Elections 2010 Kikwete na CCM kushinda kwa kishindo - REDET

Status
Not open for further replies.
Mwaka 2005 alipata 84%. Zimekwenda wapi hizo zingine? Lakini nakubali atashinda bcoz ours is a unique country -- sheep for humans!

Zak, kwanza sikukupata, lakini nilipokupata nilivunjika mbavu! Yes we have a population of sheep instead of human beings. And that is what CCM (and JK for that matter) depends to rule perpetually. Once the situation changes (and it CAN change abruptly why not?) then the mafioso will find it hard even to see the exit door! IKO SIKU! IKO SIKU!
 
Wadau nimedokezwa na Mdau mmoja hapa kwamba REDET ni ya Prof. Mukandala wa UD na kabla ya JK kuwa Presidaa, Mukandala aliahidiwa ukuu wa Chuo na JK. So Prof. Mukandala analipa fadhila kwa kampeni za chini chini na takwimu mbofu mbofu.
 
hIVI HUWA WANAPITA KWA KINA NANI NA KUFANYA TAKWIMU ZAO ZA UONGO ??

Sina uhakika kama walifika na kufanya interviews zako Kigoma, Tarime, Musoma, Buzwagi, Busanda, Moshi, Karatu, Dar na Pemba. Research inayofanyika bila uwazi inakuwa na utata sana - anyway wacha wakipe moyo chama chao.
 
Si shehe yahaya alisema hakuna uchaguzi mwaka 2010, sasa inakuwaje REDET wanatuambia Kikwete atashinda kwa kishindo.
 
Sina uhakika kama walifika na kufanya interviews zako Kigoma, Tarime, Musoma, Buzwagi, Busanda, Moshi, Karatu, Dar na Pemba. Research inayofanyika bila uwazi inakuwa na utata sana - anyway wacha wakipe moyo chama chao.

hapo ndio kitendawili..nadhani takwimu zaidi zimefanywa katika jiji la Dar es salaam ngoja waendeleea kumpotosha prezident
 
Kama asilimia 61.7 ya wabunge wanaweza kupoteza ubunge ikizingatiwa idadi kubwa ya wabunge hivi sasa ni wa CCM iweje JK ashinde kwa kishindo ? samaki mmoja akioza wameoza wote REDET waache Ushekh Yahya hapa.
 
Wadau nimedokezwa na Mdau mmoja hapa kwamba REDET ni ya Prof. Mukandala wa UD na kabla ya JK kuwa Presidaa, Mukandala aliahidiwa ukuu wa Chuo na JK. So Prof. Mukandala analipa fadhila kwa kampeni za chini chini na takwimu mbofu mbofu.

waweza kuwa correct kabisa, siamini kama Redet ni independent researching tool, lazima kuna mkono wa mtu, yaani hizo asilimia zaidi ya 70 CCM na Kikwete watazitoa wapi
 
Takwimu hizi zikilinganishwa na tafiti zilizopita za Redet inaonekana kiwango cha kuridhika na utendaji kazi wa Rais Kikwete miongoni mwa wananchi kimeanza kupanda. Oktoba 2009 ilikuwa asilimia 67.4, Oktoba 2007 ilikuwa asilimia 44.4, Novemba 2008 ilikuwa asilimia 39.5 na Machi 2010 ilikuwa asilimia 49.3.
Jamani hebu nisaidieni kutoka asilimia 67.4 Oktoba 2009 hadi asilimia 49.3 March 2010 ni kupanda au kushuka kwa utendaji kazi wa Kikwete.
 
hata huo ushindi nina wasi wasi nao, anaweza hata asishinde, kwani yeye nani jamani


Ushindi atapata hapo hakuna mjadala bwana Kabuche77..kambi za upinzani mpaka sasa hazijaonyesha mwanga wa kupata kiongozi atakayekuwa Rais ..
Hivi CCJ iko wapi mbona kimya?
 
Ni kweli wala sio tetesi Prof. Mukandala ndio alikuwa mtafiti kiongozi wa REDET kabla ya kuwa mkuu wa chuo UD.

