Kikwete na Pinda mnawachangana wananchi!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Nadhani kuna mtu anatakiwa kusema; hawa viongozi sasa hivi wanawanchanga wananchi. Wanapita mikoani wakifanya shughuli za serikali huku wakiwaasa wananchi kuwa waangalifu na watu wanaopiga kampeni kabla ya muda wake. Wanatoa maonyo kuwa "muda wa kampeni bado"!

Lakini wao wenyewe wanapigiwa kampeni na hawaoni tatizo na wakati mwingine wao wenyewe wanawapigia kampeni watu wengine. Angalia Kikwete alipoenda Tanga sijui kule na Makamba akampigia kampeni waziwazi na yeye hakusema kitu na hivi majuzi Pinda akiwa Igunda, Irambo nk ambako naye amewapigia kampeni wabunge wa sasa kuwa wachaguliwe tena; amefanya hivyo pasipo kuuma maneno!

Sasa nina ombi: Kama hawataki kumaanisha wasichosema basi wasikiseme; kama watu wengine ni makosa kuanza kupiga kampeni mapema ndani ya CCM wao ni kina nani hata waanze kuwapigia wengine kampeni? Kwanini wanaonesha upendeleo wa wazi kwa wanachama wengine wa CCM wakati jukwaa halijafunguliwa kwa wote!

Nasema mnawachanganya wananchi au nyinyi wenyewe mmechanganyikiwa!
 
Mwanakijiji,

Hivi kuna hata siku moja waliamaanisha walichokisema? Hawajiandai hata kuzungumza.
 
Siasa za bongo ndivyo zilivyo, utawasikia leo wanasema fuata maneno yangu na si vitendo vyangu.
Kesho wanakuja tena wanakuambia fuata vitendo vyangu na si maneno yangu.
Hakika viongoza wetu hawa wanatuchanganya.
 
Hivi kuna hata siku moja waliamaanisha walichokisema? Hawajiandai hata kuzungumza.
JK, ni bingwa wa kuongea yale asiyo yasimamia, ni mwepesi kuhaidi yale asiyoweza kutekeleza, ni ishara ya kiongozi legelege, hutaraji uwajibikaji toka kwake.
Pinda, huyu kalelewa ndani ya system, ni sehemu ya viongozi wanaojidai kuwa waadilifu, anaweza asiwe mdokozi ila uongozi ni SIFURI...kweli hajawahi kuwakuna waTZ kiutawala wala kiuongozi, anahadhi ya kuwa mkuu wa wilaya, Uwaziri Mkuu ni cheo kikubwa na maji mazito kwake,
kwa ujumla wo hatuna viongozi wajuu wanaoweza kusimamia yale wanayoyasema.ni wasanii tu.
 
Nadhani kuna mtu anatakiwa kusema; hawa viongozi sasa hivi wanawanchanga wananchi. Wanapita mikoani wakifanya shughuli za serikali huku wakiwaasa wananchi kuwa waangalifu na watu wanaopiga kampeni kabla ya muda wake. Wanatoa maonyo kuwa "muda wa kampeni bado"!

Lakini wao wenyewe wanapigiwa kampeni na hawaoni tatizo na wakati mwingine wao wenyewe wanawapigia kampeni watu wengine. Angalia Kikwete alipoenda Tanga sijui kule na Makamba akampigia kampeni waziwazi na yeye hakusema kitu na hivi majuzi Pinda akiwa Igunda, Irambo nk ambako naye amewapigia kampeni wabunge wa sasa kuwa wachaguliwe tena; amefanya hivyo pasipo kuuma maneno!

Sasa nina ombi: Kama hawataki kumaanisha wasichosema basi wasikiseme; kama watu wengine ni makosa kuanza kupiga kampeni mapema ndani ya CCM wao ni kina nani hata waanze kuwapigia wengine kampeni? Kwanini wanaonesha upendeleo wa wazi kwa wanachama wengine wa CCM wakati jukwaa halijafunguliwa kwa wote!

Nasema mnawachanganya wananchi au nyinyi wenyewe mmechanganyikiwa!

Thats why we call it siasa
 
Hawa kweli wanatuchanganya si kidogo kama huyu Pinda..ooh mabarabara Tabora yatajengwa ..mchague viongozi safi viongozi safi ni kina nani ,kama Cabinet lote la CCM limegubikwa na uozo mtupu??
kwani awamu hii ndo watayajenga hayo mabarabara ,maji ama wanatupumbaza wananchi ili tuwape kura zetu waendelee kutukandamiza
Very sad... cha kushangaza raia tuko very happy tunashangalia tu
 
Hivi kuna mbunge yeyote wa CCM ambaye JK au Pinda anaweza kusema hadharani asichaguliwe? Kama wote wanaungwa mkono na Rais na Waziri Mkuu wake kuna haja gani ya wagombea wengine kujitokeza kutoka ndani ya CCM si wataokoa fedha nyingi kama watawapitisha hawahawa?
 
By definition, Mwanasiasa ni mtu anayeweza kuzungumza bila kusema kitu. Hawa wa kwetu wanashindwa hilo. Kwa hiyo, wanakuwa ni wanasiasa waliomaliza muda wao wa ubora (use by date). They have expired.
 
Lakini watawatendea wananchi wema endapo aidha wataacha kuzungumza kuliko kuzungumza kitu ambacho wanajua kabisa si cha kweli. Unaweza vipi kusema wengine wasikampeni wakati muda haujafika wakati wewe mwenyewe unapigiwa kampeni na wewe mwenyewe unampigia mwingine kampeni.. au hizi siyo kampeni bali ni 'kujitambulisha'..?
 
MM umesema mengi lakini mstari wa mwisho ndio ukweli wenyewe. Kwa kawaida rafiki ya adui yako naye ni adui yako, sasa kwa Pinda (PM) alichofanya Igunga na Urambo ni kwa kuchanganyikiwa dhahiri kabisa.
 
Kwa kweli wanajichanganya kweli kweli.Yaani sijui wanamaanisha nini au inawezekana hawajui maana ya kampeni.
 
Nadhani kuna mtu anatakiwa kusema; hawa viongozi sasa hivi wanawanchanga wananchi. Wanapita mikoani wakifanya shughuli za serikali huku wakiwaasa wananchi kuwa waangalifu na watu wanaopiga kampeni kabla ya muda wake. Wanatoa maonyo kuwa "muda wa kampeni bado"!

Lakini wao wenyewe wanapigiwa kampeni na hawaoni tatizo na wakati mwingine wao wenyewe wanawapigia kampeni watu wengine. Angalia Kikwete alipoenda Tanga sijui kule na Makamba akampigia kampeni waziwazi na yeye hakusema kitu na hivi majuzi Pinda akiwa Igunda, Irambo nk ambako naye amewapigia kampeni wabunge wa sasa kuwa wachaguliwe tena; amefanya hivyo pasipo kuuma maneno!

Sasa nina ombi: Kama hawataki kumaanisha wasichosema basi wasikiseme; kama watu wengine ni makosa kuanza kupiga kampeni mapema ndani ya CCM wao ni kina nani hata waanze kuwapigia wengine kampeni? Kwanini wanaonesha upendeleo wa wazi kwa wanachama wengine wa CCM wakati jukwaa halijafunguliwa kwa wote!

Nasema mnawachanganya wananchi au nyinyi wenyewe mmechanganyikiwa!
Tatizoo tunawaaminii MNOOOO....
 
Thats why we call it siasa

Siasa = Si Hasa therefore Uongo

When asked to name the chief qualification a
politician should have. "It's the ability to
foretell what will happen tomorrow, next month,
and next year --- and to explain afterward why it
didn't happen."

- Sir Winston Churchill

He didn't say that. He was reading what was given to him in a speech. ~Richard Darman, director of the Office of Management and Budget, explaining why President Bush wasn't following up on his campaign pledge that there would be no loss of wetlands

Tatizo sio la akina Kikwete kwani wao wanatumia vema nguvu zao. Tatizo ni ubweteke wa wapinzani wanaothani wanaweza kuishinda CCM kwa kutenda kama CCM. Hivi wakiamua kupingana na hivi visheria vya kuwaminya JK atawafanya nini?
 
