Kikwete (na serikali yake) anaogopa kumshtaki Balali

Ufisadi BoT: CCM matatani

Waandishi Wetu Januari 23, 2008



CHAMA cha Mapinduzi (CCM) na Serikali yake vi mtegoni, na itabidi kuamua kusuka ama kunyoa kwa kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba fedha zilizochukuliwa kutoka Benki Kuu (BoT) chini ya Mpango wa Ununuzi Madeni (EPA), ziliingizwa katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, uliokipa chama hicho ushindi wa kishindo, Raia Mwema imedokezwa.

Vyanzo mbalimbali vya habari vimeiambia Raia Mwema kwamba kiasi cha Shilingi bilioni 40 kilichochukuliwa na kampuni ya Kagoda Agricultural Limited (KAL) ili zikafanye kile kinachoelezwa kuwa ni kazi “nyeti za usalama wa nchi” sehemu yake iliingizwa katika uchaguzi.

Baadhi ya wabunge wa CCM waliozungumza na Raia Mwema, wamesema kwamba wana taarifa kwamba baadhi yao walipata “msaada” ili kufanikisha uchaguzi wao majimboni japo kwamba “msaada” huo ulitofautiana kati ya mbunge na mwingine, kulingana na mhusika ni nani.

Kwa mujibu wa wabunge hao, ambao kwa sababu za wazi hatutawataja majina, walikuwa wakipata kati ya Shilingi milioni moja hadi milioni 20, na kwamba katika matukio kadhaa baadhi yao walilalamika Makao Makuu ya chama kuhusiana na kwa nini “msaada” huo haukutolewa kwa kiasi kinacholingana kwa wote.

Aidha, Raia Mwema imefahamishwa kwamba kwa jinsi fedha hizo zilivyokuwa nyingi, baadhi ya wajanja ndani ya CCM waliunda mpango wa kupora sehemu yake. Kati ya matukio hayo ya uporaji lipo moja la Dar es Salaam ambako kiasi cha Shilingi milioni 600,000 taslimu zilichukuliwa lakini taarifa za wizi huo hazikufikishwa Polisi.

Aidha, vyanzo hivyo vya habari vinasema katika tukio jingine, mjumbe aliyetumwa apeleke fedha kiasi cha Shilingi milioni 200 Kanda ya Ziwa, badala ya kufikisha kiasi chote, aliwasilisha Shilingi milioni 80, na aliyekabidhiwa hizo 80 naye akawasilisha milioni 20.

Ni suala hilo, kati ya mengine, vyanzo hivyo vya habari vinasema, lililosababisha mvutano mkubwa wa uongozi hasa katika Mkoa wa Mwanza, ambako viongozi kadhaa waliwajibishwa, na wengine kuhamishwa kutokana na utata katika mgao wa fedha hizo

Tayari CCM, kwa kuhisi unyeti wa suala hilo, kimekanusha kuwako kwa uwezekano wa fedha hizo kuingizwa katika kampeni. Katika mahojiano na baadhi ya vyombo vya habari vilivyochapisha habari za kuhusiana na fedha hizo mwishoni mwa wiki iliyopita, vilivyowanukuu vigogo kadhaa wa chama hicho, akiwamo Katibu Mkuu, Yusuf Makamba, CCM kimesema hakikutumia fedha hizo.

Alisema Makamba katika mahojiano ya simu na gazeti moja wiki iliyopita: "Kwanza, siijui kabisa kampuni hiyo ya Kagoda, na chama changu huwa hakipokei fedha kutoka kwenye makampuni, zikija za Msamaria mwema kama wewe, nazipokea na ninatoa risiti. hesabu zetu ziko wazi, zimekaguliwa na juzi tu tumezipeleka kwa Msajili wa Vyama.”

Akijibu gazeti jingine juu ya habari hizo Makamba alisema:"Sisi tuna wanachama, ruzuku na mali zinazokifanya chama kijitosheleze. Ballali ana ofisi yake na mimi nina ofisi yangu, mlango wa kuingilia kwake siujui na wala alivyokuwa akinunua magari sifahamu."

Aliendelea Makamba: "Hatuna deni lolote, wala hatuzijui hizo hela, wanaosema hivyo walizipitishia wapi? Wanaotaka kuja kutuchunguza waje wakati wowote".