Mimi napata shida kidogo kuwaelewa kwanini wahoji 60% ya watanzania wa vijijini na only 40% ya waTZ wa mjini? hivi si ni wazi kuwa uelewa wa waTZ wa vijijini juu ya sisa za bongo ni mdogo kiasi kuliko wale wa mjini. Huu utafiti uko very biased kwa sababu kwa uwiano huu mbovu wa asiliamia ya watu waliohojiwa ni wazi haya ni matokeo ya kutegemea hata kabla ya utafiti wenyewe!

Lakini pia matokeo ya utafiti pia huathiriwa na jinsi unavyouliza swali, nina hakika swali hilo hilo moja unaweza pata majibu tofauti kulingana na unavyoliuliza, sasa REDET waliuliza maswali ya aina gani, na mbona hawasemi walibalance vipi jinsia maana uwiano wa jinsia pia ni muhimu sana katika tafiti kama hizi, maana ni wazi na ni kweli kabisa women perception on politics ni quite different from men perception?

Mimi nafikiri haya matokeo yanaleta maswali mengi zaidi kuliko majibu! Mukangala, JK na REDET yenu hebu jipangeni upya!
 
Opinion Poll ni opinion poll. Njia pekee ya kupinga opinion poll ni kufanya another poll. Kulalama humu hakusaidii. Redet wanafanya polls miaka yote na lawama ni hizi hizi. Utasikia watu wanalalamikia sampling wakata maisha yao hawajawahi kufanya polling. Marekani yenye watu 200m plus wana sample watu wasiozidi 2000. Uingereza hivi sasa wana uchaguzi pia sample hawazidi 2000. Mbadilike watanzania.

Mmefanya poll hapa JF ambayo sio ya kisayansi maana haina representative sample na tukajisifu kweli kweli (kujidanganya) maana ni poll ya members wanaojisikia na humu kuna members wana majina mpaka 10 na wamepiga kura. Tukubali hiyo yetu na hiyo ya redet.

Changamoto kwa vyama vya upinzani ni kwenda zaidi ya kelele za ufisadi na kuonyesha watanzania kuwa wanaweza kuongoza dola. Hilo halipo kwa sasa na imbedaki kelele tu. Mnadhani huyo Slaa na Zitto watafanya nini mbele ya machinery ya CCM?

Hivi kwa nini Watanzania hatubadiliki na kuanza kuangalia mambo kisasa na kuweka mikakati ya kuleta changes nchini?

Acheni kulalama lalama
 
Haya maoni nimeyaona kule Mwananchi:



http://www.mwananchi.co.tz/componen...-hawachaguliki-uchaguzi-2010.html#comment-499
#27 masanja 2010-04-28

Hii taasisi nilifanyapo kazi ya ukibarua kwa muda wa miezi sita mwaka 2005. Imejaa wanamtandao, na uccm kwa kupita kiasi. data zilikuwa zinapikwa ili kufanikisha malengo fulani.

Hata haya matokeo siku zote najua yanapikwa ilikufanikisha mpango fulani. kwanza huwezi kuchoma pesa kutembelea majimbo 50 ukaja na wahojiwa 2500.

Uwezekano nikuwa matokeo ya watu wengine yamewekwa kapuni na kutoa yale wanayoyataka. Halafu utafiti halisi umepelekwa kwa kamati ya ufundi ya sisiem kuifanyia kazi kuokoa mambo.
 
REDET nao mara nyingine wananishangaza sana na hizi tafiti zao. Zinaleta tija gani?
Hapo zamani watawala (wafalme) walikuiwa na wapiga ramli wao wa kuwatabiria au kuwataadharisha kuhusu matukio yatakayowasibu (Julius Ceaser - "Beware the aides of March", etc.). REDET ndiyo wapiga ramli wa CCM/Kikwete. Oh, na Sheikh Yahya.
 
Wanajidanganya..Hawatazifikia hizo asilimia lakini pia hivi asilimia 70 ni kishindo?REDET ni wale wale tu...Tusubiri Oktoba tuone.

Kwani uongo???,amini nakuambia kwa aina ya upinazni tulio nao Tanzania CCM watashinda hata zaidi ya hizo asilimia 70.....Utakuja niambia
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom