Kikwete ni kiongozi mzuri sana kwa mtazamo wangu, lakini ushkaji sasa..

jamani kuwa raisi haimaanishi uadui na watu wengine, kumbuka na yeye anahitaji marafiki, kama marafiki wazingua ndio hivyo taratibu wanawajibishwa, mambo taratibu jamani
 
Let's be patients.. May be he can do somthng regards frauds of tha ministaz, as he outlined that in his speech. He is good in a sense of tolerance and smhw wisdom on decision.. Remember u must be a human for real to hear and take no actions to people insults u publiclyt (regards he holdws the authoritative power) And in most african states, presidents intervenes and effects the court proceedings and decision, so he is able to just ban some media and sue people, (unfair and unjustfiable ground)
 
Hutoba zake nyingi ni nzuri sana na hata leadership yake. Haiwezekani ukawa leader na administrator, hotuba zake ni miongozo ambayo kwayo watekelezaji wanatakiwa watafisiri katika matendo na si yeye tena. Sasa hapa ndipo swali la kuku au yai lipi linaanza katika kupata hao watekelezaji!
 
Hii ikoje - Rais Kikwete na taarifa za CAG.
Nashindwa kuelewa ni jinsi gani watawala ama viongozi wetu wanavyowachukulia wananchi, kwamba ni watu wenye upeo mdogo wa kuelewa, au hawana uwezo wa kutafakari mambo au matukio mbalimbali yanayotokea hapa nchini.