Alipoulizwa iwapo CCM haihusiki na mtandao uliochota fedha BoT ni kwa nini imekuwa ikihusishwa na kutajwa mara kwa mara, alijibu:

"Watu wanaotaja chama changu mimi sina tatizo nao, wewe mbona mke wako anakutaja taja kwani umemkosea nini?", alihoji huku akisisitiza kuwa ofisi ya Ballali na ya CCM ni vitu viwili tofauti.

Alisisitiza kuwa CCM ina vyanzo vya mapato vinavyojulikana na anayetaka kujua hayo aende akachunguze ripoti ya mapato na matumizi ya chama hicho iliyokwisha kuwasilishwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, ya kipindi cha mwaka 2005 hadi 2007.

"Hesabu za CCM zimekaguliwa na ziko wazi, tunaendesha chama kwa ruzuku na tuna rasilimali za kutosha," aliongeza Makamba.

Makamba, kwa mujibu wa gazeti hilo, alionyesha mshangao kwa wanaohoji matumizi ya chama hicho ambayo aliyaita kuwa "ni ya kawaida," wakati vipo vyama, alivyodai vina matumizi makubwa lakini watu hawavihoji.

"Hebu niambie CCM inatumia helikopta? Lakini (Chama cha Demokrasia na Maendeleo) Chadema, wanatumia helikopta, mbona hamuwaulizi walitumia Shilingi ngapi? CCM mnaitakia nini," alihoji.

Mwingine aliyezungumzia suala hilo ni Katibu wa Uenezi wa CCM, Kapteni mstaafu John Chiligati. Alisema Chiligati: "Mimi hilo silijui na wala sina taarifa nalo."

Kwa upande wake, Katibu wa Uchumi na Fedha, Amos Makalla ambaye alishika nafasi hiyo Oktoba mwaka jana, akimbadili Mbunge wa Igunga na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rostam Aziz, alisema: "Suala hilo ni uzushi unaofaa kupuuzwa. CCM ina utaratibu wa kupata mapato kupitia vitega uchumi vyake vilivyoko nchi nzima".

Aliongeza Makalla: "Hao wanaodai kuwa CCM inahusika na ubadhirifu wa fedha BoT ninawashangaa sana. Watu husema kama hujafanya utafiti, huna takwimu, huna haki ya kuongea na wanaosema hivyo ni wababaishaji wanaotaka kukipaka chama matope.

"CCM inampongeza Rais Jakaya Kikwete kwa ujasiri aliochukua wa kuweka mambo wazi na kwamba ujasiri huo ndio ambao unawafanya wananchi waendelee kumwamini katika utendaji wake wa kazi".

Mwingine aliyezungumzia suala hilo kwa mujibu wa magazeti hayo ya wiki iliyopita ni Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Phillip Mangula, aliyekuwa mtendaji mkuu wa chama hicho hadi mwishoni mwaka 2005.

"Suala hilo uongozi wa sasa unaweza kulizungumzia zaidi, lakini ninavyofahamu kwa mwaka 2005 chama kilikuwa na uwezo wa kujiendesha chenyewe bila kutegemea mtu.

"Tuna wanachama zaidi ya milioni 3.6 nchi nzima. Hao kama kila mmoja angechanga sh. 1000 tu unaweza kuona tungekuwa na fedha nyingi," alisema na kuongeza:

"Mwaka 2005 tulijipanga na tulikuwa na kamati mbalimbali ndani ya chama kama za Uchaguzi, Fedha, Vifaa na pia kuna wanachama na mashabiki wetu walijitolea kuchangia vitu kama kofia na fulana, kwa hiyo suala la chama kujitosheleza lingewezekana kabisa," alisema Mangula.

Vyanzo vya habari vilivyozungumza na Raia Mwema vinasema kwamba kujitokeza kwa vigogo hao wa CCM kuzungumzia suala lilelile, kwa wakati uleule, ni ishara kwamba hilo si jambo la kupuuza, na kama CCM haitacheza karata zake vizuri, litaibukia kuwa kashfa kubwa kwa chama hicho na Serikali kwa ujumla.

“Wako (CCM) katika harakati za kujaribu kufunika mambo. Wanazima moto. Na inaelekea hata nyinyi wenye vyombo vya habari mnataka suala hili liishe hivi hivi. Lakini hili si jambo la kumalizika hivyo. Mwaka 2010 kutakuwa na uchaguzi hapa. Mkiliacha yatajirudia hayahaya na huenda wengine wakachota tena BoT,” anasema mmoja wa vyanzo hivyo.

Vyanzo vya Habari pia vimeliambia Raia Mwema kwamba Kagoda Agriculture Company ilianzishwa kwa maelekezo ya Rais Benjamin Mkapa, na kwamba sababu za “usalama wa taifa” zilizotumiwa kuhalalisha kuchukuliwa kwa pesa hizo ndizo alizoambiwa Ballali na ndizo pia alizomwambia Meghji.

Aidha, nyaraka za kuuziana deni kati ya BoT na Kagoda zilisainiwa katika ofisi ya mwanasheria mmoja wa Dar es Salaam na katika kusaini huko, kulikuwa na Ofisa wa BoT na mmoja wa viongozi wa fedha katika kamati ya kampeni ya CCM.

Raia Mwema limeonyeshwa na mmoja wa watuhumiwa wa ufisadi huo wa BoT nakala ya hundi ya malipo kwa Katibu Mkuu wa CCM.

Habari zaidi zinasema pia kwamba kampeni za uchaguzi wa mwaka huo zilikuwa zikiendeshwa nje ya ofisi ya makao makuu ya CCM, na hivyo kumfanya aliyekuwa Katibu Mkuu, Mangula asijue kila kitu kilichokuwa kikiendelea.

“Kampeni ziliendeshwa katika ofisi binafsi ya mmoja wa wajumbe wa sasa wa Kamati Kuu ya CCM na huko ndiko fedha zote za kampeni zilipelekwa, na hivyo CCM kutaka kujiaminisha kuwa haihusiki na fedha chafu ni kujaribu kuficha ukweli,” kilisema chanzo hicho cha habari.

“Fedha zilizochotwa BoT na Kampuni ya Kagoda zililipwa kupitia benki moja ya ndani na hii inarahisisha sana kazi ya uchunguzi kwani ni rahisi sana kujua ni nani alikwenda kuchukua fedha hizo Benki,” kilisema chanzo hicho cha Habari.

Aidha baadhi ya watu ndani ya vyombo vya dola waliohojiwa na gazeti hili wanasema, kama kweli Serikali ina nia ya dhati kushughulikia wahusika, kamati inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, haipaswi kusubiri kufikisha kundi la watuhumiwa mahakamani na badala yake kufikisha wale ambao ushahidi wa jinai dhidi yao uko wazi kabisa kama ule wa Kagoda.

Katikati ya sakata hili la BoT ni Dk. Daudi Ballali - Gavana wa zamani wa BoT aliyetimuliwa kazi hivi karibuni na Rais Kikwete. Dk. Ballali, ambaye amekuwa akijiuguza nchini Marekani, ndiye anayeonekana kutwishwa mzigo wote wa ubadhirifu ndani ya benki hiyo mhimili wa uchumi wa Tanzania.

Taarifa za karibu na yeye zilizoifikia Raia Mwema, zinasema amekuwa akishangazwa na jinsi ambavyo vigogo wanavyojitahidi kumgandamiza katika suala hilo.

“Bado anaumwa. Anahisi kuwa ugonjwa wake, pamoja na sababu nyingine, umetokana na sumu, walau madaktari bingwa wa Marekani anakotibiwa wamemwambia kuwa alikula sumu. Kwa hiyo amefanyiwa operesheni ya tumbo. Haijulikani itachukua muda gani kupona, na ndiyo maana aliandika barua ambayo haikujibiwa ya kujiuzulu. Lakini Mungu si Athumani. Akijalia Mwenyezi atapona. Akipona, kama ambavyo wote tunaomba kwa Mungu, atakuja kuzungumza.

“Ana kila ushahidi. Ana kila aina ya nyaraka zilizokuwa zikimtaka afanye nini. Hakika akifanikiwa kuzungumza watu wataumbuka. Si kuwa yeye ni malaika, lakini madhambi mengi wanataka kumbebesha yeye,” alisema.

“Na hicho ndicho vigogo nchini wanachokiogopa. Akiweza kusema tutashangaa, na tutawashangaa viongozi wetu. Hivyo ili asiweze kusema ndiyo kila mara unasikia mara kafukuzwa kazi, mara visa yake imetenguliwa na mara anakaribia kufa.

“Wanataka afe ili siri isifichuke. Kuna uongo mwingi. Na mwenye ufunguo wa uongo huo ni yeye. Anajua na hata baadhi ya wafanyakazi wa BoT wanajua nani alikuwa akishinda ofisini kwake, kwa mfano, kushinikiza malipo ya kampuni ya Kagoda.”

Ndugu huyo wa karibu wa Dk. Ballali amesema Gavana huyo aliyepita wa BoT anataka afikishwe Mahakamani ili ukweli wa nani alishiriki vipi uweze kuanikwa huko.

“Ametuambia kwamba anataka sana kwenda Mahakamani. Huko anatarajia jina lake litasafishwa. Na wanaombeza leo nao sheria ichukue mkondo wake juu yao,” anasema ndugu huyo wa Dk. Ballali ambaye anazungumza naye mara kwa mara.

Baadhi ya wakongwe katika fani ya sheria wanasema endapo kweli Serikali italifikisha suala hilo Mahakamani, itasaidia kuibua mambo mengi ambayo pengine yakafungua ukurasa mpya wa demokrasia na utawala bora.

Source:

http://www.raiamwema.co.tz/08/01/23/1.php
 
baadhi ya wajanja ndani ya CCM waliunda mpango wa kupora sehemu yake. Kati ya matukio hayo ya uporaji lipo moja la Dar es Salaam ambako kiasi cha Shilingi milioni 600,000 taslimu zilichukuliwa lakini taarifa za wizi huo hazikufikishwa Polisi.

Aidha, vyanzo hivyo vya habari vinasema katika tukio jingine, mjumbe aliyetumwa apeleke fedha kiasi cha Shilingi milioni 200 Kanda ya Ziwa, badala ya kufikisha kiasi chote, aliwasilisha Shilingi milioni 80, na aliyekabidhiwa hizo 80 naye akawasilisha milioni 20.

Hii kweli inafurahisha sana. naweza kusema the most interesting of all. Sasa angalia kama ni hao hao walioko kwenye nyadhifa za serikali watafanyaje na pesa za serikali
 
Mwafrika wa kike kila kukicha inaonyesha ur not matured enough kua hapa JF.Or Usitake sisi watu wa zamani turejee ktk imani yetu ya zamani kua KINA DADA BADO MUDA WA KUWAPA PLATFORM ZA KUJADILI NA KUTOA MAAMUZI BADO MUENDELEE KUKAA JIKONI NA KULEA WATOTO.

Wewe Mwenyewe hapo ulipo ni jikoni na unalea wazee na watoto. Huoni kuwa unatia aibu kwa kudhani wenzako watafanya unachofanya?
Au unataka niwaeleza memba hapa kazi yako unayofanya nyakati za usiku?
 
Kwi kwi kwi kwiii Tueleze Mwafrika wa kike maana ID tu ndio inakatazwa usiitaje ila anapokaa na kazi yake RUKHSA!:)
 
Kwi kwi kwi kwiii Tueleze Mwafrika wa kike maana ID tu ndio inakatazwa usiitaje ila anapokaa na kazi yake RUKHSA!:)

FD,

Heshima mbele mkuu.

Leo jumatano mkuu ngoja tuendelee kukata issues for now tukisubiri weekend wakati wa free style........lol
 
Now as we guessed, Ballali is yet to be Mtuhumiwa! unless he is implicated, then exreadition process will start!
Niliwaambia hakuna shitaka la uzembe na tamko la Mwapachu lina maana kuwa Ballali si fisadi bado! The underlying word is MIGHT!

Govt might process Ballali`s extradition

2008-01-23 08:56:27
By Rose Mwalongo


The government has said it will seek extradition of former governor of the Bank of Tanzania Dr Daud Ballali, who is now in the USA, if he will be implicated in the External Payments Account (EPA) scandal.

Public Safety and Security minister Harith Mwapachu told The Guardian yesterday that all those involved in the scandal would be brought to justice.

Dr Ballali was sacked by President Kikwete early this month after the central bank under his leadership occasioned multi billion loses through dubious payments and dealing with phony companies in 2005.

Ballali was in the USA undergoing treatment when the President rescinded his appointment. He has not returned home yet.

President Kikwete had appointed a probe team to investigate companies and individuals who were involved in the shoddy deals.

Yesterday, Mwapachu said if Dr Ballali would happen to be one of the people implicated in the EPA scandal, he would definitely be required to return to the country to face justice.

Tanzania Ambassador to Washington Ombeni Sefue was quoted by the local media on Monday as saying that Dr Ballali, whose whereabouts has been the talk of town, is still in the USA.

He said Ballali, who he said was in stable condition, was receiving medical care in Boston, Massachusetts.

The US government withdrew Ballali?s visa last week following his removal from the post.

Mwapachu said the government could make use of the transnational crime treaty or the extradition treaty to get Dr Ballali back home should the presidential probe committee implicate him in the multi billion loss of public funds.

Asked as to whether they were sure that Ballali would not escape if implicated, Mwapachu said: ``You can run but you can`t hide in this world. It is the era of globalization.``

He, however, said he hoped things would not go to that extent, adding, ``He (Ballali) is aware of the allegations. We hope he will willingly come to answer the charges in case he is implicated.``

Speaking to The Guardian, Deputy Minister for Foreign Affairs and International Cooperation Dr. Cyril Chami said he did not know when Ballali would return home.

``It is up to his doctors to decide. He is an individual who has gone for treatment and the world is big,`` he said.
  • SOURCE: Guardian
 
Quote: Halisi
baadhi ya wajanja ndani ya CCM waliunda mpango wa kupora sehemu yake. Kati ya matukio hayo ya uporaji lipo moja la Dar es Salaam ambako kiasi cha Shilingi milioni 600,000 taslimu zilichukuliwa lakini taarifa za wizi huo hazikufikishwa Polisi.

Aidha, vyanzo hivyo vya habari vinasema katika tukio jingine, mjumbe aliyetumwa apeleke fedha kiasi cha Shilingi milioni 200 Kanda ya Ziwa, badala ya kufikisha kiasi chote, aliwasilisha Shilingi milioni 80, na aliyekabidhiwa hizo 80 naye akawasilisha milioni 20.


Hii kweli inafurahisha sana. naweza kusema the most interesting of all. Sasa angalia kama ni hao hao walioko kwenye nyadhifa za serikali watafanyaje na pesa za serikali

Kwa taarifa yako, hao walioiba hizo fedha mmoja alikuja kuuwawa na kina Zombe baadaye kule Kimara na kifo chake bado kina utata na ndiye ambaye gari lake limechukuliwa na Tibaigana
 
Admini: Kwanini hizi mada za sasa zaBoT zisiwekwe mahali pamoja? Mana naona kama baadhi ya mambo yanajirudia ama kuchanganya
 
"Bado anaumwa. Anahisi kuwa ugonjwa wake, pamoja na sababu nyingine, umetokana na sumu, walau madaktari bingwa wa Marekani anakotibiwa wamemwambia kuwa alikula sumu. Kwa hiyo amefanyiwa operesheni ya tumbo. Haijulikani itachukua muda gani kupona, na ndiyo maana aliandika barua ambayo haikujibiwa ya kujiuzulu. Lakini Mungu si Athumani. Akijalia Mwenyezi atapona. Akipona, kama ambavyo wote tunaomba kwa Mungu, atakuja kuzungumza.

"Ana kila ushahidi. Ana kila aina ya nyaraka zilizokuwa zikimtaka afanye nini. Hakika akifanikiwa kuzungumza watu wataumbuka. Si kuwa yeye ni malaika, lakini madhambi mengi wanataka kumbebesha yeye," alisema.

"Na hicho ndicho vigogo nchini wanachokiogopa. Akiweza kusema tutashangaa, na tutawashangaa viongozi wetu. Hivyo ili asiweze kusema ndiyo kila mara unasikia mara kafukuzwa kazi, mara visa yake imetenguliwa na mara anakaribia kufa.

"Wanataka afe ili siri isifichuke. Kuna uongo mwingi. Na mwenye ufunguo wa uongo huo ni yeye. Anajua na hata baadhi ya wafanyakazi wa BoT wanajua nani alikuwa akishinda ofisini kwake, kwa mfano, kushinikiza malipo ya kampuni ya Kagoda."

Haya maneno mbona kama yanatia kizunguzungu!!!! Enyi wafanyakazi wa BoT muliopo JF na jamaa zenu tuambieni pia ni nani aliyekua anashinda BoT kumshinikiza huyu mzee?
 
