Kikwete na semina elekezi kwa Mawaziri - Dodoma 2011

Nnamfuatilia Raisi Jakaya Kikwete,anasema "Uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi kubwa sn"Hivi uchumi wa nchi kukua kuwa na majengo marefu au hali nzuri(kujimudu kimaisha)kwa wananchi?


Alishalijibu hilo, alisema kadri traffic jam zinavyoengezeka ndio inaonesha uchumi unakua.
 
Hii naona kama inamlenga Waziri 6...manake yy ndo anatofautiana wa mawaziri wenzake mara nyingi. So kwa mwendo huu kila kitakachosemwa basi majibu...''ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI''......!!

Na mtoto wa mkulima alivyopiga kura bungeni kuunga mkono marekebisho ya mswada wa uendeshaji idara za mahakama. Halafu ukumbuke huu mswada uliwasilishwa kwa hati ya dharura bila shaka ili kuwarahisishia kuchakachua kesi za uchaguzi. Nomaaa.
 
Sisi tuliwaambia watz, ni maafa kuendelea kuwa na ccm, haya mawaziri wanafundishwa kazi na mtu asiyejua kazi, jk hajui kaz, pekee yake angeweza kuleta mabadiliko, sheria zinamruhusu lakn hazitumii. Jk aache kulaumu wapinzani, uzembe na uvivu wake ndiyo sabab ya nchi kwenda kombo. Achia nchi ukimbie.
 
eti anadai anategeneza misingi ya leo kwaajili ya 2025 huu ni uongo wa hali ya juuuu, nchi ishakushinda semina haifai hata kuangalia inaboa wala haifai nashangaa sana jk na serikali yake kuendelea kuwa madarakani mpaka sasa

hahaa,your cackling glee in expressing your hate is a little bit disturbing.naona kama unavyatuka tu as if uko mental disturbed
 
Huyu mkulo na waandishi wa habari hakuna mwenye update.
I bet anakanusha tuhuma kwamba zito kadanganya kua nchi imefilisika.anyone ready to bet ?
 
Hapa ningemuona angalau kidogo kuna akili imesaria kichwani mwake kama angevunja baraza la mawaziri, hizi semina elekezi ni mbinu mpya ya kuiba pesa za watanzania, wakati wahuzuliaji wenyewe wa semina hakuna anaesikiliza kitu zaidi ya kusubiri posho, mimi nilifikiri atakuwa ameshajifunza na semina aliofanya kipindi chake cha kwanza kule Ngurudoto Arusha kwamba ilikuwa ni waste of money.

Bora ingekuwa hivyo ila maumivu ni mara mbili KODI zetu wanachukua, DADA na WATOTO WETU huko UDOM, CBE, MIPANGO, St.John na HOMBOLO wana wachakachua tena nasikia huwa hawalipi hutumia majina yao, Bora wangekuwa wanazirudisha KODI zetu kinyume kupitia hao Dada na watoto wetu!!
 
I think there is nothing new at all.

All those are just words, and many people here in Tanzania are used to hear good words from our the political leaders, but at the end, the implementation is just at zero ground.

GOOD LEADERS are pragmatic in the sense that they deal with practical things, trustworthy, and they do things that benefit a vast majority population. What is important is that we shall judge by deeds and not words.
 
"Uadilifu ni muhimu sana waziri, naibu, katibu mkuu wanatakiwa kuwa mfano mwema. Mawaziri, naibu wasinyooshewe vidole. Siyo kufika saa 5 na kuondoka saa 7 mchana; uzembe, wizi, kuchonga line za kupata, kutumia ofisi kujunufaisha, ulevi, uzinzi wala ubabe"

Excuse me!!!!!!!! hivi kuna compromise na hayo mambo, ina maana kulu anajua kuna wanaofanya hivyo and yet hajawawajibisha?
 
Uongo ukisemwa mara nyingi hugeuka kuwa kweli

- Wananchi wanalaumu serikali kutokana na kuelezwa uongo dhidi yake

- Tuwe wepesi kusahihisha uongo dhidi ya serikali, raslimali zipo, vyombo vya habari vipo, hatuvipi habari

- Kila wizara kuna wasemaji, hawasemi, wasemasji wengine wanazuiwa kusema

- Maafisa habari wapewe fusa watuimie taaluma yao, wao wanajua; msilaumu kwamba vyombo haviwataki

- Lazima serikali iwasiliane na watu wake kupitia vyombo vya habari


... hii inanikumbusha kisa cha mlevi na mkewe walipotinga nyumbani wakiwa chakari na pale jamaa aliamrisha apewe chumba namba 17. Nyumbani kwake mwenyewe. Walevi bana! kwi kwi kwi.
 
Kama ni kuwahutubia tumeshuhudia sana, tunachohitaji tena si hotuba ndefu bali vitendo kwenye field. Asante mkuu kwa kutupa updates za huyu mcheza kiduku!
 
Hakuna mtu anayezunguka kutangaza mafanikio. Kwa mfano mtu akifanya mtihani mafanikio kila mtu ataona ni matokeo ya mtihani, kama umejenga barabara kila mtu ataiona huna haja ya kuwaeleza watu umejenga barabara. kama maisha bora kila mtu ataona ana hela za kutosha na vitu vya kununua.

Analaumu wakurugenzi wa habari hawapewi nafasi....ukweli ni kuwa hawana habari za kutoa.

Rais kweli mawazo mgando, yeye anafikiri bado Tanzania ni enzi ya Nyerere kuwa wananchi wanaamini porojo za kwenye vyombo vya habari. Mbona sasa Magazeti na vyombo vya serekali havina wateja zaidi ya wizara? Wananchi wanajua ukweli na uongo. Yeye angekuwa wa kwanza kusema uongo uliosemwa na atoe ukweli.

Unajua yeye kama raisi ndio anadanganywa kuwa kuna mafanikio...sijui yeye kipofu? Je haoni nchi ilivyo?

Sasa ndio atajidhalilisha, kaonekana akisema live kwenye TV, nina uhakika hakuna kitakachofanyika....mawaziri hawatafanya alivyosema kiasi kile na wananchi ndio watafuta kabisa imani na uwezo wa raisi.

Alipochukua nchi 2005 aliwaita mawaziri, wakuu wa mikoa, na wakurugenzi Bagamoyo na Ngurudoto kwa semina kama hizi lakini hakuna kilichofanyika. Wana vikao vya Baraza la mawaziri, katembelea wizara etc lakini hakuna kilichofanyika.
 
Unajua kila napokwenda Bongo hujaribu sana kusikiliza watumishi wa Umma wanavyozungumzia kuhusu serikali iliyopo madarakani.

Tofauti na marais waliopita mawaziri zaidi ya nusu wa JK hawajui kazi zao, yaani ni mbumbumbu kabisa ktk uongozi mara na nyingi wanaosimamia ni manaibu. Mfano mkubwa ni Chiligati, yaani hamna kitu kabisa bahati tu kampata naibu mwenye uzoefu..
 
Naomba nisahihishe kidogo.

Kikwete HAKUANZISHA kitengo/idara ya mawasiliano kwa kila wizara. Ni Mkapa ndiye aliyeanzisha hivi vitengo na kama mtakumbuka Peter Kallaghe (kwa sasa Balozi wa TZ- UK) ndiye alikuwa Director of Communications State House. Na kiutendaji ni kwamba Director wa Com State House alikuwa ana-coordinate mawasaliano toka idara/wizara zote hivyo kuweza kuifanya Serikali kuwa na sauti moja. Nisema Peter Kallaghe alikuwa amepiga hatua nzuri sana katika kuanzisha huu mfumo wa mawasiliano ndani ya Serikali huku akipata msaada mkubwa (financial & human resources) toka UNDP na DFID-UK.

Sasa hivi Salva Reywemamu ndiye Mkurugenzi na nadhani mambo yamedorora kiasi kwani Salva anaonekana kufanya kazi ya "Press Officer' na sio Director. Director maana yake una-direct na ku-coordinate govenment communication system including press officer.

Vitengo vya mawasalino/habari katika mawizara ni kama watoto yatima kwa sasa. Na mbaya zaidi vinafanya kazi kama Press angency yaani wanasubiri waziri awaambie nini cha kusema, press release mambo yamekwisha. Hakuna research, public oponion kwenye mikakati ya hivi vitengo.
Mkuuu uko sahiihi na aksante kwa mashahihisho lakini kurugenzi nyingi za habari kwenye mawizara na idara zimeanza ipindi cha JK. kabla hapo vitengo vya habri vilikuwa vina watu na iidara za kawaida tu. Chap chap watu wakisikia statement kama hizi za raisibalada ya kufanya kazi wao wanajua ulaji.

Kinachofanyika ndo wanaanza kuteuana nani awe mkurugenzi. yes aiwa mmkurigenzi TGS inakuwa kubwa. Kisiasa inaonekana wanaanza kutekeleza maagizo ya rais lakini angali uwezo na utendaji walio kwenye hivyo vitengo. wizara nyingi idara na mikoa ni aibu.


Kwa kuwa ikulu kuna mkurugenzi wa hhabri kina wizara sasa ina mkurugenzi lakini output ya haeindani na kurugenzi. Just kuongezeana mishahara.Ni kama agizo la kutoa habari limeshatekelezwa kisiasa maana vitengo vipo but habari hizo ziko wapi.......

Kweli hivi vitengo ni kama watoto yatima baadhi ya sababu ni incompetence ya wahusika wenyewe kutojujua hata kama ni propganda wazfikisheje kwa walengwa. Look kila wizara/idara ina tovuti lakini vile vibox wanaweka kwa comment hawasomi wala hawatoagi feeback.

Nakumbuka utamu ilitoa picha za JK akifanyiwa kitu mbaya binafsi niliwanaadikia Web provider wa utamu (hostgator) kulalamika but nilishindwa kuapata official email ya iwe ni ya polisi au ikulu kwamba walamike kwa niaba ya serikali kwa barua yenye nembo. Yaani ilichukua siku zaidi ya tatu ile picha kuondolewa. Shame, kasi ya dunia ya sasa huu ni uzembe.

Haya mambo yanataikiwa yafanwe na watendaji ambo wengi ni sisi vijana. Sijui hatuoni.
 
... hii inanikumbusha kisa cha mlevi na mkewe walipotinga nyumbani wakiwa chakari na pale jamaa aliamrisha apewe chumba namba 17. Nyumbani kwake mwenyewe. Walevi bana! kwi kwi kwi.

hahaaaaa.... umenichekesha sana mkuu.
 
Back
Top Bottom