Katika kikao cha bunge kilichopita, kumetolewa taarifa za ubadhirifu mkubwa wa fedha na mali ya umma kutokana na ripoti za CAG.
Viongozi kadhaa wakiwemo mawaziri na waandamizi wakuu wa serekali, wametajwa kuhusika na ubadhirifu huo.
Aidha, ni dhahiri kwamba ripoti za namna hii zimekuwa zikitolewa kila mwaka na hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa kwa wahusika, hata pale wanapobainika wazi. Kumekuwa na dhana ya kulindana na kutowajibika!
Tusisahau kwamba, kumekuwepo ushindani na tabia kwa watendaji wa serekali kama ya kuwazomea wabunge pale taratibu zinapokwama kuwawajibisha, baya zaidi, ni pale spika wa sasa anapoungana na upande wa serekali, what a shame!
Viongozi wamezifanya ofisi za serekali kama taasisi zao au miradi yao binafsi. Cha ajabu zaidi, kiongizi aliyewapa madaraka au anayewateua, amekuwa akikaa kimya kana kwamba hakuna jambo lolote muhimu lililotokea. Maswala yote mazito amekuwa akiyachukulia kirahisi rahisi tu huku akitabasamu!
Pale inapobidi, basi utaona anakimbia kuongea na wazee wa Dar es salaam! Natafuta dhumuni lake hapa huwa ni nini, lakini sipati jibu kabisa! Kwa nini asiongee na wasomi na watu wenye upeo mzuri wa kuelewa!
Ubadhirifu wa mali za umma, limekuwa ni swala la kawaida kabisa, hakuna kiongozi anayeonekana kukerwa na tabia hii, wale wachache wanaojitokeza, basi wataondolewa sehemu hizo muhimu kwa makusudi, kwa kuwa wanakwamisha mipango ya mafisadi! Miradi si miradi, mipango si mipango, ili mradi mbinu lukuki za kuongeza maeneo na mitandao wa ulaji, kasma zipatikane, mafisadi wafaidike!
Nakumbuka, kuna mbunge mmoja, [simkumbuki kwa jina] aliwahi kugusia miradi lukuki ya mashirika ya serekali likiwemo NSSF [ndani ya wizara ileile ya fedha, inayotuangamiza] kama miradi hii inalipa, na inalipa baada ya muda gani?
Mimi naungana naye, kwani hii imekuwa mbinu ya watendaji serekalini kubuni namna ya kujitengenezea pesa! Miradi imekuwa mingi, lakini hatuambiwi, what are the returns! Mfano mmoja, hivi lile jengo la NSSF pale Mwanza, bado tupu, halijajaa, litalipa lini pesa iliyowekezwa? Kodi pale haishikiki, kulikuwa na Hotel pale [Nimefanya kazi Hotelini hapo na gharama za pango nazijua, hazishikiki], mmiliki wa Hotel ameshindwa kumudu pango, amefungiwa, ameacha madeni! Najiuliza ni nani sasa ataweza kuiendesha hoteli ile kwa gharama hiyo ya pango? mifano ni mingi!
Tusahau hilo la NSSF. Katika sikukuu ya may mosi mwaka huu, kama sijakosea, Rais Kikwete, alisema kwamba, taarifa za CAG zimeanza kuwekwa wazi zaidi. Pili taarifa hizi sasa huanza kufanyiwa kazi mara moja na watedaji wa serekali hususani usalama wa taifa.
Kutoka na kauli yake hiyo, nabaki na maswali kadhaa ya kujiuliza:
1. Wakati taarifa hizi zikisomwa Bungeni, msemaji wa serekali pale bungeni au mawaziri husika, hawakuwa na majibu haya kwa ajili ya kuwapa wabunge? au waliagizwa kutosema chochote, na rais angejibu katika sherehe za May mosi?
2. Je, majibu haya, yalikuwa siri ya rais pekee na watendaji wake wa usalama wa taifa?
3. Je, hata Waziri mkuu hakujua lolote kwamba, taarifa hizo huanza kufanyiwa kazi mara moja na usalama wa taifa! Sitashangaa, kwani hata alipokuwa akifunga kikao, hakuwa na lolote la kusema, licha ya hoja zote nzito zilizojitokeza, alifunika kikombe, period!
4. Ni chombo kipi cha usalama cha serekali kinawajibika na maswala haya? usalana wa taifa na ubadhirifu wa pesa, wapi na wapi? Nashindwa kuelewa, polisi watafanya kazi gani, taasisi ya kuzuia rushwa je?
Maswali ni mengi ambayo yanakosa majibu, viongozi wa nchi wamekosa kabisa mwelekeo, wanasemana hovyohovyo jinsi wasivyoelewana katika utendaji wao, ni uongozi wa namba gani huu!
Viongozi wengine wamekiri kutokuwa na meno, kama hawana meno, ni wa nini zaidi ya kutuongezea gharama za uendeshaji.
Mawaziri ni wa nini, wana kazi gani kama hawana sauti, na wizara zinaweza kuongozwa na makatibu wakuu. Wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wana kazi gani hawa hasa, siasa hadi chumbani! [wabunge, tuangalie pia hivi viti maalumu kama vina ulazima wowote, au gharama tu] Vyeo hivi vimekuwa vya kwa ajili ya kuwazawadia watu maalum au maswahiba tu! Sioni mantiki yake kabisa! Watu wanakataliwa na wananchi katika uchaguzi, kiongozi wa nchi anawapa madaraka sehemu nyingine, kwa nini?
Imefika muda sasa, wadanganyika kuamua na kuchagua uongozi bora wanaoutaka, kuyakataa maovu yote haya yanayofanywa wazi wazi na viongozi waliopo madarakani, kwa kijitojeza kwa wingi na kuwanyima kura hawa, katika chaguzi zijazo.
Neno mafisadi, limekuwa la kawaida kabisa, maana wanalindwa, na isitoshe wana mengi mazito wanayoyajua na wanayahifadhi, kiasi kwamba viongizi wengi hawawezi kuthubutu kuwanyooshea kidole! Kwa kuwa wote, lao ni moja!
Mungu ibariki Tanganyika, maana muungano nao ni kitendawili, wazanzibar hawautaki, tunawakumbatia na kwang'ang'ania, wa nini?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom