya zaidi anaagiza, anakemea, anatishia, ananyang’anya na kugawa madaraka. kampeni ya shuka kwa shuka "hizi slogan" viongozi wa serikali mikoani na wilayani wako hoi. Hawajui wafanye nini na mama huyu.
Mmoja wa wakuu wa mikoa ameniambia, safari hii, hata kwa risasi, hatakubali kuteuliwa kuendelea na ukuu wa mkoa kama mambo yanakuwa hivi. Anadai wiki hii unampokea baba na madai yake, wiki inayofuata anakuja mtoto naye anataka uende uwanjani kumpokea, hujakaa sawa anakuja mama, unaambiwa uhame nyumba kumpisha, siku inayofuata anakuja yule mdogo wa chipukizi, unaambiwa umsindikize mpaka aondoke mkoani kwako.
Mkuu huyo wa mkoa anakang’aka: “tumeteuliwa kutumikia familia”? Polisi wanapiga saluti kwa mama, mtoto ridhiwani anadai ripoti kutoka kwa mkuu wa mkoa? watanzania tuamke kamati za siasa na kamati za ulinzi wanachanganyikiwa hawajui wafanye nini?
Mpaka hapa mtu unajiuliza: Kikwete aliposema hana ubia na mtu alimaanisha nini ikiwa watoto wake wawili na mkewe wanafanya kazi za chama na serikali kwa gharama za serikali? Hapa kinana atatoka huko usingizini na receipt na maneno chungu mbovu
matokeo ya ubia huu wa kikwete na familia yake ni kusitasita kwa kikwete kuchukua hatua muhimu za kurekebisha hali ya nchi.
Watu wamelia, vyombo vya habari vimelalamika na ripoti kadhaa zimeandikwa lakini hakuna hatua iliyochukuliwa dhidi ya mafisadi, wala rushwa, wazembe serikalini, wakwepaji kodi wakubwa, wezi wa nyara za taifa, wauza madawa ya kulevya na majambazi.
Kusitasita kwake kunatokana na hujuma iliyo ndani ya familia yake. Maadui wa ndani ya taifa letu ambao ni mafisadi ni wajanja. wanko nje wanatesa wale wen gine wanachomwa matairi
walipoona kelele za watu zinaanza kumwingia kikwete na kumnyima usingizi, wakamzunguka kupitia familia yake na wanajimu. Wanajua fika hapo hawezi kunasuka. Sasa baadhi yao wamezama katika ufisadi wa kutisha. Ni mungu tu ajuaye hatima yao.tumsaidie mungu kwani alitoa agizo tafuteni mtapata tusimwachie mwenyewe hata yeye anashangaa yanayotokea ,,,,:confused2:
kabla ya kufika mwisho wa “fitina” zangu hizi (ndivyo jk anavyoziita makala hizi), nikumbushe na kusisitiza jambo la msingi. Pamoja na wema wake na misimamo yake tata kuwanadi wenye kesi na mafisadi na kuwaacha wenye kudai haki (mwakyembe......) isiyompa nafasi ya kuwa mtendaji mzuri serikalini na kwenye chama, hivi sasa kikwete ajue yafuatayo yako ukutani (kuendekeza urafiki......).
Nitataja bila kufafanua. Kwanza, pamoja na kusita kuwachukulia hatua mafisadi, hata wao hawamtaki na hawampendi kwa sababu wanamwona ni mdhaifu asiyeweza kuwahakikishia ulinzi mbele ya wanaolalamikia ufisadi.
Wameniambia kuwa kikwete ni mzigo kwao na kwa taifa. Pili, kikwete hana risasi za kuwaua watanzania wote wanaolalamika na kuteketea kwa umaskini mbele ya utajiri wa taifa letu. Hukumu yao kuna siku itatolewa, kama si mwaka huu, basi wakati mfupi ujao.
Na wakati huo hata kama atakuwa hayupo duniani (sote twaenda huko), hata kutemea mate picha yake, kutampa mtu usingizi wa siku moja.
Tatu, uongozi usio na maadili huzaa mamluki wengi. Hivi sasa siri nyingi za ikulu zimezagaa mitaani kwa sababu tu kikwete ameruhusu ikulu pawe pango la mafisadi, wanajimu, wafanyabiashara na matapeli. Watu wasio na maadili hawawezi kutunza siri za nchi, ndo maana hata mikataba ya siri inavuja.
Hawa siku moja watasimama kizimbani, si kama washtakiwa, bali kama mashahidi dhidi ya uongozi wa kikwete uliokosa mwelekeo na kushindwa

we need to change for the best kwa kweli watanzania tuamke tupate katiba inayokubalika na kueleweka na watanzania wote.
msomaji raia​

source: Septemba 15, 2010


please kumbuka kupiga kura tarehe 31 oktoba 2010
 
Tuongee hoja na sio matusi na chuki binafsi bila kupima. matusi na maneno ya kashifa sio utamaduni wa Kitanzania.

Kuna matusi gani hapo wewe mufilisi wa mawazo!! Hata kama ni ndugu yako ukweli lazima uukubali, sisi tumechoka na usanii wake hadi nchi inaelekea pabaya!!! Aachie ngazi atoe nafasi kwa wengine wenye uwezo yeye capacity hana. am sorry to say this
 
siamini kama Lowasa na Malecela ni waoga kiasi hiki yaani mnashindwa kumwambia swahiba wenu mpaka muandike kwa kujificha,kuna mahali mmekosea na wachambuzi tumebaini "ukiwa kwenye vikao vya chama wanasema hujafika????????Lowasa ndio mtu pekee alieandikwa na gazeti langu kuwa hajafika kwenye kikao cha chama kilichofanyika recently,wandugu ujasusi unataka umakini sio kukurupuka tuu,read your steps ,brothers.Sijafurahia unafki huu kwani hata kama jk ana matatizo makubwa nyie mlioyaona na bado mnapiga makofi kuonyesha mnamuunga mkono kwenye vikao vyenu mna matatizo makubwa kuliko yeye,jiangalieni,jitambueni,jeukeni,kuweni wazi na chagueni leo hii bwana wa kumtumikia.
Na Malecela anatajwa wapi kwa muujibu ufukunyuzi wako? Dizaini kama unataka kuhamisha mada vile!!!!
 
poleni sana watanzania.mungu amesikia kilio chenu na mbadilike sasa tofauti na hivyo mtasufer miaka mingine mitano.na sio nikisema mungu amewasikia si kwamba atawachagulia mtu.tumia kura yako 31 october kumchagua dr wa ukweli SLAA.ndipo mungu ataibariki tanzania.na ataiondoa najisi iliyoingizwa ikulu.
 
JK ana sifa zote: usahaulifu na uzembe. sifa zingine ni ufundi wa kulipa kisasi na kulipa fadhila. sifa kuu nyingine ya JK ni kuwa intelligence yake iko low sana!! Pia hana attention na concentration. Kati ya side effects za dawa za kifafa ni kupunguza intelligence, attention, na concentration. Iko siku tutakuja kutawaliwa na kichaa maana ccm wanapitisha wagombea bila umakini
 
:becky: Urais ni suala la kifamilia"; Jakaya Mrisho Kikwete, President of United Republic of Tanzania
 
Kutambua ukweli ni mwanzo wa mabadiliko...watu wenye info kama hizi na zile wanazoziita siri za serikali za kutuangamiza watz basi wazitoe...hatuwezi kulala na kuamka tukute mabadiliko, huu ndo mwanzo wa mabadiliko..na siku wakiondoka madarakani hawatakaa wapate nafasi ya kurudi tena...tutatunga sheria ya kuzuia familia zilizojeruhi taifa hili kutokuruhisiwa kushika madaraka ya aina yoyote katika nchi hii...tunazitambua familia hizo
 
Big up makala hii imetulia kweli..

huyo anayesema ni matusi ndiyo moja ya mafisadi ambao hatuwataki.... kweli mtu mwenye akiliti timamu lazima atayaona hayo yote tena kwa vitendo kabisa....

mimi nasema Tanzania bila ya JK inawezekana,,, tumwache akapumzike zake bagamoyo... atuachie nchi yetu....

uwezo tunao na vijana wenye taaluma tunao na nia ni yetu ....

ALUTA KONTINUA MAPAMBANO YAMEANZA NA TUNAENDELEA.......
 
Tafakuri Jadidi


mbwambo.jpg
Kikwete wetu na Basil Pesambili Mramba!

lC.gif
Johnson Mbwambo​
Septemba 22, 2010
rC.jpg

WAPENDWA, leo, nimeshawishika kuandika rejeo (rejoinder) kuhusu makala iliyoandikwa na Msomaji Raia katika toleo la gazeti hili, wiki iliyopita, ukurasa wa 10, yenye kichwa cha habari: Rais Kikwete msahaulifu au mzembe?
Msomaji Raia alichagua kichwa cha habari chenye swali. Angeweza kuchagua kichwa cha habari hicho hicho bila ya kuweka alama ya kuuliza, lakini hakuchagua kufanya hivyo. Nadhani aliamua kumalizia kwa alama ya kuuliza ili kukwepa kuhukumu, na badala yake kumuachia msomaji aamue mwenyewe kama Rais Kikwete ni msahaulifu au ni mzembe.
Ingawa simfahamu Kikwete kwa karibu kama Msomaji Raia, lakini hata mimi nahangaishwa na kutafuta jibu la swali hilo hilo: Je, tatizo la Kikwete ni usahaulifu au ana tatizo jingine kubwa zaidi?
Yawezekanaje (kama alivyobainisha Msomaji Raia) Kikwete atoe tamko thabiti kwa Watanzania kwamba urais wake hauna ubia na mtu mwingine yeyote, na kisha miaka mitano baadaye rais huyo huyo awe na ujasiri wa kuuambia tena umma wa Watanzania kwamba urais ni suala la kifamilia? Yawezekana aliisahau kauli yake hiyo ya mwanzo?
Kwa hakika, ukitaka kuandika kauli ambazo Kikwete alipata kuzitoa na baadaye akatoa nyingine kinyume kabisa na zile za mwanzo, au hatua alizochukua na baadaye akafanya kinyume chake, unaweza kujaza kitabu kizima.
Chukulia, kwa mfano, tukio la wiki iliyopita la huko Rombo ambako alijipa ujasiri kupanda jukwaani na kuwasihi wana-Rombo wamchague tena Basil Pesambili Mramba kuwa mbunge wao kwa kipindi kingine cha miaka mitano kwa kuwa ni "mbunge safi", na kummwagia sifa kemkem.
Akiwa ameunyanyua juu mkono wa Mramba, Rais Jakaya Kikwete alisema hivi kuhusu mgombea ubunge huyo wa CCM: "Huyu kwa maneno ya mjini ni mzee kijana kwani ni mwenye mawazo mapya yenye manufaa wakati wote…siyo wale wazee ambao wakichoka la mbele linawekwa nyuma na la nyuma linawekwa mbele. Huyu ubongo wake unajadidika, ni chimbuko la maarifa mapya (rejea blogu ya kampeni za CCM inayoitwa Chagua Kikwete 2010 ambayo anuani yake ni jakayakikwete2010.blogspot.com).
Tukio hilo la Rais Kikwete kumnadi Mramba kwa kummwagia sifa kemkem liliibua maswali mengi kichwani mwangu; hasa nikikumbuka kwamba ni Kikwete huyo huyo ambaye aliidhinisha Basil Pesambili Mramba apelekwe mahakamani kujibu tuhuma za ufisadi. Je, yawezekana Rais Kikwete amelisahau hilo au rais wetu ana tatizo jingine kubwa zaidi? Jibu unalo wewe msomaji.
Novemba 23, 2008, Basil Pesambili Mramba na Daniel Yona walifikishwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7.
Kufikishwa kizimbani wakati ule kwa mawaziri hao wawili wa zamani kuliashiria mwanzo wa utekelezaji wa ahadi ambazo zimekuwa zikitolewa na Serikali ya Kikwete kuwa itawashughulikia vigogo wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi baada ya wananchi wengi kutoridhishwa na ukubwa wa majina ya watu walioshitakiwa katika kesi ya ufisadi ya EPA.
Ingawa katika mahojiano ambayo Kikwete aliyafanya na Tido Mhando na kurushwa na TBC (mwaka jana) aliahidi kwamba vigogo wengine watatu wangefikishwa mahakamani karibuni, sote tunajua kwamba mpaka leo hakuna kigogo mwingine aliyefikishwa mahakamani, na hivyo Basil Pesambili Mramba na Daniel Yona wanabakia kuwa vigogo pekee waliofikishwa mahakamani mpaka sasa.
Hivyo; inapotokea (kama ilivyotokea wiki iliyopita) Rais Kikwete anasimama jukwaani na kuwasihi wana-Rombo wamchague tena Basil Pesambili Mramba kuwa mbunge wao kwa kuwa ni ‘kiongozi safi', inatuacha sote midomo wazi kwa mshangao.
Je, amesahau kuwa serikali yake imemfikisha Mramba mahakamani kwa tuhuma za ufisadi, na kesi bado inanguruma Mahakama Kuu? Ni kusahau tu au rais wetu ana tatizo jingine kubwa zaidi?
Lakini kuna upande wa pili wa shilingi wa kauli yake hiyo aliyoitoa Rombo kuhusu Basil Pesambili Mramba. Je, Mahakama Kuu inaweza bado kuendelea na kesi hiyo na kutoa hukumu ya haki; ilhali mkuu wa nchi (ambaye yu juu ya sheria) tayari ameshamsafisha hadharani Basil Pesambili Mramba kuwa ni "mtu safi"?
