Kikwete na Bidhaa Feki Mitaani

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
Wakuu,

Kuna jambo moja nimekumbuka na ningependa kuwashirikisha humu jamvini ili muone aina ya uongozi tulio nao hapa nchini. wakati fulani rais kikwete aliitisha mkutano wa wahariri na waandishi wa habari waandamizi pale ikulu jijini Dar es salaam. nadhani ilikuwa ni miezi michache tu tangu ashike jahazi la uongozi wa ngazi ya juu hapa nchini. waandishi wa habari walikuwa wengi na nadhani pia wakati huo uhusiano wake na vyombo vya habari ulikuwa haujaingia nyongo kwani wakati huo ilikuwa ni mapema mno kutambua kama alikuwa na dhamira ya kweli ya kuwakomboa watanzania au la.

mkutano wenyewe ulikuwa ukiendeshwa kwa njia ya maswali na majibu ya papo kwa papo. nakumbuka moja ya maswali aliloulizwa lilikuwa ni je, yeye kama rais analionaje suala la kujaa kwa bidhaa feki mitaani. muuliza swali alienda mbali zaidi kwa kutaja hatari ya bidhaa feki kama vile vipuri vya magari, dawa za binadamu, n.k. katika kujibu swali hilo, kwanza kama kawaida yake, alijibu huku akiwa na tabasamu la bashasha kana kwamba suala analoongelea ni jepesi tu wala halina umuhimu wowote. jibu lenyewe alisema eti serikali yake itajitahidi kupambana nalo hata hivyo alisema kwamba wanaosema bidhaa feki ni wananchi wenye uwezo. akaendelea kusema eti mtu maskini asiye na fedha za kutosha bidhaa feki kwake ni muafaka kwa sababu kwa kawaida huuzwa kwa bei chee na kwamba hata kama atatumia muda kwa mfupi atakuwa tayari amekidhi haja yake kuliko kuikosa kabisa bidhaa hiyo. niliposikia maelezo hayo, siyo siri niliishiwa nguvu na kukosa matumaini ya nchi kupata suruhisho la kudumu la tatizo kubwa la bidhaa feki.

leo hii ikiwa ni miaka takriban minne tangu atoe jibu hilo, nchi imetapakaa bidhaa feki. kila unachonunua mitaani ni feki. imefika mahali sasa hata viongozi wanaotuongoza ni feki (rejea uchakachuaji wa kura). sijui tutaponaje??? kama kiongozi mkuu ana mtazamo huo, ndugu zangu tujue tumeliwa. bidhaa feki zitaendelea kumiminika siku hadi siku labda mwenyezi mungu atupatie kiongozi mwingine mwenye uchungu na wananchi wake. vinginevyo, miaka mitano tulioanza chini ya uongozi wa jk tusitegemee mabadiliko yoyote ya maana.

Mungu ibariki afrika,
Mungu ibariki tanzania.
 
Hakukosea kujibu hivyo maana thinking capacity yake ndio ilipogota hapo.
 
Back
Top Bottom