Kikwete na mawaziri kadhaa kuzuru Muscat Jumatatu 15, Oktoba 2012

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
Kuna taarifa kuwa mheshimiwa wetu atakuwa na safari jumatatu ya tarehe 15 kuelekea Muscat.

Anatarajiwa kuongozana na mawaziri kadhaa wakiwemo Membe, Muhongo, Kigoda, Mgimwa na baadhi ya mawaziri wa SMZ.

Safari hii amealikwa rasmi na mfalme wa Muscat.

***************
UPDATE: October 14, 2012

Tanzanian President begins visit tomorrow

1350157090038846900.jpg


MUSCAT — President Jakaya Mrisho Kikwete of Tanzania is due to pay a several-day visit to the Sultanate starting from tomorrow. This came in a statement issued by the Diwan of the Royal Court which says: "In crowning the friendship and the historic co-operation binding the Sultanate and the United Republic of Tanzania and in reply to invitation of His Majesty Sultan Qaboos, President Jakaya Mrisho Kikwete of the United Republic of Tanzania will pay a several-day visit to the Sultanate starting from Monday."

During the visit, the president will discuss matters which will boost the existing bilateral co-operation between the two countries to further heights and to serve the joint interests of the Omani and Tanzanian friendly peoples.

The president will be accompanied by an official delegation comprising Bernard Membe, Foreign Affairs and International Co-operation Minister, Prof Sospeter Muhongo, Energy and Minerals Minister, Dr Abdallah Kigoda, Industry and Trade Minister, Dr William Mgimwa, Finance Minister, Haroun Ali Sulaiman, Minister of Labour, Peoples Economic Empowerment and Co-operatives in Zanzibar and Dr Ali Ahmed Saleh, Ambassador of Tanzania to the Sultanate.


Source: Tanzanian President begins visit tomorrow | Oman Observer
 
Sijui safari inalenga kitu gani, labda yule bwana wa DOWANS aliyekuja kimya kimya. Hata hivyo ninachofahamu, Muscat ni wachunga mbuzi kama sisi. Anyway...
 
Serikali haina fedha za kutufadhili katika mipango ya kuwasaidia walio wengi kama huduma za afya, shule n.k. lakini kwa wakubwa wanatumia watakavyo hata hicho kidogo tunacokusanya kwa manufaa yao..
 
Au ndio maandalizi ya OIC? Ndugu zetu wanadai katiba mpya itambue OIC!! Elimu dunia muhimu.
 
Amealikwa au ameomba aalikwe? Maana vasco da gama kukaa ofisini nadhani mkapa alimwachia kizizi hivyo inabidi asafiri kila uchao ili amalize ngwe yake. Mwaka huu uchumi wetu utakoma.
 
Au ndio maandalizi ya OIC? Ndugu zetu wanadai katiba mpya itambue OIC!! Elimu dunia muhimu.

wana haki kikatiba kutoa maoni mkuu, sio maandalizi, utakua ni muendelezo wa utalii wa jk wenye manufaa kiduchu kwa nchi yetu.
 
wameitwa ili kupanga jinsi gani ndege ya oman itakavyokuja kutua KIA na kuchukua wale twiga, Oman watamwambia waziri mpya wa maliasili anaelewe interest zetu au? Kazi kwa k...sheki ya maige yanajirudia
 
Kwetu wananchi ni safi kupata habari hizi mapema mapema; kwa hadhi na utendaji wa Ikulu kuna kitu hakija kaa sawa kabisa ni aibu sana taarifa na picha za Mkuu na Ikulu ziko nje nje kila wakati hata kabla ya presidential press releases!

Usalama wa Taifa, Katibu Mkuu, Mkurugenzi wa Mawasiliano na hata mpiga picha Michuzi mpo????????
 
Back
Top Bottom