Je, Mahakama Kuu ambayo majaji wake huteuliwa na Rais, inaweza kuwa na ujasiri wa kumtia hatiani Basil Pesambili Mramba; ilhali mkuu wa nchi ameshamsafisha hadharani kuwa ni "mtu safi"?
Je, kauli ya Rais Kikwete aliyoitoa huko Rombo kumhusu Basil Pesambili Mramba, si kuingilia uhuru wa Mahakama? Je, Kikwete aliikumbuka kesi hiyo ya Mramba wakati alipokuwa akimnadi au aliisahau. Je, ni tatizo la kusahau au ni uzembe kama alivyouliza Msomaji Raia?
Binafsi, ningependa kuujua msimamo wa Jaji Mkuu, Augustine Ramadhani kuhusu kauli hiyo ya Kikwete juu ya Mramba; maana ni jaji mkuu huyo huyo ambaye, Februari 6, 2009, kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria Duniani, alimsifu Rais Kikwete kwa kutoingilia uhuru wa mahakama, hata mara moja, iwe ni kwa matendo ama kwa kauli tangu aingie madarakani.
Ningependa pia kusikia kutoka kwa Kikwete mwenyewe kuhusu suala hili hasa ikizingatiwa kuwa Februari 14, 2006 Ikulu ilisambaza taarifa kwa vyombo vya habari nchini iliyomnukuu Rais akisema kwamba hataingilia kamwe uhuru wa mahakama. Alitoa ahadi hiyo wakati akizungumza na uongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Sitashangaa Mahakama Kuu kuitupilia mbali kesi dhidi ya Mramba baada ya rais mwenyewe kumsafisha kuwa ni ‘mtu safi.'
Ndugu zangu, nimelijadili kwa kirefu suala hili la Rais Kikwete na Basil Pesambili Mramba, kwa sababu si mara ya kwanza kukerwa nalo.
Mara ya kwanza ilikuwa Agosti mwaka huu wakati Rais Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, aliposimamia kikao cha NEC cha kupitisha majina ya wagombea ubunge wa CCM na akawa na ujasiri wa kuruhusu majina ya Basil Pesambili Mramba na Andrew Chenge kugombea ubunge.
Nilimtarajia Kikwete angeweka ngumu majina angalau ya watu hawa wawili yasipitishwe kwa kuwa Chenge bado anaandamwa na kashfa ya rada na Mramba yeye amefikishwa kabisa mahakamani kujibu tuhuma za ufisadi baada ya serikali yake mwenyewe kusaka na kuridhishwa na ushahidi dhidi yake.
Ndugu zangu, Mwalimu Nyerere alikuwa na msemo wake: Caesar's wife must be above suspicion; yaani ile suspicion tu ingetosha kwa Kikwete kuwaengua Chenge na Mramba. Na kusema kweli, kwa Mramba si suspicion tu; kwani serikali yenyewe ilishafanya uchunguzi na kuridhika na tuhuma dhidi yake, na ndiyo maana iliamua kumpeleka mahakamani.
Sasa, Mwenyekiti huyo wa CCM kuruhusu kupitishwa jina la Basil Pesambili Mramba kugombea ubunge katika kikao kile cha NEC, lilikuwa kosa kubwa kwake kufanya lakini kurudia tena kosa hilo hilo kwa kusimama tena hadharani na kuwataka wana-Rombo kumchagua tena Mramba kuwa mbunge wao kwa kuwa ni ‘kiongozi safi', hakika kunaibua maswali kuhusu uwezo wa uongozi wa rais wetu huyu!
Najua wapo wasomaji watakaouliza: Angefanyaje? Mimi nadhani, baada ya kufanya kosa lile la kwanza, angekataa kufanya kosa la pili la kumkampenia Mramba; hasa kwa sababu kuna kesi ya ufisadi mahakamani dhidi yake.
Alipofika Rombo angekataa kabisa kumsimamisha Mramba na kumpigia kampeni. Angepanda jukwaani na kujipigia mwenyewe kampeni, na kisha kuendelea na safari yake.
Nyerere alifanya hivyo mwaka 1995 alipokataa jukwaani kumpigia kampeni mgombea wa CCM wa jimbo la Musoma Mjini, Dk. Emmanuel Magoti, kwa kuwa alikuwa na tuhuma za rushwa. Nyerere aliwaambia wapiga kura kwamba angekuwa yeye angempigia kura mgombea wa NCCR, Balozi Ndobo (na ndivyo wapiga kura wale walivyofanya).
Kwa mtazamo wangu, kama kweli Kikwete angekuwa ni mfuasi wa Nyerere, angefuata nyayo zake kwa kufanya hivyo hivyo huko Rombo kwa Mramba.
Niishie hapa, lakini huyo ndiye Kikwete wetu. Kama alivyohoji Msomaji Raia katika makala yake ya wiki iliyopita; nami sijui kama tatizo la rais wetu ni kusahau tu au ana tatizo jingine kubwa zaidi! Tafakari.
hs3.gif
 
Makala imetulia, Huyo Kikwete si msahaulifu au mzembe, bali ni mpumbavu na mpumbafuuuuuuuuuu!:A S 100:
 
Back
Top Bottom