You've hit the point. Sijaona upinzani uliolala usingizi kama upinzani wa Tanzania. Hawajui kabisa ku-capitalize kwenye makosa yanayofanywa na CCM. Wao wamekaa tuu eti wanaachia magazeti na articles za Mwanakijiji ndivyo vifanye kazi ya kuikosoa CCM ama viongozi wake badala ya wao upinzani. Wanasubiri wakati wa uchaguzi ndio waanze kupingana na Chama Tawala majukwaani na wakati huo itakuwa too late.

Jamaa zetu wa CHADEMA kama wangelikuwa serious walipaswa wawe na magazeti yao ya propaganda kama mawili ama matatu yanayotoka kila siku asubuhi na jioni na moja weekly ku-counter attack kila move ya CCM. Wamekalia helikopta tu wakidhani ndiyo itakayowaletea ushindi!
 
Tatizo la hawa viongozi wetu ni kuwa HAWAJITAMBUI. Sasa unadhani mtu asiyejitambua yeye mwenyewe ataweza kutambua kile asemacho?
 
Mwanakijiji
Hii inji inatawaliwa kijeshi ndo maana hata taratibu walizojiwekea hawazifuati na hakuna wa kuwawajibisha. kilicho baki ni amri tu

Kama rais ni Kanali. Waziri mkuu TISS mawaziri kibao ni wanajeshi wastaafu, usisisahau katibu mkuu wa CCM ni mjeshi pia, Usiseme kuhusu wakuu wa mikoa na wilaya wengi wao ni wajeshi.
Uliona wapi mwanajeshi akaongoza raia kwa HAKI? ndo maana hawa watawala hawaijui lugha yetu na sisi hatujui lugha yao hivyo tunapigiana kelele mpaka kieleweke. Kila idara wamekaa wanajeshi na kama mjuavyo wao wanajua lugha ya amri tu hawana lugha ya tafadhali.

Lakini wa kulaumiwa ni kura yako na yangu gadem!
 
MM umesema mengi lakini mstari wa mwisho ndio ukweli wenyewe. Kwa kawaida rafiki ya adui yako naye ni adui yako, sasa kwa Pinda (PM) alichofanya Igunga na Urambo ni kwa kuchanganyikiwa dhahiri kabisa.
Hivi sasa Hivi Pinda au JK akienda Moshi mjini atasema mchagueni Ndesa? au akienda Karatu atasemaje? au ukiwa sio sisiem basi hufai kuchaguliwa kabisa kwa mujibu katiba yao.
 
Kwao ni powa na hizo siyo kampeni ni mwendelezo wa yale tulozungumza katika semina yetu ngurdoto.hivyo tunawafikishia wanachi pia.
 
You've hit the point. Sijaona upinzani uliolala usingizi kama upinzani wa Tanzania. Hawajui kabisa ku-capitalize kwenye makosa yanayofanywa na CCM. Wao wamekaa tuu eti wanaachia magazeti na articles za Mwanakijiji ndivyo vifanye kazi ya kuikosoa CCM ama viongozi wake badala ya wao upinzani. Wanasubiri wakati wa uchaguzi ndio waanze kupingana na Chama Tawala majukwaani na wakati huo itakuwa too late.

Jamaa zetu wa CHADEMA kama wangelikuwa serious walipaswa wawe na magazeti yao ya propaganda kama mawili ama matatu yanayotoka kila siku asubuhi na jioni na moja weekly ku-counter attack kila move ya CCM. Wamekalia helikopta tu wakidhani ndiyo itakayowaletea ushindi!
japo sikubaliani na ww moja kwa moja lakini nakubali kuwa jamaa wamelala kidogo. inawezekana kuna tatizo la funds, kumbuka kuwa pinda akienda Urambo anatumia government funds, lakini mdomo wake unaongea upupu wa sisiem. and this is wrong.
 
Back
Top Bottom