Ikitokea samaki wameingia sumu katika bwawa humtoi samaki moja moja ili kumaliza hilo tatizo la sumu. Unachofanya ni kuyatoa maji yote kwenye bwawa na samaki wenye sumu wote watakufa, then unaweka maji mengine na kupandikiza samaki wengine mambo yanaendelea. Madamu tunaendelea kufikiri kwamba tatizo ni Balali, Kikwete, Mkapa au mtu mwingine yeyote katika CCM na sio CCM (maji) yenyewe, tutaendelea kusubiri sana hili tatizo la ufisadi kwisha. Tukubaliane basi kwamba kuwashughulikia akina Balali na wengine ni short term solution, our long term solution to our country's woes should be to uproot CCM from power.

Na pia tukumbuke kuwa Kikwete yupo ofisini sio madarakani. Wenye madaraka ni wengine na ndio maana hana ubavu wa kuwafukuza walaji kazi hata kama ushahidi utakuwa wazi namna gani. Sasa ni kazi yetu kutafuta ni nani hasa wenye madaraka katika serikali yetu ili tuwabane.
 
Watanzania tuko waoga mno. Itaenedelea hivihivi hadi taratibu itazimika tu.
Jenerali aliwahi kuandika eti "kila mtu na kamhogo kake" yaani eti tunaridhika na umaskini wetu ali mradi hako kadogo ninakokula kasiniponyoke.
Watanzania tuamke. Hata sasa ukiwauliza waTZ vipi mwaweza kuwa jasiri angalau kwa nusu ya walivyofanya wakenya? watakujibu ati mimi siwezi kufa kwa ajili ya vizazi vijavyo- mtu mzima ovyoooo!
 
Kitika umesema maneno mazito ya kumwaga maji bwawani ili kuondoa sumu yote . Ukimwaga means hata JK must go maana naye si msafi hata kidogo .Je yuko tayari kuitwa Pres wa miaka 3 ?
 
Lunyungu: Nafikiri haujampata vyema Mh. Kitila. Hajamaanisha Kikwete amwagwe immediately, ila uchaguzi ujao kwa kuindoa kabisa CCM madarakani. Hii njia muhafaka na muhimu sana katika kuutokomeza ufisadi. Kumbuka si kweli kabisa kwamba "DALALI" Balali yuko peke yake, katika hii ishu ndo maana "wenzie" wamemficha wakisuburi mambo yapoe. Hatupaswi kurudi nyuma, this is the very good stepping stone we have ever had in the history of Tanzania to take CMM out. Dalali and Co. first, then Kikwete and CCM in 2010! C'on Tanzania!!
 
Uuuwiii Mwamunyange Kaa Tayari Kijana Wangu Nchi Hiyoo Inakuja Mikononi Mwako.mungu Akupe Nini? Na Usicheke Na Kima Yeyote Piga Jela Wote Tena Usipate Tabu Tumia Hao Hao Vijana Wako Ambao Nina Imani Kwanza Walishakata Tamaa Na Wana Hasira Ya Kumvunja Mtu Kiuno
 
Halafu Ukishakamata Huo Mpini Kwanza Fanya Uhakiki Wa Biashara Zoote Zinazofanywa Na Wahindi Maana Hawa Ndiyo Sumu Ya Nchi Wabaguzi Wakubwa Halafu Hata Kama Wana Vibali Halali Futa Vyote Na Hizo Nafasi Uwape Wazawa Maana Kwa Wazawa Wa Tanzania Kupata Kibali Cha Kuagiza Chochote Imekuwa Ni Ngumu Mno Waulize Wauza Madawa Watakueleza, Na Si Pia Unakumbuka Lile Sakata La Yule Mhindi Aliyepewa Kibali Cha Kuagiza Dawa Za Kifua Kukuu Jinsi Alivyowaua Wa Tz Kwa Kuwalisha Dawa Feki Miaka Mitatu Mfululizo Na Wala Serikali Haikumfanya Chochote Jamani Jamani Sitaki Kukumbuka
 
My God!sasa Tufanyeje Na Hii Serikali? Maana Kikwete Ameshaona Kabisa Nyumba Inaungua Hii Na Hana Jinsi, Kweli Sasa Naamini Hakuna Hali Ya Kudumu Milele
 
Kila Wizi Mkubwa Uliofanyika Lazima Mhindi Yuko Ndani Sasa Wa Nini Hawa? Kwanini Msitimue Au Wana Msaada Gani Mkubwa Sana Kwetu?mlilogwa Na Nani Nyie? Au Mnataka Nani Awasemee Au Hamjakua Bado?pls Wake Up Tz
 
Back
Top Bottom