kama ni hizo hela za semina wanahitaji wangesainishana cheque tu kikaisha.. suala la kwenda kukaa dodoma sidhani kama lina maana yeyote
Natoa siku 30 kila waziri awe amehamia Domoma. Vitengo vingine vya wizara vitafuata taratibu. Nataka kuona mawaziri na manaibu waziri mnakuwa dodoma kama eneo la kazi. Nasema ndani ya siku 30............ makofiiiiii
Vile vile niliagiza yafanyike maonesho maalum katika Uwanja wa Maonyesho wa Julius Nyerere hapa Dar es Salaam na kote mikoani kwenye viwanja vya maonesho, kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika nyanja mbalimbali katika miaka 50 tangu Uhuru wa Tanzania Bara. Kwa kuwa tunakaribia nusu ya mwaka huu, ni vema sasa kukumbushana kuendelea na maandalizi ya sherehe hizo. Ni matumaini yangu kwamba kila Wizara inakaribia kukamilisha tathmini hiyo. Walio nyuma sana waongeze kasi. Tuliazimia pia kuwa tuanzishe mchakato wa kuipitia Katiba yetu.
Tumeanza, lakini kuna upotoshaji mkubwa, lakini wajibu wetu sote tuliopo hapa kukabili hila na njama hizo chafu. Naamini tutafika salama. Kinachotakiwa ni mshikamano na umoja miongini mwetu.
Hii kipande kimenibore kabisa anasema matatizo bila majibu na mahala penyewe ni kwenye semina Raisi wetu anamatatizo kabisaPamoja na nyongeza hiyo bado tunao uwezo wa kuongeza zaidi. Kuna watu wengi ambao bado hawajafikiwa na wigo wa kodi. Laiti wangefikiwa mapato ya Serikali yangekuwa makubwa zaidi ya ilivyo sasa. Tutafanyaje tufanikishe hilo ni changamoto yetu sote Serikalini. Tufanye nini ili tuzibe mianya inayovujisha mapato ya Serikali ni swali ambalo sote katika Serikali hatuna budi kutoa jibu muafaka. Kwa upande wa tozo mbalimbali karibu kila Wizara inazo tozo za namna hiyo. Wengi wenu hamjafikia hata theluthi moja ya malengo. Tutafanyaje ili tufikie malengo na kuyavuka ni swali ambalo kila mmoja wetu anatakiwa kujiuliza na kutoa majibu sahihi.
Ndugu Mawaziri na Ndugu Makatibu Wakuu;
Sote tunajua kuwa licha ya tozo na kodi, chanzo kingine cha mapato ya Serikali ni mikopo na misaada kutoka Mabenki, Mataifa Rafiki, na Mashirika ya Fedha ya Kimataifa. Tumepata misaada na mikopo mingi ya kutoka nje katika kipindi kilichopita na muelekeo ni kuwa tutaendelea kupata zaidi katika miaka mitano ijayo. Tunatambua haja na hoja ya kupunguza utegemezi wa misaada na mikopo kutoka nje kwa kuongeza mapato yetu ya ndani. Katika miaka mitano hii tumeendelea kupunguza utegemezi lakini nia yetu sote iwe kupunguza zaidi. Naamini tutafika kwenye shabaha hiyo iwapo tutaongeza mapato ya ndani. Naomba tuzungumzie namna ya kufikia shabaha hiyo.
Ndugu Mawaziri na Ndugu Makatibu Wakuu;
Usimamizi wa matumizi ya fedha tunazokusanya kama mapato ni jukumu jingine kubwa kwetu sote. Tuna wajibu wa kuhakikisha kuwa fedha za walipa kodi zinatumika ipasavyo kuwaletea maendeleo wananchi. Katika kudhibiti matumizi ni muhimu kuelewa na kusimamia sheria, taratibu na kanuni za fedha na manunuzi ya umma kwa ufanisi wa hali ya juu. Taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali zinaonyesha kuongezeka kwa ubora lakini bado tunayo kazi ya kufanya kufikia kiwango cha kusema sasa tunapumua. Bado kuna makosa mengi katika kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za mapato na matumizi ya fedha za umma. Nataka tuzungumze kwa dhati tutafikaje kwenye ufanisi wa hali ya juu kwenye eneo hilo. Hali hii hatuwezi kuiacha iendelee kuboreka kwa kasi ndogo iliyopo sasa.
Viongozi na watendaji wakuu wa Serikali, mnatakiwa kuwa mfano kwa wafanyakazi mnaowaongoza kwa kuzingatia nidhamu ya matumizi ya fedha za umma.
Hakikisheni bajeti hazikiukwi, fedha zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na sheria na kanuni za fedha zinaheshimiwa. Niliagiza Kamati za Fedha ziundwe katika kila Wizara na Idara za Serikali zinayojitegemea. Je zimeundwa? Je zinafanya kazi? Hakikisheni zipo hai na zinatimiza wajibu wake. Zitasaidia sana kwa upande wa kuongeza mapato na kudhibiti matumizi katika Wizara.
Kama matamko yote yaliyokwisha kutolewa na Jk yangekuwa yanatimizwa mbona tungekuwa mbali!!.
Hivi ni akili za Jk na Mawaziri wake wote kwenda mpaka Dodoma kuwakumbusha wajibu wao?Hivi ni kwa nini mnateketeza hizi pesa zetu(Watanzania)tukiona jamani?
Hivi Jk hao mawaziri wako uliowachagua ni kweli hawayajui majukumu Yao?Raisi 0 Wabunge 0 Baraza la mawaziri 0 wote zero mnaudhi sn.
Hotuba imetulia kweli na inatoa maelekezo ya kutosha kwa hao wakuu wa nchi. Muhimu ni wao kuyafanyia kazi ili matokeo yaonekane
Hana ujasiri huo!Au angesema hivi angeonekana shujaa
Mkuu!Bravo JK kwa kuchukua hatua wakati muafaka!!!n:israel:
Mambo yote anayoyaorodhesha leo ndio standard operation manual ya serikali.
Kuna matatizo mawili makubwa yanayomkabili Kikwete na serikali yake:
Kwanza, haya hayatekelezwi na pili, ambalo ndilo kubwa zaidi, hakuna hatua yoyote inayochukuliwa kutokana na kutotekelezwa haya zaidi ya maneno zaidi kama anavyofanya kupitia hiyo semina elekezi.
Kwa hali jinsi ilivyo hakutakiwa kuwe na semina elekezi tena. Huu ulikuwa ni wakati wa vichwa kuviringika, si kukumbushana wajibu kwa sababu kila mmoja serikalini anajua wajibu wake... kama kuna ambaye hajui, hakustahili kuwepo humo